Vita ya Kiroho:
Mwongozo wa Mkristo katika Kupambana na Dhambi

By Bartek Sylwestrzak

Original Writing was Titled “Spiritual Battle: A Believer’s Guide to Combat Sin”

Tafsiri hii ya Kiswahili na Respicius Luciani Kilambo

Permission for this Kiswahili Translation has been Kindly Granted by
Mr. Bartek Sylwestrzak
Ruksa ya Tafsiri Hii ya Kiswahili Imetolewa Mahususi na Ndugu B. Sylwestrzak

Chapisho hili haliuzwi
This publication is not for sale

Rafiki zangu,

Sisi sote ni wenye dhambi na sote tumo katika mapambano dhidi ya dhambi. Harakati hii haitaisha mpaka siku tutakapokuwa na Bwana wetu.

Mwongozo huu umeandikwa ili kutusaidia katika mapambano haya. Hili si somo pana sana kuhusiana na tatizo la dhambi na namna ya kupambana nalo, lakili ni msaada tunaoweza kuutumia wakati tunapokabiliwa na mitihani – unaweza kulihifadhi somo hili katika kompyuta yako, kompyuta-bapa yako (tablet), simu yako ya mkononi (inayoitwa rununu kwa Kiswahili!), n.k., ili iwe tayari wakati wowote unapoihitaji ikusaidie. Huu ni muhtasari wa kanuni za msingi kabisa za vita ya kiroho na una nukuu nyingi za maandiko kuhusiana na somo pana la dhambi za wanadamu. Lengo lake ni kutuwezesha kupata kwa urahisi zile kweli za kanuni za Biblia zinazohusiana na mitihani yetu tunapokuwa katikati ya mapambano hapa duniani.

Unaweza kuona kwamba sehemu fulani za mwongozo huu ni zenye faida katika nyakati tofauti za maisha yako na matumaini yangu kwamba muundo uliotumika utamwezesha kila mmoja kuitafuta na kuipata sehemu anayoihitaji kwa haraka katika nyakati za shinikizo la dhambi na mitihani. Tafadhali kuwa huru katika kuongeza msisitizo (highlighting) sehemu zozote za nukuu za maandiko au kuongeza aya unazoziona kuwa zinahusika zaidi na mapambano yako binafsi kama / ikiwa mimi sijaweka ili utengeneze waraka unaokufaa wewe binafsi kwa ajili ya matumizi yako mwenyewe.

Sehemu nyingi za kazi hii zina msingi wake katika sehemu ndogo inayoitwa “The Believer’s Dealing With Sin” ya somo linaloitwa “Hamartiology” lililotayarishwa na Dr. Robert D. Luginbill, na kwa kweli napenda kuwasisitiza wote kusoma siyo tu sehemu hiyo bali somo zima linalopatikana [bure, bila malipo] katika tovuti yake https://ichthys.com, ili uweze kujifunza na kupata uelewa wa kina wa suala la dhambi na mapambano yetu dhidi ya dhambi. Nyenzo nyingine mbalimbali zimeorodheshwa mwishoni mwa somo hili.

Ingawa kusudi la mwongozo huu ni kutusaidia kustahamili mitihani yetu, kupinga majaribu kwa ufanisi na kupata ushindi dhidi ya dhambi, taswira hii ya vita yetu ya kiroho haipaswi kuwa eneo pekee la kuzielekeza nguvu zetu au kuwa ndilo eneo lenye kipaumbele katika maisha yetu ya Kikristo. Tunafahamu kutokana na mashindano ya michezo au mapambano ya vitani kwamba ukiingia uwanjani kwa malengo ya kujilinda tu (defence) – kuzuia kushindwa – mara nyingi matokeo yake ni kuwa wakati wote utakuwa chini ya mashambulizi makali kutoka kwa adui. Hali ni hiyo hiyo katika mapambano yetu dhidi ya dhambi.

Kila siku tunahitaji kukua kiroho kwa kujifunza Neno la Mungu, kulielewa kwa kusikiliza mafundisho sahihi ya Neno hilo, kuliamini, na kulitumia katika maisha yetu – yote hayo yakifanyika katika nguvu ya Roho Mtakatifu. Jinsi tunavyotembea katika njia ya Mungu kwa imani zaidi na kutenda yaliyo sahihi, ndivyo pia itakavyokuwa rahisi zaidi kwetu kukataa maovu. Tunavyozidi kukua kiroho na kushambulia uovu, ndivyo itakuwa rahisi zaidi kuimarisha ulinzi (defence) wetu.

Kutakuwa na nyakati, hata hivyo, ambapo kuupa kisogo uovu na kuelekea wema kutakuwa jambo gumu kabisa. Ni tumaini langu kwamba mwongozo huu utakuwa na faida ya kiroho kwako msomaji katika nyakati hizo na utakusaidia kuendelea katika njia anayoipenda Mungu kwa ajili yako.

Na tumfuate Bwana wetu Yesu Kristo kwa uaminifu na tuzae matunda mengi na mema kwa ajili Yake kwa kukua katika KWELI na kutimiza [majukumu ya] utumishi Aliyotayarisha kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Wakati ni mfupi sana!

Katika neema za Bwana wetu,

Bartek.

Yaliyomo

I. Kujitayarisha kwa mapambano 7

1. Tunaishinda dhambi kwa uamuzi wetu wa utashi huru tulio nao 7

2. Msimamo wetu kama waumini 10
2.1. Tumewekwa huru kutoka nguvu ya dhambi iliyokuwa ikitutia hatiani 10
2.2. Umoja wetu na Kristo na uhusiano wetu na dhambi 11
2.3. Kristo ni uhai wetu na lengo / kusudi letu ni kuwa wafuasi wake na
kumtumikia 13
2.4. Uweza wa Mungu umo ndani yetu katika Roho Mtakatifu 15
2.5. Sisi ni watoto wa Mungu, wateule Wake na makuhani Wake. Tuliitwa
tuwe watakatifu na tuwe nuru katika ulimwengu wa giza 19

3. Tunapaswa kumweka Mungu juu ya kila kiu tuliyo nayo yenye dhambi 22
3.1. Tunapaswa kumpenda Mungu wetu na kuchukia dhambi 22
3.2. Hatuwezi kuipa nafasi dhambi 24
3.3. Tukimwita katika kweli ili atusaidie, Mungu atatuokoa 25

4. Tunahitaji kuendelea kuwa na imani 26

5. Kuvaa silaha zote za Mungu 28

6. Sala 36

II. Vita yenyewe / vita yetu 38

1. Kujiweka mbali na mambo yote yanayoweza kutuingiza katika dhambi 38
1.1. Kuendelea katika kumwogopa Mungu 40
1.2. Kuwa macho kiroho ili usiingie katika vishawishi 42
1.3. Kusimama imara dhidi ya hila za Ibilisi 44
1.4. Tumo katika himaya ya adui 46

2. Kamwe hatutopewa mtihani utakaozidi uwezo wetu wa kuhimili 47

3. Katika vita hii tunamtegemea Mungu, siyo sisi wenyewe 48
3.1. Mungu ndiye mhimili wetu, Yeye ndiye ngao yetu, Anayeturayarisha kwa
ajili ya vita, Yeye ndiye ngome yetu na kimbilio letu 50
3.2. Mungu ndiye anayetupigania 51
3.3. Mungu anajua tunahitaji msaada Wake na anataka tumwombe msaada huo 52
3.4. Mungu anatusaidia kupitia Roho Wake 53
4. Ustahamilivu 53
4.1. Katika mitihani mingi yawezekana tu kushinda kwa ustahamilivu,
lakini Mungu yuko nasi wakati wote 53
4.2. Hatimaye Mungu hutuokoa katika mitihani yetu 55

5. Motisha ya kustahamili na kutokata tamaa katika vita hii 59
5.1. Hakuna kinachofichika kwa Mungu 59
5.2. Mawazo, maneno na matendo yetu yote yatahukumiwa 59
5.3. Dhambi inaharibu ushuhuda wetu na utumishi wetu, na hivyo
inaharibu thawabu yetu ya milele 60
5.4. Tunapaswa kustahamili kwa ajili ya Bwana wetu 63
5.5. Miili yetu ni viungo vya [Mwili wa] Kristo na ni mahekalu ya Roho
Mtakatifu 65
5.6. Tunahitaji kustahamili kwa ajili ya ndugu zetu na kwa ajili ya wale
wanaoufuata ukweli 66
5.7. Tunatoa ushuhuda katika kila kitu tunachofanya 71

6. Maisha yetu yote tumo vitani, lakini tunaweza kuwa na furaha 72
6.1. Kuwa na furaha katikati ya mitihani 72
6.2. Kuwa na furaha katika ushindi 74

III. Kusimama baada ya kuanguka [katika dhambi] 76

1. Kitubio/toba 77
1.1. Adabisho kutoka kwa Mungu 78
1.2. Huruma ya Mungu ni kubwa kuliko dhambi zetu 80
1.3. Maana ya kitubio / toba 82
1.4. Toba ni lazima iwe halisi, ya kweli 83
1.5. Toba ya kweli huleta mabadiliko 84
1.6. “Unapoanguka, simama na uendelee”, haraka! 85
1.7. Kujipambanua nafsi zetu 87

2. Kuungama 89

3. Msamaha na mwanzo mpya 89
3.1. Tunasamehewa kwa msingi wa dhabihu ya Bwana Yesu Kristo 89
3.2. Tunaanza upya na kuendelea, tukisahau ya nyuma 91
3.3. Maisha ya Kikristo ni vita, na katika vita hakuna utimilifu 91

4. Tunarejea katika kumfuata Kristo na kuingia tena katika mapambano 93

IV. Vyanzo vingne vya mafundisho juu ya kupambana na dhambi 95

I. Kujitayarisha kwa ajili ya vita.

Hatua ya kwanza katika kuishinda dhambi ni azma ndani ya mioyo yetu ya kumtukuza Mungu kwa kuwa watiifu Kwake na kuondoa kila kitu [kutoka mioyoni mwetu] ambacho kinatutoa katika njia Yake na ambacho kinatuletea ukinzani katika kutimiza nia Yake [Mungu] katika maisha yetu.

1. Tunaishinda dhambi kwa uamuzi wetu wa utashi [huru]

Wokovu wetu kutoka dhambi unaweza kulinganishwa na wokovu wetu kutoka[na] na matokeo yake ya mwisho kabisa – hatia na hukumu. Kwa hakika, dhambi ina matokeo mengine pia, ambayo hutokea mara baada ya tendo la dhambi, kwa mfano tendo la kuiba husababisha mtendaji kukamatwa, kushitakiwa na kadhalika, na pia kutakuwa na adhabu kutoka kwa Mungu.

Tunaokolewa “kwa neema kutokana na imani yetu”.

2.8  Kwa maana mmeokolewa kwa neema [ya Mungu], kwa njia ya imani [yenu kwa Kristo]; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa [cha bure] cha Mungu;
2.9  [na] wala si kwa matendo [yenu], mtu awaye yote asije akajisifu.
Waefe. 2:8-9

“Kwa neema”, kwa sababu hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, kwamba Alimtoa Mwanaye wa pekee ili aje kulipia dhambi zetu na hakuhitaji malipo haya kutoka kwetu. Adhabu ya dhambi ni mauti (War. 6:23) na tusingeweza kulipia dhambi zetu sisi wenyewe. Tuligombolewa (tulilipiwa gharama) kwa dhabihu ya Kristo msalabani.

“Kwa njia ya imani”, kwa sababu hii ni azma ya utashi wetu, kumwamini Kristo na kukubali malipo Yake kwa ajili ya dhambi zetu zote. Mungu amefanya yote yaliyohitajika kufanywa ili tuweze kuokolewa; na hayo ni yale ambayo hatukuweza kuyafanya kwa ajili yetu wenyewe tukingali wanadamu wenye dhambi. Tunachokifanya katika wokovu wetu ni kutumia uamuzi wa utashi wetu katika kupokea neema hii – uamuzi wa utashi wetu unaotokana na shauku yetu ya kuokolewa.

Vivyo hivyo katika kupambana na kuishinda dhambi. Ni lazima tufanye uamuzi. Katika neema Yake, Mungu ametufanyia yote yaliyo muhimu ili tuweze kuokolewa, na katika neema Yake hiyo hiyo, Mungu ametupatia kila kitu tunachokihitaji ili tuweze kutimiza mapenzi Yake na kupambana na dhambi kwa mafanikio. Ni lazima tufanye uamuzi unaotokana na utashi [huru] tuliopewa (moja kati ya neema lukuki tulizopewa na Mungu), kwamba tunataka kuendelea katika imani hai kwa Mungu wetu na kuishinda dhambi na tunapaswa kustahamili katika uamuzi huu kwa kuamua kuutumia msaada (neema tena!) anaoutoa kwa ajili yetu. Naye atatupatia uwezo wa kustahamili katika nia yetu hiyo chanya na atatuokoa.

Katika hali ya kufunikwa na dhambi, tukingali chini ya vishawishi na katika mapambano yetu dhidi ya maeneo ya udhaifu katika mioyo yetu, tunaweza kupata ugumu katika kufanya uamuzi huo. Lakini tukifanya uamuzi unaotokana na utashi [huru] tulio nao wa kuweka imani yetu katika Kristo na kuokolewa na kuondokana na utengano na Mungu, kuondokana na giza la kutoamini na kutawaliwa na hulka yetu ya dhambi, basi hata katika wakati wa vita ngumu tutaweza kufanya maamuzi ya kuachana na dhambi na kuokolewa kutoka katika dhambi kwani sasa tukiwa katika Kristo tumo katika mwanga, wana wa Mungu anayetusaidia kwa uweza wa Roho Wake Mtakatifu ambaye ametupatia [wakati ule tulipookolewa] – neema zaidi!

Bwana wetu ndiye mwanga. Tukiwa ndani Yake tunakuwa katika mwanga Wake mkuu.

1.4 Ndani Yake (Bwana Yesu Kristo) ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
1.5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
Yoh. 1:4-5

8.12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Yoh. 8:12

12.46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.
Yoh. 12:46

5.8  Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru
Waefe. 5:8

5.5  Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
1Wathess. 5:5

2.9  Bali ninyi ni mzao mteule [jamii teule], ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki [wanaolindwa na] ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
1Pet. 2:9

Tulikuwa mbali hapo zamani, lakini sasa tumeletwa karibu Naye.
2.13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi ambao mlikuwa mbali kabisa mmeletwa karibu kwa damu ya Kristo.
Waefe. 2:13

Sisi [tunaoamini] ni watoto wa Mungu.

1.12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
1.13 waliozaliwa, si kwa damu [maamuzi ya wazazi], wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu [mume kwa mkewe], bali kwa Mungu.
Yoh. 1:12-13

3.1  Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
1Yoh. 3:1

8.16  Roho Mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
War. 8:16

3.26  Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
Waga. 3:26

Tunaye Roho Mtakatifu.

4.6  Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye/[aitaye], Aba, yaani, Baba.
Waga. 4:6

1.21  Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,
1.22  naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni (guarantee) ya [uwepo wa] Roho [Mtakatifu] mioyoni mwetu.
2Wakor. 1:21-22

Tunaweza kufanya mambo yote tukiwa katika Yeye anayetutia nguvu.
Wafi. 4:13

Tunapaswa kukumbuka kwamba hakuna dhambi, hakuna udhaifu, hakuna hata mazoea mabaya (kw. mf. ulevi) yanayoweza kutuzuia kuutumia uwezo wetu wa kuamua, yaani ule utashi ambao ndio mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26) ulio ndani yetu sote wanadamu. Suala linalobakia ni kama tunataka kufanya uamuzi wa kumtii Mungu wetu na kuachana na dhambi.

Vivyo hivyo, utakuwa ni uamuzi wetu huru kunyoosha mkono na kujitwalia nyenzo hii tuliyopewa wakati wa mitihani utakapofika.

2. Msimamo wetu kama waumini.

Uamuzi wetu [unaotokana na utashi wetu] wa kuweka imani yetu katika Kristo umetupatia wokovu, lakini haujaondoa suala la dhambi katika maisha yetu. Hata hivyo, uamuzi huu umebadilisha hadhi (status) na uhusiano wetu na dhambi; vita yetu dhidi ya dhambi inaendelea, lakini vita hii sasa inakuwa na taswira tofauti.

2.1 Tumewekwa huru kutoka nguvu ya dhambi kututawala – na kututia hatiani.

Adhabu za dhambi ambazo ni kifo (War. 6:23), na utengano na Mungu (Isa. 59:2; cf. Mwanzo 2:16-17) – zimelipiwa na Kristo pale msalabani, nasi tumeyakubali / tumeyapokea malipo haya kwa kuweka imani yetu katika Kristo. Kwa kuwa tumeamini katika Kristo, basi tumewekwa huru kutoka katika nguvu ya dhambi ya kututia hatiani.

8.1  Sasa, basi, hakuna [tena] hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
War. 8:1

1.7  Katika Yeye huyo, kwa [njia ya] damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa (kulingana) na wingi wa neema Yake.
Waefe. 1:7

1.13  Naye alituokoa [kutoka] katika nguvu (utawala) za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana [wake mpendwa];
1.14  ambaye katika Yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Wakol. 1:13-14

Hata kama vita yetu dhidi ya dhambi itachukua muda mrefu na itakuwa ngumu, hata kama mara nyingi tutakatishwa tamaa, tutashindwa na tutajeruhiwa vibaya kiroho katika mwendo na maisha yetu, tukumbuke wakati wote kwamba tumewekwa huru kutoka katika himaya yake (dhambi) na uweza / nguvu yake yenye uwezo wa kututia hatiani. Ikiwa tutaendelea na imani yetu katika Bwana, wokovu wetu wa milele utakuwa salama.

10.27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
10.28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
10.29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
10.30 Mimi na Baba tu umoja.
Yoh. 10:27-30

2.2 Umoja wetu na Kristo na uhusiano wetu na dhambi.

Imani yetu katika Kristo imetuweka katika umoja Naye na kwa njia hiyo tumekuwa wafu kwa dhambi.

6.1  Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
6.2  Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
6.3  Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
6.4  Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika maisha mapya.
6.5  Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
6.6  mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;
6.7  kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.
War. 6:1-7

Mara tulipoweka imani yetu katika Kristo, papo hapo tukaingizwa katika umoja Naye. Ubatizo huu katika Kristo (baptism into Christ) unamaanisha kwamba tumebatizwa katika kifo Chake pia – tumeshiriki katika kifo Chake, hivyo kwamba yaliyomtokea Yeye, kwa maana fulani yametutokea na sisi pia, kama vile tulikuwa Naye katika kifo Chake. Nafsi/mtu wetu wa kale (kabla ya kuzaliwa upya) aliyekuwa katika utumwa wa dhambi amekufa pamoja Naye (Kristo). Hivyo kwa ubatizo huu tumeingia katika maisha mapya na tumekombolewa kutoka katika utawala wa dhambi.

Hii haina maana ya kwamba hatutendi dhambi tena au hatuingii katika vishawishi. Tunatenda dhambi na tunaingia katika vishawishi / majaribu, lakini mabadiliko makubwa yamefanyika ndani ya mioyo yetu katika hali yetu ya kiroho na uhusiano wetu na dhambi. Nafsi yetu ya kale, [iliyokuwa] chini ya nguvu ya dhambi na [iliyokuwa] mtumwa wa dhambi, sasa imekufa – War. 6:2. Uamuzi (unaotokana na utashi wetu) wa kutenda dhambi haufanyiki kama ilivyokuwa hapo kabla [ya kuokolewa] – uamuzi ambao tuliweza kujizuia nao (dhidi yake) kwa muda mfupi tu wakati ule [kabla hatujazaliwa upya], lakini hatimaye [aghalabu] tuliingia katika dhambi. Sasa (baada ya kuzaliwa upya) uamuzi huu unamtoa mtu huyu (sisi) ambaye alikufa, aliyekuwa katika lindi la dhambi, na kumleta katika uzima. Baada ya kuzaliwa upya tutakutana tena na mambo yaliyokuwa yakitawala maisha yetu hapo kale, lakini sasa tumekufa kwayo.

Tulikuwa watumwa wa dhambi (Yoh. 8:34; War. 6:6) na tunajua jinsi maisha yetu yalivyokuwa tupu na yalivyokuwa gizani wakati tulipokuwa chini ya utumwa huo. Lakini mara baada ya kuamini, ile kweli [tuliyoiamini] ikatuweka huru, na ile nafsi yetu ya kale iliyokuwa utumwani ikafa.

