Mateso Tusiyostahili Katika Ndoa [Zetu] na Katika Maisha Yetu - na Mfano Tuliopewa na Kristo: Nyaraka za Mtume Petro #35

 

Na Dr. Robert Dean Luginbill

Wa: https://ichthys.com

 

Tafsiri ya Kiswahili na Respicius Luciani Kilambo

Wa: https://sayuni.co.tz

 

Ruksa ya Tafsiri Hii Imetolewa Mahususi na Dr. R. D. Luginbill

Permission for this Kiswahili Translation Has Been Kindly Granted by Dr. R.D. Luginbill

 

1st Peter 3:1-22

 

I. Ibara ya Kwanza (aya ya 1-7)

3.1 Kadhalika ninyi wake [mnapaswa] kuwa watiifu kwa waume zenu kwa makusudi kwamba, ikiwa kuna yeyote [katika hao waume] ambaye [kwa wakati huu] hatii ukweli wa Neno la Mungu, ikiwezekana / labda avutwe na mwenendo [wa kimungu] mnaouonyesha ninyi wake zao, bila ya ninyi kusema lolote juu ya Neno hilo,

3.2 wakiutazama mwenendo wenu [kwao], ulio na heshima kuu.

3.3 [Kuhusiana na jambo hili], kujipamba kwenu kusiwe kwa kukithiri, [kusiwe ndiyo kipaumbele cha maisha yenu], mkijishughulisha kuliko kiasi stahiki katika urembo wa nywele zenu, mkionyesha [kwa watu] mapambo yenu ya vito [vya thamani] na nguo zenu [za thamani],

3.4 bali [badala yake] mweke kipaumbele katika mtu wenu wa moyoni [asiyeonekana], (yaani kukua kiroho) kwa njia ya upole na utulivu wa roho (yaani mwenendo wa kiroho ulio stahiki) – hili ni jambo lenye thamani zaidi mbele za Mungu.

3.5 Kwa maana hivi ndivyo wanawake watakatifu wa zamani, walioweka tumaini lao kwa Mungu, walivvyojipamba, yaani kwa kuwatii waume zao,

3.6 kama vile Sarah alivyomtii Abrahamu, akimwita “bwana”. Nanyi mmekuwa watoto [halisi], ikiwa mtatenda yaliyo sahihi [na kwa nia njema] na si kwa sababu ya kuogopa kutishwa.

3.7 Kadhalika ninyi wanaume, kaeni na wake zenu kwa akili inayotokana na ufahamu wa Biblia (yaani kutokana na kile Biblia inachofundisha kwa maneno na mifano, ya jinsi ya kuishi na mkeo), mkienenda juu yao kama inavyostahili kuenenda kwa mtu aliye dhaifu kuliko ninyi [ambavyo ndivyo wanawake walivyo – dhaifu]. [Ninyi wanaume] mnapaswa kuonyesha heshima stahiki kwa wake zenu ambao ni warithi wenzenu wa neema ya uzima wa milele, ili sala zenu zisipate ukinzani (yani sala zenu zisitatanishwe na dhambi – ambayo ni matokeo ya kutowaheshimu wake zenu).

1Petro 3:1-7

 

Wajibu wa mke Mkristo katika ndoa (aya ya 1-2):

 

3.1 Kadhalika ninyi wake [mnapaswa] kuwa watiifu kwa waume zenu kwa makusudi kwamba, ikiwa kuna yeyote [katika hao waume] ambaye [kwa wakati huu] hatii ukweli wa Neno la Mungu, ikiwezekana / labda avutwe na mwenendo [wa kimungu] mnaouonyesha ninyi wake zao, bila ya ninyi kusema lolote juu ya Neno hilo,

3.2 wakiutazama mwenendo wenu [kwao], ulio na heshima kuu.

1Petro 3:1-2

 

Ni muhimu sana tangu hapa mwanzo wa sehemu hii ya kwanza tujikumbushe kwamba, ingawa mahusiano kati ya jinsia zetu mbili na masuala ya ndoa ni, kama siyo yenye umuhimu mkubwa katika fikra za wanadamu wengi basi bila shaka yako juu kabisa katika ile orodha ya yale yanayochukuliwa kuwa ni mambo muhimu kabisa, [lakini] kwa mtazamo wa Mungu wokovu, kukua kiroho na matunda ya kiroho ndiyo masuala muhimu zaidi katika maisha ya wanadamu wote. Kwa kweli maisha ya wanadamu yanamhusu tu Bwana Yesu Kristo katika kina, mapana na marefu yake. Kama suala hili ni la kweli kwa upande wa wasioamini – na kwa hakika hii ni kweli, kwani hao wote wasioamini wataukubali ukweli huu hapo mwisho (Isaya 45:23; War. 14:11; Wafi. 2:10) na watahukumiwa Naye hapo mwisho (Matt. 25:31-46; Yoh. 5:25-29; Waebr. 9:27; Ufu. 20:11-15 – basi suala hili kwa hakika ni la kweli kwa waumini ambao wanaazimia, angalau kwa midomo yao, kwamba wanamuenzi Yeye na yale anayotaka tuyafanye, juu ya kila kitu katika maisha yetu hapa duniani.

 

4.17 Kwa maana wakati u karibu wa hukumu [ya mwisho] kuanza katika nyumba ya Mungu (ling. na 1Pet. 4:7); na ikianza kwetu sisi [tunaoamini], mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje (yaani, Injili ni wokovu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo)?

4.18 Kwani imeandikwa, “Na *mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataishia wapi (Mithali 11:33)”?

1Pet. 4:17-18

 

Mfano mmojawapo wa kuokoka kwa shida ni kama mtu anayeiamini Injili katika dakika ya mwisho ya uhai wake hapa duniani, kw. mf. yule mhalifu wa pili pale msalabani (Luka 23:39-43)

 

Kutokana na hali hii, bila shaka itaingia akilini kwamba mafundisho yote kutoka katika Neno la Mungu, nia na fikra halisi za Yeye aliye Neno hai la Mungu (1Wakor. 2:16; Ufu. 19-13), yana lengo jema kwa ajili yetu katika kila taswira yake, lengo la kuboresha na kuendeleza yale yaliyo muhimu katika maisha yetu – na siyo kumpendelea mtu mmoja juu ya mwingine, kikundi kimoja cha watu juu ya kingine, jinsia moja juu ya nyingine. Kumpendelea mtu, kikundi, jinsia moja juu ya nyingine ni fikra za kidunia, fikra za kisiasa, fikra zinazotawaliwa na hisia, ambazo msingi wake ni mitazamo isiyo sahihi ambayo imeenea sana katika utamaduni wa siku na enzi hizi za sasa. Kitu ambacho kila Mkristo anapaswa kuwa na shauku nacho na kutaka kifanikiwe, awe mke au mume, awe mtu wa mataifa au Myahudi, kaolewa au kaoa, kijana au mzee, ni kimoja tu: wokovu wa wote ambao hawajaokolewa, na makuzi ya kiwango cha juu kabisa ya kiroho yanayowezekana, maendeleo ya kiroho na matunda ya kiroho ya ndugu zetu wote katika Kristo.

 

3.28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa kitu kimoja katika kuungana na Kristo Yesu.

Waga. 3:28

 

Kuuzidisha utukufu wa Kristo – jambo ambalo Wakristo wote walio hai watalifanikisha ikiwa wote watauitikia wito wa Kristo kwa namna iliyo sahihi – kunawezekana tu ikiwa kila sehemu ya Mwili wa Kristo itafanya kazi yake iliyopangiwa Naye kwa ufanisi. Sikio linalokataa kusikia, au mguu unaokataa kutembea, katika mwili wa binadamu, utakwaza ufanyaji kazi wa mwili huo kwa kiasi kikubwa sana. Katika mwili wa Kristo hii inakuwa kweli mara dufu kwa sababu yeyote [katika Mwili/Kanisa] ambaye hatatumikia inavyopasa katika namna ya Kikristo hapa duniani, atakwazwa katika shughuli zake za kiroho kwa upande mmoja, na atawakwaza waumini wenzake ambao ana ushirika nao (fellowship), na hata wale anaokutana nao kwa muda tu kwa upande wa pili. Na ushirika huo unapokuwa mkubwa zaidi, ndivyo mwenendo huo utakavyokuwa na athari mbaya zaidi kwa wenzake.

 

1Wakor. 7:28b … lakini watu kama hao [wanaooa/wanaoolewa] watakuwa na dhiki katika *mwili nami nataka kuwaepusha na hilo. *maana yake: ingawa wanaweza kuwa na amani mioyoni mwao.

 

3.7 Kadhalika ninyi wanaume, kaeni na wake zenu kwa akili inayotokana na ufahamu wa Biblia (yaani kutokana na kile Biblia inachofundisha kwa maneno na mifano, ya jinsi ya kuishi na mkeo), mkienenda juu yao kama inavyostahili kuenenda kwa mtu aliye dhaifu kuliko ninyi [ambavyo ndivyo wanawake walivyo – dhaifu]. [Ninyi wanaume] mnapaswa kuonyesha heshima stahiki kwa wake zenu ambao ni warithi wenzenu wa neema ya uzima wa milele, ili sala zenu zisipate ukinzani (yani sala zenu zisitatanishwe na dhambi – ambayo ni matokeo ya kutowaheshimu wake zenu).

1Pet. 3:7

 

Migongano katika ndoa, kama ambavyo mtu yeyote aliye katika ndoa anavyofahamu, huleta madhara makubwa kwa amani katika ndoa husika. Na tumeitwa tuishi katika amani (1Wakor. 7:15), kwani kutembea katika amani pamoja na Bwana, yaani “kupumzika katika amani” ambamo tumeacha kutegemea kazi / juhudi zetu wenyewe na badala yake tunamtumainia Bwana kwa kila kitu, ndiyo kutimizwa kwa amri ya nne [kati ya zile amri 10 za Mungu] katika enzi hii ya Kanisa ambapo tumo katika dispensation mpya ya Roho [Mtakatifu] - yaani milenia 2 za enzi ya Kanisa – (Waebrania 4:9-10; ling. na Isa. 26:3; 57:2; Yoh. 14:27; War. 5:1; Waefe. 2:14; Wafi. 4:7; Wakol. 3:15; Wathess. 3:16; 1Pet. 1:2). Hii ndiyo sababu inayomfanya Petro, akiwa katika Roho Mtakatifu, alizungumzie suala la mamlaka katika ndoa, na siyo kuipa jinsia moja madaraka / kipaumbele juu na dhidi ya jinsia nyingine: kuendelea kukua kiroho hadi kufikia kiwango cha juu kabisa, kuendelea na mchakato huo kila siku, na kuzaa matunda ya kiroho (ambavyo vinalazimu amani kama hitaji la kwanza).

 

Kwa hakika, mtazamo wa Biblia kuhusiana na suala la ndoa ni tofauti kabisa na jinsi ambayo karibu kila mafundisho ya kidunia – na kwa masikitiko makubwa hata mahubiri na mafundisho ya makanisa – yanavyolichukulia. Ndoa, katika Biblia, ni taasisi inayochukuliwa kuwa ni hitaji lililojaa majonzi / masikitiko na siyo njia ya kupata furaha katika maisha yetu ya hapa duniani. Katika kuwatia moyo wanawake wa Kikristo wawe watenda mema, Petro atawazungumzia wale wanawake waumini maarufu wanaotajwa katika Biblia. Kwa hakika tutalizungumzia suala hili hapa chini (aya za 5-6), lakini jambo muhimu hapa ni kwamba ndoa chache sana sana hapa duniani zinaweza kupewa wasifu wa “ndoa zilizojaa furaha daima” au aina yoyote (na ziko aina nyingi!) ya mapenzi ya kufikirika yanayochukuliwa kuwa ni mfano bora kabisa wa ndoa kama inavyoonekana katika utamaduni wetu wa kisasa. Sote tunaosoma Biblia kwa makini tunayafahamu fika matatizo yaliyokuwako kati ya Abrahamu na Sara. Rebekah naye alilazimika kumsaidia mwanaye katika kumdanganya mume wake ili kumwezesha mwanaye huyo – Yakobo – apate baraka alizostahili. Na ni nani anayeweza kuthubutu kudai kwamba Yakobo alikuwa na ndoa ya furaha, ingawa alikuwa na wake wanne? Hannah alikuwa muumini mkuu – lakini ndoa yake haikuwa na furaha. Hakuna dalili yoyote inayotuonyesha kwamba Daudi na wake zake (hatuambiwi idadi yao) walikuwa na uhusiano wa karibu na uliotimiza shauku zao za kuwa na furaha, na tunajua kwamba ndoa yake ya kwanza ilikuwa baa tupu. Tunaweza kuendelea na orodha hii ya ndoa zilizokuwa chini ya 100% katika Biblia. Kitu ambacho mifano hii inatuonyesha kwa uhakika ni kwamba ndoa, ingawa kwa watu wengi ni uhusiano wanaouhitaji, yaani ni wa lazima kwao (1Wakor. 7:2), hata hivyo katika maandiko inaonyeshwa, siyo kama ni ufumbuzi adhimu wa matatizo na malengo ya ulimwengu, bali inaonyeshwa katika uhalisia wake. Tunachoweza kusema ni kwamba wengi kati ya hawa watu wa Mungu, waume kwa wake, walifanikisha mpango wa Mungu juu ya maisha yao licha ya mitihani na mateso yanayotokana na ndoa, na walisaidiana na wenzi wao kupata mafanikio hayo. Hakuna fasili ya Kibiblia ya ndoa iliyo nzuri mbele ya macho ya Mungu kuliko ile ya mume na mke wanaosaidiana katika kutimiza majukumu waliyopewa na Mungu ili kufanya yale yote ambayo tumewekwa / tumeletwa hapa duniani kuyafanya, yaani kukua kiroho, kutembea karibu zaidi na Bwana, na kutimiza majukumu ya utumishi ambayo kila Mkristo amepewa ili ayatimize hapa duniani.

 

Ni kwa mtazamo huu Petro anasihi jinsia zote mbili kukumbatia na kutimiza majukumu yao kila mmoja, yanayotokana na ndoa. Hakuna hata mmoja wao anayeweza kubadilisha parameta au vigezo vinavyoifanya na kuionyesha ndoa ya kimungu [na vile inavyotakiwa kuwa]. Wote wawili, mke na mume, wanapewa majukumu ya wazi kabisa, na ni ikiwa tu wote wawili wakiyapokea majukumu haya waliyopewa na Mungu na kuheshimiana, pamoja na kuheshimu wajibu ambao Mungu amempatia kila mmoja wao [peke yake] ndipo kati yao patakuwa na kiasi cha kutosha cha amani ili ndoa yao iweze kudumu na kusitawi – na kwa pande zote mbili kukua [kiroho], na kuwa na maendeleo na kuzaa matunda kwa ajili ya Bwana Yesu.

 

5.10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya (yasiyo na thamani).

2Wakor. 5:10

 

Hii (nukuu hapo juu) ni kweli kwa waume na ni kweli kwa wake. Yawezekana tukawa na dhima (roles) tofauti hapa duniani (na kwa hakika hakuna waumini wawili walio na karama zinazofanana wala “kazi” zinazofanana walizopewa na Bwana), lakini sisi sote tumepewa kanuni zilezile tunazowajibika nazo: sote tutathawabiwa kulingana na kile tulichokifanya hapa duniani kwa ajili ya Bwana katika kutimiza maagizo Aliyotupatia, kujinyima, kubeba misalaba yetu, na kumfuata Yeye … katika kukua kiroho, kufanya maendeleo [ya kiroho] na kuzaa matunda [ya kiroho]. Kama tukifanya majadiliano ndani ya nafsi zetu yaliyo na lengo la kuepa dhima au “kazi” mahususi tulizopewa ambazo msingi wake ni karama na utumishi tuliopewa, mwisho wa siku tutakuwa tunajidhuru sisi wenyewe.

 

Kuna umuhimu wowote, kwa mfano, ikiwa katika Mwili wa Kristo sisi ni mguu na siyo mkono, ni sikio na siyo mdomo (1Wakor. 12:14-18)? Viungo vyote hivyo vina umuhimu – na vyote vina fursa kamili na sawasawa na vingine katika kushinda yale mataji matatu ya thawabu za mbinguni ili katika siku ile waweze kuisikia ile kauli ya “umefanya vema” kutoka kwa Bwana wetu. Hili ndilo lengo letu halisi – au tuseme ndilo linapaswa kuwa lengo letu. Kujihangaisha juu ya dhana mbalimbali za kutokuwako na usawa kati ya jinsia hapa duniani, ikiwa ni kati ya mume fulani na mke fulani au duniani kote kwa ujumla ni harakati za wapumbavu. Kwani kwa hakika, kama ambavyo sisi wote ni warithi wa Kristo tulio sawa mbele Yake na tulio wamoja katika Yeye hapa na sasa, pia sote tutakuwa “wamoja” [katika] milele, Mke mkamilifu na mtimilifu, bila chuki wala utengano wala doa wala dosari, tukiwa sawa katika safu [zilizopangwa] za Kanisa kwa maana ya kwamba sisi sote tutaweza kushiriki Naye kikamilifu milele yote – lakini tukitofautishwa kwa msingi wa kiasi gani tulijitoa katika kumtumikia Bwana wetu katika maisha yetu mafupi ya hapa duniani.

 

Na sisi wote, ni muhimu kusisitiza, waumini wote, bila kujali tofauti tulizo nazo sasa hapa duniani, tunapewa fursa kamili bila upendeleo, za kushinda thawabu za juu kabisa – kwa sababu Bwana wetu, Hakimu mtimilifu, anahesabu aina na ukubwa wa kipaji alichotupatia pamoja na mazingira yetu katika utondoti wake, ikiwa ni pamoja na jinsia zetu na dhima tulizopangiwa hapa duniani. Hivyo, bila kujali hali na hadhi yetu, iwe ya juu au ya chini, tunahitaji kukumbuka kwamba Bwana wetu, aliyeumba ulimwengu na ambaye ndiye Bwana na Nahodha wa ulimwengu huo, amekwishatuonyeshaa namna sahihi ya kuenenda hapa duniani, akituamrisha kutembea kama alivyotembea Yeye katika kutokuilazimisha heshima [kutoka kwa watu] ambayo kwa kweli alistahili, lakini alijishusha ili aweze kuitimiza kazi ambayo Baba alimpatia – ili aweze kutuokoa (ling. na 1Pet. 2:21-23).

 

13.15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

Yoh. 13:15 (ling. na Yoh. 14:15; 14:23-24)

 

2.5 Iweni na nia (mwelekeo) iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

2.6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

2.7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

2.8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Wafi. 2:5-8

 

12.1 Basi na sisi pia [kama waumini wanaotajwa katika sura ya 11], kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hili [watu na malaika], na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi (maeneo ya tabia zetu ambamo tuna udhaifu mkubwa zaidi); na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

12.2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu (Alfa na Omega); ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Waebr. 12:1-2

 

Kama Bwana wetu Yesu Kristo alitupilia mbali majivuno na akavumilia aibu ya msalaba kwa ajili yetu, je nasi, haitupasi kukubali yote aliyotupangia katika maisha yetu [katika namna ile ile]? Alikuwa akiitazamia ile “furaha iliyowekwa mbele Yake” (Waebr. 12:2), nasi tumeitwa ili tutembee katika nyayo Zake, tukiwa na shauku na kuistahi na kutumaini kuipata kauli ya sifa kutoka Kwake kwa kufuata mfano Wake katika maisha yetu ya hapa duniani, badala ya kufukuzia mafanikio au hadhi ya kimaisha au kuonekana wenye haki mbele ya watu hapa duniani. Tunapaswa kuwa na mtazamo wa kufuata mfano Wake kuhusiana na mambo yote ya kidunia, ikiwa ni pamoja na ndoa na masuala ya mamlaka na wajibu ndani ya ndoa hizo.

 

Biblia inaizungumzia ndoa kutoka katika mtazamo halisi wa kimungu, na siyo mapenzi ya kufikirika. Badala ya kuwa jibu la matatizo yetu yote, Biblia inatufundisha kwamba ndoa ni mzigo (nira) mzito (1Wakor. 7:32-35), ingawa mara nyingi ni mzigo wenye ulazima kwa kiasi fulani (1Wakor. 7:2; 7:9). Kama wanawake wana shuruti la kukubali kuwa chini ya mamlaka ya waume zao, [mamlaka waliyopewa na Mungu] (Waefe. 5:22-24; Wakol. 3:18), wanaume wana shuruti la kubeba jukumu/mzigo wa uongozi na ulazima unaofuatana na uongozi huo wa kuwatendea haki wake zao (Waefe. 5:26-28; Wakol. 3:19; 1Pet. 3:7). Na kwa Wakristo, jukumu lao kuu linapaswa kuwa usalama wa kiroho wa mwenza wao. Hii ndiyo sababu maandiko yanatuasa Wakristo tusipendelee ndoa – kuoa au kuolewa – (Wakor. 7:1; 7:28), na maandiko hayo hayo yanatuasa tupunguze misuguano katika ndoa ((1Wakor. 7:3-5; 1Pet. 3:7). Katika hali timilifu, mume na mke waliopevuka kiroho wataunda ndoa iliyo timilifu wakiivuta nira yao (ndoa) katika mwelekeo mmoja (badala ya kila mmoja wao kuvutia kwake) kwa ajili ya Bwana yesu Kristo na Kanisa Lake. Lakini hili litatokea tu ikiwa wanandoa wote wawili watayakubali majukumu yao ya kibiblia bila ubishi.

 

Kwa kifupi, kwa mtazamo wa Biblia, mke anapaswa kumheshimu mume wake; mume anapaswa kumwonyesha mke wake upendo unaojiwajibisha.

 

3.18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana.

3.19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao.

Wakol. 3:18-19 NEN Biblia

 

Askari bora hufuata uongozi wa kamanda wake kwa moyo wake wote; afisa/kamanda bora siku zote anajali maslahi ya askari wake kama jukumu lake nambari mbili – baada ya ulazima wa kufanikisha jukumu la kwanza la wote, yaani vita yenyewe. Vita yenyewe, kwa hakika, ndilo jukumu la kwanza la kila Mkristo, na hii ndiyo maana ndoa inaweza kutatanisha mafanikio ya vita hii, haswa pale mwenza mmoja anapoyapa kipaumbele mambo mengine na kuenenda tofauti na kanuni [za Kikristo]. Na ikiwa jukumu la kupenda kuyakubali mamlaka ya mume ambalo Biblia inampa mke likionekana kuwa zito kwake, au ikiwa jukumu la kumjali na kumpenda mke wake litakuwa zito sana kwa mume, basi ni vema kukumbuka kwamba ndoa ni uamuzi ambao hakuna mtu yeyote siku hizi analazimika kuufanya – lakini pia uamuzi huo ukiishafanywa, majukumu tunayopewa na Biblia kwa wote, mume na mke, yako wazi kabisa.

 

 

Mwenendo Wenu wa Kimungu Kwao, Ulio na Heshima Kuu (aya ya 2): Hivi ndivyo waume ambao “hawatii ukweli wa Neno” watakavyovutwa waingie katika imani katika Bwana Yesu Kristo, yaani kwa kuuona mwenendo ulio mwema na wa kimungu wa wake zao katika ndoa yao – ambao unapaswa kuwa bora zaidi ya ule waliouonyesha kabla hawajawa waumini. Mabadiliko makubwa ya mwenendo ya namna hii yanayowaletea mema katika taswira nyingi za maisha yao, na yanayoambatana na kiasi kikubwa [hivyo hivyo] cha heshima kwa waume hao hayawezi kushindwa kumvutia mtu asiyeamini ambaye anafaidika na mabadiliko hayo. Kumpatia mume Injili – katika muda muafaka kufanya hivyo – ni jambo linalofaa kufanywa na mke huyu pia. Lakini kama usemi wa kale unavyotuasa, “ada ya mja hunena, mwungwana ni kitendo”, na ni ukweli huu ambao Petro anataka tuupate pale anaposema “… wavutwe kwa mwenendo mnaouonyesha … bila ya ninyi kusema …” Na wakati ibara hii inazungumzia mahususi waume wasioamini, kwa hakika pia inatumika katika hali ya mke anayeamini ambaye anaonyesha shauku ya kujifunza kweli ya Biblia wakati mume wake anayeamini bado yuko katika hali ya uvuguvugu katika imani yake: mabadiliko makubwa katika mwenendo na tabia ya mke wake yana uwezekano mkubwa zaidi wa kuyaonyesha mafundisho anayoyapata kuwa yanafaa sana [katika macho ya mume huyo], kuliko maneno yoyote atakayoambiwa.

 

wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu katika mambo yote.

Tito 2:10b SUV

 

Vipaumbele Sahihi na Stahiki (aya za 3-4):

 

3.3 [Kuhusiana na jambo hili], kujipamba kwenu kusiwe kwa kukithiri, [kusiwe ndiyo kipaumbele cha maisha yenu], mkijishughulisha kuliko kiasi stahiki katika urembo wa nywele zenu, mkionyesha [kwa watu] mapambo yenu ya vito [vya thamani] na nguo zenu [za thamani],

3.4 bali [badala yake] mweke kipaumbele katika mtu wenu wa moyoni [asiyeonekana], (yaani kukua kiroho) kwa njia ya upole na utulivu wa roho (yaani mwenendo wa kiroho ulio stahiki) – hili ni jambo lenye thamani zaidi mbele za Mungu.

1Pet. 3:3-4

 

Mara nyingi watu (Wakristo) wanashindwa kuuona umuhimu wa aya hizi mbili. Petro, akiwa katika Roho Mtakatifu hasemi (kwa wanawake wa Kikristo wa wakati ule) kwamba mwonekano wao wa nje (yaani kujipamba na mavazi) hauna umuhimu. Badala yake, anawaambia wanawake Wakristo, wa wakati ule na wa sasa, kwamba mwonekano wao wa nje haupaswi hata kulinganishwa na kukua kiroho, maendeleo ya kiroho, na matunda ya kiroho ambayo hutokea ndani au moyoni mwa Mkristo, na ambayo yanapaswa kuwa ndiyo shabaha ya kila Mkristo, bila kujali jinsia yake au mambo mengine yoyote ya kidunia.

