Kumbukumbu la Torati 13:10:- “MTAMPIGA KWA MAWE MPAKA AFE …….”
Adhabu ya dhambi ya ibada ya sanamu katika Israeli ya Kale

Somo hili limeandikwa na Bartek Sylwestrzak; limetafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza na Respicius Luciani Kilambo, kwa ruksa ya Mwandishi.

Adhabu ya kumwua mtu hadharani kwa kumpiga na mawe mpaka afe kwa kosa la kufanya ibada ya sanamu na pia kwa kosa la kushawishi mtu au watu wengine wafanye ibada hiyo katika taifa la Israeli ya kale “ni kali kupita kiasi” anasema mtu “MSTAARABU” wa leo, mtu wa karne ya 21.
Kumb. 13:6-11. 6 Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; 7 katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; 8 usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche; 9 mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote. 10 Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 11 Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. (SUV)

Dhambi hii ya “KUABUDU SANAMU au KUABUDU miungu WENGINE – Idolatry - ” imepanuliwa mpaka kuhusisha:

Sorcery – maana yake ULOZI au kuwasiliana na ulimwengu wa roho za giza (malaika walioanguka)

Witchcraft – maana yake UCHAWI au kutumia nguvu za giza (zinazotoka kwa malaika walioanguka) kuwadhuru au kuwatawala kiakili, kimwili na kimaadili, watu wengine

Necromancy – maana yake kuwasiliana na “watu (wanadamu) waliokufa” (kitu kisichowezekana; ni walewale malaika walioanguka, wanadanganya kwa kiinimacho)

Dhambi hizi zote tatu katika uhalisia wake zinamhusisha shetani na lile jeshi lake la malaika walioasi ambao usiku na mchana hutafuta mbinu za kuwadanganya binadamu ili waende nao motoni baada ya hukumu ya mwisho. Ikumbukwe kwamba MAPEPO hawa hawafi kama sisi binadamu tunavyokufa katika mwili, hivyo wanakufahamu wewe, na baba yako, na babu yako, ……… na kuendelea. Kwa kweli walikuwako hata kabla Adamu hajaumbwa na Mungu. Hilo ni somo kwa ajili ya siku ingine.

Kuabudu sanamu ni moja kati ya dhambi kubwa sana kwa sababu ni kitendo cha kumkataa waziwazi Mungu na wokovu aliotuletea. Hivyo matokeo ya dhambi hii ni hukumu ya moto wa milele.
Isaya 66:24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao ha[wa]takufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.

Matayo 25:46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Warumi 6:23  Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Isaya 20:15 Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli [kimbunga, tufani]; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.

Ufunuo 20:10  Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

Ufunuo 20:15  Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

NB: Nukuu zote kutoka SUV

Hivyo aliyetenda dhambi hii katika taifa lile la Israeli aliuawa kwa kupigwa mawe hadharani na pia ataenda motoni baada ya kufa na baada ya hukumu itakayofuata. Ni adhabu inayotisha na kuogofya; lakini ni adhabu inayostahili kwani Mungu katika ule uongofu wake ulio timilifu hawezi kumkubali yeyote ambaye dhambi zake hazijagombolewa kwa kiwango alichokiweka yeye mwenyewe,

Zaburi 7:11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku.

Zaburi 9:8 Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa adili.

Zaburi 11:7 Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watamwona uso wake.

Zaburi 119:137 Ee Bwana, Wewe ndiwe mwenye haki, Na hukumu zako ni za adili.

Zaburi 119:142 Haki yako ni haki ya milele, Na sheria yako ni kweli.

Zaburi 145:17 Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.

Yohana 17:25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.

NB: Nukuu zote kutoka SUV

Mungu kumpokea mtu ambaye hajagombolewa dhambi zake itakuwa ni sawa na Yeye kukubali UOVU ambao ni kinyume kabisa na utakatifu Wake.

Walawi 11:44 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.

Walawi 20:26 Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba muwe wangu.