8.31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
8.32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Yoh. 8:31-32

6.11  Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
6.12  Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
6.13 Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini
kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki.
War. 6:11-13

4.17  Basi nasema neno hili, tena nashuhudia (nasisitiza) katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao [za kutoamini];
4.18  ambao; akili zao zimetiwa (uelewa wao umeingia) giza, nao wamefarikishwa (wametengwa) na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
4.19  ambao wakiisha kufa ganzi (wamepoteza dira ya kilicho chema) wanajitia katika mambo ya ufisadi (kuridhisha nafsi) wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani [tamaa isiyo kikomo] (yaani wamepata mbadala wa Mungu).
4.20  Bali ninyi, [hivi] sivyo mlivyojifunza Kristo;
4.21 ikiwa [ni kweli] mumemsikiliza Yeye na mumefundishwa Naye, kwani kweli imo katika Yeye [Kristo].
4.22 [Kwani mmejifunza ukweli] kwamba kuhusiana na ule mwenendo wenu wa kale/awali/zamani, mmemvua [kama nguo] yule mtu wenu wa kale/awali/zamani, ambaye anaharibiwa na tamaa zidanganyazo,
4.23 na kwamba sasa mnafanywa wapya [na R. M.] katika mtazamo wa nia zenu,
4.34 na pia sasa mmevaa (kama nguo) yule mtu mpya, aliyeumbwa katika uongofu / haki na utakaso wa [ile] kweli kulingana na viwango vya Mungu.
Waefe. 4:17-24

Sasa, katika Bwana wetu, sisi ni viumbe wapya. Tuliozaliwa upya, hai kutoka katika wafu – Matt. 8:21-22; Luka 9:59-60.
5.24 Amin, amin, nawaambia, yeye alisikiaye neno langu na kumwamini Yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Yoh. 5:24

5.17  Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yaliyopita, tazama! Yamekuwa mapya.
2Wakor. 5:17

3.9  Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu (nafsi ya) wa kale, pamoja na matendo yake;
3.10  mkivaa utu (nafsi) mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake Yeye aliyeuumba.
Wakol. 3:9-10

1.12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
1.13 waliozaliwa, si kwa damu (maamuzi ya wazazi), wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu (mume kwa mkewe), bali kwa Mungu.
Yoh. 1:12-13

3.3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
3.4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
3.5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
3.6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
3.7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
3.8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
Yoh. 3:3-8

5.1  Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu.
1Yoh. 5:1a

2.3 Kristo ndiye uhai wetu na kusudi letu ni kuwa wafuasi Wake na kumtumikia.

Sasa Kristo ndiye uhai wetu – Yeye anaishi ndani yetu, nasi tunaishi kwa ajili Yake.

1.21  Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
Wafi. 1:21

1.27  ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu
Wakol. 1:27

3.4  Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu [wa ufufuo].
Wakol. 3:4

3.26  Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
3.27  Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.
Waga. 3:26-27

Tunaishi kwa ajili ya Kristo. Kusudi la maisha yetu – kusudi la kila kitu tunachokifanya kila siku – linapaswa kuwa ni ili tuwe wafuasi Wake na watumishi Wake. Kuzaa matunda mengi na bora kwa ajili ya Bwana wetu bila ya kuruhusu dhambi yoyote, jambo lolote la kidunia au magugu [ya kimaisha] kupunguza kasi yetu.

12.26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Yoh. 12:26

5.14  Maana, upendo wa Kristo unatushurutisha; maana tuna uhakika huu, ya kwamba ikiwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi wote walikufa;
5.15  tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake Yeye aliyekufa, akafufuka kwa ajili yao (yaani wawe watumishi Wake).
2Wakor. 5:14-15

2.20  Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Waga. 2:20

13.22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
13.23 Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kulielewa; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.
Matt. 13:22-23 (Pia Marko 4:19-20; Luka 8:14-15)

2.3  Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
2.4  Hakuna apigaye (mpiganaji wa) vita ajitiaye katika shughuli za dunia, [kwani hujitahidi kufanya vema] ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
2Tim. 2:3-4

Kuwa wafuasi Wake maana yake ni kwamba tutalazimika kujikana sisi wenyewe.

16.24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Matt. 16:24 (Pia Matt. 10:38; Lk 9:23; 14:27)

2.4. Uweza wa Mungu umo ndani yetu katika Roho Mtakatifu.

Kama waumini katika Kristo, sote tunao uweza wa Mungu ndani yetu kutokana na kukaliwa na Roho Mtakatifu. Yeye (R. M.) ndiye anayetuwezesha na kutupatia nguvu ya kuwa wafuasi wa Bwana wetu na kumtumikia Bwana wetu.

14.16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
14.17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yoh. 14:16-17

5.5  na tumaini halitahayarishi (kwani litatimia); kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi;
War. 5:5

8.9 Hata hivyo, ninyi hamtawaliwi na hulka yenu ya dhambi, kwani mnaenenda katika Roho [Mtakatifu], ikiwa ni kweli Roho wa Mungu yuko ndani yenu. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wa Kristo.
8.10 Bali ikiwa Kristo akaa ndani yenu, hata kama mwili wako utakufa kwa sababu ya hulka ya dhambi iliyomo, roho yako itakuwa hai kwa sababu ya uongofu wako.
War. 8:9-10

3.16  Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
1Wakor. 3:16

1.21  Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,
1.22  naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni (guarantee) ya Roho [Mtakatifu] mioyoni mwetu.
2Wakor. 1:21-22

4.6  Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye/[aitaye], Aba, yaani, Baba.
Waga. 4:6

1.14  Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.
2Tim. 1:14

3.3  Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
3.4  Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
3.5  si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa [kupitia] kuoshwa kwa kuzaliwa kwa [mara ya] pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
3.6  ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
3.7  ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Tito 3:3-7

3.24  Naye azishikaye amri zake hukaa ndani Yake; Naye [hukaa] ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa Anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
1Yoh. 3:24

4.13  Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani Yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho Wake.
1Yoh. 4:13

Na sasa ni katika uweza wa Roho Mtakatifu ndiyo tunapata ushindi dhidi ya dhambi. Siyo kwa nguvu yetu wenyewe, ambayo tunajua hatimaye ilishindwa wakati ule tulipokuwa watu wasioamini. Sasa tunao uweza wa Mungu ndani yetu na ikiwa tutaamua kuutumia uweza huu, tutashinda vita zote.

6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho Wangu, asema Bwana wa majeshi.
Zakaria 4:6

3.14  Kwa [sababu] hiyo nampigia Baba magoti,
3.15  ambaye familia yote ya mbinguni na ya duniani inaitwa kwa Jina lake
3.16 awajalieni kwa kadiri ya utajiri wa utukufu Wake, mfanywe imara katika nafsi yenu ya ndani kwa uweza wa Roho wake,
3.17  ili, kwa msingi thabiti wa upendo, Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani;
Waefe. 3:14-17a

Jukumu letu ni kuutumia utashi wetu kufanya maamuzi [sahihi]. Vita yetu ya wakati wote ni kati ya kuamua kuishi katika Roho Mtakatifu na kusalimu amri kwa hulka yetu ya dhambi.

5.16  Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
5.17  Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Waga. 5:17

Dhambi yote hutoka ndani yetu na huzaliwa na nia zetu (Matt. 15:18-19; Marko 7:20-23), hivyo uwanja wa kwanza kabisa wa vita ambamo tunautumia utashi wetu au uwezo wetu wa kuamua kati ya kumfuata Roho Mtakatifu au kuifuata hulka yetu ya dhambi ni katika fikra na nia zetu.

8.5  Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
8.6  Kwa kuwa [kufuata] nia ya mwili [hupelekea katika] mauti; bali [kufuata] nia ya roho [hupelekea katika] uzima na amani.
8.7  Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
8.8  Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu (yaani wasioamini, walio watumwa wa miili yao).
War. 8:5-8

4.8  Hatimaye, ndugu zangu, [mnavyoendelea katika imani], mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi [matakatifu], yo yote yenye kupendeza [kwa Mungu], yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwa [una matumaini yoyote ya kupewa] sifa nzuri [kutoka kwa Mungu siku ya hukumu] yatafakarini hayo.
Wafi. 4:8

1.13  Kwa hiyo vifungeni [mikanda] viuno vya nia (minds) zenu, na muwe macho kiroho; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika [wakati wa] ufunuo wake Yesu Kristo.
1Pet. 1:13

Kutokana na Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu, sasa tunayo nia na fikra za Kristo ndani yetu. Kwa uweza wa Roho Mtakatifu tuna ulazima wa kutwaa mateka kila wazo na kuliweka chini ya utiifu kwa Kristo.

2.12  Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
2.13  Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya kiroho kwa maneno yanayofundishwa na Roho [Mtakatifu].
2.14  Basi mwanadamu [asiyekuwa na R. M. (yaani asiyeamini)] hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa [kuwezeshwa na R. M.]
2.15  Lakini mtu [mwenye Roho Mtakatifu] hutathmini mambo yote, wala yeye hafanyiwi thathmini za kibinadamu.
2.16  Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, aweze kumwelimisha [Bwana]? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
1Wakor. 2:12-16

10.5 kubomoa hoja za ghiliba, za uwongo; na kila kiburi au ufidhuli unaojipandisha dhidi ya ufahamu wa Mungu, na kuiteka nyara kila fikra ili ipate kumtii Kristo;
2Wakor. 10:5

Matendo yetu yataonyesha ni upande upi uaminifu wetu uliko, ule upande wa kiroho au ule upande wa kidunia / kimwili.

5.19  Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu [mwenendo wa aibu], ufisadi,
5.20  ibada ya sanamu [madawa ya kulevya, kutegemea watu, malaika], uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
5.21  husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Waga. 5:19-21

5.22  Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
5.23  upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
5.24  Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Waga. 5:22-24

Hayo ndiyo maamuzi (mazoezi ya utashi wetu) tunayoyafanya wakati wote. Hii ndiyo vita yetu ya kila siku ambamo inatulazimu kutembea na kuenenda kwa mwanga wa Roho Mtakatifu (Warumi 8:4), badala ya kuizima na kuifunika sauti Yake inayotuongoza na kutukumbusha tubaki katika njia ya Mungu.

8.12  Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni (tunawajibika), si [k]wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,
8.13  kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, [majaliwa yetu ni kifo]; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
War. 8:12-13

5.25  Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Waga. 5:25

5.19  Msimzimishe Roho;
1Wathess. 5:19

Roho Mtakatifu siku zote atashinda katika vita hii – ikiwa tutamwacha apigane kwa niaba yetu.

5.16  Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Waga. 5:16

3.9  Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi [wakati wote*], kwa sababu uzao (mbegu ya Mungu) Wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi [wakati wote*] kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
1Yoh. 3:9. *kama lifestyle / desturi.

2.5. Sisi ni watoto wa Mungu, wateule Wake na makuhani Wake. Tuliitwa tuwe watakatifu na tuwe nuru katika ulimwengu [huu] wa giza.

Tunajua uamuzi sahihi ni upi. Lakini ikiwa tumeingia katika mtego wa dhambi na tunahangaika kupata ushindi dhidi ya dhambi hiyo, au kama tuko chini ya kishawishi ambacho kina kivutio kikubwa kwetu, tunaweza kuhangaika na kupata shida katika kufanya uamuzi huo sahihi.

Hapo ndipo tunapohitaji kujikumbusha kuhusu wito wetu. Sisi ni watoto wa Mungu, wateule Wake na makuhani Wake.

3.26  Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
Waga. 3:26

1.3 Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ametubariki katika Kristo kwa kila neema ya kiroho inayotolewa mbinguni;
1.4 kwa kuwa tunajua (tumeona) ya kwamba kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, alituteua katika Yeye (Kristo) ili tuwe watakatifu , watu wasio na hatia mbele Zake.
1.5 Kwa kuwa alituteua kabla [ya kuumbwa ulimwengu] katika upendo Wake kwa nia ya kututwaa tukae Kwake kwa njia ya Yesu Kristo kulingana na furaha ya mapenzi Yake,
Waefe. 1:3-5

2.9 Bali ninyi ni jamii teule, makuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki (wanaolindwa na) ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru Yake adhimu;
1Pet. 2:9

Na ametufanya [sisi] kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba Yake – utukufu na ukuu u na Yeye hata milele na milele. Amina.
Ufu. 1:6

Kutokana na hadhi yetu ya milele, baada ya kujitwalia uongofu wa Kristo (War. 3:21-25, 4:1-5, 5:8-10; 2Wakor. 5:21; Waga. 2:16; Waefe. 1:7, 2:8-9; Wafi. 3:9; 1Pet. 2:24, 3:1; Yer. 33:15-16), sisi ni watakatifu katika macho ya Mungu na hivyo ndiyo maandiko yanavyotutambua (War. 8:27, 12:13; 1Wakor. 1:2; 2Wakor. 1:1; Wafi. 1:1; etc).

6.11  Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii (rejea aya 9-10); lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
1Wakor. 6:11

1.7  kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo
War. 1:7

1.1  Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.
Waefe. 1:1

Ijapokuwa hatutakuwa huru na dhambi mpaka hapo baada ya ufufuo, tunapaswa kuutafuta utakaso katika maisha yetu ya sasa, tukitimiza mapenzi ya Bwana wetu na tukitoa / tukionyesha ushuhuda wa hadhi yetu ya milele kwa mwenendo wetu wa hapa duniani. Ametuita tuwe watakatifu, kwani Yeye ni mtakatifu.

2 Nena na mkutano [kusanyiko lote] wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu.
Walawi 19:2

13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.
Kumb. 18:13

5.48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Matt. 5:48

7.1  Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimilisha – perfecting - utakatifu (utakaso wetu) katika kumcha Mungu.
2Wakor. 7:1

12.14  Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Waebr. 12:14

1.14  Kama watoto watiifu, msizifuate tamaa zenu mlizozifuata [wakati mlipokuwa] katika ujinga wenu [wa ile kweli];
1.15  bali kama Yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
1.16  kwa maana imeandikwa, Muwe watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
1Pet. 1:14-16

Sisi ni chumvi ya ulimwengu, sisi ni mwanga katika ulimwengu wa giza. Fikra zetu, kauli zetu na matendo yetu yanapaswa kuwa ushuhuda wa ile kweli, ili mwanga wetu wa ndani ung’are na kumletea utukufu Mungu wetu.

5.13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
5.14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika (kufichika – hidden) ukiwa juu ya mlima.
5.15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi (bakuli/kikapu), bali juu ya kiango (kinara); nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
5.16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Matt. 5:13-16

2.15  mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Wafi. 2:15-16a

3. Tunapaswa kumweka Mungu juu ya kila kiu / shauku tuliyo nayo yenye dhambi.

3.1 Tunapaswa kumpenda Mungu wetu na kuchukia uovu.

Unapaswa kumpenda Bwana Mungu wetu kwa moyo wako wote na kwa *nafsi (mwili na roho) yako yote na kwa nguvu / uweza wako wote. Bwana Yesu Kristo alitufundisha kwamba hii ndiyo amri iliyo kuu zaidi.

5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho [*nafsi] yako yote, na kwa nguvu zako zote.
Kumb. 6:5

22.37 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho [*nafsi] yako yote, na kwa nguvu zako zote.
22.38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
Matt. 22:37-38

*NB.: Soma Mwanzo 2:7.

Kwa kuwa tunampenda Mungu wetu, basi tunapaswa kuchukia uovu wa aina zote. Dhambi ni kinyume cha mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu.

10 Enyi m[u]mpendao Bwana, uchukieni uovu;
Zab. 97:10a

13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;
Mithali 8:13a

Dhambi inaweza kutupatia starehe ya muda mfupi, lakini tunajua kwamba mwisho wake ni kutuingiza katika uharibifu wa kiroho. Husababisha tupoteze ushirika na Mungu, hupunguza mazao yetu [ya kiroho] kwa ajili Yake na hutuingiza katika adhabu ya kinidhamu kutoka kwa Mungu.

3 Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga (utungu wa uzazi); Ni mkali kama upanga wa makali kuwili.
5 Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
Mithali 5:3-5

21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi (rejea aya 5-20), Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
Mithali 7:21-23

6.8  Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Waga. 6:8

2.11  Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
1Pet. 2:11

Kwa sababu ya wito wetu huu tunapaswa kuweka mapenzi ya Mungu wetu JUU ya shauku yoyote ya dhambi tunayoshawishika nayo, hamu yoyote ya starehe ya dhambi ya muda mfupi tu. Bila kujali kishawishi kina mvuto wa namna gani na bila kujali uchu wa kuridhisha kishawishi hicho una nguvu kiasi gani, tunapaswa kukitazama kishawishi hicho kama Mungu anavyokitazama – kwamba ni kiovu.

5.29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
5.30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Matt. 5:29-30 SUV

Maneno ya Bwana wetu hapa yanatufundisha kwamba katika mapambano yetu na dhambi hakuna kulegeza kamba, hakuna maridhiano – compromise - [na dhambi], ingawa maneno haya hayatakiwi kuchukuliwa kama yalivyo, kwamba tukate, tung’oe viungo vyetu! - vinginevyo muda si mrefu hatutakuwa hata na huo mkono wa kushika hilo panga la kukata ulimi. Mwisho wa yote, maneno haya yanamaanisha kwamba hali ya utimilifu katika mwenendo wetu kuhusiana na dhambi ni jambo tusiloliweza kwa juhudi zetu wenyewe, na hivyo kama ilivyo katika mengine mengi katika maisha yetu ya Kikristo, tunabaki tukitegemea neema za Mungu, na katika suala la dhambi, rehema Zake zisizo kifani. Ni kwa neema tumeokolewa – hatuwezi kupata wokovu kwa juhudi zetu sisi wenyewe. Na kwa msaada wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu tunaweza kupambana na dhambi na kufanikiwa katika vita hiyo.

Tunapaswa kufanya/kuchukua juhudi/hatua zote katika kuwa waaminifu kwa Bwana wetu. Lakini wakati huo huo ni lazima tukumbuke kwamba hatuwezi kujitegemea wenyewe – wakati wote tunahitaji msaada Wake.

3.2. Hatuwezi kuipa nafasi dhambi.

Tumepewa fursa ya kulijua Neno la Mungu ili tulitumie katika maisha yetu; tuishi kutokana na maelekezo ya Neno hilo la Mungu. Tunapaswa kuwa watendaji wa Neno, na si wasikilizaji ambao punde husahau na kujidanganya wenyewe.

1.21  Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uliobaki, na kupokea kwa upole Neno lile lililopandwa ndani [yenu], liwezalo kuziokoa nafsi zenu.
1.22  Lakini iweni watendaji (watekelezaji wa mafundisho ya) wa Neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
1.23  Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa Neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo (yaani analisikia Neno).
1.24  Maana hujiangalia, kisha huenda zake (yaani analisahau), mara akasahau jinsi alivyo (yaani akaacha kutekeleza mafundisho yake).
1.25  Lakini aliyeitazama sheria timilifu iliyo ya uhuru (yaani Agano Jipya linapotofautishwa na Agano la Kale), na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wake, huyo atakuwa na neema katika yote afanyayo.
Yakobo 1:21-25

Neno la Mungu linatushauri tumpende Bwana wetu na tuchukie uovu wa aina zote, hivyo katika vita yetu dhidi ya dhambi tunalazimika kutokuwa na huruma – dhidi ya tabia ya mioyoni mwetu sisi wenyewe ya kutaka kutenda dhambi. Isijetokea katika sehemu mojawapo ya mioyo yetu tumeweka na kuficha uchu wa aina fulani (ambao tunajua tunapaswa kuukatilia mbali) wa kutenda dhambi ili kuridhisha tamaa fulani tuliyo nayo siku za usoni. Nia yetu ya kushinda vita yetu dhidi ya dhambi inapaswa kuwa ya dhati, ya kweli. Kwani Mungu wetu anaijua mioyo yetu (Zab. 139:1; Mithali 21:2; Yer. 17:10).

1.5  Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala hamna giza lo lote ndani yake.
1.6  Tukisema ya kwamba twashirikiana Naye, [halafu] tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;
1.7  bali tukienenda nuruni, kama Yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi (pamoja na Baba na Mwana, aya ya 3), na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha [na] dhambi yote.
1Yoh. 1:5-7

13.12  Usiku umeendelea sana, asubuhi imekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
13.13  Na tuenende kwa heshima, staha kama tufanyavyo mchana; si kwa fujo na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
13:14 Basi na tuvae ngao ambayo ni Bwana Yesu Kristo, na tusifanye mipango ya kuridhisha uchu wa mwili.
War. 13:12-14

Kwa upande mmoja, hatuwezi kufikia kiwango timilifu katika utiifu wetu na katika nia zetu pia. Roho zetu zina nia njema ya kutenda mema na ziko tayari kufanya hivyo, lakini miili yetu ni dhaifu (Matt. 26:41). Na Mungu wetu anayajua madhaifu yetu – anapoona kwamba tuna nia njema, yuko tayari kutunyooshea mkono wake wa msaada. Kwa upande mwingine, tunapaswa kuweka jitihada katika kufuata mafundisho ya Neno la Mungu kwa uaminifu na kwa moyo mmoja, usiogawanyika. Na hapo ndipo tutaweza kuivunja ile dhambi inayozinga fikra, kauli na matendo yetu.