Ibara hii pia iko wazi kabisa kuhusiana na kile ambacho wanawake wa Kikristo wanapaswa kukichukulia kuwa ni kitu cha muhimu kuliko vyote, yaani siyo matamanio na matakwa ya waume zao (au matarajio ya utamaduni wa dunia kwa ujumla) pale mambo haya yanapogongana na shabaha zetu za kiroho, bali ni kumfurahisha Bwana wetu Yesu Kristo kwa kutenda kila kitu Bwana Yesu Kristo anachokitaka [kutoka kwetu], mke mwema atakuwa anatimiza msingi wa usaidizi halali na sahihi kwa mume mwema ambaye pia ana nia ya kumfuata Bwana kama kipaumbele chake [cha kwanza] katika maisha yake.

 

Ikiwa wote, mume na mke, wameazimia kufanya makuzi ya kiroho, maendeleo ya kukua kiroho, na kuzaa matunda ya kiroho kwa ajili ya Bwana kuwa ndiyo vipaumbele vya maisha yao, basi migongano yote mingine inayoweza kutokea katika maisha yao itapungua na kutatuliwa kwa urahisi – kwa sababu wote wawili wana ari kuu kwa mafanikio ya kukua kiroho, kuendelea kiroho, na kuzaa matunda ya kiroho kwa wenzi wao. Lakini bila shaka [kwa sababu ya hulka zetu za dhambi], ubinafsi na masuala yasiyo ya kiroho yatapewa, japo mara moja-moja, kipaumbele na hivyo kuingilia katika ndoa hii, basi kutakuwako na misuguano na kukwazika kwa makuzi ya kiroho. Hakuna hata mmoja wetu aliye mtimilifu. Kila mmoja wetu ana dosari za kitabia ambazo watu wengine wanakereka nazo. Dosari hizi tunaingia nazo katika ndoa zetu, na hii ina maana ya kwamba ndani ya ndoa zetu kuna seti mara dufu za dosari hizi, ambazo mara nyingi hazipatani kabisa kila moja na nyenzake. Hivyo hata katika ndoa kati ya waumini wawili waliopevuka kiroho na wote wawili wana shauku ya kumwona mwenza wake anakuwa na mfanikio ya kiroho, kutakuwa na nyakati ambamo mwafaka katika ndoa utakumbwa na changamoto – na ikiwa hili litatokea kati ya wenza waliopevuka kiroho, itakuwaje kati ya wanandoa ambao hawajapevuka au ambao hawajaweka kipaumbele katika shabaha halisi za Kikristo? Katika nyakati hizo wanandoa wa Kikristo wanapaswa kukumbuka kwamba wanawajibika kwa Bwana kutimiza majukumu yao ya kimungu, bila kujali mwenendo wa mwanandoa mwenza, yaani kutambua na kutii mamlaka ya mume wake kwa mke (hata kama mume amekosea / hayuko sahihi – lakini si kufikia kiasi cha kuvunja kanuni za msingi za kiroho), na kujali kwa upendo katika upande wa mume (hata kama mke huyo haonyeshi busara / mantiki – lakini si kufikia kiasi cha kutatanisha kanuni za msingi za kiroho).

 

2.9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri (yenye staha na heshima), pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

2.10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

1Tim. 2:9-10

 

Ibara hii hapa juu haitaji wala haizungumzii kabisa mahusiano ya ndoa, na kwa wazi kabisa inalengwa kwa wanawake wote ndani ya Kanisa [la Bwana Yesu Kristo], lakini fundisho linalotolewa na Paulo hapo ni lile lile linalotolewa na Petro katika ibara tunayoijadili hapa katika somo letu: ni katika mioyo yetu na katika juhudi zetu binafsi kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo katika kukua kiroho, kuendelea kukua kiroho, na kuzaa matunda ya kiroho (matendo mema) ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele na wanawake (walio ndani au nje ya ndoa), na si mwonekano wa nje – na kanuni hii inatumika vile vile kwa wanaume wa Kikristo (walio ndani au nje ya ndoa). Kwani ni “katika mtu wenu wa moyoni” (1Pet. 3:4) ambamo vita halisi inapiganwa, na ushindi unapatikana tu “kwa njia ya upole na utulivu wa roho”. Hii ni namna ya Petro ya kufundisha kwamba mwonekano wa nje wa mwanamke wa Kikristo aliyepevuka [kiroho] kiuhalisia unaakisi mambo mema yanayoendelea ndani ya moyo wake kwa jinsi anavyochukua hatua za kuutumia ukweli wa Neno la Mungu katika mwenendo wake – mwenendo sahihi na stahiki wa kiroho ambao waumini wote wanapaswa kuuonyesha wakati wote (hii ikiwa ni kwa waume pia).

 

Vigezo [vya Kale] vya Kibiblia (aya za 5-6):

 

3.5 Kwa maana hivi ndivyo wanawake watakatifu wa zamani, walioweka tumaini lao kwa Mungu, walivvyojipamba, yaani kwa kuwatii waume zao,

3.6 kama vile Sarah alivyomtii Abrahamu, akimwita “bwana”. Nanyi mmekuwa watoto [halisi], ikiwa mtatenda yaliyo sahihi [na kwa nia njema] na si kwa sababu ya kuogopa kutishwa.

1Pet. 3:5-6

 

Petro alikuwa na mke (1Wakor. 9:5), na hapa tunaona kuwa alihisi kutakuwa na ukinzani dhidi ya mwongozo alioutoa kwa wanawake wa Kikristo waliokuwa ndani ya ndoa, katika aya nne zilizotangulia. Wanawake wa Kirumi katika zama zile walijulikana kwa mtazamo na mwenendo wa kupenda uhuru wao, tofauti na tabia za kuwabana wanawake katika ulimwengu ule wa kale kwa ujumla, jambo lililokuwa la kawaida wakati ule. Hivyo inaonekana hapa kwamba Petro hakuwa anajidanganya kuhusu jinsi mafundisho yake yatakavyopokelewa katika maeneo fulani ya ulimwengu ule wa kale, ingawa mafundisho yale yalikuwa yanatoka kwa Mungu mwenyewe. Pia aliongozwa [na Mungu] kufahamu kwamba utiifu aliokuwa anauamrisha kwa wanawake waliokuwa ndani ya ndoa ulipaswa kuwa halisi na utokane na utashi huru kabisa wa wanawake hao ili uwe na matokeo ya kuwaongoza waume zao wakamkumbatie Kristo kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine kumtukuza Kristo na kupelekea kwa watu wasioamini kuuona mwenendo wa kimungu wa wanawake wa Kikristo. Bila shaka ni kwa sababu hii Petro anaongozwa na Roho Mtakatifu kudhihirisha kwamba kutii huku si jambo jipya, bali ni mwenendo ambao wanawake waumini wamekuwa nao siku zote kuhusiana na waume zao.

 

Kwa kuwa hakuna mume aliye mtimilifu, hata wale waume bora kabisa wa Kikristo, vivyo hivyo Abrahamu hakuwa mume mtimilifu. Alifanya kosa la kutokiri kwa Farao kwamba Sarah alikuwa mke wake wakati ule aliposafiri kwenda Misri kwa sababu ya ukame uliokuwako kwao (Mwa. 12:13-20), na alirudia tena kosa hili baadaye kule Kanaani walipokutana na Abimeleki (Mwa. 20:2-18). Alilipokea kwa haraka sana pendekezo la Sarah la kupata mrithi kwa kufanya mahusiano na Hajira, mtumishi wa kike wa Sarah, pale Sarah mwenyewe alipokuwa hawezi kumpatia mrithi, na pia alimkubalia Sarah kwa haraka na urahisi sana kumfukuza Hajira na mwanaye mara baada ya Hagar kupata mimba (Mwa. 16:1-6), halafu akawa mzito sana (kimakosa) kumfukuza Hajira na mtoto wake Ishmaeli mara baada ya Isaka kuacha kunyonya (Mwa. 21:9:12).

 

Kama ambavyo hakuna mke mtimilifu, hata wale wake bora kabisa wa Kikristo, vivyo hivyo Sarah hakuwa mke mtimilifu. Inaonekana alifikiri kwamba Abrahamu alikuwa ndiye mwenye dosari ya ugumba pale alipompatia mtumwa wake (Hajira) ili Abrahamu apate mrithi, halafu kikatili kabisa akadai Hajira afukuzwe mara baada ya kupata mimba (Mwa. 16:1-6). Sarah pia alikuwa mzito sana kumtumainia Bwana pale alipopewa ahadi ya kupata mrithi kwa Abrahamu [mwaka unaofuata] (Mwa. 18:11-15).

 

Lakini katika masimulizi yote ya kitabu cha Mwanzo, tunamwona Abrahamu akiwa mume mwema na mwenye upendo kwa Sarah kwa ujumla, na pia tunamwona Sarah akiwa mke mwema na mtiifu. Na zaidi ya hayo tunaona katika matukio ya uhusiano wao kile Petro anachotufundisha akiwa katika Roho Mtakatifu kwamba ndicho kipeo sanifu / kiwango cha juu cha ndoa ya Kikristo: waume wanapaswa kuwapenda wake zao na kujiwajibisha kwao; wake wanapaswa kuwaheshimu na kuwatii waume zao. Na katika kitabu chote cha Agano la Kale, tunapoyatizama mahusiano kati ya waumini katika ndoa, tunaiona taswira hii hii ikijirudia, tena na tena: si utimilifu, bali (kwa pande zote mbili), bali upendo halisi na heshima.

 

Kutoka katika mtazamo wetu wa kisasa, na hasa ule wa nchi za magharibi, ni jambo maridhawa kuuliza kwa nini mwanamke yeyote wa Kikristo atakubali kujiweka mwenyewe chini (na ndani) ya uhusiano wa ndoa unaombana namna hiyo. Lakini hata mwanamume Mkristo anaweza kujiuliza swali hilo hilo, ikiwa matakwa ya Biblia yanaeleweka vile wafuasi wa Bwana wetu walivyoyaelewa, kwa wazi kabisa:

 

19.10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.

Matt. 19:10 SUV

 

Hivyo jambo la kwanza kusisitiza hapa ni kwamba kwa uhakika kabisa, ndoa si mahusiano yanayoamriwa na Biblia. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu aliiweka kwa ajili wa wanadamu wote, lakini ilifanya kazi kwa mwafaka kamili katika bustani ya Edeni pekee (na hata pale, kama sote tunavyofahamu, mwafaka huu haukudumu). Lakini kwa wote wanaoamua kuingia katika mahusiano ya ndoa, matakwa ya maandiko yako wazi kabisa: waume wanapaswa kuwapenda wake zao na waenende hivyo, wake wanapaswa kuwaheshimu waume zao na waenende hivyo kwa waume hao (Waefe. 5:33).

 

Tumejifunza mahala pengine kwamba katika mazingira ya namna hii, bila shauku [ya kibayolojia] juu ya waume zao na bila shauku ya kibayolojia ya kupata watoto waliyowekewa na Mungu kama sehemu ya laana waliyopewa pale bustanini, kuna shaka ya kutosha tu kama wanawake wengi wangetaka kuingia katika ndoa, kama ndoa ingekuwa ni suala la uamuzi / kuchagua1. Ni jambo la wazi kuona kwamba kuingia katika mahusiano ambamo unakuwa chini ya mamlaka ya mtu mwingine ni kikwazo tosha. Bila ya imani tuliyo nayo – inayotupatia ufahamu wa uzima wa milele – basi mtu anaweza kujiuliza ni kwa nini wale waumini wa kike wa kale hawakuingia katika hali ya kukata tamaa. Petro anaongozwa [na Roho] ili atufundishe hapa sababu ya wanawake wale kukubali kuolewa na hawakuingia katika kukata tamaa / kufa moyo ni kwamba walielekeza mioyo yao katika masuala ya kiroho, kwamba wanawake hawa wa kimungu waliweka matumaini yao katika mema yanayokuja: “wanawake wa kale walioweka tuamaini lao kwa Mungu”. Kwani

shabaha halisi ya Mkristo, kwa wanawake na wanaume, siyo kuboresha hadhi yetu au

 

1 Tizama/soma Bible Basics 3A: Biblical Anthropology, section IV.3, “The Judgement”.

mafanikio yetu au cheo au mali hapa duniani ambapo hakuna kinachodumu. Tuna tumaini

kuu zaidi, bora zaidi (Waebr. 7:19; ling. na War. 8:20-25; 15:4; Waga. 6:9; Waefe. 1:18; Wakol. 1:27; 1Wathess. 1:3; Waebr. 6:18-20; 11:6; 1Pet. 1:3-5): tunatazamia thawabu ya milele ambayo msingi wake ni jinsi tulvyoliitikia Neno, Bwana wetu Yesu Kristo, hapa

duniani. Kwani tunaitazamia ile kauli ya “umefanya vema” kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo (Matt. 25:23; Luka 19:17).

 

Sote tuko chini ya mamlaka katika maisha yetu hapa duniani – na Wakristo wote wako chini ya mamlaka ya Bwana Yesu Kristo. Kuwa na watu wengine chini ya mamlaka yetu, kama ni mke kuwa chini ya mamlaka ya mume wake, kundi la waumini kuwa chini ya mamlaka ya mchungaji-mwalimu, au kuwa katika nafasi yoyote ambayo inahusisha kuwa na mamlaka juu ya watu au mtu mwingine, inaweza kudhaniwa au kufikiriwa na wale walio nje ya mahusiano hayo kuwa ni hali ya faida kubwa, lakini kwa uhakika nafasi yoyote yenye mamlaka inahusisha majukumu makubwa … ikiwa itachukuliwa kimungu. Kama tunavyojua kutokana na mjadala wetu wa siku za nyuma wa mahusiano mengine yanayohusisha mamlaka ya mtu mmoja juu ya mtu mwingine / watu wengine (katika masomo mengine ya mfululizo huu), lengo la mamlaka yote yanayotoka kwa Mungu katika mahusiano yote ni kuunda mfumo wenye utaratibu na uhuru wa kutosha ili kufanikisha wokovu na kisha makuzi ya kiroho. Hali ni hiyo hiyo katika uhusiano wa ndoa na mahusiano ya familia. Kwani bila ya amani na utaratibu mzuri katika mahusiano, hakuna mwanafamilia anayeweza kufanya maendeleo ya maana yakiroho, si mume, si mke, si mtoto. Hivyo basi, kila muumini katika Bwana Yesu Kristo, anapaswa kupuuza shauku binafsi na malengo binafsi na badala yake kuelekeza macho yake katika taswira na maslahi mapana zaidi, yaani ujenzi wa ufahamu na maadili ya Kanisa la Bwana Yesu Kristo.

 

Akimwita “Bwana”: Ule mfano wa kukubali mamlaka ya mume ambao Petro anatupatia hapa unatufunulia jambo muhimu hapa. Sarah alimwonyesha Abrahamu kiasi kukubwa cha heshima ya wazi kabisa kwa kumpa hadhi hii bila ya kulazimishwa. Tunaweza kuona hapa kwamba kuonyesha heshima ya wazi namna hii, wakati kuna gharama ndogo sana lakini kuna faida nyingi, haswa katika uhusiano wa mke anayeamini na mume asiyeamini. Hapa tunaona kwamba hakuna kulazimisha kwa nguvu [za kimwili] wala unyonyaji / uonevu wala madai yoyote kwa upande wa Abrahamu. Badala yake, onyesho hili la heshima linamdhihirisha mume kuwa ndiye mwenye mamlaka bila kupunguza hadhi ya mke wake kwa namna yoyote ile – isipokuwa katika mahusiano ambamo kuna kiburi katika upande mmoja au pande zote mbili, jambo ambalo sote tunapaswa kulikataa.

 

Si kwa Sababu ya Kuogopa Kutishwa: Jambo hili ni muhimu sana kulielewa. Mke Mkristo hajapewa maelekezo ya kutii matakwa yasiyo ya haki ya mume dikteta kwa sababu ya kutishwa. Kwa hakika onyo hili linatueleza mahususi kutotii madai yasiyo ya kimungu, haswa kufanya jambo / tendo lolote lisilo sahihi, au kutofanya jambo lililo sahihi (kama sala na kujifunza Biblia) ambalo Bwana wetu ameamuru mahususi tuyafanye. Zaidi ya hapo, mambo yote mema anayoyafanya kwa ajili ya mume wake, ikiwa ni pamoja na kuonyesha kiasi stahiki cha heshima kinachotokana na hadhi yake ya mamlaka, yanapaswa kutoka katika motisha sahihi, yaani ya kutafuta utukufu wa Bwana Yesu Kristo na kuifanya imani yetu ionekane ya kuvutia na inayofaa kabisa kwa sababu ya matendo mema ya mke huyu.

 

Ukristo si itikadi isiyo na kanuni inayowapa wake visingizio vya kuwavunjia heshima waume zao – kama ambavyo Ukristo haumpi Mkristo kisingizio cha kutotii mamlaka yoyote halali (tizama Petro #34). Lakini pia imani yetu hii haihalalishi kuwakabidhi waume haki ya kuwatendea wake zao [vyovyote] wanavyotaka bila haki wala maslahi ya kiroho ya wake hao – kama ambavyo haihalalishi Mkristo yeyote kutendewa isivyo haki pale anapokuwa mikononi mwa waajiri au mamlaka za kiserikali. Katika taswira inayojitokeza hapa, tukiongeza wajibu wa mume Mkristo wa kumpenda na kumjali mke wake – na usimamizi na ulinzi wa Mungu wa wale wote ambao wako chini ya mamlaka yaliyo makubwa kuliko uwezo wao – tunaona kwamba mbali kabisa na taswira ya ukatili na upendeleo kwa wanaume ambao wapinzani wa Biblia wanataka kuionyesha, tunachokiona hapa badala yake ni msingi bora kabisa wa ndoa yenye furaha, mwafaka na mafanikio (siyo lazima yawe mafanikio ya mali!), ambamo waume na wake zao wanatimiza wajibu wao kila mmoja kwa mwenzake katika mazingira ya upendo na heshima, na ambamo maslahi ya kiroho ndiyo yanayopewa kipaumbele, zaidi ya maslahi ya kimwili.

 

Wajibu wa Mume Mkristo katika Ndoa (aya ya 7):

 

3.7 Kadhalika ninyi wanaume, kaeni na wake zenu kwa akili inayotokana na ufahamu wa Biblia (yaani kutokana na kile Biblia inachofundisha kwa maneno na mifano, ya jinsi ya kuishi na mkeo), mkienenda juu yao kama inavyostahili kuenenda kwa mtu aliye dhaifu (“chombo lilicho dhaifu”) kuliko ninyi [ambavyo ndivyo wanawake walivyo – dhaifu]. [Ninyi wanaume] mnapaswa kuonyesha heshima stahiki kwa wake zenu ambao ni warithi wenzenu wa neema ya uzima wa milele, ili sala zenu zisipate ukinzani (yani sala zenu zisitatanishwe na dhambi – ambayo ni matokeo ya kutowaheshimu wake zenu).

1Petro 3:7

 

Kwanza kabisa, ingawa hapa tunayo aya moja tu inayozungumzia waume (tofauti na aya sita zanazowazungumzia wake), mzigo wote wa uwajibikaji unawekwa katika mabega ya mume. Wake, kama tulivyoona, wanatakiwa kufuata uongozi wa waume zao (na katika maandiko, muda na nafasi nyingi imetumika katika kueleza umuhimu na namna ya [mke] kufanya hivyo), lakini waume wanaamriwa kufahamu (hivyo wanapaswa kujifunza) yale yaliyo muhimu ili wawe waume wema kwa wake zao na pia kuufuatilia wajibu huu katika kuwatunza wake hao sawasawa. Na kama watashindwa katika wajibu wao huo (ukinzani kwa sala zao [waume hao] ukiwa ndiyo kipimo cha kushindwa huko), waume, kama tunavyoona katika aya ya saba, ndio wanaowajibika katika kushindwa huko, na siyo wake zao.

 

Tunaweza kujifunza kitu kimoja [kingine] pia kutoka katika ibara hii kwamba mwanaume Mkristo hapaswi [hata] kufikiria kuoa kabla hajafikia kiwango cha kupevuka kiroho. Kwa kuwa yeye (mwanaume) ndiye atakayewajibika “kufahamu” namna sahihi ya kuenenda katika ndoa ili aweze kumpa mke wake heshima stahiki na wakati huo huo aiongoze ndoa hiyo katika namna sahihi ya kibiblia, kufahamu sawia kila kitu ambacho Biblia inafundisha kuhusu ndoa, familia na namna sahihi ya Kikristo ya kutembea hapa duniani ni sharti la kwanza la kuwa na ndoa yenye mafanikio. Zaidi ya hapo, mbali na “kujua” tu kilicho sahihi kufanya katika nyanja hizi zote, ni muhimu sana kuwa na kiasi cha kutosha cha kweli ya Biblia ndani ya moyo ili kulitimiza agizo hili muhimu. Na mwisho, kujua nini cha kufanya, na kuwa na kiasi cha kutosha cha “rasilimali” ya kiroho cha kukuwezesha kutimiza kila unachotakiwa kufanya, ni utangulizi tu katika kutimiza yaliyo sahihi kwa namna ya kimungu. Kushindikana kwa ndoa hii ya Wakristo wawili hawa, iwe kwa muda tu au moja kwa moja, kunawajibishwa [na maandiko] kwa mume.

 

Chombo Dhaifu [Zaidi]: Msemo huu, “… chombo …” unatoka kwenye tafsiri ya Kiingereza ya KJV. Neno “chombo” pia linatumika kuielezea miili ya wanaume na Paulo katika 1Wathess. 4:4, hivyo tofauti kati ya wanaume na wanawake ipo katika neno “dhaifu” pekee. Ukiwalinganisha mwanamke wa kawaida na wanaume wa kawaida, unaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba wanawake si dhaifu kiakili wala katika uwezo wa kufikiri. Ni kweli pia kwamba mwanaume wa kawaida ni mwenye mwili mkubwa na mwenye nguvu nyingi zaidi ya mwanamke wa kawaida (ambayo ndiyo sababu ya tofauti halali kabisa katika michezo ya wanaume na wakawake). Lakini Petro haizungumzii tofauti hii hapa, kati ya wanawake na wanaume. Wanawake, kulingana na ufahamu wa kawaida, mara nyingi wanaelezwa kuwa ni viumbe wanaotawaliwa (kwa maana ya kuendeshwa) na hisia zao zaidi ya wanaume. Lakini wanaume wana hisia pia, nao hutawaliwa (kwa maana ya kuendeshwa) na hisia zao, na mtu yeyote aliye na kiasi cha kutosha cha uzoefu wa maisha anapaswa kufahamu kwamba wanawake wana uwezo mkubwa wa kuhimili / kuvumilia magumu. Hivyo, wakati wanawake na wanaume wanatofautiana katika namna wanavyochakata (process) na wanavyoonyesha hisia zao, huu si udhaifu per se, na wala maandiko hayaufasili kama udhaifu.

 

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Mwa. 3:1-6 SUV

 

Tumekwishajadili ibara hii katika somo jingine2. Hata hivyo, hapa tutaeleza kwa muhtasari kama ifuatavyo: Eva aliumbwa kwa ajili ya Adamu, awe mwenza mtimilifu kwake. Eva aliumbwa ili aitikie miito na maelekezo yake, ili awe “msaidizi” aliyehitajika na Adamu katika kila namna, kimwili na kihisia. Eva aliingia matatani alipoanza kusikiliza – na kuitikia wito wa kiumbe mwingine ambaye hakuwajibishwa naye na ambaye hakujali maslahi yake na badala yake alikuwa mnafiki tu moyoni mwake. Eva hakuutambua udanganyifu huu, na hii ndiyo ilisababisha kuanguka kwake. Lakini ingwa alikuwa na hatia, hakuwajibika [na kosa lile] katika namna ile ile kama Adamu alivyowajibika. Adamu alijua

 

2 Tizama Bible Basics 3A: Biblical Anthropology, section IV.1, “The Temptation”.

fika kile alichokuwa anakifanya, kwani alichagua kuishi na Eva nje ya bustani badala ya kuishi na Mungu ndani ya bustani, na hiyo ndiyo ilikuwa tofauti kati yao.

 

13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya (_laghai, _hadaa, _ghilibu), nikala.

Mwa. 3:13 SUV

 

11.3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya (_laghai, _hadaa, _ghilibu) Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu [pia], mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

2Wakor. 11:3 SUV

 

2.13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.

2.14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.

1Tim. 2:13-14 SUV

 

Kama ambavyo aya hizi zote tatu zinavyoweka bayana, uwezekano wa kudanganyika ndiyo kipengele muhimu hapa. Wanawake hutenda dhambi. Wanaume hutenda dhambi. Lakini wanawake, hata wale wenye akili sana, wenye vipaji vikubwa, wenye uvumilivu wa kiwango cha juu na wenye uwezo mkubwa, wana udhaifu mkubwa kwa udanganyifu kuliko ilivyo kwa wanaume. Hii inatokana na jinsi Mungu alivyowaumba, kwamba wana tabia ya kuitikia (wao ni responders). Na ikiwa yule mwanamke mtimilifu, aliyekuwa na mume mtimilifu, wote wawili wakiishi katika mazingira timilifu aliweza kuhadaiwa na yule mwovu, je hali ikoje kwa mwanamke aliye na hulka ya dhambi katika ulimwengu huu unaoendeshwa na yule Shetani? Hii ndiyo sababu wanaume wanawekwa na Mungu katika nafasi ya uongozi ndani ya ndoa – si kwa sababu Bwana amewaona wana thamani zaidi, hata kidogo. Bali ni kwa sababu katika mazingira ya ndani ya moyo na ya nje yanayolingana (yaani wote wawili, mume na mke wakiwa na kiasi sawa cha upevu wa kiroho), basi mume ana uwezekano mdogo zaidi wa kuhadaiwa katika kufanya maamuzi lukuki ambayo yana ulazima wa kufanywa ndani ya ndoa. Mume mwenye busara atatambua kwamba mke wake anaweza kuwa na umaizi, akili (uwezo wa kufikiri) na mtazamo ambao yeye mwenyewe hana. Na atamsikiliza kwa ukamilifu katika kila jambo linalotakiwa kufanyiwa maamuzi. Lakini waume wote Wakristo wanapaswa kutosahau kwamba wajibu wa matokeo ya maamuzi yote muhimu ni wa kwao pekee. Na hii ndiyo maana mamlaka katika ndoa wamepewa wao.

