SUALA MUHIMU LA TAFSIRI YA KING JAMES BIBLE

 

Translated from Chapter D22: THE KING JAMES BIBLE VERSION ISSUE, of “Age of Reason”, writen by Mr. Len Smith of https://www.theswordbearer.org

 

by permission

 

Tafsiri hii ya Kiswahili na Respicius Kilambo Luciani wa https://sayuni.co.tz

 

 

 

 

 

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba Wakristo wa leo wameruhusu mapokeo / desturi zao kulifanya neno la Mungu liwe batili. Mapokeo hayo ni matokeo ya karne nyingi za uasi [dhidi ya neno la Mungu] ambamo misingi ya falsafa za Kiyunani ilichukua nafasi ya imani kama msingi wa fikra zetu. Msingi huo wa Reason / Mantiki [badala ya imani] kwa upande wake ukawa ndio chanzo cha maendeleo makubwa ya kisayansi, tekinolojia na utamaduni katika nchi za Ulaya na Marekani ambayo yamewatia upofu 99% ya kanisa kiasi kwamba hata hawajui kwamba wao ni waasi. Kwa kweli, kuna uwezekano mkubwa kwamba wewe msomaji na Wakristo wengine wengi unaowastahi kama watumishi mahiri wa Kristo kiuhalisia ni Wakristo wa kimwili tu (tofauti na wa kiroho) kutoka nje hadi ndani yao. Unafikiri ninahukumu [watu] kupita kiasi? Kama wewe bado unaweza kuutathmini Ukristo kwa mtazamo wa Kibiblia, unalielewa vipi kanisa ambalo waumini wake wengi hawaamini kwamba neno halisi la Mungu (lisilo na chachu) haliko mahala popote hapa duniani? Ukweli ni kwamba, walio wengi (hao niliowataja) wakati wote wanawakejeli wale Wakristo wachache wenzao kwa sababu tu ya kwamba hao wachache wameikubali kwa imani fasili ya Mungu mwenyewe juu ya neno Lake, Biblia, Maandiko, na kwamba neno hili limevuviwa, limetunzwa, na halina makosa. Jambo la kushitusha kabisa ni kwamba walio wengi hao wameikataa fasili hii ya Mungu, na badala yake [na kwa mamlaka yao wenyewe] wameunda fasili yao wenyewe kuhusu Biblia inayomaanisha “tafsiri iliyopotoshwa”. Nasema jambo la kushitusha, kwa sababu Biblia yenyewe inasema: Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo (1Yoh. 5:10). Kutoamini huku ndiyo sababu Wakristo wengi wanajidai kwamba wanasahihisha Tafsiri zao za Biblia kwa kutumia kamusi za Kiebrania na Kiyunani. Nasema wanajidai kwa sababu hata wanateolojia na wataalamu wa lugha wanaoheshimiwa sana hawajaweza, hata baada ya kutumia mbinu za kisasa zaidi, kwa zaidi ya karne sasa, kutengeneza tafsiri ya Biblia ambayo haina makosa na ambayo haihitaji “marekebisho” ya kila wakati kufanywa na watu ambao siyo wanataaluma na ambao wanajidai ni mahiri kuliko wataalamu wenyewe.

 

Falsafa ya kipagani imefanya uharibifu mkubwa katika kanisa. Hii ndiyo sababu kanuni nyingine ninazozijadili katika kitabu hiki cha AOR (link) zimezua mijadala mingi zaidi pamoja na shauku kuliko kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakikuza hata juu ya jina Lake Takatifu (Zab. 138:2b). Wakristo wanaisifu Biblia kwa maneno matupu tu, badala ya kuikuza [hata] juu ya jina la Yesu Kristo wa Nazareti – jina pekee chini ya mbingu ambalo kwalo watu tunaokolewa (Matendo 4:10,12). Hili si suala dogo. Biblia ndiyo chanzo na msingi ulio imara wa imani na mafundisho yetu; hakuna kingine. Neno la Mungu ni jambo la lazima kiasi kwamba mimi naamini [kwamba] suala la tafsiri [mbalimbali] za Biblia kuwa ni jambo pekee linaloonyesha hali ya kusikitisha (na kushitua) ya kanisa la sasa. Kwa kuwa kulifahamu neno la Mungu ni chanzo cha kumaizi / kutambua mapenzi ya Mungu, basi pale Mkristo anapotumia mantiki badala ya kumaizi / kutambua mapenzi ya Mungu katika maisha yake, huyo ni Mkristo mchanga au ni Mkristo aliyeasi; hakuna namna ingine.