3.3. Tukimwita katika kweli ili atusaidie, Mungu atatuokoa.

Uchu wetu wa kutenda dhambi unaweza kuwa na nguvu kweli kweli. Ikiwa tutaacha dhambi fulani itutawale kwa kitambo fulani kirefu, basi dhambi hii inaweza kuwa eneo letu la udhaifu (… ile tamaa ikiishachukua mimba [yaani ikimzidi nguvu mtu] huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa [yaani akiendelea kuitenda tena na tena] … Yakobo 1:15). Lakini ikiwa tunataka kuishinda kikweli kweli na ikiwa tunataka tutembee katika ile njia ambamo Mungu anataka tutembee, basi kwa msaada Wake tutafanikiwa.

Kama ilivyokuwa katika wokovu, Mungu Mwenyewe ndiye anayetuwezesha kushinda. Na kama tutamwita Yeye katika kweli, tukiwa na nia halisi ya kuwa waaminifu Kwake na kuvunja dhambi zote zinazotuzinga, Yeye atatusaidia kushinda.

18 Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Zab. 145:18-19

15.7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lolote nanyi mtatendewa.
Yoh. 15:7

4. Tunahitaji kuendelea kuwa na imani.

Katika haya yote tunahitaji kuwa na imani (Waebr. 11). Yawezekana tumejaribu kunyanyuka baada ya kuanguka mara nyingi lakini tukajikwaa na kuanguka tena. Yawezekana tumepigana vita na kushindwa kwa muda mrefu. Yawezekana sasa tumekata tamaa na kufikiri kuwa haiwezekani kuwa huru kutoka katika mtego tulimonasa kutokana na dhambi yetu. Yawezekana tukajiona tumekuwa watumwa wa / kwa dhambi.

Vyovyote vile tunavyofikiri au tunavhohisi, inatupasa tusipoteze imani yetu kwamba mambo yote yawezekana kwa Mungu wetu na kwamba Yeye anaweza kutuokoa kutoka katika dhambi yoyote, mwenendo wowote wa dhambi au kutawaliwa kokote na dhambi. Hakuna kisichowezekana kwa Mungu wetu na hivyo hakuna kisichowezekana kwa yeye anayemwamini na kumwegemea Mungu wetu. Ikumbukwe kwamba kuamini kwetu ni matokeo ya utashi wetu huru.

14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.
Mwa. 18:14

27 Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?
Yer. 32:27

17.20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
Matt. 17:20

19.26 Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Matt. 19:26

Hivyo tunapomwomba Mungu wetu msaada Wake, tunapaswa kufanya hivyo kwa imani.

11.24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11:24

1.5  Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
1.6  Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
1.7  Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
1.8  Mtu wa nia mbili husita-sita [na kukosa msimamo] katika njia zake zote.
Yak. 1:5-8

Vishawishi vingine vinaweza kuwa na nguvu kiasi kwamba yaweza kuwa vigumu kwetu hata kudhani kwamba tunaweza kupata ushindi dhidi ya vishawishi hivyo. Hata katika hali yetu ya kuamini tunaweza kuwa na [ma]eneo letu la udhaifu na kunaswa katika mtego huo kiasi kwamba kuupata uhuru wetu yaweza kuonekana kuwa ni jambo lisilowezekana. Yaweza kuwa tulikuwa tumejiingiza katika mwenendo wa dhambi au mazoea ya dhambi fulani kabla hatujamwamini Kristo. Katika vita yetu dhidi ya dhambi tunaweza kuhisi kuwa tunakabiliana na Goliati.
Ebu tufuate mfano wa Daudi na ebu tumkabili Goliati kwa imani.

41 Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri.
43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.
44 Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.
45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti.
49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.
51 Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia.
1Samweli 17:41-51

1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
Zaburi 27:1

4.13  Nayaweza mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu.
Wafi. 4:13

5. Kuvaa silaha zote za Mungu.

Tunaanza vita yetu kwa azimio la kuwa watiifu kwa Mungu, kutimiza mapenzi Yake aliyoyaweka kwa ajili yetu na kuacha dhambi kabisa. Tunaweka azma hii tukiwa na imani thabiti kwamba hakuna kisichowezekana kwa Mungu na kwa msaada Wake tunaweza kuitimiza azma hii.

Azimio hili linapaswa kutufanya tuchukue hatua bayana na mahususi. Mtume Paulo analinganisha kuchukua hatua hizi na kutwaa silaha zote za Mungu. Tunajua ya kwamba wakati wowote tunaweza kuwekwa chini ya kishawishi cha aina moja ama ingine na tutalazimika kukabiliana na dhambi uso kwa uso. Kwa sababu hii, tunapaswa kujitayarisha [kiroho] kwa ajili ya kuyakabili majaribu haya yanayotungojea ili tusije tukanaswa na mtego wa dhambi wakati tusiotarajia.

6.10  Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza [mkuu] wa nguvu zake.
6.11  Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza [kusimama imara dhidi ya] hila za Shetani.
6.12  Kwa maana mapambano yetu sisi si dhidi ya viumbe wenye damu na nyama; bali ni dhidi ya falme na mamlaka [ya ki-malaika], dhidi ya wakuu wa giza hili [la sasa], dhidi ya majeshi ya pepo wabaya [walio] katika ulimwengu wa roho.
6.13  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, [muweze] kusimama.
6.14  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii [deraya] ya haki (uongofu) kifuani,
6.15  na kufungiwa miguu utayari tuupatao kwa Injili ya amani;
6.16  zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
6.17  Tena [katika vita hii ya kiroho] ipokeeni chapeo (helmet) ya wokovu, na [mvae kiunoni] upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Waefeso 6:10-17

Kwanza, tunafanywa wenye nguvu kwa uweza wa Mungu na si kwa uweza wetu wenyewe (aya ya 10). Tunasimama imara dhidi ya njama za Ibilisi kwa kutegemea silaha za Mungu (aya za 11 na 13).

Tunahitaji kupewa msaada wa kiroho na Mungu, kwa sababu vita yetu ni ya kiroho. Ingawa hatufanyi vita kati yetu na Shetani akishirikiana na jeshi lake la pepo moja kwa moja au uso kwa uso, wao ni adui zetu ambao wakati wote wanajaribu (kwa mbinu mbalimbali) kutuondoa katika ushirika wetu na Mungu na kutufanya tutende dhambi (aya ya 12; cf. Mwanzo 3).

10.3  Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
10.4 Kwani silaha za vita tunayopigana si za kimwili, bali zina uwezo katika Mungu, wa kuangusha ngome,
10.5 kubomoa hoja za ghiliba, za uwongo; na kila kiburi au ufidhuli unaojipandisha dhidi ya ufahamu wa Mungu, na kuiteka nyara kila fikra ili ipate kumtii Kristo;
2Wakor. 10:3-5

Tunajiandaa kwa vita hii kwa kutwaa na kuvaa silaha kamili za Mungu.

1. Mkanda wa [ile] kweli (aya ya 14a). Kweli ya Neno la Mungu, ambayo umejifunza na kuielewa kwa usahihi, ndiyo msingi wa mapambano yetu yote ya kiroho.

2. Dirii (deraya) ya uongofu (aya ya 14b). Uongofu ni matumizi sahihi ya Neno la Mungu (kwa imani) katika maisha yetu.

6.13 Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka katika mauti na kuingia katika uzima. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki.
War. 6:13

3. Tunavalisha miguu yetu [viatu vya] utayari wa Injili ya amani (aya ya 15). Kama ambavyo uwezo wa kutembea na kukimbia kwa haraka katika vita au mapambano yoyote ulivyo muhimu sana, vivyo hivyo utayari wetu katika kumtumikia Mungu na kuitangaza kweli Yake mahala na katika hali yoyote anayotupangia unatulinda dhidi ya kupotea kutoka katika njia Yake kwa kufuata shauku zetu au ushauri usio sahihi. Injili ndiyo habari njema ya wokovu wetu katika Bwana Yesu Kristo na tangu hapo mwanzo shughuli ya kuitangaza habari hii imekuwa ni sehemu muhimu ya habari yenyewe (Matt. 28:19; Matendo 1:8; 2Tim. 4:2; 1Pet. 3:15).

4.18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Ukombozi kwa waliotekwa, Na vipofu kupata kuona tena,
4.19 Na kuutangaza mwaka wa [fadhili za] Bwana (miaka 1000 ya neema Yake – mileniamu).
Luka 4:18-19 (Isa. 61:1-2)

Injili inatuletea amani, kwa sababu kwa njia ya Injili tunapatanishwa na Mungu (War. 5:1). Amani hii maana yake siyo kukosekana kwa migongano, la hasha, bali ni usitawi na baraka zinazotokana na kuwa katika ushirika na Mungu na hili huleta utulivu ndani yetu hata wakati tunapokuwa katikati ya vita yenye fujo na misukosuko tele. Katika dunia hii tutapata dhiki, lakini katika Bwana wetu tunapata amani.

16.33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo (mtapitia) dhiki (tribulation); lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu!
Yohana 16:33

4.6  Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
4.7  Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Wafi. 4:6-7

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
Isa. 26:3

4. Ngao ya imani ambayo kwayo tutaweza kuizima mishale ya moto ya yule mwovu (aya ya 16). Hii ni sehemu muhimu ya ulinzi tulio nao, kwa sababu imani ni njia ya kukua kiroho na pia ni njia ya kuenenda katika maisha ya Kikristo. Tuna ulazima wa kuiamini kweli ili iwe kitu halisi ndani ya mioyo yetu na tuweze kuitumia; tunahitaji kuiamini kweli ili tuweze kuitumia katika mazingira ya maisha yanayotukabili.

Imani yetu katika kweli ya Biblia inatupa uwezo wa kujilinda dhidi ya upotofu ulioenea kila mahala na udanganyifu wa dunia hii, ulaghai wa dhambi na pia dhidi ya hulka yetu wenyewe ya dhambi iliyo dhahiri katika miili yetu na nia zetu. Tunaweza “kuizima mishale yote ya moto ya yule mwovu” kwa kuliamini Neno la Mungu na siyo yale tunayoambiwa na ulimwengu na yale yanayotoka katika msukumo wa hulka yetu ya dhambi iliyomo ndani ya miili yetu.

5.7 Maana twaenenda kwa [kile tunachokijua kuwa ni kweli] kwa njia ya imani, na siyo kwa kile kinachoonekana machoni mwetu.
2Wakor. 5:7

11.1  Basi imani [katika Neno lililoandikwa na lenye uhai] ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, [imani] ni bayana [proof] ya mambo yasiyoonekana.
Waebr. 11:1

5. Chapeo (helmet) ya wokovu (aya ya 17a). Kama ambavyo chapeo (helmet) ilivyo sehemu muhimu katika mavazi / vifaa vya kivita kwa sababu inalinda kichwa, vivyo hivyo tunapaswa kukumbuka kwamba wokovu wetu katika Yesu Kristo unatulinda dhidi ya mashambulizi yoyote yanayoelekezwa katika uzima wetu wa milele. Hata kama vita yetu ya kiroho ikija kuwa ngumu sana kwetu na hata kama tumekuwa tukishindwa vibaya katika nyanja mbalimbali za vita hii, tunapaswa kukumbuka kwamba ikiwa tumeweka imani yetu katika Yesu Kristo Bwana wetu, hakuna kinachoweza kutupora wokovu wetu, na hakuna anayeweza kutupiga pigo la kutuangamiza. Ikiwa tunaendelea kuwa kondoo wa Bwana wetu, tutakuwa salama u salimini, hata pakitokea nini!
10.27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
10.28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe (hawataangamia milele); wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
10.29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
10.30 Mimi na Baba tu umoja.
Yoh. 10:27-30

8.1  Sasa, basi, hakuna [tena] hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
War. 8:1

8.31  Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani atakayekuwa dhidi yetu?
8.32  Yeye asiyemwachilia (ambaye hakumhurumia - SRUV) Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
8.33  Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
8.34  Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
8.35  Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
8.36  Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
8.37  Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
8.38  Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
8.39  wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
War. 8:31-39

6. Upanga wa Roho ambao ni Neno la Mungu (aya ya 17b). Neno la Mungu ndilo panga la Roho kwani ukweli wa maandiko ndicho kifaa ambacho Roho Mtakatifu anakitumia kama silaha yetu katika vita hii. Roho Mtakatifu anatusaidia tuielewe kweli, anaifanya kweli iwe kitu halisi kwetu na anatusaidia tuitumie kweli hii katika vita yetu ya kiroho. Lakini, ili Roho Mtakatifu aweze kutusaidia tuitumie kweli ya Neno la Mungu, tunapaswa kwanza kuifahamu kweli hiyo. Ikiwa hakuna kweli ya maandiko mioyoni mwetu, hii inamaanisha hakuna silaha mikononi mwetu ambayo Roho anaweza kuitumia. Na zaidi ya hapo, ikiwa kiasi cha ile kweli mioyoni mwetu (yaani kiasi cha kanuni za maandiko) ni kikubwa, basi na silaha zetu za mapambano zinakuwa bora zaidi katika kupambana na adui. Roho ndiye anayeifanya merikebu yetu ya vita vya kiroho iende mbele. Katika vita hii, Neno la Mungu linatupatia ulinzi (aya ya 14a), lakini pia ndilo silaha yetu katika mashambulizi dhidi ya adui. Tukiwa na kweli ya maandiko tayari mioyoni mwetu kwa sababu tumejifunza, tumeiamini na tumekuwa mahiri katika kuitumia, na Roho Mtakatifu akitutia nguvu katika mchakato huu, tutaweza kujibu mashambulizi yote ya yule mwovu na kuivunja ngome ya uwongo wake, tukifuata mfano wa Bwana wetu (Matt. 4:1-11; Luka 4:1-13). Pia ni kwa kutumia silaha hii ndiyo tunaweza kuwasaidia ndugu zetu katika Kristo – tunawasaidia katika mitihani yao kwa kuitumia kweli ya maandiko.

Kutwaa silaha zote za Mungu kunaweza kuelezwa kwa muhtasari kwa kutumia hatua 3 za msingi zinazoainisha misingi ya kukua kwetu kiroho:

1. Kuujua ukweli wa maandiko.
• Aya ya 14a – “Basi simameni imara, mkiwa mmejifunga mkanda wa [ile] kweli viunoni”.
• Aya ya 17 - “Tena [katika vita hii ya kiroho] twaeni chapeo (helmet) ya wokovu, na [mvae kiunoni] upanga wa Roho ambao ni Neno la Mungu.

2. Kuamini ukweli wa maandiko.
• Aya ya 16 - “Twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu”.

3. Kuishi maisha yako ya Kikristo katika uweza wa Roho [Mtakatifu[.
• Aya ya 14b - “Na kuvaa dirii (deraya) ya uongofu kifuani”.
• Aya ya 15 - “Kuvalisha miguu yetu [viatu vya] utayari wa Injili ya amani”.
• Aya ya 17 - “Upanga wa Roho [Mtakatifu]”.

Kinachotayarisha ulinzi wetu dhidi ya dhambi ni mchakato wa kukua kiroho – kuanza kujifunza Neno la Mungu, kuliamini na kulitumia katika maisha yetu katika uweza wa Roho Mtakatifu. Jinsi tunavyozidi kuendelea katika kweli na jinsi tunavyozidi kupevuka kiroho, ndivyo jinsi inavyozidi kuwa vigumu sisi kuingia katika mitego ya vishawishi. Kanuni hii ina matumizi kadhaa katika muktadha wa vita yetu dhidi ya dhambi.

Kwanza, kwa kuwa kweli ya maandiko ndiyo msingi wa silaha tulizopewa na Mungu, tuna ulazima wa kuelekeza fikra zetu katika msingi huu wakati wote. Hatua ya msingi kabisa katika kufanikisha hili ni mafunzo yetu ya kila siku ya Biblia – kama waumini, tunapaswa kujifunza Neno la Mungu kila siku. Lakini zaidi ya kujifunza Biblia kila siku, tunapaswa pia kutafakari juu ya kweli ya maandiko wakati wote katika siku yetu kwa kuitumia kila fursa tunayopata kufikiria maandiko, japo kwa muda mfupi tu.

Siku ni ndefu na ndani yake kuna mengi yanayotokea ambayo yanahitaji matumizi ya fikra na akili zetu na ambayo yanaweza kutupeleka mbali na Mungu wetu. Tunaishi katika ulimwengu potofu, ulioharibika ambao umo katika makucha ya Ibilisi (1Yoh. 5:9) na wakati wote huwa tunazungukwa na uharibifu huu. Muda mwingi wa maisha yetu ya kila siku tunautumia tukiwa kati ya wale ambao hawataki kusikia wala kujihusisha na kweli. Kusoma Biblia au kusikiliza Biblia ikisomwa wakati wowote tunapopata nafasi (kwa mfano wakati wa mapumziko kazini au wakati tukiwa njiani katika mishughuliko mbalimbali), au hata kama hivyo vyote viwili haviwezekani basi kukumbuka sisi wenyewe mistari / aya mbalimbali zilizotugusa wakati fulani (Zaburi zinaweza kuwa na msaada mkubwa!) kunaweza kuweka silaha zetu za ile kweli katika hali ya uimara na ulinzi wetu ukiwa umesimama siku nzima. Ni wakati tunapokuwa mbali na Neno la Mungu ndipo tunapokuwa rahisi kushambuliwa na kudhurika kiroho.

Pili, tunapojikuta tumeingia katika mazingira ambamo ni rahisi kuingia katika dhambi. Yaweza kuwa ni kwa sababu ya udhaifu fulani tulio nao au kutokana na mazingira tulimo ambamo dhambi inatendeka na wanaotuzunguka kama vile ni jambo la kawaida kwao. Wakati fulani tunaweza tukajua mapema kuhusu hali hii itakayotokea, na hapo ni wajibu wetu [kiroho] kufanya yote yaliyo ndani ya uwezo wetu kujitayarisha kiroho kwa changamoto zilizo mbele yetu. Inatubidi, kabla ya kuingia katika majaribu / mitihani hiyo, kukusanya na kujifunza kanuni za maandiko zinazohusiana na mazingira hayo kwa kiasi ambacho tunaweza kuona kabla, na kujipanga kwa jinsi ambayo tutayatumia maandiko hayo kwa mafanikio ili tusijejikwaa na kuanguka. Tukishindwa kuchukua tahadhari hii tutaingia katika hatari ya kudhurika [kiroho] na dhambi, kwa sababu mara tukishaingia katika mazingira hayo ni vigumu sana kuweka na kuimarisha ulinzi wa kiroho kwa haraka. Na kama mazingira hayo magumu yatakuwa na kishawishi au vishawishi ambavyo sisi wenyewe tuna udhaifu navyo, tunaweza tukawa wazito kuimarisha ulinzi wetu wa kiroho ili kupambana kwa mafanikio.

Kwa mfano, dhambi za mdomo / kauli zinaweza kuwa ni changamoto kwetu au yaweza kuwa tunafanya kazi katika mazingira ambamo dhambi za mdomo / kauli huwa ni jambo la kila wakati. Tunaweza kujitayarisha kwa kukusanya na kukariri / kujifunza maandiko yanayohusiana na kutenda dhambi “za ulimi” (kwa mfano Zaburi 34:13; 39:1; 52:2-4; 141:3; Mithali 10:8b; 10:19a; 11:12; 12:18a; 15:4b; 17:20b; 17:27-28; 18:21; 21:23; 26:28; Yeremia 9:3; 9:8; Waefeso 5:3-5; Yakobo 1:26; 3:2-12; 1Petro 3:10; etc) na jinsi tunavyoweza kushuhudia ile kweli na kumsifu Mungu katika yale tunayoyasema (kwa mfano Zaburi 35:28; 37:30; 45:1; 66:17; 71:24; 119:172; Mithali 10:8a; 10:19b; 10:20a; 12:18b; 15:4a; 15:23; 18:4; 21:23; 29:20; Mhubiri 3:7; Waefeso 4:25; 29:31; etc). Kwa msingi wa maandiko haya, tunajua kwamba inatupasa tusijihusishe na mijadala ya kijinga na isiyokuwa na maadili mema, na katika kuendelea kuwa waaminifu tunaweza kulazimika kuweka msimamo imara kati yetu na wale wanaotuzunguka.