 

Mnapaswa Kuonyesha Heshima Stahiki [kwa Wake Zenu]: Suala la kuonyesha heshima stahiki kwa wake zao ni amri ambayo waume Wakristo wanapaswa kuitii, wakikumbuka wakati wote kwamba wake zao hao ni “warithi wenzao wa neema ya uzima wa milele”. Kwa maneno mengine, sisi waumini wote tuko upande mmoja. Sote tuna dhima (wajibu) tofauti katika maisha (na sote tuna dhima tofauti ndani ya ndoa), na sote tuna karama tofauti za kiroho na utumishi tofauti katika Kanisa. Lakini sote tuko sawa ndani ya Mwili wa Kristo, na hakuna hata mmoja wetu mwenye thamani zaidi au umuhimu zaidi ya mwingine kwa Bwana Yesu Kristo.3 Ukweli kwamba dhima zetu ni tofauti ndani ya Mwili wa Kristo haumfanyi Mkristo yeyote kati yetu kuwa na thamani ndogo kuliko mwingine – kama

 

3 Tizama: Bible Basics 6B: Ecclesiology, section I.A.3, “The Body and the Head”.

ambavyo miguu ni muhimu, kama ambavyo macho ni muhimu, katika kufanya kazi kwa

mwili mzima (1Wakor. 12:14-27). Na ukweli kwamba dhima / wajibu wetu katika ndoa ni tofauti vivyo hivyo haupunguzi thamani ya Mkristo yeyote mbele za macho ya Bwana wetu, awe mwanamke au mwanaume, mke au mume, kwa sababu ndoa haifasili maisha yetu hapa katika ulimwengu huu usiodumu; kwa hakika ni uhusiano wetu na Bwana Yesu ndio ulio na umuhimu.

 

3.28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.

Waga. 3:28 SUV

 

Kama ilivyo katika amri nyingine zinazotolewa katika Biblia kuhusiana na mamlaka ndani ya mahusiano, shabaha ya maelekezo ndani ya ndoa siyo kutoa nguvu na mamlaka kwa kundi moja na kuliacha kundi lingine – kwa hakika wale wanaotaka kupata thawabu za juu kabisa katika Kanisa wanapaswa kuwa watumishi wa wote (kw. mf. Matt. 20:26; 23:11). Kwa hakika, shabaha ya kumweka mume katika nafasi ya mamlaka ndani ya ndoa ni kuendeleza na kufanikisha mpango wa Mungu kwa wote, mke na mume. Na katika kufanikisha lengo hili, wanaume wanawajibishwa kuwa na kiwango cha hali ya juu cha mwenendo na wamefanywa wawajibibike katika mafanikio (au la) ya ndoa zao.

 

5.25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa [hata kufa] kwa ajili yake;

Waefe. 5:25 SUV

 

Aya hii inatupatia kwa kifupi sana na kwa namna ya kipekee na ya nguvu kabisa wajibu wa mume kwa mke wake. Hakuna kiwango cha juu zaidi cha upendo kuliko kile cha Kristo anavyompenda Mke wake, sisi Kanisa lake, na waume wanapaswa kuelewa kwamba hicho ndicho kiwango wanachopaswa kukinakili / kukifuata. Hivyo basi mwanaume yeyote anayefikiria kuingia katika ndoa anapaswa kuweka moyoni kiwango hiki cha kujitoa mhanga kabla ya kuingia katika ndoa hiyo – na kwa sababu mwisho wa yote sisi sote tunawajibika katika matendo yetu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana aliyetupenda sana, hata akaja hapa duniani kwa ajili yetu na akafa kwa ajili yetu. Utayari huo huo wa kutoa sadaka kila kitu kwa ajili ya mke ndicho kiwango ambacho kila mume anawajibishwa nacho – na Bwana Mwenyewe.

 

II. Ibara ya Pili (aya za 8-17)

 

3.8 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu (wenye moyo mpole), wanyenyekevu;

3.9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu (kashfa kwa kashfa); bali wenye kubariki [wenzake]; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili [nanyi] mrithi baraka.

3.10 Kwa maana imeandikwa (Zab. 34:12-16), “Atakaye kupenda maisha [yake], Na [mwenye shauku ya] kuona mema katika siku zake za usoni, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila (hadaa).

3.11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.

3.12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki [kwa ajili ya kuwatendea mema], Na masikio Yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko dhidi ya watenda mabaya”.

3.13 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?

3.14 Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, mna heri. “Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike” (Isa. 8:12).

3.15 Bali mnyanyueni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu [juu ya vyote vingine]. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye sababu ya tumaini lililo ndani yenu;

3.16 lakini kwa upole na kwa heshima, mkifanya hivyo kwa dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao (wanaoukashifu) mwenendo wenu mwema katika Kristo.

3.17 Maana ni afadhali kuteswa [katika mikono ya wasioamini] kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko [kuteswa] kwa kutenda mabaya.

1Pet. 3:8-17

 

Baada ya kumaliza mafundisho yake kuhusu mahusiano kwa ujumla (1Pet. 2:13-17) na kuhusu utumwa / ajira (1Pet. 2:18-25) na haswa ndoa (1Pet. 3:1-7) Petro hapa anarudi kwenye mjadala wa mwenendo sahihi wa Kikristo wakati Mkristo huyo anapokuwa chini ya shinikizo, anapotendewa mabaya / maovu, na anapoteswa (yaliyoanza katika 1Pet. 2:11-12). Nyingi kati ya istilahi (terms) na amri zinazotolewa hapo juu zinafanana (yani ni visawe) na zinaingiliana katika namna mbalimbali. Lakini ikiwa mafundisho yangu haya yanaonyesha kujirudia-rudia kwa kiasi fulani, mimi nasema hivi: marudio ndiyo moyo wa ufundishaji / ualimu mzuri, kama ambavyo mwalimu yeyote anayeijua kazi yake vyema atajaribu tena na tena kuwafundisha wanafunzi wake kwa njia na mitazamo tofauti mpaka mwanga wa ufahamu utakapoangaza mioyoni mwao. Na hakuna mwalimu mzuri zaidi ya Roho Mtakatifu.

 

Muwe na Nia Moja: Mtume Petro anatusihi kwa njia hii muhimu na inayoonekana mara nyingi katika Agano Jipya (kw. mf. Yoh. 17:11; 17:20-23; War. 12:16; 15:5-6; 1Wakor. 1:10-17; 2Wakor. 13:11; Waefe. 4:3; Wafi. 2:2; 4:2), lakini fundisho hili mara nyingi linaeleweka vibaya.4 Hapa, Petro anamaanisha umoja wa Wakristo, kwa hakika, lakini umoja halisi wa Wakristo unapatikana siyo katika kuonyesha umoja wa nje / wa sura au uekumeni (kama ule unaopigiwa kifua na taasisi ya Wakatoliki). Umoja halisi wa Wakristo / Kikristo – ambao Kristo anataka tuwe nao – una msingi wake katika kweli. Ni pale tu waumini wanaposimama pamoja na imara katika kweli ya Neno la Mungu, wakijifunza, wakiielewa, wakiiamini na wakiitumia kweli hiyo, kweli pekee, katika maisha yao, ndipo kati yao patakuwa na umoja unaotosheleza kuleta “nia moja”, shabaha yake (umoja huo) ndiyo ambayo Petro anatufundisha hapa, akiandika katika uweza wa Roho Mtakatifu. Ni pale tu waumini wote tutakapoyaona masuala yote kwa mtazamo mmoja – kwa sababu sote tunaielewa kweli kwa utumilifu na tunaitumia kweli hiyo katika kila hali tunayokutana nayo, kwa pamoja na kila mmoja pekee, ndipo patakuwa na umoja unaofundishwa na Biblia.

 

Kwa upande mwingine, “umoja” ambao makundi ya ki-ekumeni ya kisasa yanaueneza

 

4 Tizama Bible Basics 6B: Ecclesiology, section II.C.3.f, “Christian Unity”.

unapatikana kwa gharama ya kuupoteza ukweli. Ukweli unatuunganisha – ukiwaleta pamoja wote wanaoukubali. Ukweli unatutenganisha pia – ukiwakataa na kuwatenga wote wanaoukataa. Waumini wamepewa jukumu la kuweka kando kanuni au mafundisho na malumbano juu ya kanuni hizo yasiyo na umuhimu, ikiwa malumbano hayo yana gharama ya kuuvunja umoja wao, lakini pia [waumini] wamepewa jukumu la kuwaweka kando na kuwaondoa [kutoka] katika ushirika wao wale wote wanaoukataa ukweli ikiwa kuukataa kwao ukweli kunasababisha mfarakano (1Wakor. 5:11; 2Wathess. 3:6; 3:14-15; 2Yoh. 1:9-11; ling. na 1Tim. 4:1; 2Tim. 3:1-5). Ni katika “umoja wa imani na kumfahamu sana (kwa kiwango cha juu) mwana wa Mungu” (Waefe. 4:13) pekee – imani inayookoa katika Bwana Yesu Kristo, nafsi Yake halisi, mtu na Mungu, na kazi Yake msalabani ambapo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu – hii ndiyo “inayotuunganisha”. Tunapoutatanisha na kuutia maji ukweli huu wa msingi kabisa wa imani yetu tutakuwa tunacheza na uasi.

 

4.11 Naye (Kristo mwenyewe) alitoa (aliwateua) wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

4.12 kwa kusudi la kuwakamilisha (kuwatayarisha) watakatifu [wote], hata kazi [yao] ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo (Kanisa Lake) ujengwe;

4.13 hata na sisi sote tutakapofikia [lengo la] umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata [kila mmoja wetu] kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo (kiwango cha kupevuka ambacho kipimo chake ni Kristo);

4.14 ili tusiwe tena watoto wachanga [katika kuelewa kanuni za Biblia], tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu,

15. bali tuweze, kwa kuipokea kweli katika upendo, kukua katika nyanja zote, tukimtazama Kristo, aliye kichwa cha Kanisa, kama mfano wetu.

16. Kwa namna hii, mwili wote (Kanisa zima), ukiungamanishwa na kushikamanishwa kwa uweza wake Kristo kwa njia ya viungo Anavyovitoa [kwa nguvu kuu] ili viunganishe kila sehemu, unafanikisha kukua kwake na kujijenga wenyewe katika upendo.

Waefe. 4:11-16

 

Wenye Kuhurumiana: Neno la Kiyunani linalotumika hapa ni neno ambatani lenye maana ya “kuteseka pamoja”. Kwa hiyo, maana hii ni sambamba na neno lililonyumbulishwa kutoka katika Kilatini linalotumiwa katika tafsiri mbalimbali za Kiingereza: “compassionate” (maana yake – enye huruma). Kwa wazi kabisa, ukijikata kidole, yawezekana mimi “nikajisikia vibaya” kwa sababu ya maumivu yako, lakini ni wewe mwenyewe tu utakayejua fika maumivu yanayosababishwa na kidole chako kilichoumia. Lakini badala ya kutojali maumivu na matatizo ya ndugu zetu (kama ambavyo mara nyingi ulimwengu unafanya unapoona mateso ya wengine), au kuonyesha “huruma ya uwongo” bila ya kuwa na hisia halisi za moyoni au kuchukua hatua chanya za kusaidia (kama ambavyo ulimwengu mara nyingi unafanya katika “kuonyesha wema”), waumini wanaaswa hapa kujali kutoka moyoni pale ndugu zao wanapokuwa katika shida – na angalau watoe msaada wowote unaofaa wanaoweza kuutoa, pamoja na ushauri wa kimungu. Ukijikata kidole chako naweza kukupatia bandeji. Ukimpoteza mtu unayempenda (kifo), siwezi “kulisahihisha” jambo hilo, lakini ninaweza kukusikiliza katika maumivu yako na kukupa maneno ya faraja ambayo Roho Mtakatifu ananifundisha katika utumishi wangu kwako.

 

12.15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

War. 12:15 SUV

 

Wenye Kupendana Kama Ndugu: Amri nyingi kati ya hizi zilizomo katika ibara hii (1Pet. 3:8-17) zinaweza kutumiwa na wasioamini pamoja na wanaoamini, yani Wakristo. Hii ni kusema, tunapaswa kuwa wenye kuhurumiana, wenye moyo mpole, na wanyenyekevu kwa watu wote. Lakini neno ambalo hapa limetafsiriwa “wenye kupendana kama ndugu / wenye kuwapenda ndugu” (Kiyunani philadelphos; ling. na Philadelphia, mji ulioko leo katika nchi ya USA – “the [putative] city of brotherly love”), linatumika mahususi kwa mwenendo wetu kwa waumini wenzetu katika Bwana Yesu Kristo. Wakati ni kweli kwamba maneno na makundi ya maneno katika Kiyunani ambayo msingi wake ni philia na agape ni visawe kwa ujumla, neno philia mara nyingi linatumika katika uhusiano au upendo wa karibu sana wa moyoni, kw. mf. upendo wa kijana wa kiume kwa rafiki yake wa karibu sana, na neno agape linatumika katika uhusiano au upendo ambao si wa karibu sana – kwa mfano upendo wa mwalimu kwa wanafunzi wake. Hii ni kusema, tunapaswa kumpenda kila mtu kwa upendo unaovumilia / unaostahamili (agape), lakini waumini / Wakristo wenzetu tunapaswa kuwapenda kwa ukaribu zaidi inavyowezekana: tunawaenzi ndugu zetu katika Bwana katika namna mahususi, kwa sababu sisi sote ni sehemu ya Mwili mmoja, Kanisa moja.

 

Je, muumini afanye nini katika mazingira haya? Kwanza, hii haimaanishi tuache kuutazama mwenendo wa waumini wenzetu na kuutathmini (ndugu zetu waliopotea njia tunapaswa kuwaepuka: 1Wakor. 5:11); na hii haimaanishi kwamba tuna ulazima wa kushirikiana na watu wengine kwa sababu tu wao ni waumini kama sisi (wenzetu). Lakini inamaanisha kwamba, wakati katika suala la wasioamini jambo la kwanza linalotuhusu ni wokovu wao (kwa kuwa hata ukimsaidia au kumjali kwa kiasi gani mtu asiyeamini, yaani asiye Mkristo mwenzako, hilo halina faida yoyote ikiwa matokeo yake ataendelea na kutoamini kwake), tuna shauku kubwa ya kutaka kuwaona waumini wenzetu katika Kristo wakiongeza juhudi zao katika kukua kiroho, kuendelea kukua [kiroho], na kuzaa matunda ya kiroho kwa kiasi kikubwa inavyowezekana. Njia kuu na sahihi ya kufanikisha hili ni kwa kuwatumikia ndugu zetu hao kwa matumizi ya vipaji / karama na huduma tulizopewa na Bwana. Pia sote tumeagizwa kuwasaidia ndugu zetu katika mahitaji yao ya kimwili ikiwa watajikuta katika uhaba na magumu ya maisha, na ikiwa tunayo fursa ya kufanya hivyo (1Tim. 6:18; Waebr. 13:16; ling. na Yakobo 2:15-16). Kwa maneno mengine, badala ya kuwa wavumilivu, wastahamilivu na wasiotaka kuwadhuru na kuwaudhi watu wasioamini (na wakati huo huo tukiwa na shauku ya kuwaongoza waelekee kwa Kristo ikiwa wanaonyesha nia), sisi tunatafuta njia za kuwasaidia ndugu zetu katika Kristo, katika mahitaji yao ya kimwili na zaidi ya hapo, katika mahitaji yao ya kiroho. Hivyo tuna motisha ya kutosha ya kujibidiisha katika kukua kiroho na kuendelea [kiroho] sisi wenyewe, kwani ni kwa njia hiyo ndiyo tutaweza kuwatumikia kwa ufanisi, kama ambavyo tunatakiwa.

 

Wenye Moyo Mpole: Kivumishi hiki kinatokana na neno la Kiyunani splagchnon, ambalo hutafsiriwa kama “bowels” au “tumbo/mtima” katika tafsiri ya zamani ya KJV, na kielezi eu maana yake “safi” au “mwema” au “nzuri” (linganisha na neno euphonic – enye sauti nzuri). Hizo splagchna kiuhalisia ni viungo vyote vilivyo ndani ya torso – juu ya kiuno na chini ya shingo – na hivyo neno hili linahusiana na hisia mbalimbali zinazotoka katika mwili wa mwanadamu. Wakati katika ulimwengu wetu wa sasa, fikra na hata hisia zinachukuliwa kwamba ziko “kichwani”, katika enzi za kale viungo mbalimbali vya mwili vilidhaniwa kuwa ndivyo vyanzo vya hasira, upendo, hisia kali, wivu, woga, n.k. Bado tumebaki na dhana hii katika neno “moyo”, na tunaendelea kulitumia [neno moyo] katika maana hiyo, ingawa hatuoni ulazima wa kuuona moyo kama kiungo cha mwili ambacho ndicho chanzo cha fikra au hisia.

 

Kuwa na “moyo mwema” au “moyo mzuri” katika muktadha wetu wa kibiblia inamaanisha kwamba hisia za mtu zinauitikia ukweli katika njia / namna chanya. Inamaanisha kuwa na motisha chanya na halisi katika matendo na maamuzi tunayochukua. Wakristo waliopevuka kiroho wana nia mioyoni mwao ya kutenda mema na yaliyo sahihi, haswa kuhusiana na maslahi / usitawi wa wengine, wakiwa na shauku ya kuwaona wakiokolewa na wakikua kiroho, na mengine yote mema yanayoendana na hayo. Wakristo waliopevuka kiroho si watimilifu, lakini badala ya [wao] kutawaliwa na hisia zao na kuathiriwa na hisia hizo katika namna hasi na zinazoleta madhara, mara nyingi hisia zao hufuata mwelekeo wa ile kweli iliyo ndani yao, hivyo wanakuwa na motisha ya kutenda mazuri na sahihi katika mazingira yote, wakitupilia mbali yote yaliyo hasi, ya kibinafsi, ya hasira, ya uchungu, yanayofurahia mateso ya wengine, na mengine yanayofanana na hayo, na badala yake wakienenda katika upendo, subira, na upole kwa wote.

 

2.1 Basi ikiwako faraja yo yote katika [umoja wenu na] Kristo, ikiwamo faraja yo yote katika mapenzi Yake, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema,

2.2 ijalizeni (ikamilisheni) furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja

Wafi. 2:1-2

 

3.12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo mpole na wenye huruma, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

Wakol. 3:12

 

Wanyenyekevu: Unyenyekevu halisi [wa kibiblia] hauhusiani kabisa na mwenendo wa kujitweza (kujifanya mnyonge), mwenendo wa kujishusha [kupita kiasi]. Kuwa mnyenyekevu katika maana ya kibiblia hakumaanishi kujifikiria mwenyewe kwa kiburi na kujali mwonekano wako tu. Badala ya kuelekezwa katika nafsi pekee, unyenyekevu halisi wa kibiblia unaelekezwa kwa wengine, ukimtazama Mungu na kujali maslahi / ustawi wa Wakristo wengine badala ya kujijali mwenyewe na jinsi unavyoonekana na wengine.

 

3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.

Hesabu 12:3 SUV

 

Aya hii inashangaza – kwa wale wote ambao hawajaielewa [bado] fasili ya kweli ya unyenyekevu wa kibiblia. Hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kuwa mnyenyekevu zaidi ya Musa – isipokuwa Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini pia hakuna mmoja kati ya hao wawili ambaye inaweza kusemwa [juu yake] kwamba alikosa kujiamini, au alionyesha / alidhihirisha kutokuwa na thamani. Kiburi hujichukulia na kudai kujiamini katika mambo ambayo hakiwezi kuyafanya, huonyesha thamani ambayo kiuhalisia hakina. Unyenyekevu halisi hauna majisifu, hii ni kweli, lakini pia hauna tabia ya kukataa kilicho cha kweli – au kujifanya kama vile kilicho cha kweli si cha kweli, kwa sababu tu ya kuogopa vile watu wengine watakavyofikiria (ling. na Yoh. 8:55). Musa (pamoja na Bwana wetu) hata kidogo hakuwa mzito kuyatumia madaraka aliyopewa kwa kujiamini kabisa, lakini [pia] bila ya kuwa na ubinafsi wowote – kwa faida ya wale wote aliokabidhiwa kuwaongoza. Hakufanya majisifu katika mamlaka aliyopewa, na hakuyatumia vibaya, wala kwa ubaya, [mamlaka hayo], lakini aliyatumia mamlaka aliyopewa kwa kujiamini kwani yeye mwenyewe alikuwa ni mtu anayejiamini.

 

12.3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie (asiwe na nia ya kutaka ) makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.

War. 12:3

 

Unyenyekevu ni kuyaona mambo kama yalivyo. Kiburi hupotosha ukweli [huu]. Kiburi huenenda kinyume na hivyo, kinayaona mambo tofauti na vile yalivyo. Kwa waumini wanaotembea kwa ukaribu kabisa na Bwana wetu, shabaha yetu huwa wazi wakati wote: tuko hapa duniani kwa ajili ya kupigana vita ambayo Bwana wetu ametutuma tupigane. Tunapoiweka shabaha hii moyoni mwetu wakati wote ndipo tunapoonyesha / tunapodhihirisha kwamba tunayaona mambo vile yalivyo – na ndivyo tunavyodhihirisha unyenyekevu wetu wa kibiblia. Haijalishi watu wengine wanatufikiria namna gani katika mioyo yao. Hatutafuti kujikweza mbele za macho ya wengine, tukiunda taswira bandia ya jinsi tulivyo. Na wala hatutafuti kujitweza mbele za macho ya wengine – kwani hili nalo linapotosha ukweli. Badala yake, hatujali kabisa nafsi zetu (kwani huu ni ubinafsi); bali tunayaelekeza kwa kiasi kikubwa inavyowezekana macho kwa Bwana Yesu Kristo na yale anayoyataka. Hivyo ufunguo wa unyenyekevu halisi wa kibiblia ni kumilikiwa na Bwana wetu Yesu Kristo, na siyo kumilikiwa na matakwa yetu au jinsi watu wengine wanavyotufikiria.

 

11.24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;

11.25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;

11.26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake [kwa ajili ya] Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo [yake ya milele].

11.27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye Yeye asiyeonekana.

Waebr. 11:24-27

 

Watu Wasiolipa Baya kwa Baya, au Shutuma kwa Shutuma: Baada ya kutupatia kwa utondoti mkubwa mwongozo wa nini tunapaswa kufikiria, Petro sasa anatupatia mipaka inayozinga pande zote mbili za barabara tunayopita, na katika kufanya hivyo anamulika na kutuonyesha maana halisi ya orodha ya mwenendo chanya aliotupatia hapo mwanzo. Tunapaswa kuweka akilini, hata hivyo, kwamba tabia chanya zinazotajwa hapa juu, yaani umoja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wenye moyo mpole, na wanyenyekevu, yote ni mienendo ambayo matokeo yake ni matendo ya kimungu. Kuhusiana na upande wa pili ambao ni tabia hasi, Petro hazungumzii kwa undani zile fikra potofu ambazo matokeo yake ni visasi vya maneno na matendo, lakini anatudhihirishia badala yake matokeo hasi ya kutokuwa na fikra chanya za kimungu alizotufundisha tuwe nazo. Tunaposhindwa kuelekeza fikra zetu katika umoja, kuhurumiana, kupendana kama ndugu, kuwa na moyo mpole, unyenyekevu, na mwenendo unaofanana na huo katika Roho Mtakatifu (Waga. 5:13-26), kutapelekea kwenye hali ya sisi kuwa dhaifu katika kujizuia na lugha chafu na matendo yasiyofaa wakati tunapokuwa chini ya shinikizo la ghafla.

 

Wakati kurudisha kisasi kwa maneno au kwa matendo ni jambo / mwenendo unaotokana na hulka yetu ya dhambi, kwa hakika huu ndio mwenendo tunaosisitizwa mahususi kujitenga nao.

 

7.12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Matt. 7:12 SUV

 

6.31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.

Luka 6:31 SUV

 

Hii “kanuni ya dhahabu” – the “golden rule” – kama inavyojulikana [siku hizi], ina maana pana zaidi katika aya tunayoijadili hapa, 1Pet. 3:9, kuliko inavyochukuliwa [kwa kawaida]. Katika suala la mahusiano yetu na wengine, hitaji letu kuu mara nyingi ni kuachwa tufanye mambo yetu na hivyo kutoingiliwa kwa namna yoyote yenye nia mbaya na yenye lengo la kutudhuru, kuliko kupata faida fulani kutoka mikononi mwa watu wengine. Hili la pili, yaani kupokea msaada kutoka kwa wengine, wakati mwingine ni jambo “jema” kweli kweli katika macho ya Mungu (ingawa hata hapa msaada wa kiroho tunaoutoa kwa ndugu zetu [katika Kristo] kulingana na karama tulizopewa ndiyo kutimiza kwa kiwango cha juu kabisa kwa amri hii; ling. na Waga. 6:8-10). Lakini lile la kwanza ndiyo hali tunayoiona zaidi – au kukosekana kwake, yaani tunapenda kutosumbuliwa au kutodhuriwa na wengine, ambayo inaendana na uamuzi wetu wa kimungu wa kutorudisha kisasi pale tunapotendewa mambo hayo, hata kama tunakasirishwa na mambo hayo.

 

Ghadhabu ni hisia ya hatari sana, ni aina fulani ya wazimu / kichaa cha muda mfupi (hii ndiyo sababu katika Kiyunani na Kiingereza usemi “he got mad”, yaani alikasirika, hutumika kuielezea hali hii inapotokea). Wakristo wenye desturi ya kukiri na kutubu dhambi zao kila siku (kwa mfano kusali ile “sala ya Bwana” kila siku “… utusamehe dhambi zetu …”) wanaweza, kwa urahisi kabisa, kufuata ule mwongozo wa maandiko wa “jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka” (Zab. 4:4; Waefe. 4:26). Kitu cha hatari zaidi ni ku-react kwa haraka [kwa hasira] mara mtu unapotendewa mabaya. Hii ni ya kujiepusha nayo kabisa! Misemo kama “tulia”, “shusha pumzi”, “hasira, hasara” inafaa kukumbukwa katika nyakati hizi.