Ni kwa nini Mungu alisema adui zetu watakuwa Wakristo wenzetu (Matt. 10:36; Zab. 55:12-15)? Ni kwa sababu tishio letu halisi linatoka kwa Wakristo wenye nia ya kimwili (badala ya nia ya kiroho) ambao wanauficha uadui wao dhidi ya Mungu (War. 8:7) kwa kuvaa ngozi ya kondoo. Watu wasiomjua Mungu hawajawahi kuwashinda Wakristo katika vita yoyote ile – siku zote tumekuwa tukishindwa na chachu iliyomo ndani ya kambi yetu sisi wenyewe. Kwa sababu ya uwepo wa mafundisho ya kanuni za uwongo [katika makanisa yetu] kuhusiana na Biblia Takatifu, wahubiri wa leo wanaoamini “higher textual criticism” (“uhakiki wa juu wa maandishi”) wanatupeleka vitani tukiwa na silaha potofu za neno la mwanadamu badala ya Upanga wa Bwana. Hata wengi kati ya wale wanaoitumia King James Bible wanafanya hivyo bila imani kwani hawaamini kwamba hili ndilo neno lililovuviwa / lililofunuliwa la Mungu. Kitu kinachoonyesha kwa wazi kabisa uwepo wa kutoamini katika kanisa la leo ni kukataa kwa uwepo wa neno halisi la Mungu hapa duniani. Katika miaka ile ya 1800 “uhakiki wa juu wa maandishi” (higher textual criticism) ulikuwa na lengo la kulisaidia kanisa kwa kuwapa Wakristo “silaha imara zaidi” katika tafsiri mpya za Biblia. Lakini tunajua leo hii, kwa matunda yake, kwamba umefanya kinyume chake: mamilioni ya Wakristo sasa wanafikiri neno la Mungu lililovuviwa, lisilo na makosa, halipatikani katika tafsiri ya Biblia yoyote hapa duniani! Hii imekuwa na matokeo ya Wakristo wengi kutokuwa wajuzi stadi wa Biblia kwa sababu kujifunza kitu usichokiamini ni kupoteza muda tu. Na Wakristo wenye imani katika Biblia sahihi wanaonukuu Maandiko kwa usahihi, zaidi na zaidi wanaingizwa katika mgongano na Wakristo wenzao wanaojiona wajuvi ambao [katika mjadala] wanabadilisha mada, wanapiga chenga, na “wanawasahihisha” kwa kugeukia kamusi za Kiebrania na Kiyunani na kurasa za mwisho za vitabu vya concordance za Biblia.

 

Kama una ufahamu katika suala hili, utakuwa umekwishachanganua jinsi ninavyochagua maneno kwa uangalifu ili uweze kujua nini ninamaanisha kila ninaposema neno la Mungu, Biblia, na Maandiko. Ngoja sasa nirahisishe suala hili kwako: bila shaka yoyote Biblia ya mwaka 1611 iliyoidhinishwa na Mfalme Yakobo ni neno la Mungu (The Authorized 1611 King James Bible is, without a doubt, the word of God). Ninaposema hivi ninamaanisha kwamba Mungu alichagua kila neno katika Biblia hii – hata maneno yaliyo katika italiki / hati mlazo. King James Bible imevuviwa-na-Mungu, yenye uhakika, isiyo na kosa, neno takatifu la Mungu lisilo na migongano au uwongo wa aina yoyote. Tafsiri au nyaraka zote nyingine za Biblia zilizoko leo hii siyo neno la Mungu – zote zimeharibika; hii ni pamoja na New King James Version na Textus Receptus.

 

Watu wengi wanapoizungumzia Biblia kuwa ni neno la Mungu huwa wanaiandika n katika neno kwa herufi kubwa ili kuifanya nomino halisi (proper noun). Mimi sifanyi hivyo. Mara nyingi mimi sitaangalia kanuni za sarufi na tahajia (spelling) ili niweze kuendana na neno la Mungu. Katika Biblia, Neno la Mungu huandikwa kwa herufi kubwa N wakati Neno linapotumika kama moja kati ya majina ya Bwana Yesu Kristo (Yoh. 1:1,14; Ufu. 19:13). Pale Biblia inapoandika n katika neno la Mungu kwa herufi ndogo, hapo inazungumzia maneno yenyewe katika Biblia (Waebr. 4:12; 1Pet. 1:23,25; 2:2). (Licha ya hayo, ukifanya word study katika Biblia utagundua kwamba mambo yaleyale [Biblia] inayoyasema kuhusu neno la Mungu pia inayasema kuhusu Yesu Kristo; Neno la Mungu ni muhimu kwelikweli!)