Sasa, unafikiri kama dhambi ya kuabudu sanamu (badala ya kumwabudu Mungu) ni mbaya kiasi cha kumfanya anayeitenda kuhukumiwa adhabu ya milele, je yule anayemshawishi mwenzake kutenda dhambi hii atapewa adhabu gani? Bwana Yesu alifundisha kuhusu adhabu watakayoipata wale wanaosababisha wenzao kutenda dhambi (kujikwaa) katika Matayo 18:1-7:

18.1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema, 18.2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, 18.3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. 18.4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. 18.5 Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; 18.6 bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari. 18.7 Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!

Luka 17:1-3 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! 17.2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. 17.3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. 17.4 Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

Sasa, tumeona kwamba ibada ya sanamu siyo tu kumkataa Mungu aliyemtoa Mwana wake wa pekee ili kwa sadaka yake dhambi zetu zote ziweze kugombolewa na hivyo kufanya wokovu uwezekane kwa WOTE, bali pia ni matendo na mienendo yote inayohusiana na ibada hiyo. Katika ibada zao za kipagani watu wa Kanaani, ambao ardhi yao Mungu aliahidi kuwapa wana wa Israeli, walikuwa wakifanya zinaa, ngono na ndugu zao wa damu na wasio wa damu, ushoga, ngono na wanyama, ulozi, uchawi, “kuwasiliana” na wafu na walitoa watoto wao sadaka kwa sanamu hao.

Walawi 18:1-30: 1 Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 3 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao. 4 Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 5 Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana. 6 Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana. 7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. 8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. 9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. 10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. 11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. 12 Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. 13 Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. 14 Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. 15 Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. 16 Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo. 17 Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. 18 Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai. 19 Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. 20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. 21 Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana. 22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. 24 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Kumb. 18:9-14: 9 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri [mchawi], 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. 14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.

Mungu alitoa onyo kwa wana wa Israeli kwamba kama hawataishi kwa kufuata amri zake basi nchi itawatapika kama ambavyo iliwatapika Wakanaani wale ambao wao wana wa Israeli waliongozwa kuwavamia na kuwaondoa.

Kumb. 28:63-68: 63 Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi Bwana juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi Bwana juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki. 64 Bwana atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe. 65 Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini Bwana atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika; 66 na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako; 67 asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona. 68 Bwana atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena po pote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.

Kwa masikitiko makubwa wana wa Israeli hawakufuata amri hizi za Mungu kwa muda mrefu; na matokeo ya uasi huo ni yale ambayo Mungu aliwaonya yatatokea, kwani karne kadhaa baadaye walivamiwa na ufalme wa Siria na Israeli ya Kaskazini ikateketea; baadaye Yuda ilivamiwa na Babiloni na wana wa Israeli walichukuliwa mateka wakapelekwa utumwani. Matokeo haya yanaonyesha kwamba wana wa Israeli hawakutii siyo tu amri ya kutofanya ibada ya sanamu, bali hata ile amri ya kumtoa hadharani yule mtu atakayeanza kufanya ibada hiyo kati yao. Kitu muhimu cha kukumbuka ni kwamba taifa la Israeli la wakati ule, Mfalme wake alikuwa ni Mungu Mwenyewe, akiliongoza taifa lake kupitia Manabii kama Musa na kwa njia ya sheria yake aliyompatia Musa katika mlima Sinai. Hivyo uasi dhidi ya sheria hizi ulikuwa ni uasi dhidi ya Mungu mwenyewe katika nafasi yake kama Mfalme wa Israeli. Maana yake ni kwamba hizi ndizo sheria zilizokuwa zinaliongoza taifa hili; kila raia wa taifa la Israeli alipaswa kutii sheria hizi. Siku hizi vilevile tunatakiwa kutii sheria zinazotumika katika nchi tunamoishi, ijapokuwa nchi hizo zinaweza kuwa sio za Kikristo.

Warumi 13:1-7: 1  Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 13.2  Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 13.3  Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 13.4  kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
13.5  Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 13.6  Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 13.7  Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.