 

Wale wanaotembea kwa ukaribu na Bwana Yesu Kristo inawalazimu kujiweka mbali kabisa na vitendo vya kisasi au / na maneno ya shutuma, siyo tu kwa malengo ya kuweka dhamiri safi bali pia kwa ajili ya kuepuka migongano inayopoteza muda tu. Kwani hata katika matukio yanayoudhi [lakini] yasiyo na umuhimu kabisa ya matendo au maneno, hili ni eneo ambalo sote tuna udhaifu wa kufanya maamuzi ya haraka na ambayo hayajafikiriwa kwa undani, ya [kujibu mapigo], na, kinyume na matarajio ya kawaida, jambo hili linaweza likakuzwa na kuwa na matokeo mabaya zaidi licha ya kwamba makosa tuliyotendewa ni madogo tu na uwezekano wa madhara ya sisi kurudisha kisasi yanaweza yasionekane kwa haraka.

 

14 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.

Mithali 17:14 SUV

 

Mwisho wa yote, kulifuata Neno la Mungu ni njia njema zaidi. Unaweza kupata furaha ya kiasi fulani kutokana na kurudisha kisasi (furaha hii yaweza kuwa ndogo au kubwa!), lakini hisia hii ya furaha haiwezi kulinganishwa na maumivu utakayopata kutokana na adabisho utakalolipata kutoka kwa Mungu au/pamoja na matokeo asilia yatakayosababishwa na [wewe] kushindwa kuufuata mwongozo huu unaotolewa kwa wazi kabisa. Lakini kwa wote wanaoitii sheria ya upendo na kuvumiliana, mambo yao huishia mahala pema.

 

12.17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni [kutenda] yaliyo mema machoni pa watu wote.

12.18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.

12.19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana (Kumb. 32:35).

12.20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.

12.21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

War. 12:17-21

 

5.15 Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

Wathess. 5:15 SUV

 

Bali Wenye Kubariki [Wengine]: Kinyume cha kurudisha [kisasi cha] shutuma kwa shutuma na uovu kwa uovu kinaelezwa hapa kama “kuwabariki wengine”. Neno la Kiyunani eulogeo ni moja kati ya maneno mawili katika Agano Jipya linalotumika kutafsiri kitenzi cha Kiebrania kinachomaanisha “kubariki” (barach), na katika etimolojia (elimu ya asili na historia ya neno) yake neno hili linamaanisha kubariki kwa kutamka (kiambishi-awali eu kikimaanisha “-ema” au “nzuri”, na neno log likihusiana na kusema au maneno). Hata hivyo, maana ya neno katika lugha yoyote inatokana na namna na jinsi neno hilo linavyotumika au muktadha wa neno hilo, kwani etimolojia yake, ingawa inaweza kutupatia dalili au dokezo la maana yake, lakini inaweza kutupoteza njia.

 

3.25 Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa (Mwa. 22:18; 26:4; 28:14).

Matendo 3:25 SUV (ling. na Waga.3:8-9)

 

Baraka” zinazozungumziwa hapa, kwanza zinatoka kwa Mungu, na pili, kwa wazi kabisa ni kitu (au vitu) halisi badala ya matamko ya mdomoni [tu]. Zaidi ya hapo, katika Agano la Kale, matamko yaliyotolewa na mitume kwa nguvu ya kitume yalikuwa na matokeo halisi, yanayoonekana, kama katika mfano hapo juu (kwa mfano pale tunapomwona Isaka akimbariki Yakobo na Yakobo anapowabariki watoto wake [wa kiume]). Pia, hii ni aina ile ile ya “baraka” ambayo kwayo “tumeitwa ili tuweze kurithi baraka” (1Pet. 3:9). Baraka zetu katika Bwana, za sasa na za baadaye, ni za kustaajabisha na za namna nyingi (Waefe. 1:3). Tunaye Roho Mtakatifu. Tumezaliwa upya, tumezaliwa kutoka juu. Tu wamoja na Bwana Yesu Kristo. Tunao urithi unaotungojea mbinguni, ufufuo na uzima wa milele, na maskani inayotungojea katika Yerusalemu Mpya.5 Lakini “kuwabariki wengine” maana yake nini?

 

Kitu kimoja tunachoweza kukisema kwa uhakika kabisa ni kwamba Petro hamaanishi kwamba “kuwabariki wengine/wenzetu” maana yake ni kusema tu “ubarikiwe!” au “Mungu akubariki!”, kama ilivyo desturi ya watu wengi. Kwanza, sisi wanadamu hatuna uwezo wa kutoa wito kwa Mungu ili ashushe baraka kwa watu wengine (ling. na Waebr. 7:7). Tunaweza kumwomba Mungu kwa niaba ya mtu yeyote yule, lakini ni ufidhuli kudhani – pia ni hatari kuwaonyesha watu wengine kwamba sisi tunaamini – kwamba sisi tunao uwezo huo. Chanzo cha msemo huu [usiofaa] ni, kwa hakika, matakwa [kwa niaba ya], na msemo wenyewe unasimama badala ya “Ningependa Mungu akubariki!” Angalau msemo kamili unaonyesha dhahiri kwamba tunawatakia [tu] baraka za Mungu watu fulani, badala ya kumwamrisha Mungu (ambalo kwa uhakika hatuna uwezo wa kufanya), lakini hata hili lina mgogoro kwa sababu matakwa yetu hayana faida yoyote [ya kiroho] ndani yake. Kama tumepanga kuomba kwa ajili ya mtu fulani, basi inatupasa kufanya hivyo, lakini mara nyingi ni bora kufanya hivyo bila kutamka kwamba tuna mpango wa kufanya hivyo kwa kutamka msemo huu (ambao kwa kweli ni mara chache sana kuusikia ukiambatanishwa na sala).

 

Pili, wakati kuwatia moyo watu wengine yaweza kuwa ni “baraka” kwao, hii ni sehemu tu ya taswira nzima hapa. Kwani kuna namna nyingi ambazo Wakristo - badala ya kuwa ni watu wanaolipiza kisasi kwa maneno na matendo – wanaweza kuwa ni neema kwa watu wote wanaowazunguka. Mtu mchangamfu, mwenye mtazamo chanya, na asiyetoa kauli za kashfa, siku zote huvutia wengine, nao hupenda kuwa naye wakati wote. Na Wakristo wanaotembea kwa ukaribu kabisa na Bwana Yesu Kristo, waumini waliopevuka kiroho ambao kipaumbele chao ni kuutafuta ufalme wa Mungu, hao ni “chumvi” kwa watu wote wanaowazunguka (Matt. 5:13): Mungu hubariki maeneo wanamofanya kazi na kila mmoja anayehusiana nao kwa sababu wao wanafanya mapenzi ya Mungu kama vile alivyokuwa Abrahamu, nukuu ya hapo juu (Matendo 3:25; ling. na Mwa. 9:24-27; 30:30; Zab. 37:26b; Mithali 11:11; 14:26; 1Mambo ya Nyakati 13:13-14; Matendo 27:24). Waumini pia mara nyingi hupewa fursa za kuwasaidia watu wengine katika mahitaji mbalimbali, kuwapa maneno ya kuwatia moyo na ushauri, kuwafadhili wengine – jambo jema kabisa pale fadhila hizo zinapotolewa moja kwa moja kwa mtu mwenye uhitaji na ikiwa tendo hili jema litaambatana na ujumbe wa Injili. Na mwisho, Wakristo wote tuna karama za kiroho, na tumebarikiwa kuzitumia karama hizi kwa faida ya waumini wenzetu, na pia, kulingana na karama zenyewe, kwa faida ya kuiendeleza Injili ya Bwana Yesu Kristo: yote haya ni baraka halisi, na ndiyo shabaha ya maisha ya kila Mkristo – kinyume na yote tunayotahadharishwa nayo katika aya hii.

 

5 Baraka tunazozipata hapa duniani na tutakazozipata katika milele ijayo hazina kikomo. Ili uone orodha fupi tu ya makundi makuu ya baraka hizi tafadhali tizama: Bible Basics 4B: Soteriology, section III, “What it means to be saved”.

 

Auzuie ulimi wake:

 

3.10 Kwa maana imeandikwa (Zab. 34:12-16), “Atakaye kupenda maisha [yake], Na [mwenye shauku ya] kuona mema katika siku zake za usoni, Auzuie ulimi wake usinene

mabaya, Na midomo yake isiseme hila (hadaa).

1Pet. 3:10

 

Lile tamko katika aya ya 9 linalomaanisha kwamba tumeitwa ili tuwe warithi wa baraka linaainishwa na hii nukuu kutoka Zaburi 34:12-16, ambayo inaifasili ile kanuni maarufu ya [ki]biblia inayofundisha kwamba baraka katika maisha zinatokana na mwenendo wa kujiweka mbali na tabia zilizo kinyume na amri za Mungu (kwani kufuata amri za Mungu huleta baraka), ukianzia na dhambi za mdomo / kauli, ambazo ziko nyingi (maandiko yana tahadhari nyingi zinazotuamuru kutoutumia mdomo kutenda dhambi nyingi za hatari). Kuutawala mdomo, hata hivyo, siyo jambo rahisi kufanikisha, na hata waumini waliopevuka [kiroho] ambao wamepiga hatua kubwa katika eneo la kuutawala mdomo wao wakati mwingine wanaweza kurejea katika tabia ya “kupiga domo” wanaposhawishika kufanya hivyo.

 

1 Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu (wakati) mtu mbaya yupo mbele yangu.

2 [Basi] nalikuwa sisemi, nalinyamaa kimya [hata lililo jema sikulitamka], Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.

3 Moyo wangu ukawa moto ndani yangu, Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka; [basi nikashindwa], nikasema kwa ulimi wangu,

Zab. 39:1-3

 

3.2 Maana twajikwaa (mara nyingi twatenda dhambi bila kukusudia, kwa kughafilika) sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia (kuutawala) na mwili wake wote kama kwa lijamu (hatamu).

3.3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili watutii, hivi twageuza mwili wao wote [upande huu na huu].

3.4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.

3.5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

3.6 Nao ulimi ni moto [kama huo]; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile (huwasha moto katika taswira za mfumo mzima wa wanadamu), nao huwashwa moto na jehanum.

3.7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

3.8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

3.9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

3.10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.

Yakobo 3:2-10

Katika nukuu kutoka Zaburi 34:13 inayofanywa na Petro, “auzuie ulimi wake usinene mabaya”, chochote tutakachosema ambacho inatupasa tusikiseme ni “kibaya” na kiovu mbele za macho ya Mungu – hakuna tofauti kati ya maneno haya na yale ya Kiebrania cha Agano la Kale ambako Petro anayachukua. Kwa kifupi, kulingana na motisha ya mtu, karibu kila kitu kinachotamkwa kinaweza kuwa na dosari ya dhambi, na hii ndiyo maana kimya (kunyamaza) ni jambo jema dhidi ya neno lolote ambapo kinywa kinaachwa huru na matokeo yake yakiwa kwamba kinachosemwa hakisemwi kwa uangalifu wa kimungu (Mithali 13:3; 17:28; 21:23; Yakobo 1:19; ling. na Zab. 141:3).

 

19 Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.

Mithali 10:19 SUV

 

12.36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

12.37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

Matt. 12:36-37 SUV

 

4.29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Waefe. 4:29 SUV

 

5.4 wala aibu (matusi) wala maneno (utani) ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali (ni muhimu) kushukuru.

Waefe. 5:4

 

3.8 Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano (kashfa), na matusi vinywani mwenu.

Wakol. 3:8

 

Kutokana na upana wa vyanzo vya nukuu hizi hapa juu, hata uchunguzi usio na kina [sana] wa aina za kauli zinazotoka midomoni mwa wanadamu unatosha kudhihirisha kwamba aina na makundi ya dhambi za kauli ni yenye taswira nyingi na yanaweza kustahili uchunguzi wa kina ili kubainisha kila kitu kinachofundishwa na kuamriwa na Biblia kuhusiana na somo hili. Hivyo, orodha fupi ifuatayo hapa chini haina shabaha ya kujadili dhambi za kauli / mdomo kwa utondoti mkubwa, bali shabaha yake ni kutoa mwongozo wa yale Biblia inayoyafundisha kwamba ni kauli za dhambi (na vingi kati ya vipengele vikiingiliana na kuchanganyikana).

 

a) Umbeya / udaku: Hatari za kumsingizia mtu uwongo, hatari za kumkashifu mtu, hatari za kumhukumu mtu na kumwingilia mtu kwa maneno ya uwongo katika maisha yake, zinajulikana vyema na mtu yeyote ambaye amesoma Biblia, na haswa kitabu cha Mithali (Mithali 10:18; 11:16: 16:28; 17:9; 18:8; 19:22; 25:23; 26:20; 26:22; 30:10; Matt. 7:1; Luka 6:37; Waefe. 4:31; 1Tim. 5:13; 1Pet. 4:15).

 

19 Mwenye kitango akisingizia (yaani mbeya/mdaku) hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.

Mithali 20:19

 

b) Maneno ya Upumbavu (Mithali 17:28; 2Tim. 2:23; Tito 3:9; ling. na Isaya 32:6): Waumini ni wawakilishi wa Bwana Yesu Kristo, mabalozi kwa ajili Yake na kwa ajili ya kweli Yake (2Wakor. 5:20). Kwa hiyo, kuenenda kwa kiasi fulani cha staha – kwa [ajili ya] utukufu wa Nahodha tunayemwakilisha – ni jambo jema zaidi kuliko kujulikana kama watu wanaoropoka ambao wakati wote wanabwabwaja kila aina ya mazungumzo ya kipumbavu – haswa ikiwa upumbavu huo unaegemea kwenye mambo yasiyo ya kweli (na kwa hakika maneno kama haya hayatakuwa na ukweli ndani yake).

 

5.4 wala aibu (matusi) wala maneno (utani) ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali (ni muhimu) kushukuru.

Waefe. 5:4

 

6.20 Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo [ya kimungu], yasiyo na maana, na mashindano (mabishano) ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;

1Tim. 6:2

 

2.16 Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si [ya kimungu]; kwa kuwa [wanaofanya hivi] wataendelea zaidi katika maovu,

2Tim. 2:16

 

c) Ugomvi: Migongano, mabishano, mashindano, mizozo na mambo kama hayo yanavuruga amani na hupelekea kwenye dhambi nyengine za mawazo, za maneno na za matendo pia; hivyo, waumini waliopevuka wanashauriwa kujiepusha na mabishano ya maneno yasiyo ya lazima kila inapowezekana (Zab. 31:19-20; Mithali 15:18; 17:14; 18:6; 18:19; 25:23; 26:17; 26:21; 30:33).

 

3 Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.

Mithali 20:3 SUV

 

10 Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma.

Mithali 22:10 SUV

 

20 Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma.

Mithali 26:20 SUV

 

2.23 Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.

2.24 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;

2.25 akiwaonya kwa upole wao washindanao [wabishanao] naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli;

2.26 wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.

2Tim. 23-26

 

3.9 Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na [mambo ya] nasaba, na magomvi, na mashindano [kuhusu] sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.

Tito 3:9

 

d) Ulalamishi (Wafi. 2:14; Yak. 5:9; 1Pet. 4:9; ling. na Isa. 29:24; Luka 5:30; 15:2; 19:7; Yoh. 6:41; 6:43; 7:12): Maduka makubwa [ulimenguni kote] huwa na idara zinazoshughulika na malalamiko ya wateja, na kwa kweli katika masuala ya mapungufu katika huduma zinazotolewa na ambayo yanapaswa kushughulikiwa ili kuboresha huduma inayotolewa, kuna kila sababu ya kutoa taarifa ya mapungufu hayo pale yanapoonekana. Pia ni kweli kwamba ni wachache kati yetu tunaoweza kumaliza siku bila kuzungumza na wenzetu juu ya “mapungufu” tunayoyaona katika jambo au mtu fulani. Tumekwishaijadili tabia ya umbeya / udaku hapo juu na pia tumezungumzia mtazamo na mwenendo stahiki ambao Wakristo wanapaswa kuwa nao kuhusiana na mamlaka yanayotawala katika maeneo wanamoishi, katika sura zilizopita katika mfululizo wa masomo haya. Bila ya shaka ni wachache sana kati yetu wanaoweza, bila kuogopa, wakati wote kuwa na mtazamo na msimamo ule wa zamani wa “ikiwa huna jambo zuri la kusema, basi bora unyamaze”, haswa wanapozungumziwa wanasiasa, watu mashuhuri na watu wakorofi katika maisha yetu. Lakini kuna aina fulani ya ulalamishi ambayo Wakristo wanapaswa kujiepusha nayo kwa gharama yoyote ile, yaani kumlaumu Mungu.

 

Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

1.15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.

1.16 Watu hawa ni wenye kunung'unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi,

Yuda 1:14b-16a

 

Hivyo kulalamika, kunung’unika, kulia-lia, yaweza kuwa mambo ya kila siku (kwa mfano, ni vigumu kufanya kazi jeshini bila kuwa na njia [kama hii] ya kulalamikia magumu yaliyopo ili kupunguza ghadhabu), lakini waumini wanapaswa kuwa waangalifu sana katika kutenganisha mwenendo wao wa kutoridhika na sehemu fulani za maisha yao zinazopelekea wao kulalamika na kuweka lawama ya kutoridhika huko katika mikono ya Mungu. Mungu wetu hahusiki kabisa na maovu yanayotokea katika maisha yetu. Na kwa kuwa Mungu wetu ndiye mwenye madaraka juu ya kila kitu kinachotokea katika maisha yetu, kwa hakika ni vigumu sana kuwa na tabia ya ulalamishi bila ya kuanza kutupa lawama katika namna Mungu anavyosimamia maisha yetu – na kwa kweli yule mwovu hutumia fursa zote anazozipata kutuwekea vikwazo katika njia tunamopita ili tuwe na tabia mbaya ya aina hii. Ingawa jambo hili halitakuwa la wazi sana pale tunapoanza kuonyesha tabia hii [ya kumlalamikia Mungu], Wakristo wanaotumia kiasi fulani cha muda wao katika kuyatafakari maisha yao na mwenendo wao wa kiroho pale wanaponung’unikia shida wanazopitia mara moja wataona kwamba wanapoalalamikia mazingira waliyomo kwa kiasi chochote kile – hata kidogo tu(!) - basi mwisho wa yote malalamiko hayo yatamlenga Yule ambaye anatupangia mazingira hayo, na huu ni mwenendo hatari sana.

 

10.5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.

10.6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

10.7 Wala msiwe waabudu [miungu]-sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.

10.8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

10.9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu (yaani kizazi cha Kutoka Misri), wakaangamizwa na nyoka.

10.10 Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaangamizwa na mharabu [Destroying Angel].

10.11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani (tunaoishi enzi za mwisho).

1Wakor. 10:5-11

 

Kile kizazi cha Kutoka kimekuja kujulikana kwa sifa / tabia hii mbaya ya ulalamishi. Wakati wowote mambo yao “yalipoharibika”, badala ya kupambana kwa imani dhidi ya mitihani ile ambayo Bwana aliiweka mbele yao, wao wakamlaumu Musa – na hivyo kiuhalisia walimlaumu Mungu - kwa yote yaliyowasibu. Na hapa ndipo tunapoona kitu kibaya kilicho katika tabia ya ulalamishi [wa kunung’unika] ambayo ni tofauti na kutoa taarifa ya matatizo kwa wanaohusika katika namna isiyo na hisia kali: kunung’unikia mazingira tunamoishi ni kuonyesha kutokuwa na tumaini na Mungu – na kukosa imani katika wema na huruma Yake.

 

6 Musa na Haruni wakawaambia wana wote wa Israeli, Jioni ndipo mtakapojua ya kuwa Bwana amewaleta kutoka nchi ya Misri;

7 na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa Bwana; kwa kuwa yeye asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia Bwana; na sisi tu nani, hata mkatunung'unikia?

Kutoka 16:6-7 SUV

 

e) Kulaani: Hapa, neno hili tunalitumia si kwa maana ya kutumia lugha chafu, ya matusi (ambayo pia inakatazwa na maandiko; kw. mf. Waefe. 4:29; 5:4; Wakol. 3:8), bali ni kuwatakia / kuwaitia viapo watu wengine, kuwatakia mabaya badala ya mema yatokayo kwa Mungu.6

 

12.14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

War. 12:14 SUV (ling. na Luka 6:28)

 

3.9 Kwa huo [ulimi] twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

3.10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.

Yakobo 3:9-12

 

f) Kutoa Vitisho: Kama kuna yeyote aliyekuwa na sababu ya kutoa vitisho (kwa sababu

 

6 Kufanya viapo au kuapa kwa Jina la Mungu kumekatazwa na maandiko ya Agano Jipya (Matt. 5:33-37; Yak. 5:12).

mateso aliyofanyiwa yalikuwa na matokeo ya kuogofya yatakayowakuta watesi wake) na

pia uwezo na mamlaka ya kutimiza vitisho hivyo, basi huyo alikuwa Bwana wetu. Lakini maandiko yanatuambia nini kuhusiana na jinsi Yeye alivyoenenda chini ya mateso na manyanyaso ya uonevu makali kuliko yote katika historia?

 

2.21b kwa sababu Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachia kielelezo / mfano, ili mfuate nyayo zake.

2.22 “Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake” (Isa 53:9b).

2.23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya (hakumtishia mtu); bali alijikabidhi (alimtumaini) kwake Yeye ahukumuye kwa haki.

1Pet. 2:21b-23

 

Yeye ndiye mfano wetu katika kila kitu, hivyo tunapaswa kuuzuia mdomo dhidi ya kutoa vitisho, hata pale tunapokabiliwa na uonevu (Waefe. 6:5-9).

 

12.19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana (Kumb. 32:35).

War. 12:19

 

g) Kutoa Sifa za Uwongo [kwa Lengo la Kujipendekeza]: Hapa hatumaanishi kutoa sifa stahiki kwa wenzetu. Dhambi hii ya kusifia kwa uwongo inahusiana kwa ukaribu kabisa na udanganyifu wa makusudi, kumsifia mtu kwa lengo la kumtendea uovu au kutenda dhambi fulani (yaani kupotosha ukweli kwa lengo la kumpoteza mtu kutoka njia aliyomo), na mara nyingi huambatana na mwenendo mwingine wa hila (Zab. 12:2-3; Mithali 28:23; ling. na Ayubu 32:21-22).

 

9 Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Mtima wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza.

Zab. 5:9 SUV

 

28 Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.

Mithali 26:28 SUV

 

5 Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.

Mithali 29:5 SUV

 

16.17 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.

16.18 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu (the naive).

War. 16:17-18

 

1.16 Watu hawa ni wenye kunung'unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, waki[ji]pendekeza kwa watu wenye cheo kwa ajili ya faida.

Yuda 1:16

 

h) Kufuru: Maneno ya Kiyunani ambayo neno letu la Kiswahili na Kiingereza linalomaanisha “kufuru” linatoka, wakati mwingine humaanisha “kusema vibaya” kwa ujumla (dhambi ambayo pia tunapaswa kujiepusha nayo: ling. na 2Pet. 2:10-12; Yuda 1:9), lakini katika maandiko maneno haya mara nyingi yanamaanisha “kusema vibaya dhidi ya Mungu (Matt. 15:19; Marko 7:22; Matendo 26:11; 1Tim. 1:20; 2Tim. 3:2; Ufu. 13:1-6; 17:3). Hakuna hata haja ya kusema hapa kwamba hii ni moja kati ya (kama siyo) dhambi kubwa kabisa ya mdomo – kwani moja kati ya amri 10 za Mungu imeweka katazo dhidi yake (Kutoka 20:7; Kumb. 5:11). Kama ambavyo amri ya 3 inaweka wazi, kufuru haina maana ya kusema maneno hasi dhidi ya Mungu pekee; ina maana pia (na hili ni jambo muhimu kuliweka moyoni) kwamba ni kosa kumpatia Mungu sifa ambazo si za Kwake, au kusema uwongo katika Jina lake. Kila Mkristo anapaswa kuwa mwangalifu pale anapolitaja Jina la Mungu katika mazingira yoyote yale (Walawi 24:16; Waefe. 4:31; Wakol. 3:8).

 

28 Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako.

Kutoka 22:28 SUV

 

12.31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.

Matt. 12:31 SUV

 

i) Majigambo: Mwongozo wa kibiblia kwamba “[acha mtu] mwingine akusifu na wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mgeni [akusifie na] wala si mdomo wako mwenyewe”, ni busara ya kiwango cha hali ya juu sana (Mithali 27:2). Kwa masikitiko sana, “majigambo [ya kiburi ya mtu] juu ya alicho nacho” ni sehemu kubwa ya hulka ya dhambi ya wanadamu wote (1Yohana 2:16)7, hivyo kwamba kila mmoja wetu anashawishika “kupiga tarumbeta lake mwenyewe” nyakati fulani. Kimsingi, kuzungumzia mafanikio au uwezo wetu hakuna ulazima wa kuvuka msitari na kuingia katika kujisifu “[zaidi] ya kadiri yetu” (2Wakor. 10:13), sote tunayatambua majigambo ya kujisifia pale tunapoyasikia, na kujikuza zaidi ya ukweli ulivyo hutofautisha kati ya sifa stahiki na majigambo ya kujikweza – hii ya pili haiendani kabisa na mwendo halisi wa Kikristo (Zab. 12:3; War. 1:30; 2Tim. 3:2; Yak. 3:14; 2Pet. 2:18; Yuda 1:16).

 

13.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

1Wakor. 13:4 SUV

 

6.14 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.

Waga. 6:14 SUV

 

 

 

 

7 Neno la Kiyunani linalotafsiriwa mara nyingi kama “kiburi” au “pride” katika 1Yohana 2:16 (ἀλαζονεiα / alazoneia) lina uhusiano wa karibu sana na majigambo (kitenzi asilia chake kinamaanisha “kujigamba / kujisifu”; ling. na Warumi 1:30; 2Tim. 3:2).