Ebu tuone mfano mmoja. Tutafanya nini ikiwa katika mazungumzo ya kawaida ofisini mtu mmoja anasema kwa utani juu ya mtu mwingine maneno ambayo ni machafu, ya matusi na ya kufedhehesha? Je, tutacheka na kujifanya kama vile tumefurahia “utani” huo ijapokuwa tunajua kwamba tunajutia na kukwazika mioyoni mwetu? Au tutaonyesha wazi kwa mtu huyo kwamba alichokisema hakitufurahishi na ni machukizo kwetu – hata kama matokeo yake ni kutengwa na wenzetu hapo ofisini? Kwa hakika tunajua, au tunapaswa kujua kwamba kuwa waaminifu kwa ile kweli kunahitaji ujasiri.

10.32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
10.33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
10.34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
10.35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
10.36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
Matt. 10:32-36 (Pia Luka 12:8-9)

Kwa hakika tunajua ya kwamba katika hii dunia sisi ni wageni.

11.13  Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
11.14  Maana hao wasemao maneno kama hayo (ya imani yao) waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe (tofauti na ile walimo kwa sasa).
11.15  Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, [ya kutoamini] wangalipata nafasi ya kurejea.
11.16  Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji (Yerusalemu Mpya).
Waebr. 11:13-16

(1) Petro, Mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule ambao japo wametengwa na kutawanywa katika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia, (2) wamechaguliwa na Mungu Baba ...
1 Pet. 1:1-2a

Tunapaswa kujitayarisha kukabiliana na mambo kama hayo kwa kujifunza maandiko yanayohusika, kwa kutafakari namna tutakavyoyatumia maandiko pindi tutakapokabiliwa na hali hiyo, na kumwomba Mungu wetu atupatie nguvu na ujasiri wa kufanya hivyo pale muda wa mitihani unapofika. Hatua mbili za mwanzo katika mchakato huu – kuendelea kuwa na msimamo imara katika Neno na kweli Yake siku nzima na kujitayarisha kwa ajili ya magumu tutakayoyakabili – zinaonyesha wazi kwamba zile silaha za Mungu zinapaswa kutwaliwa na kuvaliwa kabla ya vita na siyo wakati vita imeshaanza.

Tatu, ikiwa baada ya kujihusisha na mwenendo fulani wa dhambi tumekuwa dhaifu kwa dhambi hiyo, tunapojiona tunahangaika kupambana na hata kishawishi kidogo cha dhambi hiyo, basi ufumbuzi wa tatizo hili ni kuendelea na mchakato wetu wa kila siku wa kukua kiroho, na siyo tu kujitahidi kuepuka dhambi hiyo pekee. Kama tunakua kiroho, tutakuwa tunajenga ulinzi wetu na kuimarika na tutakarabati silaha zetu za kiroho. Kujifunza Neno la Mungu kunatusaidia kurejesha macho, akili na nia yetu kwenye kweli na kuondoka kwenye dhambi. Mara nyingi ni katika wakati wa mgogoro wa kiroho, tunapohangaika, bila mafanikio, na dhambi fulani au mwenendo wa dhambi, na ndipo tunahitaji sana msaada wa Neno la Mungu, na hapo ndipo hulka yetu ya dhambi inapigana na roho zetu kwa nguvu sana. Matokeo yake ni kwamba sisi wenyewe tunakuwa wazito kufanya lililo sahihi na kuchukua hatua za kurejea kwenye msitari ulionyooka.

6. Sala.

Sala na maombi ni sehemu muhimu ya mapambano yetu. Kwa njia ya sala na maombi tunajiweka tayari kwa ajili ya mitihani yetu, tunakuwa macho kiroho, tunapata kimbilio katika Bwana wetu, tunaomba msaada Wake na tunatiwa nguvu na Roho Mtakatifu. Kwa njia sala tunalitafakari Neno la Mungu ili tuweze kupita katika njia Yake. Mwongozo huu unaweza kuchukuliwa / kueleweka kama ni msaada wa kuziongoza sala zetu.

Bwana wetu alituambia tuombe kile tunachokihitaji na tutapewa (Luka 18:1-8).

7.7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
7.8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Matt. 7:7-8 SUV

14.13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
14.14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
Yoh. 14:13-14 SUV

Tunapaswa kusali na kuomba kwa ajili ya mahitaji yetu yote.

4.6  Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
4.7  Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Wafi. 4:6-7 SUV

Tunahitaji kusali na kuomba bila kukoma.

5.17  ombeni bila kukoma;
1Wathess. 5:17 SUV

Tunahitaji kusali na kuomba katika imani.

11.24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11:24 SUV

1.5  Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
1.6  Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
1.7  Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
1.8  Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.
Yak. 1:5-8 SUV

Lakini katika hayo yote tunapaswa kukumbuka vipengele muhimu vinavyohusiana na sala na maombi – sala zetu zinapaswa kuwa halisi na zinapaswa kutoka moyoni. Sala na maombi yasiwe maneno matupu yanayosemwa kama namna / jinsi ya kutimiza wajibu fulani na mazoea fulani tuliyoyakariri hapo zamani, namna ya kuonyesha watu wengine na sisi wenyewe kwamba tumefanya yanayotakiwa kufanyika.

Ikiwa tunasali na kuomba katika ukimya na faragha ya vyumba vyetu au tukiwa katikati ya vita ya kiroho mbele ya mazingira ya uhasama / uadui (cf. Daudi alipomkabili Goliati), sala na maombi yetu yanapaswa kutoka moyoni kwa mtiririko wa kusihi, kuheshimu, kuomba msaada wa Baba Mungu wetu. Kwa sala na maombi, tunajitoa kwa muda kutoka duniani, tunaingia katika mahala patakatifu pa Mungu Baba na tunasogea mbele ya kiti Chake cha enzi ili tupate neema. Wakati wote tunapaswa kufanya hivyo katika taadhima na kweli.
Kwani Yeye ni Kuhani Mkuu mwenye kuyaelewa na kuwa na rehema kuu juu ya madhaifu yetu, kwa kuwa hata Yeye alipitia mitihani kama ambayo sisi tunapitia, bali bila ya kutenda dhambi.

4.16  Basi na tukikaribie kiti cha neema [cha Baba] kwa ujasiri, ili tupewe rehema [Yake], na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waebr. 4:15-16

16 Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo; Ikawa taabu machoni pangu;
17 Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu,
Zab. 73:16-17a SUV

II. Vita Yenyewe.

1. Kujiweka mbali na mambo yote yanayoweza kutuingiza katika dhambi.

Hatua muhimu katika kujitenga na dhambi ni kujiweka mbali na mambo yote yanayoweza kupelekea sisi kuingia katika dhambi. Kwa hakika sisi wote tunayajua madhaifu yetu na maeneo ya tabia zetu yaliyo na madhaifu. Tunapaswa kujiweka mbali na mazingira ambamo tunajua udhaifu wetu au maeneo ya udhaifu wetu yatakuwa ni rahisi kujitokeza na vishawishi kuweza kuamsha udhaifu huo kwa urahisi. Tunapaswa kujiweka mbali na kila aina ya uovu.

10.16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Matt. 10:16 SUV

16.19  Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
War. 16:19 SUV

14.20  Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili (fikra) zenu mkawe watu wazima.
1Wakor. 14:20 SUV

5.3  Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
5.4  wala aibu (matusi) wala maneno ya upuzi (utani/mizaha) wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali (ni muhimu) kushukuru.
5.5  Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, [kwani mwenye tamaa] ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
5.6  Mtu asiwadanganye kwa maneno [matupu] yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi [na wasioamini].
5.7  Basi msishirikiane nao.
5.8  Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,
5.9  Sasa, tunda linalotokana na nuru huendana na wema, haki/uongofu na kweli yote,
5.10  katika kila kitu [muwe] mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.
5.11  Wala msishiriki katika matendo yasiyozaa ya giza, bali [myafichue na] myakemee;
5.12  kwa kuwa yanayotendeka kwa siri na wale walioikataa kweli, ni aibu hata kuyanena.
5.13  Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru [na kuonyeshwa ubaya wake].
5.14  Hivyo husema,
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke katika wafu,
Na Kristo atakuangaza.
5.15  Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
5.16  mkiukomboa wakati (yaani mkiutumia wakati vyema), kwa maana zamani hizi ni za uovu.
Waefe. 5:3-16

2.15  mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
2.16  mkishika [imara] neno la uzima;
Wafi. 2:15-16a SUV

5.21 Kila jambo na mlifanyie tathmini; halafu myashike imara yale mnayoona ni mema kuyafanya.
5.22 Mjitenge na kila kitu chenye taswira ya uovu.
1Wathess. 5:21-22

2.22  Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
2Tim. 2:22 SUV

1.27  Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Yakobo 1:27 SUV

1.1 Kuendelea katika kumwogopa Mungu.

Kinachotusaidia sisi kujiweka mbali na uovu ni woga tulio nao kwa Bwana wetu.

24 Bwana akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche Bwana, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo.
Kumb. 6:24 SUV

12 Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho [*nafsi] yako yote;
Kumb. 10:12 SUV * mwili na roho, pamoja cf. Mwanzo 2:7

10.28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
Matt. 10:28 SUV

1.17  Na ikiwa mnamwita (mnaomba msaada wa) Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu [ya hukumu Yake] katika wakati wenu wa kukaa hapa [duniani] kama wageni.
1Pet. 1:17 SUV

Kumwogopa Mungu ndiyo kiini cha busara ya muumini na kwa njia hiyo tunaendelea katika njia anayotupangia Mungu wetu.

28 Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Ayubu 28:28 SUV

10 Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.
Zab. 111:10 SUV

7 Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Mithali 1:7 SUV

10 Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua [Yule aliye] Mtakatifu ni ufahamu.
Mithali 9:10 SUV

Kumwogopa Mungu ni kuchukia uovu. Katika kumwogopa Mungu tunaacha uovu na tunatimiza mapenzi ya Mungu.

7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu.
Mithali 3:7 SUV

13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;
Mithali 8:13a SUV

6 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.
Mithali 16:6 SUV

7.1  Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimilisha (perfecting) utakatifu (utakaso wetu) katika kumcha Mungu.
2Wakor. 7:1

Tunapomwogopa Mungu, Yeye anatulinda, anatuelekeza na anatubariki.

12 Ni nani amchaye Bwana? [Bwana] atamfundisha katika njia anayo[paswa ku]ichagua.
Zab. 25:12 SUV

18 Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake.
19 Yeye huwaponya nafsi zao na mauti, Na *kuwahuisha wakati wa njaa.
Zab. 33:18-19 SUV *kuwaweka hai

11 Ee Bwana, unifundishe njia Yako, ili niweze kuutegemea uaminifu Wako; nipe moyo wenye nia moja, ili niweze kulicha Jina lako.
Zab. 86:11

1 Heri mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.
Zab. 128:1
19 Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Zab. 145:19 SUV

13 Hii ndiyo hatima ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana ndivyo impasavyo mtu.
Mhubiri 12:13

1.2 Kuwa macho kiroho ili uepuke kuingia katika vishawishi.

Tunahitaji kuwa macho, ili punde tunapoona kwamba nia yenye dhambi inaweza ikaanza kujitokeza, basi inakatwa mzizi wake hapo hapo kabla haijakusanya nguvu na kuendelea kukua. Tusiache hata ufa mdogo utokee katika ngao yetu ya ulinzi dhidi ya dhambi. Tusimwache adui aingie katika lango. Tunajua kwamba ikiwa tutamwacha adui aingie [katika lango], basi vita itakuwa ngumu zaidi, na huenda tukaanguka. Tundu dogo tu likitokea katika ukuta unaozuia maji ya bwawa kupenya, basi mambo yanaweza kuharibika haraka sana.

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Mwanzo 4:7 SUV

23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 Ulisawazishe (lifikirie kwa makini) pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike (zitakuwa thabiti);
27 Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.
Mithali 4:23-27

16.13  Kesheni (chukueni tahadhari), simameni imara katika Imani, fanyeni kiume (kuweni shupavu), mkawe hodari.
1Wakor. 16:13

1.13  Kwa hiyo vifungeni imara viuno vya nia [minds] zenu, na muwe macho kiroho;
1Pet. 1:13

Sote tunayo hulka ya dhambi ndani yetu ambayo wakati wote inatuvuta tuelekee katika dhambi. Sisi wanadamu hupotea kwa urahisi sana katika fikra na nia zetu na tunadanganyika kwa urahisi sana. Mara nyingi ni vigumu kutambua / kumaizi motisha na malengo ya mioyo yetu wenyewe!

9 Moyo huwa mgumu kueleweka kuliko vitu vyote, [na] una ugonjwa usiopona, kwa sababu ya udanganyifu wake; nani [kati ya wanadamu] awezaye kuujua [unachofikiria]? 
10 Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, [na kupima motisha za watu], hata kum[li]pa kila mtu kiasi [kinachotokana na] njia zake, kiasi cha matunda (matokeo) ya matendo yake.
Yer. 17:9-10

Hivyo si vema kujiamini na kujitegemea sisi wenyewe, bali tumwombe Mungu atusaidie katika kutambua nia yoyote na zozote zenye dhambi ndani ya mioyo yetu, ili tuweze kudumu katika njia Yake.

23 Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
Ayubu 13:23 SUV

2 Ee Bwana, unichunguze na unipime; Unipime nia yangu na moyo wangu.
Zab. 26:2

AU

2 Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.
Zab. 26:2 SUV

KIMOMBO:

2Test me, O Lord , and try me, examine my heart and my mind;
Psa. 26:2 NIV

23 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
24 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.
Zab. 139:23-24

Ni lazima tuwe waangalifu na tuwe katika sala wakati wote.

37 Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako.
Zab. 119:37 SUV

26.41 Kesheni, mkiomba, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu. Matt. 26:41 SUV

5.4  Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
5.5  Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
5.6  Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
5.7  Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
5.8  Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani [deraya ya] imani na upendo, na chapeo (helmet) yetu iwe tumaini la wokovu.
1Wathess. 5:4-8
5.17  ombeni bila kukoma;
1Wathess. 5:17 SUV

1.3. Kusimama imara dhidi ya hila za Ibilisi.

Adui yetu Ibilisi “anazunguka-zunguka kama simba anayeunguruma” na wakati wote yeye na majeshi yake wanajaribu kutukwaza ili tuanguke katika dhambi kwa kutuletea vishawishi ambavyo vina mvuto kwa hulka yetu ya dhambi – na hulka yetu hii inamsaidia sana Ibilisi – iliyo ndani ya miili yetu.

5.8  Mwe na kiasi [watulivu - “sober”] na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
5.9  Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale [kama mnayopitia ninyi] yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.
1Pet. 5:8-9

Shetani ana[ji]geza kama malaika wa nuru, uwongo na udanganyifu ndiyo njia na mbinu zake tangu mwanzo (cf. Wathess. 2:9-10; Ufu. 13:13-14; 19:20; 20:3).

4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3:4-5 SUV

8.44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo (kutokana na hulka) yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo [uwongo].
Yoh. 8:44 SUV

11.14  Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
2Wakor. 11:14 SUV

12.9  Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote, akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.
Ufu. 12:9 SRUV

Na hivyo fikra na taswira (vishawishi) zinazopelekea kwenye dhambi zitakuwa na mwonekano wa kuvutia na usio na madhara – au angalau mwonekano wenye madhara kidogo tu. Na kwa hakika vitakuwa na raha tele. Lakini kwa kutunza kweli ya maandiko mioyoni mwetu, tutaweza kuona uwongo na udanganyifu wa vivutio hivyo na tutaweza kuviepuka.

Hususan katika maeneo yetu ambamo tu dhaifu (dhambi ina wigo mpana sana, na kila mwanadamu ana madhaifu yake) tusikubali kushawishiwa na vivutio vile vile (na hivyo kujikwaa / kuanguka) kila wakati. Kama tunajua kwamba kitu fulani kinatupeleka katika dhambi, basi inatulazimu tujiweke mbali na kitu hicho na tukatae udanganyifu wote wenye nia ya kututoa kwenye njia ya Mungu na kutuingiza kwenye dhambi (kwa mfano, “kuna madhara gani yatakayokufika ukitazama tu?!”, au “hakuna ubaya ukijaribu tu!”, n.k.).

Tunashawishika pale tunapoisikiliza sauti ya tamaa zetu, hivyo tuna ulazima wa kukaa mbali na viashiria vinavyopandisha tamaa hizo {Hii ni pamoja na kutosikiliza mafundisho ya uwongo, kwa mfano mafundisho kwamba kuna watu walioingiliwa na kutawaliwa na “pepo wa mahaba”(!?)}. Tunapaswa kuondoa vikwazo vyote na kumnyima Ibilisi fursa yoyote anayoweza kuitumia.

5.29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
5.30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Matt. 5: 29-30 SUV

4.27  wala msimpe Ibilisi nafasi.
Waefe. 4:27

1.13  Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu [hahusiki na majaribu], wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
1.14  Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa (udhaifu wake mwenyewe) yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
1.15  Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba [i.e. ikimshinda nguvu] huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa [akiendelea kutenda dhambi tena na tena] huzaa mauti [i.e. kifo cha kiroho, kifo cha imani].
Yakobo 1:13-15

Kama itatulazimu, basi tuache ushirika na wale wote wanaotushawishi tuachane na Bwana wetu (kwa maneno na/au matendo yao) na ambao wanatufanya tuingie katika matendo ya dhambi.
16.17  Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya ku[wa]kwaza [ninyi] kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
War. 16:17 SUV

15.33  Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
1Wakor. 15:33 SUV

6.14  Msifungiwe [/msifungane] nira (yoke) pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
2Wakor. 6:14 SUV

1.4. Tumo katika himaya ya adui.

Tunapaswa kukumbuka wakati wote kwamba tunapigana vita hii ya kiroho tukingali katika himaya ya adui – yaani ulimwengu huu mharibifu.

Katika kuanguka kwa Adamu, wanadamu wote tumesalimisha ukaimu wetu juu ya dunia hii kwa Shetani, na sasa, kwa njia ya mfumo wa udanganyifu, vivutio na vitu vyote vingine visivyo na thamani wala maana yoyote ambavyo [Shetani] amekusudia na kupanga vimiliki akili, nia, mioyo na wakati wetu, anaushikilia ulimwengu huu imara katika makucha yake. Ibilisi ana ushawishi na mvuto mkubwa katika ulimwengu kiasi kwamba kuendelea katika uaminifu kwa Mkristo imekuwa jambo gumu sana sana.

4.5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
4.6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo [*imeachwa] mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.
Luka 4:5-6 SUV
*imeachwa mikononi mwa Shetani kwa sababu ya kuanguka kwa Adam, aliyekuwa mtawala hapo mwanzo – Mwa. 1:26-28

5.19  Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika [mamlaka ya ] yule mwovu.
1Yoh. 5:19 SUV

Kama askari mpiganaji yeyote aliyeingia katika eneo / himaya ya adui, inatulazimu tuwe macho wakati wote, tukiishika imara kweli ya Neno la Mungu kwa imani. Kwa imani tunaushinda ulimwengu na uovu wote uliomo [ndani yake].

5.5  Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?
1Yoh. 5:4 SUV

5.7  Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.
2Wakor. 5:7 SUV

AU

Maana twaenenda kwa [kile tunachokijua kuwa ni kweli] kwa njia ya imani, na siyo kwa kile kinachoonekana machoni mwetu.
2Wakor. 5:7

2. Kamwe hatutopewa mtihani utakaozidi uwezo wetu wa kuhimili.

Tunapojikuta chini ya kishawishi, tunapaswa kukumbuka kwamba hata kama kishawishi hicho ni kikubwa kiasi gani na hata kama sisi wenyewe ni dhaifu kiasi gani [kwa kishawishi cha aina hiyo], Mungu wetu hatuachi tujaribiwe kupita uwezo wetu wa kuhimili jaribu hilo na siku zote huweka namna ya sisi kuhimili au kutoka katika jaribu hilo.

10.13  Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida [katika maisha] ya wanadamu; ila [zaidi ya hapo] Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo [kustahamili]; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea [namna ya kutatua tatizo], ili mweze kustahimili [shinikizo].
1Wakor. 10:13 SUV

Aya hii hunukuliwa mara nyingi sana, lakini ni mara ngapi tunaliweka / tunalikumbuka fundisho lake mioyoni mwetu wakati tukiwa chini ya kishawishi? Vishawishi fulani vinaweza kuonekana kama vile haiwezekani kwetu kupambana navyo kwa mafanikio, na majaribu mengine yanaweza kuonekana kama vile haiwezekani kuyashinda, lakini tunapaswa kukumbuka kwamba yanawezekana kuyahimili na kuyashinda – bia kujali yanavyoonekana katika macho na hisia zetu.