1Petro 2:13-21: 2.13  Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; 2.14  ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. 2.15  Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; 2.16  kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu. 2.17  Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme. 2.18  Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wao walio wema na wenye upole tu, bali nao walio wakali. 2.19  Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki. 2.20  Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu. 2.21  Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

Tusisahau pia kwamba sheria hii ya kukataza kuabudu sanamu au miungu wengine bado ipo hata katika enzi hizi ijapokuwa iko katika mfumo tofauti; nchi nyingi bado zinatoa adhabu ya kifo kwa mtu yeyote anayehukumiwa mahakamani kwa kosa la uasi au uhaini kwa serikali iliyoko. Kosa hili ni la kukataa utawala ulioko na kukusudia utawala mwingine.

Somo hili linaelekezwa kwa wale wenzetu wanaojiona kuwa ni “watu walioendelea” au watu wa “kisasa au ki-leo” n.k. ambao wanasoma Biblia bila ufunuo wa Roho Mtakatifu (kwa sababu wanasoma wakiwa nje ya imani, ili kukosoa, sio kujifunza neno la Mungu) ambao wanaiona sheria hii ya Mungu ya kumpiga mawe hadi afe, mtu ambaye amemwasi Mungu, kuwa ni ya “kikatili” na ya “kizamani”, haiendani na “nyakati za kisasa, za maendeleo.”

Sasa, Wakristo wa leo hawajapewa amri hii ya kumwua anayefanya ibada ya sanamu, wala kumshitaki serikalini isipokuwa kumripoti kwa Kanisa ili atengwe mpaka atakapojirekebesha (mfano: 1Wakorinto 5.1  Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. 5.2  Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.

MTU HUYU ALIAMRIWA NA MTUME PAULO ATENGWE; NA BAADAYE ANAREJESHWA KATIKA KUNDI.

2Wakorinto 2:6-11 2.6  Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi; 2.7  hata kinyume cha hayo, ni afadhali mumsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi. 2.8  Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu. 2.9  Maana naliandika kwa sababu hii pia, ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote. 2.10  Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo, 2.11  Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.)

Hii ni kwa sababu taifa linalotawaliwa na Mungu Mwenyewe moja kwa moja katika nchi moja halipo tena, Hekalu halipo, na sisi wafuasi wa Mungu sio tena wafuasi kwa kuzaliwa katika taifa moja bali ni kwa KUZALIWA UPYA KATIKA KRISTO. Imani kwa Bwana Yesu ni chaguo-huru la kila mmoja wetu linalofanywa na kila mmoja wetu katika nchi anamoishi; hatutakiwi kutoa adhabu kwa mtu yeyote anayeamua kutomwabudu Mungu, na kwa kweli Bwana Yesu anatufundisha tusimshawishi mtu yeyote kuja katika Imani kama hataki.

Matayo 10:12-14: 12 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. 10.13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 10.14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.

Katika jamii ya leo adhabu ya kifo haifanyiki waziwazi, mbele ya kadamnasi, hivyo watu wengi kwa kutosikia habari zake wanaiona kama kuwa ni ya kikatili wanaposikia kwamba mhalifu fulani amenyongwa; hii inatokana na UNAFIKI wa nafsi ambapo wanajali muonekano wa nje na kutoona au kusahau uhalisia wa matokeo ya maamuzi yetu ya hapa duniani katika ulimwengu wa kiroho AMBAO NDIO ULIMWENGU HALISI.

Luka 11:37-40: 37 Alipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia, akaketi chakulani. 11.38 Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula. 11.39 Bwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang'anyi na uovu. 11.40 Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia?

Ndugu yangu, utaishi hapa duniani kwa miaka michache sana, lakini utaishi katika ulimwengu wa kiroho – peponi au motoni – MILELE! Matokeo ya maamuzi yako ya hapa duniani ndiyo utakayoishi nayo milele. Tafakari kwa hilo!