2.8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema [ya Mungu], kwa njia ya imani [yenu kwa Kristo]; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa [cha bure] cha Mungu;

2.9 [na] wala si kwa matendo [yenu], mtu awaye yote asije akajisifu.

Waefe. 2:8-9

 

4.16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.

Yak. 4:16 SUV

 

j) Kusema Uwongo: Yamkini dhambi ya mdomo inayojidhihirisha sana na iliyoenea sana ni ile ya kusema uwongo. Kama Wakristo, tunaokolewa kwa kuiamini Injili ya Bwana Yesu Kristo, na tunakua, tunaendelea kukua, na tunamtumikia Bwana wetu kwa njia ya kuuzingatia na kuushuhudia ukweli huu wa Ufalme [wa Mungu]. Hakuna hata haja ya kusema, ukweli ni pingamizi dhidi ya kila uwongo, kama ambavyo yeye ambaye ni Kweli yenyewe, Yesu Kristo Bwana wetu (Yoh. 1:9; 14:6; Ufu. 19:11) anampinga kabisa yeye ambaye anatupinga sisi sote [tulio Wake] na Yeye Mwenyewe – baba wa uwongo [wote], Ibilisi.

 

4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

Mwa. 3:4 SUV

 

8.44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema [kutokana na hulka] yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo [uwongo].

Yoh. 8:44

 

Bila ya shaka, aina za uwongo huzidiana katika ubaya wake. Uwongo unaosemwa kwa kusudi la kuwadanganya wengine ili wadhurike na ili ujinufaishe mwenyewe, kama ilivyokuwa katika udanganyifu (hadaa) wa Eva na Shetani, kwa uwazi kabisa ni uwongo mbaya kuliko wote. Mafundisho ya uwongo yanayotokana na motisha za kibinafsi nayo yanaingia katika kundi hilo hilo.

 

16.17 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.

16.18 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu (the naive).

War. 16:17-18

 

Ni kweli pia kwamba kutakuwa na mazingira fulani ambamo kwa muumini kufichua taarifa fulani [kuhusu waumini wenzake] yaweza kuwa ni hatari kwao, na hivyo ni dhambi [kwa muumini huyu]. Halikuwa kosa, na wala maandiko hayakuhukumu uwongo wao, wale wakunga waliokataa kuwaua watoto waliozaliwa na Waebrania na [wao] kumdanganya Farao ili kuwanusuru watoto wale pamoja na wao wenyewe; kwa hakika walibarikiwa na Mungu kwa kitendo kile (Kutoka 1:15-21); vivyo hivyo ilikuwa kwa Rahabu katika uaminifu wake kwa wapelelezi wa Kiebrania aliouonyesha kwa kumdanganya mfalme wa Yeriko (Yoshua 2:3-6; ling. na Waebr. 11:31; Yak. 2:25). Udanganyifu wa Yaeli dhidi ya Sisera pia unapewa sifa katika maandiko (Waamuzi 5:24); wakati katika 2Samweli 15:35 tunaona sala/maombi ya Daudi kwa Mungu yakijibiwa kwa ushauri mmbovu wa Hushai kwa Absalomu uliokuwa na shabaha ya kuuvuruga ushauri mzuri kabisa wa Ahithofeli. Mifano yote hii na mingine mingi kama hiyo inafanana katika ukweli kwamba badala ya kuwa na kusudi la kuwadanganya watu wema wa Mungu kwa faida ya nia mbaya, udanganyifu huu ulikuwa na lengo la kuwazuia watu wabaya wasiwadhuru watu wema [wa Mungu] – na kwa kweli ulihatarisha uhai na usalama wa watu wale wema katika kuwalinda wenzao dhidi ya uovu.

 

Kama hakuna aina hii (kama ya hapo juu) ya shinikizo la kutoa taarifa kwa mamlaka [ma]ovu (wakati taarifa ya kweli itahatarisha usalama wa wasio na hatia), Wakristo wanapaswa kukumbuka kwamba jibu kamili, la kweli na lenye lengo la kutuonyesha sisi kwamba tu wema na wenye haki mbele za wasioamini si jambo la lazima, kwa ujumla. Hatuna ulazima wa kufanya mazungumzo madogo-madogo (small talk) na watu wasioamini, na pale mazingira yanapohitaji, basi tunaweza kusema na kuongea machache tu, badala ya mengi. Hatuna ulazima wa kuelezea kwa undani kwa nini tunadhani nguo iliyovaliwa na mtu fulani haimpendezi, kwa mtazamo wetu, au kwa nini chakula tulichokula kwa mtu fulani siyo kitamu. Kiasi fulani cha hekima katika kuwalinda wengine dhidi ya maumivu ya mioyo yao inaruhusiwa na ni mwenendo wa kibiblia kabisa.

 

13.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

13.5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

13.6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

13.7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote [yanayopaswa kustahamili].

1Wakor. 13:4-7

 

Mahala na wakati pa kuweka msimamo huu wa kibiblia ni jambo litakalotokana na mazingira na dhamiri ya Mkristo husika – na haiwezekani na pia haifai kutunga na kuweka kanuni fulani [ya kisheria]. Kwa upande mwingine, katika mahusiano yetu na waumini wenzetu, wakati wowote na mahala popote pale ambapo utetezi wa ile kweli ya Neno na misingi ya Biblia iliyo muhimu kabisa kwa uzima wetu [wa kiroho], kusema ukweli tupu kutoka moyoni ni jambo la lazima kabisa.

 

4.25 Basi uvueni uongo, “mkaseme kweli kila mtu na jirani yake” (Zakaria 8:16); kwa maana [sisi waumini] tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.

Waefe. 4:25

 

3.9 Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu (nafsi ya) wa kale, pamoja na matendo yake;

Wakol. 3:9 SUV

 

Palipo na upendo, Roho yupo pia. Ikiwa motisha zetu ni za kibinafsi, udanganyifu wote unaofanyika unatoka kwa yule mwovu.

 

3.13 N'nani aliye na hekima na ufahamu kati yenu? Na aonyeshe katika mwenendo wake mwema kwamba kazi zake zinafanywa katika upole wa hekima.

3.14 Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.

3.15 Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.

3.16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.

3.17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

 

Na aache Mabaya, Atende Mema: Kwa sababu nzuri kabisa, kujikana mwenyewe na kuuacha uovu kunawekwa mwanzo kabla ya kutenda yaliyo sahihi na mema, yaani kuubeba msalaba wako na kumfuata Bwana Yesu Kristo. Haiwezekani kamwe “kutenda mema”, yaani kufanya yale Mungu anataka tuyafanye – kuhakikisha tunajiweka katika mchakato wa kukua kiroho, kuendelea [kiroho], na kuzaa matunda [ya kiroho], na kufanya hivyo tukingali tunaukumbatia uovu, kwani hilo ndilo Mungu wetu analichukia kabisa. Haiwezekani kumtumikia Mungu na Ibilisi kwa wakati mmoja.

 

10.21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

1Wakor. 10:21 SUV

 

Waumini wanaligundua hili mapema sana katika maisha yao ya Kikristo, na kuwa “mhalifu sugu wa kiroho”, yaani mtenda dhambi asiyerekebishika kutakuwa na matokeo ya muumini huyu kukutana na hatua za nidhamu kali kutoka kwa Mungu.

 

12.11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani (yanamfanya muumini aelekee kwenye ukamilifu).

Waebr. 12:11

 

Kwa wale wanaoitika na kukubali kubadilishwa na kurekebishwa na Mungu baada ya kufanya makosa, matokeo yake ni kurejea katika njia sahihi ya kiroho na kuongezeka nguvu kiroho. Kwa wale wanaofanya mchezo na uvumilivu wa Bwana wetu juu ya dhambi zao, uhaba wa makuzi ya kiroho na ukiukaji wa amri za Bwana wa kila mara unapelekea kwenye kupoteza ubora wa maisha yao ya Kikristo na hata kuingia katika hatari kiroho: bila ya toba ya kweli, kushindwa kurudi “kutoka maovuni” kuna matokeo ya uchakavu wa kiwango cha maisha yao ya kiroho, kitu ambacho kitaishia katika dhambi inayopelekea kwenye kifo (1Yoh. 5:16-17), au hata kifo cha imani yenyewe (uasi), ambayo ndiyo inamfanya awe Mkristo (hii itategemea na jinsi Mkristo huyu atakavyozipokea hatua za kinidhamu kutoka kwa Mungu, ambazo zitakuwa zinaongezeka katika maumivu yake, kulingana na jinsi maadili yake yanavyozidi kuporomoka).8

 

16.24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, [kwanza] na ajikane mwenyewe (aache matamanio yake binafsi), ajitwike msalaba wake, anifuate.

Matt. 16:24 (ling. na Marko 8:34; Luka 9:23)

 

8 Tizama Bible Basics 3B: Harmatiology, section IV.6, “Apostasy and the Sin Unto Death”.

Atafute Amani, Aifuate Sana: Neno la Kiyunani linalomaanisha amani lililotumika hapa katika 1Pet. 3:11 (eirene / ερηνη, ling. na jina binafsi: Irene) ndilo linalotafsiriwa kutoka

katika neno la Kiebrania Shalom (שלוח) lenye maana ile ile. Wakati maneno yote mawili yanaweza, na kwa kweli yanaashiria kutokuwapo kwa uhasama kati ya mataifa na kati ya watu katika mahusiano yao, amani inayomaanishwa na matumizi yake katika Biblia inadokeza zaidi dhana chanya ya amani katika matumizi yake, ikisisitiza siyo kinachokosekana (yaani uhasama) bali hali ya ukamilifu na baraka katika matukio ambamo mambo ni sawia kati ya mataifa, kati ya watu, na, cha muhimu zaidi, kati ya Mungu na wale walio Wake. Sasa hili la mwisho (mahusiano kati ya Mungu na wale walio Wake) ndilo linalohusika katika muktadha wetu.

 

1.19 Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamilisho wa mpango Wake utimizwe katika Kristo pekee;

1.20 na kwa Yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi Yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba Wake; kwa Yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.

Wakol. 1:19-20 (ling. na Waefe. 2:13-18)

 

Amani ya awali – kurejeshwa kwa Mungu na kupata ukamilifu – ambayo kila mwanadamu anapaswa kuitafuta ni upatanishi na Mungu Baba ambao umewezeshwa na msalaba, sadaka ya mpendwa Bwana na Mwokozi wetu kwa ajili ya dhambi zetu zote (2Wakor. 5:18-21).9 Dhambi huleta uhasama kati ya Mungu na mwanadamu; ni kwa njia ya damu ya Kristo, kifo Chake cha kiroho kwa ajili ya dhambi zote za ulimwengu, ndiyo uhasama huo unaotutenganisha na Mungu unaondolewa. Neema hii isiyo na kifani – ya kuondolewa kwa uhasama wa Mungu dhidi yetu na badala yake kuwa na upendo na huruma Yake kuu – hupokelewa na waumini wote mara wanapofanya uamuzi binafsi wa kumwamini Bwana Yesu Kristo. Na matokeo yake ni kwamba “tuna amani na Mungu …” kwa sababu sisi sasa ni watu wa Bwana Yesu Kristo. Amani hii, kama ilivyo kwa neema nyingi tunazozipata mara baada ya kuokolewa, inategemea mwendelezo, kwa upande wetu, wa imani katika Bwana Yesu Kristo bila ya imani hiyo kusitishwa. Mungu Baba anakuwa [sasa] na fadhili juu yetu kwa msingi wa umoja wetu na Mwana Wake. Na katika milele ijayo, amani hii itakuwa kamilifu, isiyoweza kubadilika tena, timilifu katika kila taswira yake. Hata hivyo, katika maisha yetu hapa duniani, ubora na kina cha amani yetu vinategemea ni kwa kiasi gani tunaiitikia kweli. Kwa sasa amani yetu inaonekana katika tukio hadi tukio la maisha yetu, kwani kina, ubora na mwendelezo wa amani hii vinategemea kukua kwetu kiroho siku hadi siku. Hii ndiyo sababu aya tunayoijadili inatusihi (“na atafute amani, aifuate sana”), ikitusihi tuitafute na kuifuatilia neema ya amani hii kwa kuwa amani hii ni kitu kinachoweza kuboreshwa katika maisha yetu [hapa duniani] kwa jinsi tunavyokua [kiroho], tunavyoendelea [kiroho], na tunavyozaa matunda [ya kiroho] kwa ajili ya Bwana wetu.

 

5.1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

War. 5:1

 

Katika aya hapa juu, uhalalisho wetu, yaani kuwa na uongofu wa Mungu ambao tunaupata

 

9 Tizama Bible Basics 4A: Christology, section II.9, “Reconciliation”.

kwa njia ya imani (War. 3:28; 4:26; 5:910:10; 1Wakor. 6:1; Waga. 3:16; 3:24; Tito 3:7), ni neema ambayo kila Mkristo amepewa; sote “tumehesabiwa haki kwa njia ya imani”, lakini

kuipata na kuitumia amani kwa ukamilifu, amani ambayo Mungu anaitoa kwetu katika Bwana Yesu Kristo si jambo linalofanikiwa bila juhudi zozote kwa upande wetu. Kufanikisha hili kunahitaji juhudi kwa upande wa muumini, jitihada za kiroho ambazo ni kinyume na “kazi/matendo – works” (linganisha na Waefe. 2:9). Katika namna ambayo ni kinyume na matarajio ya kawaida, kile ambacho muumini wa kawaida anapaswa kufanya ili aweze kuingia katika amani ambayo Mungu anaitoa kwetu – na kwa hakika anatuamrisha tuitafute (kwa kuwa kufanya hivyo ni kutimiza amri ya 4 kati ya zile 10) inatupasa tuachane na kazi/matendo yetu sisi wenyewe na badala yake kutumainia kazi (matendo) ambazo Mungu anazifanya kwa ajili yetu.

 

4.9 Hivyo, sasa limesalia pumziko la siku ya Sabato kwa watu wa Mungu (yaani amani inayoendelea siku hadi siku, ambayo ndiyo kutimizwa kwa amri ya 4 katika enzi hii ya Kanisa).

4.10 Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko [la Mungu] ameacha kufanya kazi/matendo yake mwenyewe, kama Mungu alivyopumzika kutoka katika kazi/matendo Yake.

4.11 Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo [endelevu ya kiroho], ili kwamba asiwepo yeyote atakayeanguka [kutoka katika neema] kwa kufuata mfano wao wa kutotii (yaani wale wa kizazi cha Kutoka).

Waebr. 4:9-11

 

Amri ya 4 ndiyo amri pekee ambayo hairudiwi kutajwa katika Agano Jipya, na ibara inayonukuliwa hapa inaeleza kwa nini. Chini ya Sheria, siku maalum ilitengwa kwa ajili ya Bwana, siku ambayo wakati wake uliwekwa kwa ajili Yake, na muda wa siku hiyo ulitumika katika kujifunza mafundisho Yake, badala ya kufanya kazi kama zile za kila siku; mafundisho Yake pia yameashiriwa katika maandiko yote ya Sheria. Lakini Sheria [sasa] imebatilishwa na msalaba (War. 6:14-16; 10:4; 1Wakor. 9:20; Waga. 5:18; Waefe. 2:15; Waebr. 7:12; 8:13). Kristo sasa ameshinda ushindi mkuu wa enzi zote, na kanisa Lake sasa linafanya mashambulizi, likiwa na silaha mahususi kwa ajili ya vita ya kiroho ambayo tumeitwa kuipigana (Matt. 16:18; Waefe. 4:8; 6:12). Tumeitwa kufanya mashambulizi 24/7 (kila saa ya kila siku) – na si kukaa tu na kujilinda (kama ilivyo desturi ya wengi katika zama hizi za Laodikia), bali kuzaa matunda kwa ajili ya Bwana wetu ambaye hakawii, atatokea muda si mrefu (Luka 19:16; 2Wakor. 5:10; Tito 2:13). Hivyo "pumziko" letu siyo la kuitumia siku moja halisi ya wiki tukijifunza juu ya Bwana; pumziko letu ni endelevu – siyo la kuacha kufanya yale Bwana anayotaka tufanye, bali ni kujiweka katika mikono Yake na kumwacha Roho Mtakatifu atupatie nguvu katika kukua kiroho kwa bidii, kufanya maendeleo katika kukua huko kiroho, na kuzaa matunda aambayo Bwana Yesu Kristo anatarajia tuyazae kila siku, "maadamu ikiitwa 'leo'" (Waebr. 3:13; ling. na Zab. 118:24; 2Wakor. 6:2), tukijikumbusha kila wakati kwamba zile thawabu kuu zinaenda kwa wale walio tayari kuitikia [wito Wake] na kujitoa Kwake ili atutumie kwa njia ya Roho Mtakatifu (War. 6:13; 6:19; 12:1-2; Waga. 5:16-18).

 

2.13 Kwa maana Mungu [kwa njia ya Roho Wake Mtakatifu] ndiye atendaye kazi ndani yenu, [katika] kutaka kwenu [yaliyo mema] na [katika] matendo yenu [mnayotenda ili] kulitimiza kusudi lake jema.

Wafilipi 2:13

 

1.28 ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.

1.29 Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.

Wakolosai 1:28-29 (ling. na 1Wakor. 15:10; Waefe. 3:9)

 

Kwa wale ambao wanaweka maisha yao 100% katika mikono Yake, wakipumzika katika Yeye, tukiacha kuwa na wasiwasi juu ya juhudi zetu sisi wenyewe, tukimwacha Yeye abebe mzigo wetu (Zab. 37:5; 1Pet. 5:7; ling. na Matt. 11:29-30), na matokeo yake ni kwamba tutakuwa na amani ya kweli ndani yetu tukingali katikati ya dhoruba za maisha (Matt. 8:23-26). Tunapata amani hii na tunaendelea nayo kwa kumwamini Yeye na kuendelea kuitimiza kazi Yake [aliyotutuma] mpaka mwisho.

 

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu (mara dufu), kwa kuwa anakutumaini.

Isaya 26:3 (ling. na Isa. 30:15)

 

4.6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

4.7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

4.8 Hatimaye, ndugu zangu, [mnavyoendelea katika imani], mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi (matakatifu), yo yote yenye kupendeza [kwa Mungu], yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwa [una matumaini yoyote ya kupewa] sifa nzuri [kutoka kwa Mungu siku ya hukumu], yatafakarini hayo.

4.9 Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

Wafi. 4:6-9

 

3.15 Na amani ya Kristo [iwe ndiyo mwamuzi] mioyoni mwenu [wa nini na namna ya kufikiri]; [hii] ndiyo [amani] mliyoitiwa katika Mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

Wakol. 3:15

 

Aya hizi pamoja na nyingine nyingi zinaweka wazi kwamba hali / msimamo wa kawaida wa kila siku wa Mkristo ni ule wa amani [moyoni] (kwa mf. Isa. 26:3; 57:2; Yoh. 14:27; War. 5:1; Waefe. 2:14; Wafi. 4:7; 2Wathes. 3:16; 1Pet. 1:2), tukiitekeleza amri yetu mpya ya 4 ya kupumzika katika Bwana si tu katika siku moja ya wiki, bali katika kila hatua ya njia tunayopita katika safari yetu kuelekea Sayuni.

 

 

 

Macho ya Bwana:

 

3.12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki [kwa ajili ya kuwatendea mema], Na masikio Yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko dhidi ya watenda mabaya”.

1Pet. 3:12

 

Mungu ni mwenye fadhila kwa waongofu lakini ni mwenye uhasama dhidi ya watenda maovu. Ndani ya kanuni hii ya wazi ya maandiko kuna dhana kwamba waumini – ambao wote "wamehesabiwa haki kwa imani [yao]" na hivyo ni waongofu, na wenye uongofu wa Mungu (kwa mf. War. 4:1-5) – wanatenda yaliyo sahihi na ya haki, na kwamba wasioamini ndio wanaotenda yaliyo maovu, na hivyo kujiletea [wenyewe] ghadhabu ya Mungu. Ni jambo rahisi kuona hapa kwamba waumini [wenzetu] ambao hawaishi kulingana na "maelekezo yao ya kazi" waliyopewa na Mungu wanajiweka katika hatari kubwa.

 

3.6 Kila akaaye ndani Yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona Yeye, wala hakumtambua.

3.7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama Yeye alivyo na haki;

3.8 anayeishi maisha ya dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

3.9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi [wakati wote*], kwa sababu uzao Wake (mbegu ya Mungu) wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi [wakati wote*] kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

3.10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi [ni dhahiri pia]. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

1Yoh. 3:7-10

 

Tumethibitisha mara nyingi kwamba hakuna hata mtu mmoja hapa duniani anayeishi katika mwili wa dhambi atakayekuwa huru na dhambi akingali hapa duniani – na kwa hakika ni uwongo kusema kinyume na hili (1Yoh. 1:8-10) – lakini hatujasahau kuthibitisha kwamba Mungu ametupatia njia yenye neema kuu ya kujitakasa mara tunapoingia katika dhambi, yaani kukiri dhambi zetu moja kwa moja kwa Bwana (1Yoh. 1:9; ling. na Zab. 32:6). Bwana Yesu Kristo amekwishakufa kwa ajili ya dhambi zote za wanadamu wote, na kwa njia hii amefanya wokovu uweze kupatikana na kila mwanadamu na kurejeshwa kwa ushirika (fellowship) na Mungu kupatikane na waumini wote wakati wote – Yeye ni Wakili Mtetezi wetu (1Yoh. 2:1; ling. na War. 8:26; 8:34). "Wale watendao mabaya", katika muktadha wetu siyo waumini wanaopigana vita njema – na wanaofanya toba pale wanapoanguka [mara moja-moja], bali wao ("watendao mabaya") ni wote wanaopigana dhidi ya Mungu kwa matendo yao ya uovu na ufisadi, wakienda kinyume na yaliyo mema katika yote wanayoyafikiri na kuyasema na kuyatenda. Mkristo yeyote aliye katika kundi hili [baya] atajikuta, ikiwa hafanyi toba, chini ya hatua za kinidhamu kutoka kwa Mungu, ambazo mwisho wake ni kifo chenye maumivu makali katika "dhambi inayopelekea kwenye mauti" – vinginevyo shinikizo la adhabu zinazoongezeka [kutoka kwa Mungu] zisababishe yeye kuanguka kutoka katika imani kabisa (apostasy).10

 

10 Soma Bible Basics 3B: Harmatiology, section IV.6, "Apostasy and the Sin Unto Death".

Hata hivyo, wakati hatari za kutelekeza mwenendo wetu mwema katika Kristo ziko wazi na kwa kweli zinatutia woga, faida za kuendelea kuwa wafuasi Wake katika uongofu wa mwenendo wetu ambao unaendana na uongofu unaotokana na msimamo wetu wa sasa kama waumini ni kuu pia; faida hizi kuu ni: macho yake yanaelekezwa kwetu [wakati wote], kwa mema; masikio yake yanasikiliza sala zetu. Faida hiyo ya kwanza inatokana na usimamizi Wake wa maisha yetu wakati tunapotembea kama vile Anavyotaka (Zab. 90:1ff); faida hiyo ya pili inamaanisha kwamba tumeahidiwa msaada mahususi tunaouhitaji wakati wowote tunapouomba (Matt. 7:7-8). Baraka (faida) hizi zote mbili zinahusiana kwa sababu Mungu alijua yote tunayoyahitaji hata kabla hajaumba ulimwengu (rejea fundisho la kanuni ya kudura au predestination ... katika https://sayuni.co.tz). Naye hututimizia tunayohitaji atutimizie hata bila ya sisi kuomba – na kwa kweli baraka hizi zote zilikwishawekwa katika mpango Wake, tangu milele iliyopita. Ni vyema kukumbuka kwamba tunaye Baba aliye mbinguni ambaye wakati wote anatulea na kuchunga usalama wetu, akifanya hivyo kwa utimilifu na akitupatia mahitaji yetu kila wakati wa maisha yetu.

 

8.28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu huwafanyia kazi wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

War. 8:28

 

Kupata majibu [chanya] ya sala zetu ni jambo zuri na la kutia moyo sana. Sala na maombi ni jambo muhimu sana katika maisha ya Mkristo, na majibu [chanya] kwa sala zetu siku zote husababisha furaha kuu. Mungu yuko upande wetu – na anajibu sala zetu! Petro aliuelewa vizuri sana umuhimu wa sala. Aya kadhaa kabla ya hii ya 1Pet. 3:12, aliwaonya waume kuhusu kuwatendea haki wake zao ili sala na maombi yao yasipitie katika ukinzani (katika 1Pet. 3:7b). Na baadaye katika waraka huu huu, Petro atasisitiza tena kwa wasomaji wake, wa wakati ule na wa sasa, kuhusiana na umuhimu wa utulivu katika sala pamoja na kusali mara kwa mara haswa ukichukulia kwamba nyakati za mwisho zinakaribia.

 

4.7 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.

1Pet. 4:7 SUV

 

Moja kati ya mambo mazuri na yenye baraka kuu katika kusogea kwetu karibu na Bwana kutokana na kukua kwetu kiroho na maendeleo yetu [kiroho] katika maisha yetu ya Kikristo ni ule urafiki wa karibu sana tulio nao na Bwana – na pia kujiamini kwetu kunakoongezeka kila wakati, kwamba Yeye anasikiliza sala zetu.

 

5.14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

5.15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.

1Yoh. 5:14-15 SUV

 

Wenye Juhudi Katika Mema:

 

Ikiwa tuna ari (tafsiri sisisi ya neno "ari" hapa ni wakereketwa) ya kutenda kile ambacho Mungu ametufundisha kuwa ni chema, yaani siyo tu kujiepusha na yote ambayo ni machukizo Kwake, bali kuwa na ratiba mahususi katika kusoma na kujifunza Neno Lake ili kukua kiroho, kuendelea na mchakato huo [wa kukua kiroho] na kuzaa matunda ya kiroho, basi hapo tutakuwa na haki ya kutarajia kwamba Yeye atatuepusha na migongano dhidi ya mamlaka za nchi tunamoishi au mabosi wetu kazini au yeyote tutakayekutana naye (ling. na War. 13:3). Hata hivyo, kama ambavyo matukio aliyokutana nayo Ayubu yanavyotukumbusha, ziko nyakati ambazo waumini wanaoelekea kwenye upevu wa kiroho watapitia "mateso wasiyostahili" kama mtihani wa hadhi yetu hiyo (Ayubu 1:7-8) na pia kuendeleza upevu huo wetu wa kiroho.