Mungu wetu ni mwenye uweza kwa kiasi kisichomithilika zaidi ya adui yetu anayetushawishi tuingie katika dhambi.
4.4  Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda (wale wa aya ya 3), kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
1Yoh. 4:4 SUV

Hii ndiyo maana tunaposhawishiwa tunamtegemea Mungu.

3. Katika vita hii tunamtegemea Mungu.

Katika mapambano yetu yote Mungu wetu ndiye kimbilio letu. Kama vile tunavyotegemea rehema / huruma Zake katika [kupata] wokovu wetu, vivyo hivyo tunamtegemea Yeye katika kupambana na vishawishi na dhambi.

11 Nawe, Bwana, usinizuilie rehema zako, Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.
12 Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Na moyo wangu umeniacha.
13 Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa, Ee Bwana, unisaidie hima.
Zab. 40:11-13 SUV

17 Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Zab. 40:17 SUV

20 Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.
Zab. 68:20 SUV

Sisi ni dhaifu, lakini uweza wa Mungu unaufanya udhaifu wetu uweze kushinda magumu yote kwa kiwango timilifu pale tunapomtegemea Yeye.

12.7  Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi kwa [sababu ya] wingi wa mafunuo hayo, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
12.8  Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.
12.9  Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu [wako]. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
12.10  Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
2Wakor. 12:7-10 SUV

Tunahitaji kumtegemea Mungu kwa ajili ya utatuzi wa shida zetu za hapa duniani badala ya kutegemea nguvu zetu au juhudi zetu wenyewe. Tahadhari: hii haimaanishi kwamba tusifanye kazi, tusiende hospitali, tusiombe msaada kwa wenzetu pale tunapopata magumu. Tizama na utafakari kwa makini mfano wa Paulo hapo katika 2Wakorintho 12:7-10, nukuu hapo juu. Ni Yeye pekee anayeweza kutuokoa katika shida.
1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;
4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
Zab. 121 SUV

1 Bwana asipoijenga nyumba, Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, Yeye aulindaye akesha bure.
Zab. 127:1 SUV

4.7  Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Yak. 4:7 SUV

2.9  basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu,
2Pet. 2:9a

Pale tunapoona kwamba mapambano (au vishawishi / mitihani) yanataka kuanza, tunapaswa kujipa nguvu katika Bwana.

1 Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;
2 nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao.
3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka.
4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena.
5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli.
6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.
7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko.
8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.
1Samweli 30:1-8
Kama tukistahamili tukiwa na Yeye kama tegemeo letu, tutakuwa salama.

1 Aketiye katika ulinzi wake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao (ngome).
5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele (tauni) uharibuo adhuhuri,
7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.
Zab. 91:1-7 SUV

3.1 Mungu ndiye mhimili wetu, Yeye ndiye ngao yetu, anayetutayarisha kwa ajili ya vita, Yeye ndiye ngome yetu na kimbilio letu.

3 Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
Zab. 3:3 SUV

7 Ndiwe sitara yangu (unayenisitiri), utanihifadhi na mateso, Utanizungusha (Utanifanya nizungukwe na) nyimbo za wokovu.
Zab. 32:7 SUV

17 Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote.
18 Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.
19 Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.
Zab. 34:17-19 SUV

5 Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu; Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.
6 Maana sitautumainia upinde wangu, Wala upanga wangu hautaniokoa.
7 Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu; Na watuchukiao umewaaibisha.
Zab. 44:5-7 SUV

5 Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.
6 Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka
7 Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.
Zab. 84:5-7 SUV

6 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
Zab. 107:6 SUV

1 Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana.
2 Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu.
Zab. 144:1-2 SUV

14 Bwana huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini.
Zab. 145:14 SUV

3.2. Yeye ndiye anayetupigania.

Kwa hakika, Yeye ndiye anayepigana vita yetu kwa ajili yetu.

13 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
14 Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Kutoka 14:13-14 SUV

3 Bwana ni mtu wa vita (mpiganaji wa vita), Bwana ndilo jina lake.
Kutoka 15:3 SUV

21 Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda Bwana, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda Bwana kila ufalme huko uvukiako.
22 Msiwache (msiwaogope), kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye awapiganiaye.
Kumb. 3:21-22 SUV

1 Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.
2 Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na kusema na watu,
3 awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche (msiogope), wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao;
4 kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
Kumb. 20:1-4 SUV

6 Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.
Kumb. 31:6 SUV

9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.
Yoshua 1:9

3.3. Mungu anajua tunahitaji msaada Wake na Anataka tumwombe msaada huo.

15 Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.
Zab. 50:15 SUV

Mungu wetu katika ufahamu Wake wa kila kitu (omniscience) anajua kwamba tunahitaji msaada Wake, lakini pia Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikuwa mtu katika wakati wake hapa duniani na Anaelewa magumu tunayopitia kwani hata Yeye alipitia magumu hayo hayo, ijapokuwa Yeye hakuanguka katika dhambi. Hivyo kwa kuwa Yeye anaomba kwa Baba wakati wote, tunaweza kujongea mbele ya kiti cha enzi cha neema kwa kujiamini wakati tunapokabiliwa na magumu.

4.15 Kwani Yeye ni Kuhani Mkuu mwenye kuyaelewa na kuwa na rehema kuu juu ya madhaifu yetu, kwa kuwa hata Yeye alipitia mitihani kama ambayo sisi tunapitia, bali bila ya kutenda dhambi.
4.16  Basi na tukikaribie kiti cha neema [cha Baba] kwa ujasiri (lugha huru ya kujiamini), ili tupewe rehema [Yake], na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waebr. 4:15-16 SUV

8.34  Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
War. 8:34 SUV

Anasikia maombi yetu yanayotolewa kwa unyenyekevu.

6 Na ahimidiwe Bwana. Maana ameisikia sauti ya dua yangu;
7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
8 Bwana ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi (mpakwa mafuta) wake.
9 Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele.
Zab. 28:6-9 SUV

3.4. Mungu anatusaidia kwa njia ya Roho Wake Mtakatifu.

Tunajua kwamba Mungu wetu anatusaidia kwa njia ya Roho Wake Mtakatifu ambaye yumo ndani yetu. Kama tukiitegemea nguvu Yake [Roho Mtakatifu], tutaweza kustahamili na kushinda katika majaribu.

5.16  Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Waga. 5:16 SUV

Lakini tunapaswa kumsikiliza Yeye na tusiizime sauti Yake ndogo, ya utulivu ambayo mara nyingi tunaisikia ikituonyesha njia ya kutokea wakati wa vishawishi. Kama maandiko yanavyosema, sauti ya Roho Mtakatifu ni ndogo, ya utulivu, kwa sababu Yeye hashurutishi, hushauri tu ili asiingilie utashi wetu katika masuala ya mwenendo.

5.19  Msimzimishe Roho;
1Wathess. 5:19

11 Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;
12 na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.
13 Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya?
1Wafalme 19:11-13
Mungu ni mwaminifu siku zote, na kamwe hatotutelekeza. Lakini tunapaswa kumwamini na kumtegemea.

4. Ustahamilivu.

4.1. Katika mitihani mingi tutakayopitia yawezekana kushinda kwa ustahamilivu pekee, lakini Mungu yuko nasi wakati wote.

Ijapokuwa Mungu ametuhakikishia kwamba hatutapewa mitihani inayoweza kutuzidi nguvu, yaani magumu yote atakayoruhusu tuyapitie tutakuwa na ubavu nayo, ijapokuwa Mungu wetu, kwa njia ya Roho wake Mtakatifu anatusaidia katika magumu yetu ikiwa tu tutaomba msaada Wake, na ijapokuwa Yeye anaweza kutuokoa kutoka katika kila kishawishi, inatulazimu tustahamili katika nia na uamuzi wetu wa kuwa watiifu Kwake na tunapaswa kuungojea wokovu Wake.

Mitihani mingi haitakwisha mara tu baada ya sisi kuamua kuendelea kuwa waaminifu Kwake na kuomba msaada Wake ili tuweze kujizuia na dhambi na uasi. Sehemu ngumu yaweza kuwa si mtihani wenyewe, bali ni katika kustahamili katika uamuzi wetu wa kuungojea wokovu wa Mungu, ambao unaweza kuchukua muda mrefu (kwa mtazamo wetu - Zab. 90:4; 2Pet. 3:8-9), kabla ya mtihani huo kumalizwa / kusitishwa na Mungu. Baadhi ya mitihani yetu migumu kabisa haitaisha mara moja au haraka – itaisha kwa sisi wenyewe kuendelea kuwa waaminifu siku hadi siku hadi / mpaka hapo mateso hayo, mitihani hiyo, inapofika mwisho wake.

1.12  Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
Yak. 1:12 SUV

21.19 Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.
Luka 21:19 SUV

Lakini kwa hakika Mungu wetu yuko pamoja nasi katika kipindi chote cha mitihani hiyo na hatuachi kamwe maisha yetu yote.

9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu [yake mwenyewe] hakuna [mtu] atakayeshinda;
1Samweli 2:9 SUV

10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Isa. 41:10 SUV

28.20b … na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Matt. 28:20b SUV

3.3  Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.
2Wathess. 3:3 SUV

4.2 Hatimaye Mungu hutuokoa katika magumu yetu.

Bwana wetu yuko nasi katika mitihani yetu na ni Yeye anayetuokoa na magumu hayo. Yaweza kutulazimu tuungojee wokovu Wake kwa lisaa moja, siku moja, au hata mwaka mzima. Lakini hatimaye wokovu utakuja.

Njia itapatikana katikati ya bahari.

13 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
14 Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Kutoka 14:13-14 SUV

21 Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; Bwana akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika.
Kutoka 14:21 SUV

14 Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
Zab. 27:14 SUV

1 Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana.
Zab. 40:1-3 SUV

5 Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia.
6 Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.
Zab. 130:5-6 SUV

Inatulazimu kuyakumbuka maandiko haya ya kweli haswa katika nyakati za udhaifu tukingali katika magumu au wakati tunapokuwa chini ya shinikizo la kishawishi kikubwa. Bwana wetu alikwishatuambia kuwa mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo kwenye uzima wa milele.

7.13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
7.14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Matt. 7:13-14 SUV

Na katika zile nyakati ngumu kabisa, njia hii yaweza kuwa nyembamba sana kiasi cha kufanana na kamba nyembamba kabisa! Sote tunawafahamu wale wanamichezo ya sarakasi wanaotembea kwenye kamba iliyoning’inizwa juu kabisa, kati ya nguzo mbili. Kwa hakika tendo lile si rahisi hata kidogo, ni jambo gumu sana. Kwa kimombo mchezo huu unaitwa “walking a tightrope”. Kwa kutumia mfano wa mchezo huu tunaweza kusema kwamba wakati mwingine njia nyembamba ya majaribu yaweza kuwa kama kutembea juu ya “tightrope” ya kiroho ambapo tunasali na kumwomba Bwana wetu atusaidie tupige hatua moja tu mbele tukiwa katika / juu ya kamba hiyo, tukiogopa lakini pia tukimwamini Yeye, atupe nguvu na kutujaza imani ili tuweze kupiga hatua hiyo bila ya kuanguka (Yuda 24). Yaweza kuwa ni magumu, mitihani ya moto kabisa ambapo hatuwezi kuondokana na maumivu makali (ugonjwa), majaribu / vishawishi, tamaa / uchu juu ya hisia ya kitu fulani, hisia kali zinazotokana na kuchokozwa kila wakati, n.k. Mungu, hata hivyo, yuko nasi katika bonde la kivuli cha kifo.

4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Zab. 23:4 SUV

Tunapaswa kumgeukia Yeye katika sala na ku[m]shika mkono imara kabisa, tukiweka fikra zetu katika hatua tunayopiga wakati huo na kuyasahau mengine yote (Matt. 6:34). Kama tukifanya hivyo, ingawa twaweza kuwa ndani ya tanuu la moto, ingawa morale yetu yaweza kuwa imeshuka kwa sababu ya dhiki ya muda mrefu, tukiwa tumepondwa kwa sababu ya kuanguka mara kadhaa, au tukiwa tukihangaika kwa maumivu – Mungu hatatuacha tuangamie, na uweza Wake utatusaidia tufike salama. Hii ni kweli iwe tumo katikati ya magumu, au chini ya shinikizo la kishawishi, au kama tumo katika adhabu ya Mungu inayotokana na kuanguka katika dhambi, au kuteswa na wasioamini kwa sababu tumeshuhudia Neno la Mungu kwao, n.k.

4.7  Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.
4.8  Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;
4.9  twaudhiwa, bali hatuachwi (hatutelekezwi); twatupwa chini, bali hatuangamizwi;
4.10  siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu.
4.11  Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.
2Wakor. 4:7-11

Ikiwa tutaushika mkono wake Bwana wetu, basi tutaona yakuwa saa hata saa, siku hata siku, ile kamba inaanza kuwa imara na ‘balance’ yetu inaongezeka, hatua zetu zinazidi kuwa za uhakika. Hata uwezekano wa kuanguka unazidi kuwa mdogo. Tutajiona tunaweza kujizuia na vishawishi ambavyo hapo mwanzo vilikuwa vinatufanya tupepesuke kila wakati tunapokutana navyo, wakati mwingine tukijikwaa na wakati mwingine tukianguka, lakini kwa sasa mvuto wake umeanza kuwa hafifu. Na ghafla tutaona kwamba baada ya kutegemea nguvu ya Mungu, hatuko tena juu ya kamba, bali tunatembea tena juu ya barabara. Na pia tunajiona tuko huru. Ikiwa tutaendelea kuwa waaminifu Kwake, tutaushuhudia ushindi wetu (Zaburi ya 107).

4 Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.
5 Wakamwelekea macho wakatiwa nuru (wanaoelekeza macho yao Kwake hutiwa nuru), Wala nyuso zao hazitaona haya.
6 Maskini huyu aliita, Bwana akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.
7 Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Zab. 34:4-7 SUV

13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.
Zab. 56:13 SUV

[Mfalme] Daudi anatusimulia juu ya wokovu wa Mungu katika Zaburi ya 18 (Pia 2Samweli 22).

1 Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana;
2 Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
3 Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.
4 Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.
5 Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili.
6 Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
Zab. 18:1-6 SUV

16 Alipeleka kutoka juu akanishika (Aliagizia kutoka juu Aliko, Akanitwaa), Na kunitoa katika maji mengi.
17 Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
18 Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini Bwana alikuwa tegemeo langu.
19 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
Zab. 18:16-19 SUV

Anajua kwamba “alipewa thawabu kutokana na uongofu wake”.

20 Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.
21 Maana nimezishika njia za Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu.
22 Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu, Wala amri zake sikujiepusha nazo.
23 Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake, Nikajilinda na uovu wangu.
24 Mradi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
Zab. 18:20-24 SUV

Ikiwa tutajiweka mikononi mwa Bwana, atatupatia nyenzo zote tunazohitaji ili tuweze kustahamili hata mitihani migumu kabisa.

30 Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.
31 Maana ni nani aliye Mungu ila Bwana? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu?
32 Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.
33 Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu (deer), Na kunisimamisha mahali pangu pa juu (kileleni).
34 Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.
35 Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.
36 Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.
Zab. 18:30-36 SUV

Tunayo ahadi Yake.

14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
Zab. 91:14-16

5. Motisha ya kustahamili na kutokata tamaa katika vita hii.

5.1. Hakuna kinachofichika kwa Mungu.

Dhambi ni tendo la giza na mara nyingi hutendeka gizani. Tunapaswa kukumbuka kwamba ijapokuwa dhambi yetu inaweza kuwa haionekani na watu wengine, kamwe haijifichi mbele za macho ya Mungu.

13 Toka mbinguni Bwana aitazama dunia, Huwatazama wanadamu wote pia.
14 Toka mahali pake aketipo Huwaangalia wote wakaao duniani.
Zab. 33:13-14 SUV

9 Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione?
Zab. 94:9 SUV

21 Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya Bwana, Na mienendo yake yote [Bwana] huitafakari.
Mithali 5:21 SUV

4.13  Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu (vi uchi) na kufunuliwa machoni pake Yeye tunayepaswa kujihusisha naye.
Waebr. 4:13

5.2. Mawazo, maneno na matendo yetu yote yatahukumiwa.

Mungu anazijua fikra zetu zote, anasikia maneno yetu yote na anaona matendo yetu yote, na yote hayo yataletwa mbele ya kiti cha hukumu. Hii inapaswa kutupatia motisha ya kuwa na rekodi nzuri ili tusitiwe aibu siku ile tutakapokuwa mbele ya kiti cha enzi cha hukumu cha Bwana wetu Yesu Kristo.

7 Bali Bwana atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.
8 Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa adili.
Zab. 9:7-8 SUV

11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
12 Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo, Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;
13 Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.
Zab. 96:11-13 SUV

14 Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.
Mithali 12:14 SUV

17.31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa Mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
Matendo 17:31 SUV

14.10b … Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
14.11  Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.
14.12  Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
War. 14:10b-12 SUV

4.5  Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
1Wakor. 4:5 SUV

5.10  Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya (yasiyo na thamani).
2Wakor. 5:10

5.3. Dhambi inaharibu ushuhuda na utumishi wetu na hatimaye – thawabu zetu za milele.

Yawezekana tu kuzaa matunda ya kazi ya Kikristo ikiwa tutakaa ndani ya Bwana wetu na kumtegemea Yeye.

15.4 Kaeni ndani yangu, nami [nitakaa] ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
15.5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
15.6 Mtu asipokaa ndani yangu, ni kama tawi linalokatwa na kutupwa nje na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
Yoh. 15:4-6

Kila mara tunapoanguka katika dhambi basi tunafanya kile tulichokatazwa kukifanya, lakini pia tunapoteza fursa ya kukifanya kile tunachotakiwa kufanya. Tunatelekeza jukumu ambalo Bwana ametutayarishia tulitimize na ambalo ni wajibu tulilopewa na Bwana mwenyewe.

2.10  Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza [tayari] ili tuyatimize.
Waefe. 2:10

Tuna kiasi kidogo sana cha muda [wa kuishi] hapa duniani. Wakati wowote ambao tunakuwa nje ya ushirika (fellowship) na Bwana wetu unakuwa ni wakati uliopotea.

5.15  Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
5.16  mkiukomboa wakati (yaani mkiutumia wakati vyema), kwa maana zamani hizi ni za uovu.
Waefe. 5:15-16 SUV

4.5  Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje [ya imani yetu], mkiukomboa wakati (mkiitumia vyema kila fursa).
Wakol. 4:5

Waumini fulani wataliacha Neno la Mungu lililo ndani ya mioyo yao lisongwe na magugu na miiba, na hivyo hawatazaa matunda. Wengine wanazaa matunda, lakini kwa viwango tofauti. Dhambi hutufanya tushindwe kuzaa matunda kwa ajili ya Bwana wetu. Dhambi inapingana na mchakato wetu wa kukua kiroho na inapunguza matunda tunayozaa.

13.22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
13.23 Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kulielewa; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.
Matt. 13:22-23 SUV (Pia Marko 4:19-20 na Luka 8:14-15)

Shughuli zetu za hapa duniani, ziwe za kutafuta kipato, za kukuza akili yetu – elimu, au za malengo yoyote mengine, zinatufundisha mambo mawili. Kwanza, kufanikisha lengo lolote lile kunalazimu nidhamu, kujitoa na juhudi – na mara nyingi maumivu tele ya kimwili na kiakili. Kujitenga na dhambi wakati mwingine kuna gharama hiyo hiyo. Yaweza kuwa na maumivu. Pili, katika shughuli fulani, tunapofanya juhudi ambazo kwa wakati ule zinaonekana kama vile ni kubwa sana na tumechoka, lakini baadaye mara nyingi tunahisi kwamba tungeweza kuongeza juhudi hizo, kwamba bado tulikuwa na nguvu za ziada. Vivyo hivyo katika juhudi zetu za kiroho. Na katika juhudi na kazi za kiroho tuna faida kwamba tunaweza kuomba msaada wa Roho Mtakatifu kutuongeza nguvu – na kwa msaada wake tunaona kwamba hakuna kiwango ambacho hatuwezi kufikia katika kumtumikia Bwana wetu.

Mara nyingi tunajitoa kwa moyo wote na kutumia juhudi kubwa katika kufanikisha mambo ambayo tutakapokufa tutayaacha hapa duniani – yote! Tunawaona watu wasioamini wakionyesha uvumilivu mkubwa, wakitumia juhudi kubwa, wakijitoa kwa kiwango cha juu wakipigania malengo ya dunia hii tu. Ni kwa kiasi gani basi tunapaswa kutumia juhudi zote na kujitoa kwa moyo wote tunapopigana vita hii na kukimbia mbio hii ili tuweze kupata thawabu itakayodumu milele?