Yule mtu wa “kisasa, mpenda maendeleo, aliyestaarabika” anaiona adhabu hii kuwa ni kali kupita kiasi na watu hao wanapata picha kwamba Israeli ilikuwa nchi ya wafia-dini wapendao kumwaga damu, wanaoongozwa na Mungu mkatili! Lakini kwa kweli kweli kosa lile lilistahili adhabu hiyo na kama wana wa Israeli wangeitekeleza adhabu hii kikamilifu pale ilipoanza, taifa zima lisingeingia katika kushiriki kosa hili na Mungu asingeliangamiza taifa lake. Lakini historia inatuonyesha yaliyotokea – Israeli ilivamiwa na hawakuwa na uwezo wa kujitetea, kwani Mungu, mlinzi wao, aligeuza uso wake kutoka kwao. Ule ufalme imara uliotukuka aliouacha Mfalme Daudi na kisha Mfalme Solomoni umesambaratika, mpaka hapo Mwana wa Mungu mwenyewe atakapoiongoza tena Israeli kutoka Jerusalemu baada ya kumshinda mpinga-Kristo katika vita ya Armagedoni.

Danieli 11:36-45: 36 Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa yatafanyika. 37 Wala hatahijali miungu ya baba zake; wala yeye aliyetamaniwa na wanawake; wala hatamjali mungu awaye yote; maana atajitukuza mwenyewe juu ya wote. 38 Lakini katika mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua atamheshimu, kwa dhahabu, na fedha, na vito vya thamani, na vitu vipendezavyo. 39 Naye ataziteka nyara ngome zenye nguvu kwa msaada wa mungu mgeni; na yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa, 40 na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati. 41 Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni. 42 Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. 43 Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake. 44 Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi. 45 Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri (Jerusalemu); lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.

Ufunuo 19:19-21:  Kisha nikamwona huyo mnyama (mpinga Kristo), na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na Yeye aketiye juu ya farasi yule (Bwana Yesu), tena na majeshi yake. 19.20  Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; 19.21  na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake Yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.

Biblia ni Neno lililofunuliwa na Mungu 2Timoteo 3:16:  Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; Biblia ni Neno la kweli, Yohana 17:17: Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli; ambalo haliwezi kutanguka au kuvunjwa Yohana 10:35: Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka). Tunapaswa kukumbuka haya pale tunapokutana na mistari ya Biblia ambayo ni vigumu kwetu kuielewa kwa sababu zozote zile, kama hii ya Kumb. 13:10. Maandiko haya ni KWELI na tukitafuta kuyaelewa kwa moyo wote, tutagundua maana yake, kwa uongozi wa Roho Mtakatifu.

Matayo 7:7: Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

Hivyo badala ya kuacha mafundisho magumu ya Biblia (maana yapo!) yatukwaze, tuwe na imani, tuendelee kutafuta ile KWELI iliyo ndani ya maandiko kwa moyo mkunjufu, bila kukata tama, na kwa matumaini.

Yohana 6:34-66: Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia? 6.61 Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung'unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza? 6.62 Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza? 6.63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. 6.64 Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti. 6.65 Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu. 6.66 Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.

Mungu anataka tufike kwenye ile kweli.

1Timoteo 2:3-4: 2.3  Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; 2.4  ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli; lakini pia anatuwekea MITIHANI katika mapito yetu ili kupima kama KIU yetu ni ya kweli, na kuwatenga wale wanotaka kuijua na kuifuata ile kweli na wale ambao ni WANAFIKI TU. Hivyo tukiitafuta ile kweli kwa moyo wote, Yeye atatupatia thawabu yake – na tutafika katika ukweli.

Kumb. 4:29: Lakini huko, kama mkimtafuta Bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.

Jukumu la mfuasi wa Bwana Yesu ni moja: Baada ya kuzaliwa upya anza kujifunza Neno la Mungu, ishi maisha yako kwa kufuata Neno hilo, endelea kukua kiroho na kusoma Neno kila wakati, wasaidie wengine nao walijue Neno kulingana na vipaji alivyokupa Mungu kupitia Roho Mtakatifu (Pastor/Mwalimu/Msimamizi/Mhudumu/Mwandishi/n.k.).

Bwana Asifiwe sana na mbarikiwe katika Jina lake.

https://sayuni.co.tz