 

1.2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;

1.3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

1.4 Basi acheni saburi na ifanye kazi [yake kwa] ukamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila ya ninyi kuonekana wenye mapungufu.

Yak. 1:2-4

 

1.12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Yak. 1:12 SUV

 

Hivyo ikiwa tunatenda mapenzi ya Mungu na kujiepusha na yaliyo maovu, tunapaswa kujiamini pale tunapokabiliwa na mateso, tukifahamu kwamba dhiki tunayopitia ni mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu, na kwamba atatuvusha salama, hata ikibidi aitenganishe bahari kwa ajili yetu. Kwa hiyo, tunayo haki ya kuiweka kando hofu, tukijua kwa uhakika kwamba Bwana Mchungaji wetu atatuvusha salama.

 

3. Nitakaposhikwa na hofu, nitakutumainia Wewe;

4. Nitalisifu jina Lake, na katika Yeye ninaliweka tumaini langu; mwenye mwili atanitenda nini?

Zab. 56:3-4

 

1.27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;

1.28 wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu.

Wafi. 1:27-28 SUV

 

Badala Yake, Mnyanyueni Kristo:

 

3.15 Bali mnyanyueni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu [juu ya vyote vingine]. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye sababu ya tumaini lililo ndani yenu;

1Pet. 3:15

 

Yani "badala ya" kuingiwa na hofu tunapokuwa katika shinikizo, tukiteseka kwa ajili ya Jina Lake. Katika hili tunapaswa kuweka akilini ule mfano wa mitume na ndugu zao [katika Kristo] ambao waliimba sifa za Bwana pale walipokabiliwa na manyanyaso na kuteseka kwa sababu walikuwa wakieneza Injili kwa faida ya Kanisa Lake (Matendo 16:25-26; ling. na Wafi. 1:29).

 

5.40b … wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao.

5.41 Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo.

Matendo 5:40b-41 SUV

 

"Kumnyanyua Kristo" katika mioyo yetu, yaani "kumtakasa Kristo" au "kumchukulia kuwa ni mtakatifu" ndani ya mioyo yetu, maana yake ni kuweka "nafasi takatifu" ya ushirika na Bwana ndani ya mioyo yetu ambamo mambo yote machafu yameondolewa, maana yake ni kumpenda Kristo kwa moyo wote, ni kuelekeza macho yetu [ya kiroho] Kwake.11 Kama tunatembea kwa ukaribu na Kristo, hatuwezi kujizuia kuwa na furaha tunapokabiliwa na mateso / dhiki, kwani Yeye ndiye furaha yetu, nasi tunafurahi kwamba tu Wake.

 

8 Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.

Zab. 16:8

 

1.21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.

Wafi. 1:21 SUV

 

11.27 Kwa imani [Musa] akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye Yeye asiyeonekana.

Waebr. 11:27 SUV

 

12.1 Basi na sisi pia [kama waumini wanaotajwa katika sura ya 11], kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii [watu na malaika], na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi (maeneo ya tabia zetu ambamo tuna udhaifu mkubwa zaidi); na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

12.2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu (Alfa na Omega); ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Waebr. 12:1-2

 

Hali hii [ambayo ni ya wakati wote] ya kuelekeza macho yetu kwa mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, Nafsi Yake, alichokifanya kwa ajili yetu, na atakayoyafanya kwa ajili yetu, yote ni matokeo na malengo ya kupevuka kiroho, ambavyo navyo msingi wake ni bidii katika mchakato wa kukua kiroho. Ni lazima tufanye bidii katika mchakato wa kukua kiroho ili tufikie mahala ambapo tutakuwa na kiwango cha kutosha cha ile kweli ya Biblia ndani ya mioyo yetu ili Roho Mtakatifu aweze kuitumia [kweli hiyo] katika kutusaidia kuelekeza macho yetu kwa Kristo, na baada ya hapo kuifanya hiyo kuwa ndiyo kipaumbele cha kimungu katika maisha yetu ili kuendelea "kumwona Yeye asiyeonekana".

 

11 Soma Bible Basics 6A: Peripateology, section I.B.6, "Focusing on Christ".

Kwa wale wanaofanya juhudi katika hili, yaani kuufikia upeo wa kupevuka kiroho kunakohitajika, na kuweka kipaumbele cha kuelekeza macho yetu Kwake wakati wote, hakuna furaha iliyo kuu zaidi ya hiyo katika maisha yetu hapa duniani.

 

8. Ijapokuwa hamjamwona, mnampenda tu. Ijapokuwa hamwezi kumwona kwa wakati huu, mna imani juu Yake. Kwa sababu hii mna furaha ambayo hamwezi hata kuielezea, ambayo inaonyesha ile milele ijayo yenye utukufu,

9. pale mtakapokabidhiwa ule ushindi mkuu wa siku ya mwisho – wokovu wa maisha yenu – ambao ndiyo lengo na nia ya imani yenu hii.

1Pet. 1:8-9

 

Mwe Tayari Siku Zote Kumjibu [Mtu Aulizaye]:

 

... Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye sababu ya tumaini lililo ndani yenu;

1Pet. 3:15b

 

Aya hii mara nyingi hutumika katika majadiliano ya utetezi mahususi wa kimfumo wa imani ya Kikristo (Christian Apologetics), na hii ni sahihi. Lakini wakati huduma hii ya 'Christian Apologetics' kwa Mkristo aliyeitwa [na Bwana] afanye hivyo mbele ya kadamnasi ni jambo stahiki kwa mtu wa aina hiyo, aya hii inafaa kwa Wakristo wote. Pale tunapoulizwa na watu wasioamini kuhusu chanzo cha tumaini letu, tunapaswa kupenda na kuwa tayari wakati wote kuitangaza habari njema ya uzima wa milele na ufufuo kwa njia ya imani katika Bwana Yesu Kristo, Mungu-mtu aliyekufa kwa ajili ya dhambi zetu zote na hivyo kutuokoa kutoka katika maangamizi yaliyo mabaya zaidi ya kifo.

 

Kitu muhimu cha kuweka akilini ni muktadha wa fundisho lenyewe. Wakati watu wasioamini wanaoishi katika maeneo tunamoishi sisi pia wanaweza kufahamu kwamba sisi ni Wakristo – nasi tuna tumaini hilo – sababu yao ya kuja kwetu na kutuuliza kuhusu tumaini tulilo nalo haitokani na kauli zetu za utetezi wa Kikristo tulizozitoa (au labda kuvaa mkufu wa msalaba, au kuweka kibandiko chenye maandiko WWJD – What Would Jesus Do? - kwenye vioo vya magari yetu, n.k.); bali, katika aya zilizopita tumeelekezwa kuwa shupavu na wenye ujasiri tunapokabiliwa na mateso, haswa ikiwa mateso hayo hatustahili. Hili ndilo jambo muhimu: kuwa na mwonekano [wa sura] tulivu na wenye furaha wakati ni wazi tunateseka ni ushuhuda ambao watu hawa wasioamini wanaona ni jambo la ajabu. Na kwa kweli hili ni jambo la ajabu na la kushangaza. Hii ni kwa sababu hata mtu asiye Mkristo ambaye ni shupavu na anayejiamini kwa kiasi kikubwa anaweza kushikwa na uchungu na kutaka kurudisha kisasi pale anapoteseka kutokana na uonevu. Unahitajika msaada kutoka juu – msaada wa Roho Mtakatifu – akifanya kazi pamoja na roho ya Mkristo aliyepevuka, kutenda na kuenenda katika namna iliyo tofauti na ile inayotarajiwa na ulimwengu. Ukweli ni kwamba waumini wengi [pamoja hata na] wale waliopevuka, hupata shida katika "kuhesabu kuwa ni furaha" wakati wanapopitia magumu, na haswa magumu hayo yanapotoaka na uonevu (Yakobo 1:2-4). Hivyo, katika zile nyakati nadra sana ambazo Mkristo anaelekeza nguvu zake katika kumfurahisha Bwana Yesu Kristo, tukitazamia thawabu zetu za milele na hivyo kwa wazi kabisa tukiwa na tumaini licha ya kuwa chini ya shinikizo na ndani ya dhiki – kwa sababu tumaini letu, "hazina yetu", iko ng'ambo ya haya maisha mafupi (Matt. 6:19-21) – hii itawafanya watu wanaotuzunguka watutazame na kujiuliza furaha yetu inatoka wapi? Na hapo kama kuna yeyote 'aliyechaguliwa' kwa ajili ya uzima wa milele, basi fursa nzuri sana ya ushuhuda (ndani yake mkiwa na uinjilisti) itatokea. Hivyo, hatupewi fursa kama hizo bure au kiurahisi tu, bali ni matokeo (faida) ya mchakato wa kukua kiroho pamoja na matumizi shupavu ya ile kweli tunayojifunza chini ya hayo mazingira magumu tuliyoyazungumzia hapo juu ("shinikizo na dhiki").

 

4 Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako (dhidi yako), Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.

Mhu. 10:4 SUV

 

Kwa Upole na kwa Heshima:

 

3.16 lakini kwa upole na kwa heshima, mkifanya hivyo kwa dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao (wanaoukashifu) mwenendo wenu mwema katika Kristo.

1Pet. 3:16 SUV

 

Kuhusiana na upole pale tunapotoa ushuhuda wetu kwa ajili ya Bwana wetu, mwongozo unaotolewa na Petro hapa juu ni muhimu sana kuukumbuka. Sisi wenyewe si kitu chochote – sisi ni vyombo tu vinavyotumika kutoa ushuhuda. Mhusika mkuu hapo ni Bwana Yesu Kristo aliyekufa kwa ajili ya mtu au watu tunaowashuhudia. Kama wataipokea kweli ambayo Roho Mtakatifu anaiweka wazi kupitia maneno tunayotamka mbele za watu hao, au la, ni kati yao na Mungu. Sisi hatuwi Wakristo bora zaidi ikiwa wataipokea kweli tunayoitamka na wala hatui Wakristo wabovu ikiwa wataikataa kweli hiyo – na kwa kweli tusifanye kosa la kujitathmini [sisi wenyewe] kwa jinsi watu tunaowashuhudia wanavyoipokea kweli ya injili au wanavyoshindwa kufanya hivyo (Wakor. 4:5). Bwana Yesu Kristo ndiye aliyekufa kwa ajili yao (na kwa ajili yetu). Roho Mtakatifu anaiweka kweli hii bayana mioyoni mwao. Na Mungu Baba anawafanya wazaliwe upya, wazaliwe kutoka juu – ikiwa watauitikia wito huu kwa imani. Sisi ni "watumwa wasio na faida, ambao walikuwa tu wakitimiza wajibu wao katika mazingira walimojikuta" (Luka 17:10).

 

Kuhusiana na heshima, kila mwanadamu ameumbwa katika mfano wa Mungu, ambao ni haki ya utashi huru alio nao ya kufanya maamuzi ya kujipatanisha na Mungu au la, kuikubali na kuipokea ile Tunu ya Bwana Yesu Kristo kwa njia ya imani, au la. Kukubali au kukataa kwao hakutatokana na umahiri wetu katika balagha (elimu ya usemaji) wala uwezo wetu katika kushawishi, na wala tusijipe thamani yoyote ikiwa watampokea Kristo au la: hili ni suala linalomhusu Bwana Yesu Kristo. Hivyo, ikiwa nafsi zetu zinashabihiana na wale ambao Mungu anatuletea kama fursa za ushuhuda wetu au hatushabihiani nao (katika Kiingereza limetumika neno "like"), tunapaswa kuelewa kwamba damu ya Bwana Yesu Kristo ilimwagika kwa ajili yao kila mmoja – Yeye alikufa kwa ajili ya dhambi zao zote, na Baba anataka wote waokolewe (Eze. 18:23; Matt. 18:14; Yoh. 12:47; 1Tim. 2:4; 2Tim. 2:23-26; 2Pet. 3:9). Na Roho Mtakatifu atalifanya suala la wokovu wao wazi kabisa mioyoni mwao. Lakini kwa hakika uamuzi ni wa kwao, na sisi Wakristo tunaoshuhudia tunapaswa kuyaheshimu maamuzi yao [kuhusiana na suala hili] wakati wote.

 

Katika kuonyesha heshima, pia ni muhimu kuweka msisitizo katika Injili na Bwana Yesu Kristo, na si kuruhusu mambo yasiyostahili kuingilia ushuhuda tunaoutoa. Tunapotoa ushuhuda wa Injili, kamwe tusifanye kosa la hata kudokeza [tu] kwamba wokovu unahusiana na mwenendo [binafsi], au kuitumia fursa hiyo katika kufundisha kwamba mtu tunayemshuhudia anapaswa "kuanzia sasa" kuacha dhambi hii au ile. Injili, katika tafsiri yake sisisi, ni habari njema – habari njema ya uzima wa milele kwa njia ya imani katika Kristo pekee, uzima unaotolewa [bure] kwa neema ya Mungu (Waefe. 2:8-9)! Wote wanaompokea Kristo wanabadilishwa – na wataendelea kubadilishwa ... ikiwa watakuwa wafuasi Wake. Si kazi yetu kuingilia ratiba ya Mungu na kuivuruga Injili kwa kuitia chachu ya usheria-sheria.12

 

5.20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu;

twawaomba (twawasihi) ninyi kwa ajili ya (kwa niaba ya) Kristo mpatanishwe (mfanye upatanishi) na Mungu.

2Wakor. 5:20

 

Ikiwa tutakabiliana na mateso tusiyostahili katika uadilifu na tumaini la Kikristo, na ikiwa tutaishuhudia nguvu ya ile kweli ya Injili kama ambavyo Bwana Yesu Kristo ametutuma, kwa unyenyekevu na heshima, basi tutawanyima fursa wale wanaotupinga na kutuzushia uwongo. Badala yake, mwanga wa kweli katika uweza wa Roho Mtakatifu utaangaza katika nafsi zetu katika namna ambayo haiwezi kukanushwa, ukiwatia aibu wazushi wote.

 

21.15 kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

Luka 21:15 SUV

 

Afadhali Kuteswa kwa [Sababu ya] Kutenda Mema:

 

3.17 Maana ni afadhali kuteswa [katika mikono ya wasioamini] kwa [sababu ya] kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko [kuteswa] kwa [sababu ya] kutenda mabaya.

1Pet. 3:17

 

Fundisho la muhimu katika sehemu hii ya masomo yetu ni kwamba Mungu wetu siku zote anamfanyia kazi kila mtu kwa ajili ya mema [yake]. Mpango wa Mungu ni [m]timilifu. Kama tunauitikia uongozi wa Mungu tunaopewa hapa, basi hata kama mambo yanaenda kunyume na matarajio yetu na tunaingia katika dhiki, basi kiuhalisia hayo ndiyo matokeo ya Mungu "anapowafanyia kazi wale wampendao katika kuwapatia mema" (Warumi 8:28). Hivyo, hata kama ni mapenzi ya Mungu kwamba tupitie mateso, basi tunapaswa kufahamu kwamba kuna sababu njema nyuma yake. Katika mfano hapo juu, ushuhuda wetu shupavu tukingali katika tanuri la moto mkali [wa mitihani] ni jambo la kushangaza kwa watu wasioamini ambao wanahisi mioyoni mwao kwamba kuna nguvu isiyo ya kibinadamu inayotulinda tusiteketezwe na mateso hayo (Maombolezo 3:21-23). Petro hapa anaona [na kutarajia] kwamba matukio kama haya yanatupatia fursa za kutoa ushuhuda wetu kwa ajili ya Mungu – ili ushuhuda huu uwe na matokeo ya wokovu wa wale watakaiona nguvu ya Mungu ikifanya kazi ndani yetu. Yosefu aliuzwa utumwani na ndugu zake, akashitakiwa kwa [ushahidi wa] uwongo na mke wa tajiri / bwana wake, akafungwa gerezani, akasahauliwa na mtu aliyemsaidia – lakini mwisho wa yote alitolewa gerezani na Mungu na

akafanywa mtawala wa Misri yote.

 

12 Tizama Bible Basics 4B: Soteriology, section II.6.f, "False Issues".

20 Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.

Mwa. 50:20 SUV

 

III. Ibara ya Tatu (aya za 18-22)

 

3.18 Kwa maana Kristo naye aliteswa [na akafa] mara moja kwa ajili ya dhambi [zetu], Mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; katika mwili wake akauawa, bali akahuishwa na Roho [Mtakatifu],

3.19 Naye kwa uweza wa huyo huyo Roho Mtakatifu aliwaendea roho (malaika, wale wa Mwanzo 6) waliokaa kifungoni, akawatamkia ushindi Wake;

3.20 hawa ndio wale malaika wasiotii hapo zamani, uvumilivu (ustahamilivu) wa Mungu ulipokuwa ukingoja, katika siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, walioko[lewa] kutoka kwa maji.

3.21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo [wa Roho Mtakatifu], unaowaokoa ninyi pia siku hizi; siyo kuwekea mbali (kutoa) uchafu wa mwili [kwa kuoshwa na maji], bali [kwa njia ya kumwomba Mungu atupatie dhamiri safi kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.

3.22 Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini [ya miguu] yake (Zab. 110).

 

Kwa Maana Kristo Alikufa Mara Moja kwa Ajili Yetu:

 

Bwana Yesu Kristo ndiye mfano nambari moja kwa waumini wote (Matt. 16:24; Wafi. 6:2-8; 1Pet. 2:21; Waebr. 12:2; 1Pet. 4:13). Kazi yetu hapa duniani baada ya kuokolewa na kuwa wafuasi Wake, tukipita katika hatua/nyayo Zake, tukifuata mfano aliouweka, tukishiriki katika mateso Yake ikiwa tutaitwa kufanya hivyo (War. 8:17; 2Wakor. 1:5; Wafi. 1:29-30; 3:10; Wakol. 1:24; 2Tim. 2:12; ling. na 2Tim. 3:12). Petro anaposema “kwa maana” katika mwanzo wa aya ya 18 hapo juu, anaunganisha aya na ibara hii na mjadala / mafundisho yaliyotangulia. Sisi waumini wa Kristo tunapaswa kuvumilia mateso tusiyostahili kwa kufuata mfano wa Bwana wetu Yesu Kristo. Hakuna muumini yeyote aliyestahamili mateso asiyostahili kama Bwana wetu, wakati wote wa miaka 33 ya maisha Yake kabla ya msalaba, wakati wote wa dhihaka, matusi, vipigo katika masaa yale kadhaa yaliyopelekea kwenye msalaba, na haswa baada ya kutundikwa msalabani, wakati wa yale masaa matatu katika giza pale msalabani alipokufa kwa ajili ya dhambi zetu zote, akilipa gharama yote ya moto kwa kila dhambi ambayo wewe na mimi tumeitenda, “ili aweze kutuleta kwa Mungu” (1Pet. 3:18). Aliteseka akiwa ndiye pekee mwongofu kwa ajili yetu sisi tusio na uongofu, ambao sasa tumeipokea haki / uongofu wa Mungu kwa njia ya imani katika Yeye (War. 3:21-24; 3:28; 4:4-5; 4:13; 5:1; 5:8-9; 8:1; 9:30-31; 10:6; 2Wakor. 5:21; Waga. 2:16; Waefe. 2:8-9; Wafi. 3:9; Waebr. 11:7). Hivyo, Bwana wetu ndiye mfano wetu nambari moja wa jinsi ya kuonyesha staha wakati tunateswa kwa uonevu – kwa kuwa hakuna aliyekaribia kiasi cha mateso alichostahamili, hata kabla ya kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu, na hata kabla ya mateso yaliyopelekea kwenye msalaba.

 

Lakini kustahimili [mateso] mtendapo mema, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.

2.21 Ninyi mliitwa kwa makusudi haya, kwa sababu Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachia kielelezo, ili mfuate nyayo zake.

2.22 “Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake” (Isa 53:9b).

2.23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya (hakumtishia mtu); bali alijikabidhi (alimtumaini) kwake Yeye ahukumuye kwa haki.

2.24 Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili Wake ili sisi, baada ya kuwa wafu kwa dhambi, tuweze kuishi kwa haki / uongofu. Kwa majeraha Yake sisi tumepona.

1Pet. 2:20b-24

 

Hivyo Petro alikwishatupatia fundisho hili kabla, na analirudia hapa kwa msisitizo, na pia kuifunga / kuitamatisha sehemu hii ya mafundisho yake yanayohusu mateso ya uonevu kwa kutukumbusha kwamba Mwokozi wetu alitembea barabara hii [ya mateso] kabla yetu, na kwamba kwa kuwa sisi ni watu Wake, tuna wajibu wa kufuata mfano Aliouweka, ikiwa tumepangiwa kustahamili mateso tusiyostahili kwa ajili ya Jina Lake takatifu.

 

Lakini hii si sababu pekee ya Petro katika kutukumbusha mfano wa ustahamilivu wa Kristo katika mateso kwa ajili yetu. Baada ya kutukumbusha kwamba Bwana wetu alipitia mateso hayo yote kwa ajili yetu na kutuwekea mfano wa jinsi ya kuenenda ikiwa ni mapenzi ya Mungu kwa sisi kupitia dhiki tusiyostahili, Petro sasa anatudhihirishia jinsi Kristo alivyoweza kufanya hivyo, yaani kwa njia ya kuwezeshwa na Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana halisi na mada kuu ya hii ibara ya mwisho ya sura ya tatu, na hii dondoo kuu ndiyo ambayo mara nyingi watu hawaioni kabisa na kutoielewa.

 

Akauawa Katika Mwili Wake; Akahuishwa kwa Uweza wa Roho Mtakatifu; Ingawa Bwana wetu alibeba dhambi zetu katika mwili Wake pale msalabani ili tuweze kuokolewa – na baada ya hapo akaipumua [nje] roho Yake na kufa – alifufuliwa na Roho Mtakatifu kabla ya mwili Wake kuharibika (Zab. 16:10; Matendo 2:32; 13:35).

 

1.3 [Injili] ambayo ni habari ya Mwana [wa Mungu], Yeye ambaye ni uzao wa Daudi katika mwili Wake,

1.4 na akafanywa kuwa Mwana wa Mungu kwa uweza wa Roho wa Utakatifu kwa njia ya ufufuo kutoka kwa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu.

War. 1:3-4

 

8.11 Lakini, ikiwa Roho Wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

War. 8:11 SUV

 

4.14 tukijua ya kwamba Yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha (present us) pamoja nanyi.

2Wakor. 4:14

 

Pamoja na msalaba, ufufuo ni tukio adhimu na la kustaajabisha kuliko yote katika historia ya wanadamu. Ufufuo ndio shabaha ya tumaini letu kama ambavyo ibara za hapo juu zinavosimulia, na ile ahadi ya kunyanyuliwa kutoka mauti – licha ya yote ambayo macho yetu ya kibinadamu yanatuonyesha – ndiyo kiini cha mvuto wa Injili: kwa njia ya imani katika Bwana Yesu Kristo, sisi Wakristo si watumwa tena na uhalisia wa kifo uliomo ulimwenguni kote, uhalisia ambao unawatia hofu wale wote wasiokuwa na tumaini hili kuu (Waebr. 14-15; ling. na 2Tim. 1:10). Hivyo, siku zote ufufuo umesisimua akili na mioyo ya wale wanaotangaziwa Injili (kw. mf. Matendo 4:2; 17:18; 23:6 na aya zinazoifuata). Hivyo kwa hakika ni jambo la kufaa sana kwamba Petro anaitumia hii huduma kuu ya Roho Mtakatifu (“atahuishwa na Roho Mtakatifu”), pamoja na msalaba, ambapo Bwana wetu alipata ushindi unaotupatia sisi haki ya kuokolewa na kuzawadiwa uzima wa milele (“akauawa katika mwili Wake”), kutamatisha ibara hii kwa kuelezea kwa kifupi ile kazi ya Roho Mtakatifu katika ujio wa kwanza wa Bwana Yesu Kristo.

 

3.34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu [Mungu] hamtoi Roho [Mtakatifu] kwa kipimo [… Jesus had the Spirit “without measure/limit”].

Yoh. 3:34

 

Kwa hakika, Roho Mtakatifu ndiye aliyemwezesha Bwana wetu katika kila taswira ya maisha yake [Bwana wetu]. Kila kitu katika ujio wa kwanza wa Bwana wetu kilihusishwa kwa undani na ukaribu kabisa na Roho Mtakatifu. Roho alihusika katika kutungwa kwa mimba ya mama Yake (Matt. 1:18-20; Luka 1:35); Bwana wetu alijazwa na Roho Mtakatifu tangu kuzaliwa Kwake (Isa. 11:2; 42:1; 48:16; Mika 3:8; Matt. 12; 17-18; Ufu. 5:6; Yoha. 3:34-35; Lk. 1:15); Bwana wetu alikuwa katika neema na akajiandaa ili atoe huduma / utumishi uliozidi utumishi wote wa wanadamu kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu (Isa. 53:1-2a; Lk. 2:40; 2:52; ling. na Zab. 1:1-2; 16:8; 119;9); ishara ya wazi ilitolewa na Roho Mtakatifu katika kuuthibitisha mwanzo wa utumishi Wake (Matt. 3:16; Mk. 1:10; Lk. 3:22; Yoh. 1:33b); na akaongozwa na Roho Mtakatifu kuelekea nyikani ili akajaribiwe (Matt. 4:1; Mk. 1:12; Lk. 4:1); matendo makuu ya utumishi Wake yaliwezeshwa na Roho Mtakatifu katika kila nyanja yake (kw. mf. Matt. 12:28; 1Tim. 3:16); na sadaka Yake kwa ajili yetu pale msalabani Kalvari iliwezekana tu kwa njia ya kuwezeshwa na Roho Mtakatifu (Waebr. 9:14).13

 

Hivyo ndivyo Petro, katika kutukumbusha ufufuo kwa faida yetu kama ule mwujiza mkuu wa Roho Mtakatifu kwa niaba ya Kristo, kwa kifupi tu na kwa ujumla, anatukumbusha taswira mbalimbali za huduma ya Roho Mtakatifu kwa Kristo wakati wa maisha Yake hapa duniani, maisha yaliyotamatishwa na ufufuo huo (tukio lililofuatiwa na kupaa Kwake mbinguni, kukaa Kwake katika mkono wa kuume wa Baba, na kutukuzwa Kwake).