16.27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Matt. 16:27 SUV

12.11  kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
12.12  kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
War. 12:11-12 SUV

9.24  Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate [tuzo].
9.25  Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote [anayoyatamani]; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo [hatimaye]; bali sisi [twashindana ili] tupokee taji isiyoharibika.
9.26  Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
9.27  bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri[a] wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
1Wakor. 9:24-27 SUV

1.5 Na kwa lengo hilo hilo, pamoja na imani yenu, kwa ari kuu endelezeni wema, na pamoja na wema, ufahamu [wa kanuni za Neno];
1.6 Na pamoja na ufahamu, kiasi [kujitawala nafsi], na pamoja na kiasi, saburi [uvumilivu], na pamoja na saburi, uchamungu;
1.7 Na pamoja na uchamungu, endelezeni upendo kwa ndugu zenu, na pamoja na upendo kwa ndugu, endelezeni upendo.
1.8 Maana mkiwa na maadili hayo, na ikiwa mnayaongeza kila siku, yatawafanya ninyi kuwa mnaofaa na wenye kuzaa matunda, katika kumjua na kumtii kwenu Bwana wetu Yesu Kristo.
2Pet. 1:5-8

22.12  Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Ufu. 22:12 SUV

Thawabu hii ni kubwa sana na inazidi kwa kiwango kisichomithilika starehe yoyote ile ambayo kitendo cha dhambi kinaweza kutupatia. Kwa hakika hatuwezi hata kukadiria kwa sasa ubora, ukubwa, n.k. wa thawabu tutakazopata.

8.18  Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu [katika Ujio wa Pili].
War. 8:18 SUV

2.9  lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
1Wakor. 2:9 SUV

5.4. Tunapaswa kustahamili kwa ajili ya Bwana wetu.

Kutakuwa na nyakati ambazo vishawishi vinaweza kuelekea kutuzidi nguvu au yaweza kuwa dhambi tulizotenda zinatishia kuwa nzito mno kwetu kiasi kwamba tutakuwa tayari kusalimu amri na kuitelekeza imani yetu na kuacha vita hii. Inapofikia hali hii tunapaswa kukumbuka kwamba hii vita tuliyomo siyo yetu, na siyo sisi tuliyoianza.

Tunashiriki katika mgongano ulioanzishwa na uasi wa Shetani, ambapo mafanikio ya Bwana wetu Yesu Kristo msalabani yaliashiria kushindwa kwa Shetani katika vita hii. Bwana wetu Yesu Kristo, kwa mateso na kufa kiroho na kimwili pale msalabani, alilipia dhambi za wanadamu wote katika historia yote, na kutuokoa kutokana na hatia ya milele, ikiwa tutamwamini Yeye na kazi Yake. Tunapokuwa katika magumu ya mitihani mizito tunapaswa kujikumbusha kwamba sisi ni watu wa Bwana Yesu Kristo na maisha yetu yana kusudi la kumtumikia Yeye.

5.14  Maana, upendo wa Kristo watubidisha (unatushurutisha); maana tuna uhakika huu, ya kwamba ikiwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi wote walikufa;
5.15  tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake Yeye aliyekufa [na] akafufuka kwa ajili yao.
2Wakor. 5:14-15

2.20  Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Waga. 2:20 SUV

Sisi ni askari, wapiganaji wa Kristo. Tunapaswa kufanya yote yaliyo ndani ya uwezo wetu kumfurahisha na kumletea heshima Bwana wetu katika utumishi wetu na hatuwezi kuacha kitu chochote kituondoe katika msitari huu. Kusikia “umefanya vyema!” kutoka Kwake katika siku ile Atakapokuwa ameketi katika kiti chake cha enzi itakuwa ni jambo la maana na kubwa zaidi ya “mafanikio” yoyote tunayoweza kuyapata hapa duniani.

2.3  Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
2.4  Hakuna apigaye (mpiganaji wa) vita ajitiaye katika shughuli za dunia, [kwa maana anajiepusha na hayo] ili ampendeze Yeye aliyemwandika awe askari.
2Tim. 2:3-4

Tunaonyesha upendo na uaminifu wetu kwa Bwana wetu kwa kuendelea kuwa watiifu Kwake.

14.21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Yoh. 14:21 SUV

Na kutakuwa na nyakati zingine ambapo ili tuendelee na utiifu huu tunapaswa kujinyima mambo mengi katika dunia hii kwa usalama wetu wa kiroho, kwa kutenga muda kwa ajili ya kazi ya Bwana, n.k.

16.24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, [kwanza] na ajikane mwenyewe (aache matamanio yake binafsi), [pili] ajitwike msalaba wake, [tatu] anifuate.
Matt. 16:24 (Pia Matt. 10:38; Luka 9:23; 14:27)

Yeye mwenyewe alitupatia mfano mkubwa kuliko mifano yote ya kujikana na kustahamili katika mateso. Tunapaswa kuuweka mfano Wake katika mioyo yetu wakati wote. Yeye ndiye tunayemfuata.

12.1  Basi na sisi pia [kama waumini wanaotajwa katika sura ya 11], kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii (watu na malaika), na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi (maeneo ya tabia zetu ambamo tuna udhaifu mkubwa zaidi); na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
12.2  tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
12.3  Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao (waliotenda) dhambi [dhidi ya nafsi yake], msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu [na kukata tamaa].
Waebr. 12:1-3

Yesu Kristo ni Bwana wetu ikiwa sisi ni wafuasi Wake wa kweli.

11.29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
11.30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Matt. 11:29-30 SUV

6.46 Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?
Luka 6:46 SUV

12.26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Yoh. 12:26 SUV

2.3  Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.
2.4  Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.
2.5  Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
2.6  Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.
1Yoh. 2:3-6

5.5. Miili yetu ni viungo vya [Mwili wa] Kristo na ni mahekalu ya Roho Mtakatifu.

Sisi ni mali ya Kristo na miili yetu ni viungo vya Mwili Wake. Miili yetu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu na tunapaswa kumpa utukufu Mungu wetu kwa mema tunayotenda [tukingali] katika miili hii. Ebu tukumbuke hili pale tunaposhawishika kuitumia miili yetu hii katika kutenda dhambi.

6.11  Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
6.12  Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
6.13 Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini
[na] kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki.
War. 6:11-13

12.1  Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, [hii] ndiyo ibada yenu [kama makuhani] yenye [kumfurahisha Mungu, mnayoifanya kiroho].
War. 12:1

Kwa kuwa sasa sisi ni Wakristo na tunaye Roho Mtakatifu ndani yetu, kwa sasa tuifanye miili hii kuwa ni watumwa wetu, na si mabwana wetu.

9.27  bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri[a] wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
1Wakor. 9:27 SUV

5.6. Tunahitaji kuendelea kustahamili kwa ajili ya ndugu zetu na kwa ajili ya wale wanaoutafiti ukweli.

Katika vipindi vya udhaifu, tunapokaribia kukata tamaa, tunapaswa kumkumbuka Bwana wetu na utii / wajibu wetu Kwake, lakini pia tunapaswa kuwakumbuka ndugu zetu na wale wanaoutafuta ukweli na wajibu wetu kwao.

Bwana wetu alitupatia mfano mkuu kuliko yote ya upendo unaojitoa mhanga, unaojitoa sadaka kwa ajili ya wale anaowapenda. Tangu milele iliyopita, Yeye alikuwa Mungu katika ushirika mmoja na Baba [na Roho Mtakatifu] (Yohana 1:1-2), lakini Alijishusha katika kitendo kikuu cha unyenyekevu (Wafi. 2:5-8) na akawa mwanadamu (Yoh. 1:14; 2Wakor. 8:9) ili aweze kulipia dhambi zetu msalabani (War. 3:21-25; 4:25; 5:10; Waefe. 1:7; 1Pet. 3:18).

2.3  Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora (muhimu) kuliko nafsi yake.
2.4  Kila mtu asiangalie mambo [yenye faida] yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo [yenye faida kwa waumini] wengine.
2.5  Iweni na nia [mwelekeo] iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
2.6  ambaye Yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu (Uungu Wake) kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
2.7  bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
2.8  tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Wafi. 2:3-8

20.25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao (maafisa wao) huwatumikisha.
20.26 Lakini hali [haiko] hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;
20.27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;
20.28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumik[i]a, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Matt. 20:25-28

15.13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
Yoh. 15:13 SUV

2.24  Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake [akiwa pale] juu ya mti, ili tuweze kuwa wafu kwa dhambi na tuishi katika uongofu; kwani kwa majeraha Yake sisi tumepona.
1Pet. 2:24

Nasi tunapaswa kuwapenda majirani zetu kama vile Mungu alivyotupenda sisi.

13.34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
13.35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
Yoh. 13:34-35 SUV

15.12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
Yoh. 15:12 SUV

3.14  Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa (asiyekuwa na upendo), akaa katika mauti.
1Yoh. 3:14 SUV

3.16  Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.
1Yoh. 3:16 SUV

4.9  Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
4.10  Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
4.11  Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.
1Yoh. 4:9-11 SUV

4.19  Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.
1Yoh. 4:19 SUV

Hii ni amri kuuya pili.

12.30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa *nafsi yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
12.31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Marko 12:30-31 (Pia Matt. 22:37-40) SUV

*NOTE: Ref. Mwanzo 2:7 SUV

Upendo ni utiifu na utumishi. Tunaonyesha upendo wetu kwa utumishi wetu (kuwatumikia) ndugu zetu katika Kristo.

21.15 Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
21.16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.
21.17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.
Yoh. 21:15-17 SUV

Bwana wetu hakutoa amri kwa Petro ya ‘kuwalisha kondoo wake’ bila sababu. Kama kweli tunampenda Bwana wetu, tutamtumikia na tutawatumikia kaka na dada (ndugu) zetu. Tutaweka mahitaji yao juu ya mahitaji yetu.

12.10  Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
War. 12:10 SUV
5.13  Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili (hulka ya dhambi), bali tumikianeni kwa upendo.
Waga. 5:13 SUV

5.21 hali mkinyenyekeana katika kumcha Kristo.
Waefe. 5:21

5.5  Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu [kama mkanda viunoni], mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
1Pet. 5:5 SUV

Pia kuna wale ambao hawajaweka imani yao katika Kristo na hivyo bado wanaishi ndani ya giza la kutoamini, lakini wanaitafuta kweli. Sisi ndio mwanga wa ulimwengu huu na hivyo tunapaswa kuufanya mwanga huu wetu ung’are kwa nguvu sana ili uweze kuonekana na wale wanaoitafuta kweli ya Mungu, kwa sababu yaweza kuwa ni sisi ambao Mungu anataka kututumia ili kuwaongoza watu hao kwa Kristo na hivyo waokolewe kutoka katika hatia na hukumu ya milele.

17.24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
17.25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
17.26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika [mtu] mmoja (Adam), wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
17.27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.
Matendo 17:24-27 SUV

Na sisi sote tunapaswa kutafakari juu ya ukali wa mateso yaliyomo katika ziwa la moto, mateso ambayo hayatakwisha. Katika dunia hii ni watu wachache wanaochagua mwanga wa kweli na kumwamini Kristo, na sehemu kubwa wanaamua kuishi gizani. Lakini pia kati ya hao wachache wanaomwamini Kristo, ni wachache zaidi wanaojitoa Kwake na kumfuata kikweli kweli, na kuufanya mwanga wao ung’are. Tunapaswa kuwa tayari na kukataa kuiacha taa yetu ififie mwanga wake.

20.15  Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufu. 20:15 SUV

25.46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Matt. 25:46 SUV

1.9  watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
Wathess. 1:9 SUV

1.23  na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto;
Yuda 23a SUV

Yawezekana pia ndugu zetu wakatoka kwenye msitari wa ile kweli na hivyo wakahitaji msaada wetu ili wasiangukie katika mtego wa kutoamini – apostasy.

5.19  Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;
5.20  jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.
Yakobo 5:19-20 SUV

Tunapoamua kutenda dhambi, tunajiweka sisi wenyewe na kuiridhisha tamaa au kuuridhisha uchu wetu juu ya mahitaji ya wenzetu. Tunawatelekeza ndugu zetu katika Kristo na wale wote wanaoitafuta kweli. Kila mmoja wetu ana jukumu la pekee la kutimiza katika njia ya kiroho wanayopita wengine – karama yetu inaweza kuwa ni kuwaongoza wengine ili waione kweli, au kuwasaidia wakue katika kweli, au kuwatia moyo na kuwatia nguvu. Ikiwa tunaitelekeza huduma yetu, waumini wengine katika Mwili wa Kristo wanaweza kupungukiwa na nyanja fulani muhimu katika maendeleo yao ya kiroho au wanaweza kulazimika kutumia juhudi kubwa zaidi kufidia sehemu yenye mapungufu ambayo ingeweza kuhudumiwa kwa urahisi zaidi na sisi.

4.10  kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.
1Pet. 4:10 SUV

AU

Kila mmoja wenu na aitumie karama aliyopewa katika kuwahudumia wengine, kwa uaminifu akiitumia neema ya Mungu [inayotolewa Naye] katika namna [zake – (neema hiyo)] mbalimbali.
1Pet. 4:10 (Tafsiri yangu)

3.9  Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
1Wakor. 3:9 SUV

12.26  Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
12.27  Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake [vya Mwili huo].
1Wakor. 12:26-27 SUV

4.15  Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.
4.16  Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili [Kanisa] upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Waefe. 4:15-16 SUV

AU

15. bali tuweze, kwa kuipokea kweli katika upendo, kukua katika nyanja zote, tukimtazama Kristo, aliye kichwa cha Kanisa, kama mfano wetu.
16. Kwa namna hii, mwili wote (Kanisa zima), ukiungamanishwa na kushikamanishwa kwa uweza wake Kristo kwa njia ya viungo Anavyovitoa [kwa nguvu kuu] ili viunganishe kila sehemu, unafanikisha kukua kwake na kujijenga wenyewe katika upendo.
Waefe. 4:15-16 (tafsiri yangu)

20.25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala [watu] kwa nguvu, na [maafisa wao] huwatumikisha.
20.26 Lakini [hali haiko] hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;
20.27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;
20.28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumik[i]a, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Matt. 20:25-28

5.7 Tunatoa ushuhuda katika kila tunachokifanya.

Mawazo yetu, maneno yetu na matendo yetu ni ushuhuda (mwema au mbaya) mbele za wale wanaotutazama [kwa makini sana]. Tunapaswa kustahamili kwa faida ya wale wanaoweza kutiwa moyo na jambo hili.

12.1  Basi na sisi pia [kama waumini wanaotajwa katika sura ya 11], kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii [watu na malaika], na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi (maeneo ya tabia zetu ambamo tuna udhaifu mkubwa zaidi); na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
12.2  tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahamili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
Waebr. 12:1-2

Na wakati wote kuna wale wanaotutazama kwa makini sana. Malaika, wema na wabaya, wanatutazama wakati wote, hata kama wakati fulani hakuna mwanadamu anayetuona.

15.10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Luka 15:10 SUV

4.9  Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume [tuonekane kuwa watu wa chini kabisa], kama watu waliohukumiwa wauawe; kwani tumekuwa tamasha kwa dunia [nzima]; kwa malaika na wanadamu.
1Wakor. 4:9

6. Maisha yetu yote tutakuwa vitani, lakini tunaweza kuwa na furaha katika vita hii.

6.1. Kuwa na furaha katikati ya mitihani.

Maisha haya kwa Mkristo, katika miili hii na ndani ya ulimwengu huu siku zote yatakuwa ni uwanja wa vita wa kudumu [mpaka tutakapoondoka hapa duniani]. Ndani ya miili yetu tunayo hulka ya dhambi inayotushawishi wakati wote [ili] tuanguke katika dhambi. Nje ya miili yetu, adui wetu Ibilisi wakati wote anajaribu kututoa katika njia nyembamba tuliyomo inayoelekea kwenye uzima wa milele na anatumia vile vishawishi ambavyo [kutokana na kututizama wakati wote] anajua tuna udhaifu navyo. Na hayo yote yanatukia [wakati] tukingali ndani ya himaya yake. Tunalazimika kuyakubali mazingira haya ya hapa duniani kwani hatuwezi kuyabadilisha – lakini ijapokuwa yaweza kuwa ni vigumu kuhisi furaha wakati wa magumu, hili ni jambo linalowezekana; kwa hakika Neno la Mungu lina mifano mingi ya jambo hili.

1.2  Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
1.3  mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
1.4  [Basi acheni] Saburi na ifanye kazi [yake kwa] ukamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila [ya ninyi] kuonekana wenye mapungufu.
Yak. 1:2-4

Yaweza kuwa mara nyingi tunatamani kwamba mambo yangekuwa rahisi zaidi. Kwamba mapambano yetu na dhambi yasingekuwa magumu na ya muda mrefu namna hii – kwa hakika vita yetu dhidi ya dhambi ni ya mpaka pumzi ya mwisho! Kwamba vishawishi vyetu visingekuwa vya kuvutia kiasi hiki! Lakini tukiunyamazisha moyo kwa muda – ambao hulalamika daima – na tukayatafakari majaliwa yetu kama askari wa Kristo katika ulimwengu huu ulioharibika, tukishambuliwa kutoka ndani ya miili yetu (na hulka yetu ya dhambi) na kutoka nje ya miili yetu na Shetani na majeshi kutoka kila upande, kama tukiyatafakari haya majaribu ya moto tunayopitia, tukiitafakari hii njia nyembamba ambayo wakati mwingine inafanana na kamba ya mcheza michezo ya sarakasi ambapo tunahisi tu wadhaifu sana wakati mwingine – tutaanza kuona kwamba katika mwendo wetu huu kuna furaha iliyojificha ambayo ni muumini katika Kristo pekee anaweza kuielewa.

Kuridhisha tamaa, uchu, shauku zetu za dhambi kunaweza kutuletea starehe ya haraka na kubwa katika hisia zetu, lakini starehe hii hugeuka na kuwa utupu mwisho wake.

1.14  Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa (udhaifu wake) yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
1.15  Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba [i.e. ikimshinda nguvu] huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa (akiendelea kutenda dhambi tena na tena) huzaa mauti [i.e. kifo cha kiroho, kifo cha imani yake].
Yak. 1:14-15

6.21  Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa (yaani matendo ambayo sasa mnaona aibu kuwa mliyatenda)? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.
War. 6:21

Lakini – kustahamili chini ya majaribu kwa uaminifu, kupinga kishawishi na kuishinda dhambi kunatuletea furaha tulivu ya kudumu ya ndani ambayo tunaipata kwa kutembea katika njia aliyotupangia Mungu. Ni furaha ya kuwa mtumishi mwaminifu anayeitikia na kutimiza wito wa Mungu wa kuwa watakatifu waliochaguliwa Naye, mwanga katikati ya ulimwengu huu wa giza.

Kuna furaha katika kuiona nguvu ya Mungu ikifanya kazi na kutusimamia katika vita hii tulimo – na nguvu hii tunaishuhudia pale tunapotambua jinsi tulivyo dhaifu. Wakati mambo yanapoenda sawa, sote tuna tabia ya kuisahau neema kuu yaMungu. Nyakati za mitihani huwa ndipo tunaikumbuka neema hii.

12.9  Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu [wako]. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
12.10  Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
2Wakor. 12:9-10

Kwa hakika tunayahitaji haya magumu ili, katika kupambana nayo kwa kutumia nyenzo tulizopewa na Mungu, tuweze kukua kiroho. Msuli unahitaji kufanyiwa mazoezi ili uongezeke nguvu. Imani ni kama msuli. Mitihani yetu ni mazoezi ya misuli yetu ya imani na bila ya mitihani hii haiwezekani kukua katika imani. Tunapaswa kuikumbatia kila fursa ya kuendelea kiroho.

5.3  Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;
5.4  na kazi ya saburi ni [kuleta] uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni [kuleta] tumaini [la thawabu ya milele];
5.5  na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
War. 5:3-5 SUV

4.4  Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
Wafi. 4:4 SUV

6.2. Kuwa na furaha katika ushindi.

Kustahamili katika majaribu na mitihani ni chanzo cha furaha ya kweli ambacho hakiwezi kufanikishwa na kitu chochote kingine. Baada ya kuonyesha uaminifu wetu kwa Bwana na baada ya kumwona Yeye akitupigania na kutuokoa, basi tutakapokuwa upande wa pili wa bahari [ya Shamu] tutaweza kuimba wimbo wa ushindi wa Musa.

