UTANGULIZI

Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.

Yakobo 5:16 SRUV

Wakristo wenzangu, karibuni katika kurasa ya tovuti hii ambayo imewekwa mahususi kwa ajili ya Sala na Maombi. Unaweza kunitumia mahitaji yako ambayo yanahitaji nguvu ya maombi na sala iongezeke kutoka kwa Wakristo wenzako walio sehemu mbalimbali. Ikiwa unahitaji Maombi & Sala zifanyike juu ya hitaji lako ambalo linaweza kuhusiana na ajira, mahusiano, ugonjwa, masomo, shida unazopitia kama Mkristo, na kadhalika, unaweza kunitumia kwa namba za simu zilizotolewa au kwa FB au kwa e-mail, nami nitaziorodhesha ili Wakristo wenzako, pamoja na mimi, sote tuweze kukuombea kwa Mungu wetu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

5.17 ombeni bila kukoma;

1Wathessalonike 5:17 SUV

Maandiko yanatuagiza tusali na kuomba kila wakati. Bwana wetu ametufundisha namna ya kuomba; ametutaka tusihofu juu ya mahitaji yetu na ametuhakikishia kwamba ikiwa tutaomba na kusali, Baba wa mbinguzi atasikia na kutusaidia.

6.31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

6.32 Kwa maana hayo yote Mataifa (wasioamini) huyatafuta; na Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

6.33 Bali utafuteni kwanza ufalme Wake, na haki Yake; na hayo mengine yote Atawapa, tena kwa ziada.

Mathayo 6:31-33
Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

Luka 11:9 SRUV

Mimi sitakuahidi miujiza, bali naahidi kuwa nitapiga magoti na kumwomba Mungu wetu kwa ajili yako! Halafu tunamwachia Yeye maombi yetu kwa amani tele moyoni. Tuma shida zako, tutakuombea!!

Respicius Luciani Kilambo.