 

16.7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi (paraclete, ‘Anayetia moyo’ / Anayewezesha) hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

Yoh. 16:7

 

12.4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

12.5 Tena pana tofauti za huduma (ministries), na Bwana ni yeye yule.

12.6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

 

13 Haya ni maelezo mafupi tu; kwa maelezo ya kina kuhusu huduma ya Roho Mtakatifu kwa Bwana wetu katika ujio Wake wa kwanza, tizama BB5: Pneumatology, section II.C, “The Example of Christ”.

12.7 Lakini kila mmoja [wetu sisi Wakristo] hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya Kanisa.

1Wakor. 12:4-7

 

12.11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo Yeye.

1Wakor. 12:11 SUV

 

Kama ambavyo ibara zinazonukuliwa hapo juu zinavyodhihirisha, ile Tunu ya Roho Mtakatifu ndiyo faida ya msingi kabisa ambayo sisi waumini wa Enzi hii ya Kanisa tunayo. Ni kwa kupitia Kwake, uweza Wake, na karama anazotupatia sisi kama wale walio wafuasi wa Bwana Yesu Kristo, ndiyo tunawezeshwa kufanikisha maagizo tuliyopewa na Bwana wetu Yesu Kristo, ya kukua, kuendelea, na kuzaa matunda kwa ajili Yake. Bwana Yesu Kristo ndiye mfano wetu. Alitimiza mapenzi ya Baba, ushindi wa msalaba ulio msingi wa mapenzi hayo [ya Baba] na yote yaliyotangulia msalaba, kwa njia ya Roho Mtakatifu, nasi hatuwezi kufuata nyayo za Bwana wetu bila kuitumia huduma ya Roho Mtakatifu kikamilifu katika kufuata mfano wa Bwana wetu.

 

8.14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana [wa kweli] wa Mungu.

War. 8:14 SUV

 

5.18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi [ambao unafuja tabia njema mliyokuwa nayo awali]; bali mwendelee kukamilishwa (kufanya maendeleo katika kukua kiroho) na Roho Mtakatifu (yaani tofauti na ufisadi, mpate kujifunza na kuelewa maandiko);

Waefe. 5:18

 

4.14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo basi hiyo ni baraka ya kweli kwenu, kwa kuwa Roho wa utukufu, yaani Roho wa Mungu, anawakalia (ili mumtegemee katika mtihani huo mnaopitia).

1Pet. 4:14

 

Roho Mtakatifu ndiye Mwelekezi na Msaidizi katika mambo yote, na, kama ibara ya mwisho hapo juu (1Pet. 4:14) inavyoweka wazi, Yeye ndiye anayetuhimilisha katika nyakati za mitihani na [ma]shinikizo magumu kabisa. Ili tuweze kustahamili aina ya mateso tusiyostahili yanayokaribia kiwango cha yale mateso aliyostahamili Bwana wetu (yaani “kushiriki [katika] mateso ya Kristo”, yanayojadiliwa katika mwanzo wa sehemu ya III), kama Yeye alivyoweza, sisi waumini tunapaswa kuitumia kikamilifu huduma ya Roho Mtakatifu.14 Ni kwa njia hii tu, [kwa hakika], ndiyo tunaweza kuwa na tumaini la kutimiza maagizo yaliyotolewa katika ibara iliyotangulia. Kama ambavyo Roho alikuwa na Bwana Yesu, akimwezesha katika kila hatua, katika kila shinikizo na katika kila mtihani aliohimili, nasi pia tunahitaji kuchukua hatua za kumfuata Roho Mtakatifu, tukijazwa na kukamilishwa Naye, tuwezeshwe na kutiwa nguvu Naye, ili tutimize yale maagizo tuliyopewa na Bwana

Wetu katika kila hatua tunayotembea, bila kujali mateso tunayoitwa kupitia kwa niaba ya Bwana wetu Yesu Kristo.

 

14 Tizama BB5: Pneumatology, section II.B, “Empowerment of the Believer”, na BB6A: Peripateology.

Hiki ndicho kiini cha ibara ya 3, kikiandikwa kwa kifupi kwa maneno “akihuishwa na Roho Mtakatifu”: Kristo alifanikisha kila kitu alichokifanya kwa njia ya Roho Mtakatifu, na hii ndiyo njia ambayo nasi tutaweza kuhimili kimungu mateso tusiyostahili yanayosimuliwa katika aya hapo juu (1Pet. 3:13-17). Kwa kufuata uongozi wa Roho na kujiweka katika hali ya kuwezeshwa Naye, mambo yote mema yatakuja kwetu, ufufuo na yote yanayohusishwa nao na yote mengine yanayotangulia neema hiyo kuu katika maisha ya Mkristo, kama ilivyokuwa kwa Bwana wetu. Ikiwa tutakuwa na subira na tutazitumia nyenzo (za kimwili na za kiroho) tunazotunukiwa na Roho Mtakatifu,15 tunaweza kuwa na tumaini kamili siyo tu la ufufuo (kama ilivyokuwa kwa njia ya Roho Mtakatifu Bwana wetu alifufuliwa baada ya mauti Yake kwa ajili yetu), lakini pia [tunaweza kuwa] na uhakika wa kutiwa moyo kila wakati, kusaidiwa na kuhimiliwa katika kuishi maisha yetu kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo – vyote vikipokelewa kutoka kwa Mungu Roho Mtakatifu ambaye yuko ndani yetu.

 

5.16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

5.17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

5.18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria [ya Musa].

5.19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu [mwenendo wa aibu], ufisadi,

5.20 ibada ya sanamu [madawa ya kulevya, kutegemea watu, malaika], uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

5.21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

5.22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

5.23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

5.24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

5.25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

Waga.5:16-25 SUV

 

Kwa Uweza wa Huyo Huyo Roho Mtakatifu:

 

3.19 Naye kwa uweza wa huyo huyo R.M. aliwaendea roho (malaika, wale wa Mwanzo 6) waliokaa kifungoni, akawatamkia ushindi Wake;

3.20 hawa ndio wale malaika wasiotii hapo zamani, uvumilivu (ustahamilivu) wa Mungu ulipokuwa ukingoja, katika siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokolewa kutoka kwa maji.

1Pet. 3:19-20

 

Baada ya Bwana wetu kupumua [nje] roho Yake ya kibinadamu na mwili Wake kufa,

alishuka mpake Hades / Sheol, akaingia katika paradiso iliyoko chini ya dunia (1Sam. 28:15; 28:19; 2Sam. 12:23; Lk. 16:19-31; 23:43), ambamo waumini wale walioaga dunia walipelekwa [na kukirimiwa] kabla ya kupelekwa mbingu ya tatu na Kristo pale alipopaa

 

15 Tizama BB5: Pneumatology, section II.B.3.b.3, “Walking in the Spirit”.

(Zab. 68:18; Waefe. 4:8-10; ling. na Yoh. 12:26; 14:1-3; 17:24; 2Wakor. 5:8; Wafi. 1:23). Kwa sasa waumini wote wanaoaga dunia wanapelekwa moja kwa moja mbinguni / mbingu ya 3. Hivyo Bwana wetu, katika kipindi kifupi kati ya tukio la msalaba na lile la ufufuo, alijistarehesha kwa ushirika na Abrahamu, Lazaro na yule mwivi aliyeokolewa msalabani Kalvari – na waumini wengine wale walioaga dunia kabla ya tukio hilo – halafu, baada ya zile siku 40 alizokuwamo duniani baada ya ufufuo (Matendo 1:3), aliwachukua waumini wote waliokuwako katika paradiso hiyo na kuwaongoza kuelekea mbinguni / mbingu ya 3, akipaa katika utukufu na kuwafikisha kwa Baba (Zaburi 68:18; Waefe. 4:8; ling. na Zab. 68:24-27; Yoh. 14:2-3; Wakol. 2:15; Ufu. 1:18).16

 

4.7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha [karama] / kipawa chake Kristo.

4.8 Hivyo husema, “Alipopaa juu Aliteka mateka (yaani, wale waumini waliookolewa kabla ya msalaba), Akawapa wanadamu vipawa”.

4.9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?

4.10 Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote (mpaka mbingu ya tatu, makazi ya sasa ya Baba), ili atimize mambo yote (yaani kuukamilisha ushindi uliopatikana msalabani; ling. na Zab. 110:1).

Waefe. 4:7-10

 

Aya tunayoijadili sasa, 1Pet. 3:19, inatusimulia kwamba katika matembezi Yake ya muda mfupi katika “pande zilizo chini ya nchi”, Bwana wetu pia alitoa tamko la ushindi Wake pale msalabani kwa wale malaika walioanguka (pepo) ambao hadi sasa ni wafungwa katika Abyss – lindi au shimo kuu. Hades / Sheol, iliyoko chini ya dunia, kama ilivyo mbingu ya 3, “si sehemu ya uumbaji huu” tuliomo. Hii ni kusema, Hades / Sheol siyo sehemu ya “mbingu na nchi / dunia” za sasa (zilizoundwa upyarestored – katika zile siku 7 za kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza kuanzia aya ya 3 na kuendelea) ambazo zitaharibiwa (Ufu. 20:11; ling. na Zab. 102:26; Isa. 13:13; 34:4; 51:6; Hagai 2:6; 2:21; Matt. 24:35; Waebr. 1:11-12; 12:25-29; Ufu. 6:14) na mahala pake patachukuliwa na mbingu mpya na nchi mpya hapo mwishoni mwa historia ya wanadamu (Ufu. 21:1; ling. na Zab. 102:25-26; Isa. 65:17; Isa. 66:22; 2Pet. 3:7-13). Hades / Sheol ina sehemu 4: Paradiso (aka “Abraham’s Bosom”, “Kifuani mwa Abrahamu”), Torments (sehemu ya Mateso, ambamo wasioamini walioaga dunia wanakaa kwa sasa), Abyss (lindi / shimo kuu, aka, “Tartarus”, ambamo idadi fulani ya pepo wamefungwa kwa sasa), na Ziwa la Moto (ambamo kwa sasa hamna mkaaji, lakini hapo ndipo patakuwa “maskani” ya [wanadamu] wote wasioamini na pepo).17 Tunajua kwamba yule tajiri aliweza kuzungumza na Abrahamu “kwa kupaza sauti yake ili iweze kuvuka lile shimo kubwa” lililokuwa kati ya Paradiso na Torments, kwenye mateso,

(Luka 16:26), lakini hatuambiwi kama kuna uwezekano wa pepo waliofungwa ndani ya Abyss kuwa na mawasiliano, hata ya mbali kabisa, na zile sehemu nyingine mbili zenye wakazi, za Hades / Sheol. Kwa sababu hii, ili Bwana wetu aweze kutangaza ushindi Wake

 

16 Tizama BB 4A: Christology, section I.5.o.23, “The Transfer of Believers from the Subterranean Paradise to the Third Heaven”.

17 Tizama chati “The Waters Above” and the following discussion in BB 2B, and also the posting, “The Geography of Heaven and Hell” in https://ichthys.com

kwa hawa waasi – viumbe pekee katika ulimwengu ambao hawakuwa na namna yoyote ya kuujua ushindi wa Bwana wetu ulioamua hatma yao ya milele – Roho Mtakatifu aliiwezesha safari ya kipekee na ya kimwujiza ya Bwana Yesu Kristo ili aende Tartarus (Abyss) kwa shabaha ya kuwataarifu rasmi pepo hawa kwamba kwa sasa wameshindwa kabisa, na hatma yao ni Ziwa la Moto.

 

2.14 [Mungu] akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki pamoja na hukumu zake (yaani, hulka yetu ya dhambi na dhambi binafsi tulizotenda), iliyoleta uadui katika uhusiano wetu na Yeye; Akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

2.15 [kwani kwa njia ya msalaba] *Aliwavua enzi na mamlaka ule uweza wao, na kuwaaibisha hadharani, Alipopata ushindi dhidi yao katika Kristo.

Wakol. 2:14-15 * Hawa ni pepo

 

Idadi kubwa tu ya pepo waliofungwa wamekuwako katika Abyss tangu walipopelekwa mle kama adhabu ya kufanya mahusiano ya kimwili na wanawake wa kibinadamu kabla ya gharika na hivyo kuvunja amri na maelekezo ya Mungu aliyoyaweka kwa ajili ya wakati wote wa historia ya wanadamu (1Pet. 3:19-20a; 2Pet 2:4-10a; Yuda 1:5-7). Pale Bwana wetu alipowatokea akiwa katika mwili Wake wa ufufuo ambao ni mwili mng’aavu kweli kweli na wenye utukufu mkuu, hii [lazima] ilikuwa ni mara ya kwanza kwa viumbe hawa wa kale kupata ahueni dhidi ya giza totoro la pale Abyss ambalo ndilo adhabu yao ya sasa (2Pet. 2:4; Yuda 1:6; ling. na Isa. 24:21-23; Luka 8:31; 2Wakor. 11:14) – na katika muda huu mfupi ambapo walipata ahueni ya kuuona mwanga mtukufu wa Bwana wetu walipewa taarifa kwamba hawana tena tumaini la kuushinda mpango wa Mungu! Maandiko yanawaita roho / malaika hapa, ingawa kuna majina mengine yanayotumika kwa ajili ya pepo katika Agano Jipya18, na hili limefanywa kwa kusudi, ili kuonyesha utofauti kati ya wafuasi hawa wa Shetani ambao kwa sasa hawana uwezo wowote, wameshindwa kabisa, wakilinganishwa na uweza usio mfano wa Roho Mtakatifu ambao ulimwezesha Bwana wetu afanye safari hii ili akatoe tamko Lake hili la ushindi.19

 

14.16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine (yaani Roho Mtakatifu), ili akae nanyi hata milele;

14.17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Yoh. 14:16-17

 

Kama ambavyo Roho Mtakatifu alikuwa na Bwana wetu, wakati akishuka Hades, pia wakati akisafiri kwenda Abyss isiyo hata na chembe ya mwanga, vivyo hivyo Roho Mtakatifu ambaye anakaa ndani ya kila Mkristo “atakuwa nasi milele”, yaani mpaka mwisho, hata kama mwisho huo unaenda mpa mwanzo na mwisho wa Dhiki na Dhiki

Kuu na hadi ujio wa pili wa Bwana wetu – Yeye atakuwa nasi na ndani yetu, hata kama mambo yetu yataingia giza kiasi gani.

 

18 Tizama BB 2A: Angelology, section II.9.6, “The Organization of the Fallen Angels”.

 

19 Tizama kitabu cha Colonel R. B. Thieme, Jr., Victorious Proclamation (Houston 1977).

 

Kumwezesha Bwana wetu ili atembelee sehemu ambayo haijawahi kufikiwa na yeyote isipokuwa wale wafungwa ndani yake, ulikuwa ni mwujiza mkuu. Na Roho Mtakatifu anaendelea kufanya miujiza ya kustaajabisha kwa ajili yetu na kupitia kwa sisi Wakristo kila siku. Pengine miujiza hii si kama ile iliyoonekana wazi na iliyokuwa na shabaha ya kuwafanya watu wamgeukie Mungu ya enzi ile ya Mitume (katika kitabu cha Matendo), bali matendo makuu ya kimwujiza ya matumaini na ustahamilivu, ya kuamini kweli na kuitangaza, ya kutembea na Bwana wetu na kumtumikia katika namna ambayo haitowezekana bila Roho Mtakatifu kuwa ndani yetu – kama kustahamili mateso ambayo vinginevyo yasingewezekana kustahamili, kwa kufuata mfano wa Bwana wetu, kwa kuwezeshwa na huyu huyu Roho Mtakatifu.

 

14.12 “Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba (yaani, na nitamtuma Roho Mtakatifu; Yoh. 14:16ff).”

Yoh. 14:12

 

Ingawa Bwana wetu “aliuawa katika mwili Wake”, lakini “alihuishwa na Roho Mtakatifu”. Kwa jinsi hiyo hiyo, sisi waumini kwa njia ya Kristo ni “wafu kwa tamaa za mwili [wetu] na tumezaliwa upya, tumezaliwa kutoka juu, tumepewa uzima mpya, uzima wa milele” na Roho “Mtakatifu]” (Waga. 2:20; 6:14; ling. na War. 6:6). Na kama ambavyo Bwana wetu aliutamka ukweli katika sehemu ya mateso ya Hades/Sheol, akiing’arisha sehemu ile ya giza kwa muda kwa utukufu Wake, nasi pia tunapaswa kuwa minara ya taa [ya ile kweli] katika ulimwengu huu wa giza, tukiutangaza mwanga wa utukufu wa Injili ya kweli kwa watu wote, kwa njia ya huyu huyu Roho Mtakatifu (Matt. 5:14-16).

 

Malaika Wasiotii:

 

3.20 hawa ndio wale malaika wasiotii hapo zamani, uvumilivu (ustahamilivu) wa Mungu ulipokuwa ukingoja, katika siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, walioko[lewa] kutoka kwa maji.

1Pet. 3:20

 

Kama tulivyoeleza hapo juu, pepo wanaozungumzwa hapa ni wale waliohusika katika jaribio la Mwanzo sura ya 6 la kuiangamiza mbari (race) ya wanadamu kwa njia ya kuharibu zile nasaba / jeni zinazotufanya sisi “kuwa wanadamu”. Nuhu alikuwa “mkamilifu katika vizazi vyake” (Mwanzo 6:9), maana yake Nuhu na familia yake walikuwa kati ya wanadamu wa mwisho ambao “vinasaba vyao (damu yao) vilikuwa havijachafuliwa [kwa kuchanganywa] na ile ya malaika walioanguka – wale “wana wa Mungu” wanaotajwa katika Mwanzo 6:2. Kama maradhi yaliyoenea dunia nzima, mabadiliko ya nasaba ya wanadamu ambayo matokeo yake ni kuzaliwa kwa Wanefili, wale [ma]chotara waliozaliwa kutokana na muungano wa pepo na wanawake wa kibinadamu (Mwanzo 6:2), yalienea hadi kufikia kukaribia kumaliza kabisa wanadamu halisi – matokeo ambayo yangefanya ujio wa Masihi (“uzao wa mwanamke”: Mwanzo 3:15) kama mwanadamu halisi usiwezekane.

 

Katika Siku za Nuhu: Tunapaswa kuuona ukuu wa Nuhu hapa, muumini ambaye alisimama imara kama kiungo cha sisi wanadamu wote tulioko leo. Kwanza, alikataa kusalimu amri – na aliiongoza familia yake katika hili – mbele ya vishawishi na [ma]shinikizo kutoka katika jamii iliyomzunguka ya kuchanganya damu yake na ile ya watoto wake pamoja na damu ya wale waliodhaniwa kuwa ni wanadamu wasio wa kawaida, yaani waliokuwa na uwezo wa hali ya juu. Pili, na cha muhimu zaidi, Nuhu alimtii Bwana kwa kiwango ambacho kimeonekana mara chache sana katika historia ya wanadamu (Mwanzo 7:5; 7:9; ling. na Ezekiel 14:14; 14:20;).

 

22 Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.

Mwa. 6:22 SUV

 

2.5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;

2Pet. 2:5 SUV

 

11.7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

Waebr. 11:7 SUV

 

Kama ambavyo Nuhu anatofautishwa na waovu – na anaokolewa wakati wao wanaangamizwa – nasi pia tunapaswa kufuata mfano wake ili tuweze kuongozwa kwa usalama na tuvushwe katika gharika la uovu linalotuzunguka katika ulimwengu huu wa Shetani. Nuhu alifanikiwa kiroho kwa sababu alimsikiliza na kumtii Bwana. Mafanikio yetu ya kiroho vivyo hivyo yanategemea sisi kumsikiliza Mungu – kumsikiliza Roho Mtakatifu aliye ndani yetu na anayezungumza nasi kwa njia ya Neno lake – ili kwa mfano wa Bwana wetu Yesu Kristo nasi pia tuweze kutekeleza na kutimiza wito wetu kila mmoja ambao Mungu ametupangia, hata kama hii itahusisha kuteseka kwa mfano wa mateso Yake (jambo ambalo haliwezekani kufanikisha bila msaada wa Roho Mtakatifu).

 

Nuhu alijitayarisha kwa bidii ili aweze kuukabili mgogoro uliokuwa siku za usoni [mwake], akiijenga safina katika kipindi cha miaka 120 licha ya kudhihakiwa na kupingwa. Tunaweza [kutafuta visingizio] na kusema kwamba Nuhu alikuwa na maelekezo mahususi kuhusiana na mgogoro uliokuwa mbele yake – na kwa kweli alipewa maelekezo hayo mahususi kabisa. Lakini hata sisi tumepewa maelekezo mahususi kama hayo. “Safina” yetu ni kupevuka kiroho ambako sote tunakuhitaji kufanikisha ili tuweze kukabili migogoro inayotungoja katika maisha yetu, haswa katika kile kipindi cha Dhiki na Dhiki Kuu, na kwa hakika Biblia imejaa maelekezo, mifano ya kuiga na mafundisho ya kututia moyo kwa ajili ya kutusaidia. Je, ingekuwaje kama Nuhu asingejenga ile safina? Hata hilo wazo tu linatetemesha, tukilifikiria! Lakini itakuwaje ikiwa hatutaweza kufanikisha jukumu tulilopewa ambalo ni kama lile alilopewa Nuhu la kujitayarisha kiroho na kujiendeleza kiroho kwa ajili ya mitihani iliyoko mbele yetu, hasa ikiwa tumepangiwa kuwapo hapa duniani wakati wa Dhiki na Dhiki Kuu? Kutetemeka ni stahiki pale tunapotafakari kushindwa pia, na si kwa ajili yetu pekee. Alichokifanya Nuhu, yaani utiifu wake, kiliwezesha wokovu siyo tu wake mwenyewe, bali na wokovu wa familia yake [pia].

 

16.31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na [watu wa] kaya yako.

Matendo 16:31

 

Nuhu na familia yake “waliokolewa” katika gharika ile, wakielea salama katika safina ile juu ya maji yaliyokuwa yakiongezeka; halitakuwa jambo la kushangaza ikiwa Bwana atayatumia matayarisho yetu ya kiroho katika kuzifusha familia zetu [salama] katika “gharika” inayokuja [hivi karibuni], ya Dhiki, akituokoa sisi na familia zetu (ling. na Matendo 27:24).

 

Mungu alingojea kwa ustahamilivu:

 

3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye anaenenda kwa njia ya mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Mwanzo 6:3

 

Shambulizi la Shetani dhidi ya wanadamu walioishi siku zile za kale za kabla tu ya gharika kuu lilikaribia kabisa kuwaangamiza wanadamu halisi kwani uharibifu wa nasaba halisi, ule uliotokana na kujamiiana moja kwa moja na Wanefili, na ule usio wa moja kwa moja – yaani uharibifu wa nasaba kwa njia ya kujamiiana na “wanadamu waliochafuka”, ulienea zaidi na zaidi. Gharika ile, badala ya sisi kuichukulia kwamba ilikuwa na shabaha ya kuharibu uhai tu, badala yake tunapaswa kuielewa kuwa ni chombo adhimu cha wokovu – wokovu wako msomaji na wangu na waumini wote wa siku zijazo, kwani vinginevyo Masihi asingekuja na hivyo sisi tusingeokolewa.

 

Katika miaka ile 120 ya pauzi (pause) kabla Mungu hajaleta gharika ile, tunaona hapa bayana hekima na neema za Mungu kucheleweshwa kwa gharika ile kulimpa Nuhu muda wa kutosha wa kuijenga safina lakini pia ulitoa fursa iliyodumu miaka mingi ya kutubu kwa upande wa wote ambao [labda] wangekuwa na shauku ya kuokolewa. Mungu ni mwenye huruma na mwenye haki kwa kiwango timilifu. Bwana Yesu Kristo alikufa ili wote wapate fursa ya kuokolewa, ingawa Mungu, kwa uweza Wake, alijua tangu kabla ya kuumba ulimwengu nani wataikataa neema Yake hii. Na kama ilivyo leo hii wasioamini wanapewa neema ya kuishi miaka ya kutosha ili kuwadhihirishia [wao] pamoja na watu wengine kwamba kukataa kwao ni uamuzi wao huru (kama itakavyodhihirishwa katika hukumu ya mwisho), vivyo hivyo katika suala hili la tukio la gharika tunamshuhudia Mungu akiwapa watu wa enzi ile zaidi ya muda wa kutosha ili waweze kujirudi – kwa wale walio tayari kufanya hivyo. Kwa hakika, ujenzi wa safina ile ulikuwa kazi kubwa na ngumu sana na bila shaka wakazi wote wa dunia wa wakati ule walikuwa wanafahamu juu ya ujenzi wake – na bila shaka walimkejeli Nuhu kwa kazi yake ile. Maandiko yanasema “Nuhu alikuwa mjumbe (mhubiri) wa haki” (2Pet. 2:5), na hivyo tunaweza kuelewa kwa kauli hii kwamba safina ile ilikuwa ndiyo “kazi yake ya ‘kuhubiri’”, ishara bayana ya uweza na uwepo wa Mungu na kwamba bila Yeye safina ile isingewezekana kujengwa.