1 Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
3 Bwana ni mpiganaji wa vita, Bwana ndilo jina lake.
4 Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida wake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
5 Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe.
6 Bwana, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, Bwana, mkono wako wa kuume wawaseta-seta (shatters) adui.
7 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.
8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
9 Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
10 Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu.
11 Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
12 Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza.
13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.
14 Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika.
15 Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.
16 Hofu na woga umewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee Bwana, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.
17 Utawaingiza, na kuwapanda katika mlima wa urithi wako, Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae, Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana, kwa mikono yako.
18 Bwana atatawala milele na milele.
Kutoka 15:1-18 SUV

Kustahamili na kushinda mitihani kunathibitisha uhalisia wa imani yetu na ithibati hii ni yenye thamani zaidi ya dhahabu.

1.6 Katika kutazamia kwa hamu wokovu wa siku ile ya mwisho, furaha yenu inazidi sana, japokuwa kwa sasa yaweza kuwa mnateseka kwa muda mkipitia mitihani ambayo malengo yake ni kwamba imani yenu idhihirike kuwa ni halisi.
1.7 Uthibitisho huu wa imani yenu una thamani kuu zaidi ya dhahabu, kwani dhahabu, japo nayo hupimwa ubora wake kwa moto, mwisho wake huharibika. Bali imani yetu, inapohakikishwa kuwa ni halisi katika majaribio makali ya maisha, itawasababishia sifa, utukufu na heshima kwenu pale Bwana Yesu Kristo atakaporudi katika utukufu wake.
1Pet. 1:6-7

Mwisho, magumu, majaribu, mitihani na mateso hayawezi kulinganishwa na utukufu unaotungojea. Kutakuwa na furaha tupu [bila simanzi] pale tutakapokuwa na Bwana wetu milele.

8.18  Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama/[yakilinganishwa na] utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.
War. 8:18 SUV

Baada ya kuiweka imani yetu katika Yesu Kristo, maisha yetu yanakuwa mfululizo wa mitihani; tunatarajiwa kufaulu mitihani hii kwa imani. {NOTE: Tizama mfano wa jibu la Ayubu kwa mtihani wake wa kwanza: Ayubu 1:13-22. Hata hivyo, mitihani ya waumini haifanani}. Badala ya kuepa mitihani hii, tunahitaji kuipokea na kustahamili shinikizo la mitihani hii kwa furaha. Kuna furaha ya ndani ya moyo, ambayo ni ya kudumu, katika kupigana vita hii ngumu, katika kuwa mwaminifu kwa Bwana wetu tukingali katikati ya ulimwengu huu wa uharibifu, katika kuona uweza Wake ukifanya kazi ndani yetu, katika kufahamu kwamba tunayo fursa ya kukua kiroho. Kuna furaha halisi katika kila jaribu tunaloshinda.

Na kuna furaha ya ndani ya moyo katika kufahamu kwamba licha ya magumu, mitihani na mateso tunayolazimika kupitia hapa duniani, licha ya sisi wenyewe kuwa dhaifu, tukianguka mara nyingi na tukipitia maumivu ya kushindwa, kuanguka [na kusimama tena!] - bado tupo katika upande ambao majaliwa yake ni ushindi kwani Bwana wetu anayetuimarisha ni mkubwa kuliko adui yeyote tunayekabiliana naye. Mwisho wa yote, na mwanzo wa milele ijayo, furaha hii itatimia na kuwa timilifu (perfect) katika namna ambayo kwa sasa hatuwezi kuwa na taswira yake.

III. Kusimama baada ya kuanguka katika dhambi.

Sisi sote hutenda dhambi. Dhambi hututenganisha na Bwana wetu, na hivyo inatulazimu kutubu dhambi hii ili tuweze kurudi katika ushirika Naye.

1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha (yamewafarakanisha) ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Isa. 59:1-2 SUV

3 Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa Kwa kuugua kwangu mchana kutwa.
4 Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
Zab. 32:3-5 SUV

13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Mithali 28:13

1.8  Tukisema kwamba hatuna [hulka ya] dhambi (inayomfanya kila mmoja wetu atende dhambi), twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
1.9  Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi [hizo] zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
1.10  Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala Neno Lake halimo mwetu.
1Yoh. 1:8-10

Ijapokuwa dhambi zetu zote zilisamehewa [mara] tulipoweka imani yetu katika Kristo na kukikubali na kukipokea kifo chake kama dhabihu kwa niaba yetu, tunahitaji kukiri na kutubu mbele ya Mungu dhambi yoyote tunayotenda ili tuweze kuendelea na ushirika Naye. Wakati tulipoamini, tulioshwa mwili mzima na kusafishwa dhambi zetu zote (Yoh. 13:10a). Kwa sasa tunahitaji tu kuosha miguu yetu mara kwa mara [punde tunapokanyaga ‘uchafu’ - dhambi] kutokana na kutembea katika ulimwengu huu ulioharibika. Bila ya kujisafisha hivi mara kwa mara hatuwezi kuwa na ushirika na Bwana wetu (Yoh. 13:8).

13.5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
13.6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe waniosha miguu mimi?
13.7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
13.8 Petro akamwambia, Wewe hutaniosha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokuosha, huna shirika nami.
13.9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.
13.10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kuosha miguu tu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.
Yoh. 13:5-10 SUV

Kurekebisha uhusiano kati ya watu wawili ambao umeharibika kunalazimu mabadiliko ya mtazamo wetu na kisha kuombana msahama, na hayo hupaswa kufanywa haraka iwezekanavyo – ikiwa kosa tulilotenda dhidi ya mtu ni kubwa, inakuwa vigumu zaidi kumtazama usoni. Vivyo hivyo katika uhusiano wetu na Mungu. Tunahitaji kukiri na kutubu dhambi zetu Kwake haraka inavyowezekana.
Makosa na dhambi zote zinazoturudisha nyuma zinatufundisha kwamba tunapozidi kusogea mbali na njia iliyo sahihi, ndivyo inavyozidi kuwa vigumu zaidi kurejea. Uharibifu unapokuwa mkubwa, basi na marekebisho yanakuwa makubwa na yanagharimu zaidi pia. Siku zote tunapaswa kutubu na kunyanyuka haraka iwezekanavyo, ili tusitoe upenyo kwa dhambi kutusogeza mbali na Bwana wetu na pia ili uharibifu wa kiroho usiwe mkubwa kupita kiasi.

1. Toba.

Ili tuweze kurejeshwa katika ushirika na Mungu wetu, kuendelea kutembea na Kristo na kuendelea na utumishi wetu Kwake, tunapaswa kufanya toba.

16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
17 jifunzeni kutenda mema;
Isa. 1:16-17a SUV

6 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Isa. 55:6-7 SUV

3 Basi, uwaambie, Bwana wa majeshi asema hivi, Nirudieni mimi, asema Bwana wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi.
Zakaria 1:3 SUV

4.8  Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
4.9  Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.
4.10  Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Yak. 4:8-10 SUV

Kusudi la toba ni kujifunza kutokana na kushindwa na kuanguka kwetu, na kuanza kujitayarisha upya kwa ajili ya mapambano, hivyo vipengele vyote vinavyohusiana na kujitayarisha na vita ambavyo tumejifunza katika sura ya kwanza vinahusika hapa pia.

1.1. Adibisho kutoka kwa Mungu.

Dhambi siku zote ina matokeo. Matokeo haya yapo katika makundi mawili. Kundi la kwanza linajumuisha matokeo ya dhambi yanayohusiana na maisha yetu ya hapa duniani na maisha ya wale wanaotuhusu (yaani matokeo ya dhambi katika akili zetu, miili yetu, mahusiano yetu na wengine, kazi / shughuli tunazozifanya, n.k.) na la pili ni lile la mahusiano yetu na Mungu wetu. Mara tunapotenda dhambi tunapaswa kuchukua hatua za kukiri na kutubu haraka iwezekanavyo ili kupunguza ukali wa matokeo yake ya hapa duniani (hata watu wasioamini wana shauku ya kufanya hili – Waebr. 12:16-17 na Matt. 27:3-4), lakini juu ya yote, kupunguza matokeo ya adibisho kutoka kwa Mungu. Mungu wetu anatupatia motisha ya kufanya hivyo (kukiri na kutubu) kutokana na adibisho analotupatia kwa sababu ya dhambi tunazotenda, cf. 1Yoh. 5:16; 1Wakor. 5:1-5.

Mungu ni mtakatifu kwa kiwango timilifu (Walawi 11:45; Zab. 99:9; Isa. 6:1-3; Isa. 44:15; Matt. 4:48; Ufu. 4:8) na hawezi kutetea chochote kilicho kiovu. Dhambi zetu zote tunazitenda dhidi Yake (Zab. 41:4; 51:4) na dhambi zote ni machukizo Kwake. Dhambi inavuruga ushirika wetu na Yeye na inatuletea hatua za adibisho kutoka Kwake. Kutokana / kulingana na uzito wa dhambi tuliyotenda / tulizotenda na muda ambamo tulichelewa katika kumgeukia na kumwomba msamaha, bali tuliendelea kutenda dhambi hiyo / hizo – mara nyingi kwa kiburi na kudharau hatua za mwanzo za adibisho kutoka Kwake – adhabu / adibisho kutoka Kwake linaweza kuwa kali sana.

Hata hivyo, tunapaswa kukumbuka wakati wote kwamba adibisho / adhabu ya Mungu inatoka katika upendo alio nao kwetu. Adibisho Lake halina kusudi la kutufanya tulipie dhambi zetu (jambo ambalo hatuwezi kulifanya kwa ufanisi na pia Kristo alikwishalipia dhambi zetu zote msalabani), wala halipizi kisasi, wala kutuangamiza. Mungu ni Baba yetu anayetupenda ambaye anatumia adibisho / adhabu kwa kusudi / lengo la kutufanya tuache dhambi na kumrudia Yeye.

11 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.
12 Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba [amrudivyo] mwanawe ampendezaye.
Mithali 3:11-12 SUV

12.4  Hamjafanya vita hata kumwagika damu [yenu], mkishindana na dhambi;
12.5  tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
12.6  Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye [na kumpokea kama mwana].
12.7  [Basi chukueni adhabu yenu kwa mtazamo huu] -- Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
12.8  Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.
12.9  Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na/[ili] kuishi?
12.10  Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
12.11  Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani [yanayomfanya muumini aelekee kwenye ukamilifu].
Waebr. 12:4-11

3.19  Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Ufu. 3:19 SUV

1.2. Huruma ya Mungu ni kubwa kuliko dhambi zetu zote.

Ikiwa tunapewa adibisho – adhabu - kali kutoka kwa Baba yetu wa mbinguni ambaye kutokana na hulka Yake hawezi kupuuza makosa yetu; ikiwa tunazidiwa nguvu na matokeo ya dhambi zetu; au ikiwa majuto yanayopita kiasi, hisia za hatia (guilt) au masikitiko yatatuzuia tusiweze kurudi Kwake, basi tunahitaji kuikumbuka huruma Yake Bwana wetu. Huruma Yake ni kuu kuliko dhambi zetu zote na matokeo ya dhambi hizo.

Tunapomtelekeza, Yeye hutungojea turudi Kwake ili atuonyeshe upendo wake wenye upole mwingi ambao yuko tayari kuuelekeza kwetu.

4 Mwimbieni Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
5 Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai
(AU bali fadhili zake hudumu maisha yako yote). Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa [kuna] furaha.
Zab. 30:4-5

12 Enenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema Bwana; sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema, asema Bwana, sitashika hasira hata milele.
Yer. 3:12 SUV

21 Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini.
22 Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
23 Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.
24 Bwana ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.
25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu.
27 Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake.
28 Na akae peke yake na kunyamaza kimya; Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake.
29 Na atie kinywa chake (uso wake) mavumbini; Ikiwa (kwani) yamkini liko tumaini.
30 Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake; Ashibishwe mashutumu [ya ulimwengu].
31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele.
32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33 Maana moyo[ni m]wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.
Maombolezo 3:21-33 SUV

1 Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu.
Hosea 6:1 SUV

Kama ambavyo Mungu wetu alitungojea ili tuikubali zawadi Yake ya kuokolewa katika Mwana wake Yesu Kristo, na kama ambavyo anatupatia yote ambayo tunahitaji ili tuweze kushinda katika vita yetu dhidi ya dhambi mara tunapoamua kufanya hivyo, vivyo hivyo anataka turudi Kwake mara baada ya kutenda dhambi, ili tuweze kurejeshwa katika ushirika Naye na tuendelee kumtumikia.

19 Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu (kunitumikia); ukitamka maneno ya maana, ukaacha yale yasiyo ya maana, utakuwa msemaji Wangu; acha watu hao wakufuate wewe [wakitaka], bali wewe usiwafuate hao.
Yer. 15:19

3 Basi, uwaambie, Bwana wa majeshi asema hivi, Nirudieni mimi, asema Bwana wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi.
Zekaria 1:3 SUV

Na tunaporejea Kwake, anatuokoa na matokeo ya ukaidi wetu.

10 Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti, Wamefungwa katika taabu na minyororo,
11 Kwa sababu waliyaasi maneno ya Mungu, Wakalidharau shauri lake Aliye juu.
12 Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa wala hakuna msaidizi.
13 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
14 Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti, Akayavunja mafungo yao.
15 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
16 Maana ameivunja milango ya shaba, Ameyakata mapingo (bars) ya chuma.
Zab. 107:10-16 SUV

1 Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,
2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.
3 Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani (weeds) ulikizinga kichwa changu;
6 Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo (bars) yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,
7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.
8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe;
9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.
10 Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.
Yona 2:1-10 SUV

Kwa kweli, adibisho – adhabu kutoka kwa Mungu - pamoja na kumbukumbu ya huruma Yake kuu vinapaswa kutupatia motisha ya kutubu na kurejea kwa Mungu wetu haraka iwezekanavyo mara baada ya kutenda dhambi.

1.3. Maana ya toba.

Tunapotenda dhambi, tunapaswa kwanza kukiri ukweli huo katika mioyo yetu sisi wenyewe na kuiona dhambi hiyo kutoka katika mtazamo wa Mungu (kwamba ni suala au tendo la uvunjaji wa amri Yake) badala ya kujaribu kuihalalisha kwa kiasi au namna yoyote ile au kuchukulia kwamba haina umuhimu. Halafu tunapaswa kukiri na kutubu dhambi hii mbele ya Mungu. Mwisho tunapaswa kuonyesha nia ya kuacha dhambi kabisa na kumgeukia Mungu.

Toba haina maana ya kuitazama dhambi tuliyotenda kwa majuto na masikitiko; inamaanisha kuwa na nia ya kuwa mwaminifu kwa Mungu kuanzia sasa na kuendelea. Ni mabadiliko ya mtazamo na mwenendo wetu kuanzia sasa na kuendelea, kama inavyoonyeshwa na etimolojia, yaani elimu ya asili na historia, ya maneno yanayotumika kumaanisha “toba” au “kitubio” katika maagano yote mawili, la Kale na Jipya. Katika Kiebrania – lugha iliyotumika kuandika Agano la Kale – neno shubh (שוב) {Kiebrania husomwa kutoka kulia kwenda kushoto} linamaanisha “kugeuka, kurejea”, na katika Kiyunani neno metanoeoo (μετανοέω) linamaanisha “kubadilisha nia”. Maneno yote haya mawili hayana dhana ya kuwazia kujuta na kuweka fikra zetu katika dhambi tulizotenda zamani, bali yanamaanisha kubadilisha mwelekeo kunafanyika.

Tunapotubu, tunapaswa kukumbuka utakatifu na upendo wa Mungu. Kwa upande mmoja, dhambi yetu ni machukizo Kwake. Kwa upande mwingine, Yeye anatupenda [sana] na anataka turejee Kwake ili atuonyeshe huruma Yake. Ikiwa tutakumbuka utakatifu na uongofu Wake ulio mtimilifu lakini tukasahau upendo Wake, tunaweza kutishika na kuanguka kwetu na hivyo tukaogopa kujongea mbele ya kiti Chake cha enzi ili kukiri na kisha kuendelea na mwendo wetu wa Kikristo. Ikiwa tutakumbuka upendo na huruma Yake lakini tukasahau utakatifu Wake, tunaweza kupuuza uzito wa dhambi [tuliyotenda] mbele ya macho Yake kama / kuwa ni jambo la kawaida, na hivyo tukaanza kurudia-rudia dhambi yetu. Tunapaswa kuyaweka mambo yote haya mawili akilini mwetu wakati wote, tukiikagua mioyo yetu kwa unyenyekevu.

1.4. Toba ni lazima iwe halisi na ya kweli.

Toba inaanza na uamuzi unaotoka katika utashi wetu huru, [uamuzi] wa kurudi kwa Mungu na kuwa watiifu Kwake kwa kuyaweka mapenzi Yake juu [na dhidi] ya kila shauku ya dhambi tuliyo nayo. Si jambo jema kukiri dhambi kwa Mungu ikiwa hatuna nia halisi ya kujitenga na dhambi zetu zote (cf. Kumb. 29:18-21; Isa. 55:6-7; Yer. 2:35; Yer. 3:10). Tunahitaji kurudi kwa Bwana wetu kwa moyo mmoja, moyo wote. Hapo ndipo atatupokea Kwake.

18 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.
Zab. 66:18 SUV

12 Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;
13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema [au upendo], naye hughairi mabaya.
Yoeli 2:12-13 SUV

1.5  Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala hamna giza lo lote ndani yake.
1.6  Tukisema ya kwamba twashirikiana Naye, [halafu] tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;
1.7  bali tukienenda nuruni, kama Yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi (pamoja na Baba na Mwana, aya ya 3), na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha [na] dhambi yote.
1.8  Tukisema kwamba hatuna [hulka ya] dhambi (inayomfanya kila mmoja wetu atende dhambi), twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
1Yoh. 1:5-8

Ukweli kwamba huwa tunajutia dhambi zetu hauvifanyi vishawishi ambavyo tuna udhaifu navyo vipungue mvuto wake. Kwa hakika, wakati wa vishawishi vya namna hiyo ndio wakati wa kuwa na nia imara na thabiti dhidi ya dhambi na dhidi ya vishawishi vinavyopelekea kwenye dhambi. Kwa hakika huwa tunavijua vishawishi ambavyo tuna udhaifu navyo na ambavyo ni vigumu kwetu kushinda, na kwa hivyo basi tuelekeze macho yetu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tuweke mikono yetu katika plau (jembe la kulimia) na tusitazame nyuma.

12.1  Basi na sisi pia [kama waumini wanaotajwa katika sura ya 11], kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii (watu na malaika), na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi (maeneo ya tabia zetu ambamo tuna udhaifu mkubwa zaidi); na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
12.2  tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
Waebr. 12:1-2

9.62 Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.
Luka 9:62 SUV

1.5. Toba halisi huleta mabadiliko chanya.

Toba ya kweli huonekana katika matunda yake.

3.8 Basi zaeni matunda yapasayo toba;
Matt. 3:8 (Pia Luka 3:8a)

Tunapoamua kuacha dhambi na kurudi kwa Mungu, tunapaswa kufanya mabadiliko yanayohitajika kwa kuondoa au kujiondoa kutoka katika vishawishi vyote vinavyopelekea kurudi katika dhambi. Tunavijua vishawishi vinavyosababisha tujikwae na tunapaswa kutembea katika njia iliyonyooka.

12.12  Kwa hiyo (tukirudi kwenye analojia yetu ya mashindano ya mbio ya aya ya kwanza) inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
12.13  mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete [kiungo kilichoumia] kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.
Waebr. 12:12-13

1.6. Unapoanguka, simama na uendelee, haraka!

Dhambi inavunja ushirika (fellowship) tulio nao na Mungu wetu na inatufanya tusimame (tushindwe kuendelea) katika ufuasi wetu na Bwana wetu Yesu Kristo. Inaharibu ushuhuda na utumishi wetu, inapunguza thawabu yetu ya milele na inavuruga ushirika (fellowship) yetu na ndugu zetu wa kiroho. Lakini pia tukipoteza muda katika kufikiria, kujilaumu, kujutia dhambi tuliyotenda, matokeo yake yatakuwa ni hayo hayo.

Dhambi inaweza kusababisha simanzi / uchungu halisi wa moyoni na Shetani anajua namna ya kutufanya tujione tuna hatia kwelikweli kwa kucheza na hisia zetu. Yote yanayoweka upinzani katika juhudi zetu za kurudi kwa Mungu wetu – hisia zilizokithiri za hatia (excessive feelings of guilt), uchungu wa moyoni, kukataa kukubali kwamba umetenda dhambi, kuwalaumu wengine, n.k. - hayatoki kwa Mungu, na yanaleta maumivu kwetu tu. Tunahitaji kuondoa vikwazo vyote.