 

11.7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

Waebr. 11:7

 

Ukweli kwamba ni familia ya Nuhu pekee walioitikia wito wa Bwana hauna maana ya kwamba utumishi wa Nuhu ulikuwa batili, wala [ukweli huu] haukubatilisha neema ya Mungu katika kuchelewa hukumu Yake na kuwapa kizazi kile tahadhari ya kutosha – badala yake unathibitisha hayo yote mawili. Kwa wazi kabisa, Roho Mtakatifu alisimamia kila taswira ya mfululizo wa matukio yale ya kimwujiza, aliongoza na aliwezesha kila tukio, kutoka katika amri za mwanzo kabisa alizopewa Nuhu, hadi ujenzi wa safina, hadi shughuli ya makusanyiko ya wanyama, ulinzi wa kila mmoja ndani ya safina pale gharika ilipoanza, kote, mpaka kutoka nje ya safina baada ya maji kupungua. Ni kwa njia ya Roho Mtakatifu pekee Nuhu aliweza kufanya yote aliyotenda. Ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu pekee ndiyo kila mmoja kati ya sisi Wakristo tunaweza kutenda yote tunayoitwa kutenda, haswa katika nyakati na mazingira ya shinikizo na mateso, tukifuata mfano wa Bwana wetu. Na ni kwa njia ya kuwezeshwa na Roho Mtakatifu pekee ndiyo sisi “tunaoishi enzi hizi za mwisho” (1Wakor. 10:11) tutafanikiwa kujitayarisha na kisha kustahamili [ma]shinikizo ya Dhiki na Dhiki Kuu inayokuja. Utii wa Nuhu kwa Mungu, katika kujitayarisha kwa ajili ya janga lililokuwa mbele yake katika namna mahususi ambayo Mungu alimwelekeza unapaswa kuwa fundisho kwetu, hata zaidi ya safina yenyewe, ambayo inadhihirisha tu utiifu huo. Kwa wakati huu, sisi waumini tulio hai leo tuna muda mfupi zaidi ya ule aliokuwa nao Nuhu kwa ajili ya kujitayarisha kwa kile kilicho usoni. Lakini kama ilivyokuwa kwa Nuhu, kwa hakika tunajua ni kwa jinsi gani tunapaswa kufanya matayarisho hayo: kwa kukua kiroho na kuendele [kiroho] kwa kuitumia kweli ya maandiko. Wakati gharika yetu itakapokuja, basi nasi tuwe tayari kama Nuhu alivyokuwa tayari.

 

5.1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira (yaani mfululizo wa matukio ya siku za mwisho), hamna haja niwaandikie.

5.2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana (yaani ujio wa pili ukitanguliwa na Dhiki Kuu) yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

5.3 Wakati [watu] wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

5.4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

5.5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

5.6 Basi tusilale usingizi kama wengine [wasioamini], bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

5.7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

5.8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani [deraya ya] imani na upendo, na chapeo (helmet) yetu iwe tumaini la wokovu.

5.9 Kwa kuwa Mungu hakututeua tupitie ghadhabu Yake, bali kwa ajili ya kutwaa ( peripoiesis / περιποίησις) wokovu wetu (katika ufufuo) kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

5.10 Yeye aliyekufa kwa ajili yetu, ili kwamba, tukiwa hai au tukiwa katika usingizi (kifo cha mwili huu wa sasa), tutakuwa wazima pamoja na Yeye (katika siku ya ufufuo).

1Wathess. 5:1-10

 

[Safina] Ambamo Ndani Yake: Inashangaza kidogo kwamba ibara hii ndiyo mahala pekee katika maandiko (nje ya Mwanzo sura ya 6 na ya 7) ambapo safina inazungumziwa. Mahala pengine, kama katika ibara zinazonukuliwa hapo juu, Nuhu ndiye anayekumbukwa – kwa sababu ushindi wake wa imani ndio wenye umuhimu, na siyo safina ambayo inadhihirisha tu imani hiyo (ling. na Yakobo 2:14-26). Kwa maana ya kuyatumia maandiko, kwa msingi wa yaliyojadiliwa hapo juu, kwamba ile safina ni analojia ya makuzi yetu ya kiroho, kwani ni ile kweli [ya maandiko] tuliyoiweka ndani ya mioyo yetu kwa imani (ling. na Waefe. 3:17) ambayo itakuwa ndiyo chombo ambacho Roho Mtakatifu atakitumia ili kutuokoa tukingali katikati ya Dhiki Kuu (ikiwa Mungu wetu ametupangia tuwe hai katika wakati huo) kama ambavyo safina aliyoijenga Nuhu ilikuwa ndiyo chombo kilichotumiwa na Mungu katika kumwokoa Nuhu.20

 

 

Ndugu msomaji, tafadhali elewa kwamba ingawa neno "ark" katika msemo wa Kiingereza (na Kiyunani) "the ark of the covenant" ni lile lile kama linalotumika katika msemo "Noah's Ark", katika Kiebrania (na Kiswahili) haya ni maneno tofauti (אָרוֹן /aron ni Sanduku la Agano – Ark of the Covenant, Kutoka 25:22; na תֵּבָה tebhah ni safina – Noah’s Ark, Mwanzo 6:19). Vipimo vyake pia havina uwiano: dhiraa (wastani wa inchi 18) 2.5 X 1.5 X 1.5 kwa Sanduku la Agano na dhiraa 300 X 50 X 30 kwa safina. Hata hivyo, hizi “ark” mbili zinafanana kabisa katika maana ya kwamba zote ni mfano wa Bwana Yesu Kristo.21 Fundisho la Sanduku la Agano kuwa ni mfano wa Kristo ni maarufu zaidi ya lile la safina kuwa ni mfano wa Bwana Yesu Kristo pia, na hili la safina kuwa ni mfano Wake linawekwa wazi na ibara yetu hapa. Petro anawatumia Nuhu na familia yake kama mfano wa waumini wa siku za leo, na yale waliyoyapitia yanatumiwa ili kutuongoza na kututia moyo na motisha. Kama ambavyo Nuhu na familia yake “wanavyobatizwa katika safina” kwa msaada wa Roho Mtakatifu (ambaye huduma Yake ndiyo sababu ya Petro kuacha kwa muda mjadala wake hapa – digression) na hivyo wakavushwa salama katika maji yale ambayo vinginevyo yangewaua, vivyo hivyo waumini wa leo wanabatizwa katika Kristo na huyo huyo Roho Mtakatifu (Matt. 3:11; 28:19; Matendo 1:4-5; War. 6:3-5; 1Wakor. 12:13; Waga. 3:26-28; Waefe. 4:3-6; Wakol. 2:9-10), na wanavushwa salama hapa duniani, wakipitia vitisho, dhiki, kwa kufuata uongozi na maelekezo ya Roho Mtakatifu.

 

1.21 Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta (Roho Mtakatifu), ni Mungu,

1.22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni (guarantee) ya Roho [Mtakatifu] mioyoni mwetu.

1Wakor. 1:21-22

 

(13) Katika Yeye nanyi pia, mlipolisikia neno la [ile] kweli, Injili ya wokovu wenu, na mkaamini katika Kristo, mkatiwa muhuri wa ahadi wa Roho Mtakatifu,

(14) ambaye ndiye dhamana ya urithi wetu mpaka hapo tutakapoutwaa [urithi huo], kwa sifa ya utukufu Wake,

Waefe. 1:13-14

 

4.30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi (yaani siku ya ufufuo).

Waefe. 4:30

 

20 Tazama katika CT 7, section III.I, "The Analogy of Noah and the Great Flood".

 

21 For the symbolism of the ark of the covenant, see in CT 2B: "The Earthly Tabernacle and Temple as types of the Heavenly Temple".

Roho Mtakatifu ndiye anayetuweka salama katika Yesu Kristo: tumewekwa muhuri na Roho Mtakatifu na tuna usalama kamili hadi tutakapokamilisha wokovu wetu siku ya ufufuo – ikiwa tunaendelea kuwa "katika Kristo" kwa kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu (ling. na Yoh. 15:1-8). Kama ambavyo Nuhu na familia yake waliwekwa salama ndani ya safina ambayo ni mfano wa Kristo, lakini kwa hakika wasingekuwa salama kama wangetoka nje ya safina ile kabla ya wakati, vivyo hivyo nasi tuna ulazima wa kukaa ndani ya Kristo Yesu mpaka siku atakapokuja, kwa kutegemea uweza wa Roho Mtakatifu. Kama ambavyo [wao] "walivushwa salama katika gharika ile", vivyo hivyo Bwana wetu atatuweka salama katika Yeye kwa msaada wa Roho Mtakatifu na kutuvusha salama katika maisha haya, hata katika gharika la Dhiki na Dhiki kuu, ikiwa tu tutakuwa waangalifu na kutomwasi Yeye, ambaye ndiye msaada na tumaini la kweli katika dunia hii.

 

5.5 Maana sisi kwa [kuwezeshwa] na Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.

Waga. 5:5

 

2.11 Hili ni neno la kuaminiwa: kama tukifa pamoja Naye, tutaishi pamoja Naye pia;

2.12 Kama tukistahimili [katika mateso na mitihani], tutamiliki [tutatawala] pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;

2.13 Kama sisi hatuamini, Yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

2Tim. 2:11-13

 

Ubatizo Unaowaokoa Ninyi Siku Hizi:

 

3.21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo [wa Roho Mtakatifu], unaowaokoa ninyi pia siku hizi; siyo kuwekea mbali (kutoa) uchafu wa mwili [kwa kuoshwa na maji], bali [kwa njia] ya kumwomba Mungu atupatie dhamiri safi kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.

1Pet. 3:21

 

Neno "ubatizo" limesababisha utata mwingi wa kutafsiri vibaya ndani ya ibara hii na haswa ndani ya aya ya 21. Kwanza, (tofauti na tafsiri za Kiingereza kama NIV, NLT, nk) neno "maji" halimo kabisa katika Kiyunani hapa, ambayo ndiyo lugha "original" iliyotumika kuandika Agano Jipya. Kuweka neno "maji" ni kutafsiri vibaya maana aliyoikusudia Petro, kwani inageuza kabisa kile Petro alichokikusudia: "ubatizo" anaoutaja Petro hapa ni ubatizo "mkavu", sio wa maji:

 

10.1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

10.2 wote wakabatizwa kwa/katika (into) Musa katika wingu na katika bahari;

1Wakor. 10:1-2

 

NB: Naona kuna umuhimu hapa wa kuiweka tafsiri mojawapo ya Kiingereza inayoelezea kanuni hii kwa ufasaha zaidi; hivyo nitanukuu hapa tafsiri mojawapo - R. Kilambo:

 

10.1 For I do not want you to be ignorant of the fact, brothers, that our forefathers were all under the cloud and that they all passed through the sea. 10.2 They were all baptized into Moses in the cloud and in the sea.

1Cor. 10:1-2 NIV 1984

 

Kama inavyodhihirishwa katika ibara hii hapa juu (na katika mifano kadhaa iliyo ndani ya Biblia pia)22 ubatizo katika Biblia hauhusishi maji wakati wote unapofanyika. Ubatizo halisi wa maji unahusisha kumchovya mtu katika maji na hapo panakuwa na muungano wa aina fulani, mtu anayechovywa sasa akitambulishwa na kufunganishwa na maji alimochovywa. Hivyo, ule ubatizo “kwa/katika Musa” (1Wakor. 10:2) na ubatizo mwingine unaosimuliwa katika maandiko ambao ni “ubatizo mkavu” (yaani hauhusishi maji) ni ufungamano wa sitiari (metaphorical identification) na siyo kuchovywa katika maji kiuhalisia. Kwa maneno mengine. Wana wa Israeli “walichovywa katika Musa” lakini siyo kama unavyomchovya mtu katika maji: “walitambulishwa na Musa mbele ya macho ya Bwana” ili waweze kupokea neema zilizopelekwa kwa Musa. Hawakuangamizwa kwa sababu Musa hakuangamizwa, kwani Mungu aliwahesabu kuwa ni watu wa Musa (kw. mf. Kutoka 32:10-14; Hesabu 14:12-20), kwa hivyo waliokolewa pamoja naye (kw. mf. Kutoka 14:10-15).

 

Ubatizo muhimu kuliko wote katika maandiko kwa hakika ni ule ubatizo wa Roho Mtakatifu – na hii maana yake ni kwamba watu wote wanaomwamini Kristo wanawekwa katika umoja Naye na hivyo wanakuwa “ndani ya Kristo”: wanatambulishwa mahususi na Kristo kwa kuwekwa ndani Yake na Roho Mtakatifu.23 Huuu ndio ubatizo unaozungumzwa hapa. Kama ambavyo Nuhu na familia yake wali[vyo]batizwa na safina, walivyoingia ndani ya safina, walivyofungamana na safina, vivyo hivyo waumini wa leo wanabatizwa, wanafunganishwa, na wanaingia katika Bwana Yesu Kristo. Hii ndiyo analojia yake. Na kama ambavyo Nuhu na familia yake “walivyovushwa salama” katika maji ya uharibifu ya gharika ile kuu kwa njia ya “kuwamo katika safina ile” (ambayo ni mfano wa Kristo), iliyopigwa muhuri na Roho Mtakatifu, vivyo hivyo sisi waumini wa leo tunavushwa salama katika ulimwengu huu wa giza, na hata katika Dhiki na Dhiki Kuu ikilazimu sisi tupitie tukio hili la kutisha, kwa kuwa sisi tumo “katika Kristo”, tumefunganishwa na kupigwa muhuri ndani Yake na huyo huyo Roho Mtakatifu. Huu ndio “ubatizo unaotuokoa”, na sio

ule ubatizo wa maji – ambao kwa hakika hauna nafasi katika Kanisa la leo.24

 

 

 

22 Kwa mfano, “ubatizo wa moto” ambapo wasioamini “wanaingizwa / wanachovywa” katika moto na si maji (Matt. 3:11; Lk 2:16; ling. na Marko 1:8; Ezek. 39:6; Zak. 14:12-13; 2Wathess. 1:6-9; Ufu. 14:17-20).

 

23 Tizama BB5: Pneumatology, section II.B.2.b, “The Baptisma of the Spirit”. Ubatizo wa Roho Mtakatifu unahusisha sehemu mbili, kwanza ni “ubatizo wa Roho” ambapo Roho Mtakatifu anatuweka “ndani ya Kristo” na hivyo tunakuwa “katika Kristo” (ling. na War. 8:1-2 na katika maeneo mengine ya Agano Jipya), na pili ni “ubatizo wa Roho” ambapo Roho Mtakatifu anaingia ndani yetu sisi tulioamini.

 

24 Tizama BB 6B: Ecclesiology, section II.C.3b, “Water-Baptism”.

 

Neno lililotafsiriwa kama “mfano” (tunaweza kusema “analojia”) hapa juu katika 1Pet. 3:21

(yaani “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo [wa Roho Mtakatifu], unaowaokoa ninyi pia siku hizi), limetafsiriwa kutoka neno la Kiyunani antitypon / ἀντιτυπον ambalo ndilo chanzo cha neno la Kiingereza “antitype”. Hivyo Petro anatuondoa shaka yoyote tunayoweza kuwa nayo kuhusu ukweli kwamba hapa anatuonyesha analojia / mfano – siyo kati ya gharika na ubatizo wa maji (jambo / analojia / mfano ambao hautaleta maana hata kwa kuutazama kwa juu-juu tu kwani gharika iliangamiza uhai, na ubatizo huu “unatuokoa”), bali ni analojia kati ya kuwa ndani ya safina na kuwa ndani ya Kristo. Kuwa ndani ya Kristo ni “ubatizo unaotuokoa”, muungano / umoja wetu na Kristo ukifanywa na Roho Mtakatifu mara tunapomwamini Kristo (ling. na War. 8:9). Hii ndiyo maana Petro anaeleza kwa uwazi kabisa:

 

“…siyo kuwekea mbali (kutoa) uchafu wa mwili [kwa kuoshwa na maji], bali [kwa njia ya kumwomba Mungu atupatie dhamiri safi kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.

1Pet. 3:21b

 

Sehemu ya kwanza ya sentensi hii hapa juu sasa inapaswa kueleweka kwa urahisi: aya hii haizungumzii ubatizo wa maji, bali inazungumzia ubatizo wa Roho Mtakatifu, yaani pale tunapowekwa umoja na Bwana Yesu Kristo kwa uweza wa Roho Mtakatifu mara tunapoamini, na hapo sasa tunakuwa "katika Kristo" (kw. mf. Yoh. 13:20; 15:1ff; War. 16:7; 2Wakor. 5:17; Waefe. 2:6; 2:10; Waebr. 3:14; 1Pet. 5:14). Na sehemu ya pili inaainisha jinsi jambo hili linavyotokea [mioyoni mwetu] kutoka katika mtazamo wa yule mtu anayeamini / anayebatizwa na Roho Mtakatifu. Hili "ombi kwa Mungu atupatie dhamiri safi" ni ombi letu Kwake kwamba sasa tunamwamini Bwana Yesu Kristo, nia yetu ya kuokolewa kutoka dhambi na kifo, tukifanya toba ya yote mabaya tuliyotenda hapo kabla na kiu yetu ya wokovu kama inavyoonyeshwa [nasi] pale tunapoweka imani yetu katika Bwana Yesu Kristo.

 

10.8 Lakini [maandiko] yanenaje? “Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako” (Kumb. 30:14) yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.

10.9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

10.10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

10.11 Kwa maana andiko lanena, “Kila amwaminiye hatatahayarika” (Isa. 28:16 – LXX).

War. 10:8-11

 

Tunaokolewa kwa neema [ya Mungu] kwa njia ya imani [yetu] – na si kwa matendo [yetu] (Waefe. 2:8-9), hivyo kutamka / kutangaza rasmi [kwa watu] imani yetu si jambo linalotakiwa tufanye (kama watu wanaozitafsiri aya hizi mbili kutoka waraka kwa Waefeso kama sheria wanavyodai)25; badala yake, kuieleza imani yetu ni jambo ambalo waumini

wote wanafanya kwa utashi wao bila kufanya kama ni jambo la sheria / kanuni, haswa kwa Baba yetu, mara tunapoamini – hilo ndilo “ombi letu kwa Mungu [ili] atupatie dhamiri

safi”, yaani tamko tunalilitoa la imani yetu katika Bwana Yesu Kristo na tumaini la uzima

 

25 Tizama BB.4B: Soteriology: section II.6.f, “False Issues”

 

wa milele na wokovu kutoka dhambi na kifo. Hii ndiyo sababu Petro anaongeza pale mwisho wa aya hii, “kwa kufufuka Kwake Yesu Kristo”: Kufufuka kwake Kristo kutoka katika wafu – kwa uweza wa Roho Mtakatifu – ndiyo ithibati kwamba nasi pia tutafufuliwa kwa njia ya imani yetu katika Yeye, na hivyo hii ni sehemu muhimu ya fundisho la Injili (Matendo 2:24; 2:32; 3:15; 3:26; 4:10; 5:30; 10:40; 13:23; 13:20; 13:33-34; 13:37), na pia ni njia ya kututia moyo sisi tunaoamini kuitazamia ile enzi ya milele ijayo, lile “tumaini lenye baraka” (Tito 2:13), na kujitahidi wakati huo huo kufuata nyayo za Bwana wetu kwa kuutumia uweza wa Roho Mtakatifu (aliye ndani yetu) ambaye alimwinua kutoka katika wafu – na ambaye atatuinua sisi katika ile siku ya siku inayokuja.

 

1.3 [Injili] ambayo ni habari ya Mwana [wa Mungu], Yeye ambaye ni uzao wa Daudi katika mwili Wake,

1.4 na akafanywa kuwa Mwana wa Mungu kwa uweza wa Roho wa Utakatifu kwa njia ya ufufuo kutoka kwa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu.

War. 1:3-4

 

8.11 Lakini, ikiwa Roho Wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

War. 8:11

 

15.20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko (zao la mwanzo) lao waliolala.

15.21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu (yaani Adamu wa kwanza), kadhalika na kiyama (ufufuo) ya wafu ililetwa na Mtu (Yesu Kristo, Adamu wa Mwisho).

15.22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa (yaani wote wako chini ya laana ya Adamu), kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa (yaani wote wataokolewa kutoka laana ya Adamu kwa kubatizwa katika Kristo na Roho Mtakatifu).

1Wakor. 15:20-22

 

4.14 tukijua ya kwamba Yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi.

2Wakor. 4:14

 

Yesu Kristo:

 

3.22 Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini [ya miguu] yake (Zab. 110).

1Pet. 3:22

 

Zawadi kuu ya Roho Mtakatifu, (somo lililomfanya Petro atoke nje ya mada [yake] kwa muda mfupi hapa), hakuweza kupelekwa kwa waumini mpaka ushindi wa msalaba ufanikishwe na Bwana wetu na mpaka Bwana wetu alipopaa na kutukuzwa kama inavyoelezwa katika aya hapo juu (pia Yoh. 7:39). Kwa njia ya kifo Chake kwa ajili yetu, Mwokozi wetu mpendwa Yesu Kristo si tu aliondoa dhambi zetu zote na kuifungua njia inayotuwezesha sisi tuufikie uzima wa milele, lakini pia aliuwezesha ubatizo wa Roho Mtakatifu ambapo kila muumini leo hii anakaliwa [na Roho Mtakatifu] katika namna ile ile ambayo Kristo alikuwa nayo, kwa kuwa waumini wote ni Wake (Waefeso 4:7-10), “ahadi ya neema ya Roho Mtakatifu, inayotufanya wamoja na Bwana wetu, akitupatia kila mmoja wetu karama za kiroho zinazotuwezeshewa kumtumikia Bwana wetu kwa ubora zaidi na kwa njia hiyo pia kupata thawabu adhimu, na anatupatia uongozi mwema na kututia moyo kwa msaada na uhimili tunaopewa na Roho Mtakatifu – pindi tunapokuwa tayari kuitikia wito Wake.

 

16.7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi (paraclete, ‘Anayetia moyo’ / Anayewezesha) hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

Yoh. 16:7 (ling. na Yoh. 14:22; 14:26; 15:26)

 

2.33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.

Yoh. 2:33

 

Hivyo basi, pointi za mwishoni za Petro alipoondoka kwa muda mfupi kutoka mada ambapo siyo tu anatukumbusha na kupendekeza mfano / analojia ya Bwana wetu bali pia anadhihirisha kwamba ni kwa njia ya uweza wa Roho Mtakatifu Yeye aliitimiza kazi aliyopewa na Baba kwa namna timilifu kabisa, yaani kuufuata uongozi wa Roho Mtakatifu kikamilifu kabisa, na hapo Petro anakamilisha mzunguko wa analojia hiyo: sasa tunaweza kuona matunda ya mwenendo wetu wa kimungu, uvumilivu wetu wa mateso tusiyostahili, uvumilivu wetu wote katika maisha haya magumu, katika [ma]shinikizo yote tuliyolazimika kustahamili – na kwa mara nyingine tena Bwana Yesu Kristo ndiye mfano wetu na analojia yetu, kwani Yeye “aliwezeshwa na Roho Mtakatifu bila kikomo”, nasi tumepewa fursa hii kuu tuitumie kwa mfano ule ule wa Bwana wetu. Kama ambavyo ufufuo Wake umewezesha ufufuo wetu, [ulio] msingi wa tumaini la wokovu wetu, uzima wa milele na wokovu kutoka kaburi, kifo, na dhambi milele na milele, hivyo, kufuatia ufufuo Wake, tunaona kwamba kupaa Kwake mbinguni (“amekwenda zake mbinguni”), kukaa Kwake (“amekaa mkono wa kuume wa Mungu”), na kutukuzwa Kwake (“malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini ya miguu Yake”) pia vinatupatia mfano wa neema zinazotungojea sisi, Kanisa Lake, pale atakaporudi. Nasi pia tutapaa – tutapaa katika ufufuo ili tukaonane Naye (War. 6:5). Nasi pia tutachukua nafasi zetu katika safu za Kanisa – tukipanga paredi yetu mawinguni katika ujio [Wake] wa pili (1Wathess. 4:13-18). Nasi pia tutapokea utukufu pamoja na thawabu tunazozikusanya tukingali hapa duniani kwa kukua [kiroho] na kuendelea [kiroho] na kustahamili na kuvumilia na kuteseka katika maisha ya sasa yaliyo ya muda tu kwa uweza wa Roho Mtakatifu (War. 8:30).

 

16.27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Matt. 16:27 SUV

 

22.12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

Ufu. 22:12 SUV

 

Kila kitu sisi Wakristo tunachojitahidi kukipata katika maisha ya hapa duniani na [hatimaye] yale ya milele kinahusishwa kwa ukaribu kabisa na Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo (Wafi. 1:21). Yeye ni kila kitu kwetu, na ni mfano Wake tunaotakiwa tuufuate, tukijifunza kuacha [kufuata] mapenzi yetu na kuyapisha mapenzi ya Roho Mtakatifu [yafanyike katika maisha yetu] kama alivyofanya Yeye kwa utimilifu kabisa (ling. na Isa. 11:1-3), tukiufuata ukweli tuliofundishwa na Roho Mtakatifu na ambao tumeuamini kwa njia ya huyo Roho Mtakatifu, tukifuata nyayo za Bwana wetu kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, tukiwa na ari ya kimungu inayotokana na Roho Mtakatifu (1Wathess. 5:19), tukipumzika / tukistarehe katika amani inayopita maelezo na ambayo inailinda mioyo yetu kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu (Wafi. 4:6-7), hata tunapokuwa katikati ya mateso makuu na dhiki – tukifuata mfano wa Bwana na Mwokozi wetu.

 

6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho Wangu, asema Bwana wa majeshi.

Zak. 4:6

 

8.9 Hata hivyo, ninyi hamtawaliwi na hulka yenu ya dhambi, kwani mnaenenda katika [Roho] Mtakatifu, ikiwa ni kweli Roho wa Mungu yuko ndani yenu. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wa Kristo.

War. 8:9

 

8.15 Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa iwarejeshayo katika hofu; bali mlipokea Roho aliyewaingiza katika familia ya Mungu, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

8.16 Roho Mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

8.17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

War. 8:15-17

 

5.25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

Waga. 5:25 SUV

 

2.13 Kwa maana Mungu [kwa njia ya Roho Wake Mtakatifu] ndiye atendaye kazi ndani yenu, [katika] kutaka kwenu [yaliyo mema] na [katika] matendo yenu [mnayotenda ili] kulitimiza kusudi Lake jema.

Wafi. 2:13

 

=0=

 

Translated from: Undeserved Suffering in Marriage and in Life – and the Example of Christ

1Pet. 3:1-22

 

=0=

 

Basi na tuonane katika Somo #36 la mfululizo huu, kwa neema ya Mungu, Amina!

 

 

 

 

 

=0=

 

NB.: Rejea zote (1-25) zilizo katika superscript (kama xy2) zinapatikana katika tovuti ya https://ichthys.com tafadhali tembelea tovuti hii kwa maelezo ya kina kuhusu somo husika.

 

=0=