Inapotokea kwamaba tunahangaika na kusumbuliwa na hisia zetu baada ya tendo la dhambi [nzito], ebu tukumbuke kwamba muda wetu hapa duniani ni mfupi sana.

5 Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri (ni urefu wa kiganja tu); [urefu wa] Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili [upepo tu].
Zab. 39:5

4 Binadamu amefanana na ubatili, Siku zake ni kama kivuli kipitacho.
Zab. 144:4 SUV

Inatulazimu tuutumie muda huu vizuri.

5.15  Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
5.16  mkiukomboa wakati (yaani mkiutumia wakati vyema), kwa maana zamani hizi ni za uovu.
5.17  Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Waefe. 5:15-17
Kila saa inayopita ni fursa ya kukua kiroho, ni fursa ya kuzaa matunda kwa ajili ya Bwana wetu, ni fursa ya kuwatumikia ndugu zetu katika Kristo, na kwa njia hii tunaongeza thawabu yetu ya milele.

Pia, matunda haya tunayozaa katika uweza wa Roho Mtakatifu na juu ya msingi wa Bwana Yesu Kristo ndiyo yanayodumu, kazi nyingine zote zitachomwa moto – 1Wakor. 3:10-15. Tukiwa kama wale waliojitwalia uongofu wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa kuyakubali na kuyapokea malipo Aliyoyafanya kwa ajili ya dhambi zetu kwa njia ya imani yetu Kwake, sisi waumini hatutopitia mchakato wa hukumu kwa ajili ya dhambi zetu – na kwa sababu hii tukitenda dhambi na baadaye tukakiri na kutubu, basi tusikae na kuiwazia dhambi hiyo; ilimwengu huu wa sasa na dhiki na masikitiko yake yote vitateketea kwa moto.

3.10  Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa; dunia na vyote vilivyofanyika juu ya dunia vitawekwa wazi [ili Bwana aweze kuvikagua].
3.11  Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
3.12  mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
3.13  Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambamo haki yakaa ndani yake.
2Pet. 3:10-13

21.1  Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufu. 21:1 SUV

21.3  Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
21.4  Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Ufu. 21:3-4 SUV

Hata kama matokeo ya dhambi zetu ya hapa duniani yatakuwa machungu na yenye maumivu mioyoni mwetu na magumu kuyapokea, ebu tuelekeze macho yetu katika mambo ya milele na tukumbuke nyumbani kwetu halisi ni wapi.

6.20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
6.21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Matt. 6:20-21 SUV

3.20  Kwa maana sisi, [u]wenyeji (uraia) wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
Wafi. 3:20 SUV

Mwisho, hata tukingali hapa duniani, Mungu anafanya kuanguka kwetu kuwe na matokeo mema kwa namna ambayo hatukutegemea – ikiwa tutaendelea kuwa waaminifu Kwake.

8.28  Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu huwafanyia kazi wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
War. 8:28

20 Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.
Mwa. 50:20 (Soma katika muktadha wake)

1.7. Kujipambanua nafsi zetu.

Mwisho, kabla ya kukiri dhambi zetu, tunahitaji kuzichunguza nafsi zetu kwa undani kabisa.

39 Mbona anung'unika mwanadamu aliye hai Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?
Maombolezo 3:39 SUV

AU:

[Kwa nini mwanadamu anung’unika anapoadhibiwa kwa dhambi zake mwenyewe?]
Maombolezo 3:39

11.31  Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.
1Wakor. 11:31 SUV

Tunapaswa kuzingatia ukweli kwamba tunaweza kuingizwa katika njia tofauti na ile tuliyopangiwa na Bwana wetu kutokana na kushiriki katika mambo ambayo kama yalivyo yenyewe siyo dhambi, lakini yana uwezo wa kutuingiza katika dhambi. Shughuli nyingi ambazo ni za lazima, muhimu au zina faida wakati zinafanywa kwa kiasi (kwa mfano michezo, mazoezi, burudani mbalimbali, n.k.) zinaweza kuchukua muda wetu mwingi hata kufikia kiasi cha kumgeuka Bwana wetu. Tunaweza kuanza kupuuza mchakato wetu wa kukua kiroho na kuzaa matunda [ya kiroho] na kujiingiza katika dhambi mbalimbali kama tamaa / uchu na majivuno. Shetani hawezi kujizuia kutumia mbinu yoyote inayoweza kutufanya tujitoe katika njia ya Mungu. Mitego yake mingi ni rahisi kuiona na kujiepusha nayo, lakini mingine imefichwa kwa werevu mkubwa – naye Ibilisi ni mwongo na mdanganyifu stadi (Mwa. 3:4-5; Yoh. 8:44; 2Wakor. 11:14; Ufu. 12:9). Mfano: miaka ya hivi karibuni kumekuwa na utitiri wa hadithi za watu ambao “walikufa kwa muda” na mara baada ya “kifo” hicho wakakutana na “Bwana Yesu Kristo” au “malaika” ambaye anawaonyesha ‘mbinguni’ na ‘motoni’ kulivyo, na halafu wakaruhusiwa kurejea katika miili yao ili wawasimulie “Wakristo” na kuwapa tahadhari za aina mbalimbali. Hadithi hizi zote zikichunguzwa katika mwanga wa maandiko, zinaonekana kuwa zina udanganyifu mkubwa uliofichwa kwa werevu mwingi ndani yake. Tunapaswa kuwa waangalifu, tusiache kitu chochote kiingilie uhusiano mwema ulioko kati yetu na Bwana wetu.

Tumeamriwa na Bwana wetu kuwa tumpende Mungu wetu kwa moyo wetu wote na kwa nafsi yetu yote na kwa nguvu zetu zote. Hii ndiyo amri kuu kuliko zote.

5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa *nafsi yako yote, na kwa nguvu zako zote.
Kumb. 6:5

*Mwanzo 2:7

22. 37 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa nafsi yako yote, na kwa nguvu zako zote.
22.38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
Matt. 22:37-38

Tunapojitayarisha kwa ajili ya kutubu dhambi zetu, ebu tujichunguze ili tuone kama kuna jambo linalochukua muda wetu zaidi ya ule muda tunaoutumia katika shughuli za kumtumikia Yeye au jambo linalotutoa katika au kutuzuia kufuata msitari aliotupangia Bwana wetu.

5.29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
5.30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Matt. 5:29-30 SUV

6.12  Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo (mamlaka ya) wa kitu cho chote (yaani sitaruhusu mwenendo wangu ulegee kiasi cha kupunguza kasi yangu ya kukua kiroho).
1Wakor. 6:12

5.13  Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili (hulka ya dhambi), bali tumikianeni kwa upendo.
Waga. 5:13

2. Kuungama.

Baada ya kutubu/toba na kujitayarisha, inafuata hatua ya kukiri dhambi zetu kwa Mungu Baba katika sala. Zaburi zinaweza kutusaidia kueleza yaliyomo mioyoni mwetu tunaposogea mbele za Bwana – Zaburi zile zinazojumuisha sala ya kukiri dhambi (kwa mfano Zaburi 32, 51, 130, 143) na pia Zaburi zingine kama ile ya 25. Tunapaswa kuchagua Zaburi ambazo zina msaada zaidi kwetu na zile ambazo zinashabihiana kwa karibu na dhambi tulizotenda.

Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema Bwana; sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema, asema Bwana, sitashika hasira hata milele. 
13 Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi Bwana, Mungu wako
Yer. 12b-13a SUV

Ingawa kuna sala za kukiri / kuungama dhambi ambazo madhehebu fulani yanawapatia waumini wao kuzitumia, na ingawa sisi wenyewe tunaweza kuwa na sala zetu wenyewe tulizozizoea katika kukiri / kuungama dhambi zetu mbele ya Mungu Baba, tunapaswa kuchukua tahadhari kuhakikisha sala zetu hizi hazitaanza kuharibika na kuwa maneno matupu tuliyokariri na kuyasema bila kuguswa nayo moyoni mwetu (a legalistic rite). Ungamo ni sala inayotiririka kutoka moyoni kutokana na shauku ya kukubali mbele za Mungu kwamba tumetenda dhambi ili tuweze kurejea Kwake – inapaswa kuwa ya unyofu, ya ukweli na inayotolewa kwa moyo safi. Mungu wetu anatazama nia iliyoko moyoni mwetu, na siyo mwenendo wetu wa nje (1Samweli 16:7).

3. Msamaha na mwanzo mpya.

3.1. Tunasamehewa kwa msingi wa dhabihu ya Bwana Yesu Kristo.

Mara baada ya kuungama dhambi zetu kwa Mungu Baba, Yeye anatusamehe kwa msingi wa dhabihu ya Bwana wetu Yesu Kristo.

1.9  Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi [hizo] zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
1.10  Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala Neno Lake halimo mwetu.
1Yoh. 1:8-9

2.1  Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2.2  naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
1Yoh. 2:1-2 SUV

Tunapaswa kukumbuka kwamba msamaha wa Mungu juu ya dhambi zetu una msingi wake katika sadaka ya Bwana wetu Yesu Kristo. Sisi wenyewe hatuna uwezo wa kulipia dhambi zetu wala kufidia kwa Mungu maovu tunayotenda. Ni Kristo pekee aliyekuwa na uwezo wa kugomboa dhambi zetu, na katika kifo chake msalabani alilipia gharama ya wokovu wetu kwa ukamilifu, Alipokubali na kubeba adhabu ya kila dhambi [iliyotendwa] katika historia ya wanadamu na hivyo ilitosheleza matakwa yanayotokana na uongofu wa Mungu. Tunapoongeza kazi zetu wenyewe juu ya dhabihu ya Kristo, ni kama vile tunasema kwamba tunaiona kuwa haitoshi – God forbid!

Tunapaswa kuonyesha shukrani yetu kwa msamaha tunaopewa na Mungu juu ya dhambi zetu kwa kudhihirisha huruma yetu katika mahusiano yetu na watu wengine, haswa katika mahusiano yetu na ndugu zetu katika Kristo. Tunapaswa kuiga mtazamo wa Mungu kwa dhambi zetu pale tunapotubu kwa kuwasamehe wenzetu wanapotutendea makosa ikiwa tunataka kupokea huruma Yake (Matt. 18:23-34).

5.7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
Matt. 5:7 SUV

6.12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Matt. 6:12 SUV

6.14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
6.15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Matt. 6:14-15 SUV

6.37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.
6.38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Luka 6:37-38 SUV

11.4 Utusamehe dhambi zetu, [nasi tunawasamehe wale wanaotukosea sisi];
Luka 11:4a

3.13  mkivumiliana, na kusameheana [pale] mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Wakol. 3:13

2.13  Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
Yakobo 2:13 SUV

3.2. Tunaanza upya na kuendelea, tukisahau ya nyuma.

Baada toba na kisha ungamo, tunaanza upya, tukisahau ya nyuma.

3.12  Si kwamba nimekwisha kufika [katika lengo la kila mmoja wetu kama Mkristo], au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
3.13  Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha ku[li]shika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
3.14  nakaza mwendo, niifikilie mede [winning post, utepe] ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Wafi. 3:12-14

Mungu wetu anatupatia msamaha Wake na anatutaka tupige hatua mbele na tuendelee kumtumikia. Ikiwa hisia hasi zinabaki mioyoni mwetu baada ya kuungama, na hisia hizo zinapunguza kasi yetu katika mwanzo wetu mpya kwa kuturudisha nyuma kimawazo katika kumbukumbu zetu, tunapaswa kuukumbuka uhalisia wa huruma Yake na kuzima hisia hizi. Hisia kama hizi hazitoki kwa Mungu.

Tunapoanguka, tunaposhindwa, tunapaswa kusimama na kuendelea, tunapaswa kuelekeza macho yetu mbele ya safari na siyo nyuma, ili tumtumikie Yeye vyema. Baada ya kufanya toba na kujifunza kutokana na makosa yetu, tunapaswa kuyaacha [makosa hayo] na kutoyafikiria tena.

3.3. Maisha yetu ya Kikristo ni vita, na katika vita hakuna utimilifu.

Kushindwa na kurudishwa nyuma ni mambo yanayotokea katika vita. Kama ambavyo tunapaswa kujifunza kwamba tunapaswa kusimama haraka na kuendelea na vita badala ya kuwazia jinsi tulivyoshindwa na kuwa na masikitiko (kwa sababu mambo hayako, na hayatakuwa vile tunavyofikiria), vivyo hivyo tunaposimama na tunapoanza upya mapambano tukiwa na nia halisi ya kuendelea katika njia tuliyowekewa na Bwana, tusitegemee kwamba itakuwa au itapiganwa kwa utimilifu kuanzia hapo na katika siku za usoni. Mambo yote yatakuwa [ma]timilifu pindi tutakapokuwa na Bwana wetu. Kwani kwa sasa tutaendelea kuwa katika uwanja wa vita – mahala pa mapambano ambapo sote huanguka na kupata majeraha [mara mojamoja!].

Hivyo inatupasa tusifanye kiapo na tusiweke nadhiri na pia tusitoe ahadi kwa Mungu. Ikiwa katika saa ya udhaifu tunashindwa kutimiza kiapo au nadhiri au ahadi hiyo, itatusababishia tuingie ndani zaidi ya masikitiko na kukata tamaa.

5.34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
5.35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
5.36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
Matt. 5:34-36 SUV

5.12  Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.
Yakobo 5:12 SUV

Kanuni hizi zinaelekezwa kwa waumini kati yetu ambao wakati wote wanatarajia maisha yao yasiwe na mawaa, yasiwe na dosari. Ukweli ni kwamba hili haliwezekani tukingali hapa duniani; hata hivyo, tusiache shauku yetu ya kuwa watimilifu na pia tusiache shauku halali ya kuwa waaminifu kwa Bwana wetu igeuke na kuwa tabia ya kukataa kukubali makosa yetu ya zamani (kwamba tuliyatenda tukiwa Wakristo) na kwamba imetupasa tuyasahau na tuendelee; au shauku hii isitufanye tuchukue hatua za kufanya / kuweka kiapo / ahadi / nadhiri ambazo zinaonyesha kwamba tumesahau ukweli kwamba hata tukiwa na nia njema kiasi gani, bado sisi ni wenye dhambi, bado tungali na hulka ya dhambi ndani yetu na bado tungali ndani ya ulimwengu wa Ibilisi. Macho yetu yanapaswa kuelekezwa katika wakati huu, siku ya leo – tuweze kuutumia wakati huu, siku hii, ili kukua kiroho katika Neno Lake na kumtumikia Bwana wetu kwa uaminifu katika nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu.

6.34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Matt. 6:34 SUV

Yaweza kuwa kwamba licha ya juhudi zetu, kupata ushindi dhidi ya dhambi fulani inayotusumbua itachukua muda [mrefu] kidogo. Mwanzo tunaweza kuanguka mara kadhaa, lakini tunavyozidi kuendelea kiroho, kushindwa kwetu, kuanguka kwetu katika dhambi hiyo kutakuwa kunatokea mara chache zaidi na zaidi mpaka tutakapoona kwamba udhaifu wetu [kwa dhambi hiyo] umekwisha kabisa na tunaweza kukitizama kishawishi kile bila ya woga tena. Na kwa msaada wa Mungu wetu, hakuna udhaifu wala kishawishi ambacho hatuwezi kushinda.

Hii ndiyo sababu maandiko mara nyingi yanatusihi tuwe na ustahamilivu. Nyakati fulani sisi sote tutaanguka, tutashindwa. Hakuna anayeweza kupigana vita hii bila kuumia na hakuna anayeweza kumaliza mbio hii (vita ikifananishwa na riadha) bila kuanguka. Hii ndiyo maana ustahamilivu wetu katika kujitafutia ahueni ya kiroho baada ya kujeruhiwa na kunyanyuka baada ya kuanguka ni mambo muhimu yatakayoamua ni kwa kiasi gani tutaendelea [katika vita yetu hii]. Kama ilivyo katika maeneo mengine ya mafanikio ya wanadamu, wale walio na nia madhubuti ya kujitoa na kuvumilia na kustahamili ndio watakaofanikiwa zaidi.

Kuanguka na kushindwa [mara moja moja] ni mambo yatakayotokea katika vita hii, na mara baada ya kujifunza kutokana na makosa na kuanguka huko, kutubu na kukiri dhambi zetu, basi tusiyaweke hayo moyoni kwani yataathiri mwendo wetu na Kristo. Kufikiria kupita kiasi matukio ya kushindwa kwetu na kuanguka kwetu kwa masikitiko na kukata tamaa kutaifanya vita yetu hii iwe ngumu zaidi. Shetani anajua fika ya kwamba hisia za hatia (guilt), aibu, majuto yanayokithiri, kukataa kukubali kwamba tulishindwa, na kuchelewa kusimama [tena] na kuendelea, ni silaha zenye nguvu alizo nazo mikononi mwake ambazo anaweza kuzitumia dhidi yetu na kwa kweli ni silaha zinazoweza kumfanya Mkristo akwame katika mwendo wake.

Mwisho, tunapaswa kukumbuka kwamba kujilinda katika vita hii ni taswira / upande mmojawapo tu wa vita yetu hapa duniani.

4. Tunarejea katika kumfuata Kristo na kuingia tena katika mapambano.

Tunapaswa kukua kiroho na kufanya maendeleo ya kila siku katika mwendo wetu wa kila siku na Kristo. Jinsi tunavyozidi kuwa waaminifu katika kufanya yaliyo sahihi, ndivyo tunavyozidi kuwa na ufanisi zaidi katika kukataa yote ambayo ni mabaya, kwa kuwa kutokana na uweza wa Roho Mtakatifu tutazidi kuuweka utashi wetu chini ya mapenzi ya Mungu.

Katika vita yoyote ile, haitoshi tu kufanya juhudi za kujilinda ili kuzuia kushindwa na kuanguka, na mifano kutoka katika nyanja za mashindano ya michezo na vita inatufundisha kwamba kuelekeza juhudi zetu katika kujilinda pekee kunatufanya tuwe tunashambuliwa wakati wote na adui. Vivyo hivyo katika vita yetu dhidi ya adui. Wakati wote tunapaswa tuwe tunapambana tukiwa na mtazamo wa kutafuta ushindi, kwenda mbele kwa kiasi tunachoweza kwa ajili ya Bwana wetu na kuzaa matunda yaliyo mema na mengi kwa ajili Yake. Mwisho wa yote, hatutahukumiwa kutokana na matukio ya matukio yetu ya kuanguka na kushindwa, bali tutapewa thawabu kutokana na matunda yetu tunayozaa kwa ajili ya Bwana wetu. Kujifunza Neno la Mungu – kwa kulisikiliza, kulisoma sisi wenyewe, kufundishwa kanuni zake na Mwalimu-Mchungaji mahiri; kulitumia Neno katika maisha yetu; kuwasaidia wenzetu kufanya vivyo hivyo – yote haya yakifanywa katika uweza wa Roho Mtakatifu – ndizo mbinu za kujitayarisha na vita hii, ndizo mbinu za kupigana vita yenyewe, na ndizo mbinu za kupata ahueni na kunyanyuka ikiwa tunaanguka na kujeruhiwa vitani.

Basi na tupigane vita hii njema ya imani!

6 Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.
Kumb. 31:6 SUV

45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
1Sam. 17:45-47 SUV

10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Isa. 41:10 SUV

… na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Matt. 28:20b SUV

4.13  Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Wafi. 4:13 SUV

6.12  Piga vita vile vizuri vya imani;
1Tim. 6:12a SUV

IV. Vyanzo vingine vya mafundisho juu ya kupambana na dhambi.

https://ichthys.com:

1. Hamartiology

2. The Believer’s Dealing With Sin

3. The Christian Walk

4. Peter’s Epistles – Coping With Personal Tribulation, AU tafsiri yake ya Kiswahili: Nyaraka za Petro na R. Kilambo

https://bibleacademy.com/omo:

1. Basic Training Lesson 9: Preventive Measures for Sin Part 1

2. Basic Training Lesson 10: Preventive Measures From Sin Part 2

3. Basic Training Lesson 6: The Holy Spirit Part 1: The Coming of The Spirit

4. Basic Training Lesson 7: The Holy Spirit Part 2: Living by The Spirit

5. Basic Training Lesson 8: The Holy Spirit Part 3: The Spirit and the Flesh

6. Galatians – Union with Christ: Lesson 10

7. Doctrine of the Judgement Seat of Christ:
Romans 14:10 – Lesson 67
Romans 14:11 – Lesson 68

8. Doctrine of the Flesh
Galatians 5:13a - Lesson 21
Galatians 5:14 – Lesson 22

Katika Neema za Bwana Wetu!