 

Ninaposema Mungu alichagua kila neno katika Biblia iliyoidhinishwa ya 1611, ninajua pia kwamba Mungu alitumia watenda dhambi kama Musa, Isaya, wana-kamati waliyoagizwa na Mfalme Yakobo kutafsiri Maandiko, Yeremia na Paulo katika kuliandika neno Lake, lakini tofauti na Wakristo wengi wengine mimi sitatoka kwenye msitari wa ukweli kwamba hili ni neno la Mungu. Mimi nampa Yeye sifa zote na utukufu wote. Watu wengine wanajaribu kumlinganisha Mtume Paulo na wana-kamati wa Mfalme Yakobo wa Uingereza waliotafsiri Maandiko na wanautumia ukweli kwamba Paulo alitenda dhambi “kubwa” zaidi [kuliko wao] (1Tim. 1:15) ili “kuthibitisha” kwamba Mungu hawezi kutumia chombo cha udongo kilichofinyangwa kama Paulo katika kuliandika neno Lake. Lakini sitapoteza muda wako katika majadiliano [haya] ya neno la Mungu kwa kuzungumzia idadi ya dhambi watu mbalimbali walizotenda.

 

Ninapotumia msemo “tafsiri za Biblia” katika marejeo ya tafsiri zote zile ambazo hazijaidhinishwa, mimi huutumia msemo huu ili kurahisisha mawasiliano tu na wewe msomaji wangu. Kama nitatumia msemo sahihi na unaofaa zaidi kama “takataka zisizofaa kitu” watu wengine wanaweza kuvurugwa na kuanza kudhani kwamba ninalitumia neno takataka kama tasifida (euphemism) tu, na mimi ninataka kujibu maswali hapa, na si kusababisha maswali mapya!

 

Ni jambo la kusikitisha kwamba nimelazimika hapa kubainisha “neno la Mungu”, “Biblia”, na “Maandiko”, lakini uhalisia unaoshitua sana ni kwamba tunazungukwa na waasi wa imani ambao upofu wao unawafanya waenende kama vichwamaji wenye migongano ya ndani. Kwa mfano, inanivunja moyo pale Wakristo wanaporejea, au wanaponukuu bila kufikiri, tafsiri yoyote ya Biblia na kusisitiza kwamba hiyo ni “neno la Mungu” (ingawa huwa wanaiandika ile n kwa herufi kubwa), au “Maandiko” au “Biblia” au “Biblia Takatifu”, wakati hawaamini kwamba hilo ni neno la Mungu kama alivyolifasili Mungu mwenyewe. Kutokana na kauli ya Mungu mwenyewe, tunaposema “neno la Mungu” au “Maaandiko” tunatakiwa kumaanisha kuwa ni kitu kilichotunzwa, kilichovuviwa / kilichofunuliwa, cha uhakika, kisicho na makosa, si neno la watu, bali kiuhalisia, ni neno la Mungu (1Wathess. 2:13). Ni makosa makubwa kuirejea Biblia iliyopotoshwa kama neno la Mungu. Watu hawa, wanapokuwa pamoja na Mungu katika sala, huwa hawachunguzi mioyo yao wenyewe? Hawatubu makosa ya dhambi zao za kila siku za kufuru na upujufu? Mungu analifasili neno ‘upujufu’ kuwa ni kuchukua kitu kitakatifu – kama neno Lake – na kulifanya kuwa la kawaida au la chini (Ezek. 22:26; 44:23; Walawi 19:12). Kwa hivyo, wanapoutumia msemo “neno la Mungu” kwa kitabu wasichokiamini kwamba ni neno halisi la Mungu, hiyo inakuwa ni [dhambi ya] kufuru na upujufu. Na wanapothubutu kupuuza fasili ya Mungu ya neno Lake mwenyewe, hii inakuwa ni kiburi cha aina inayoshitua na kuudhi Wakristo waliopevuka na wenye uelewa, hata kama ufahamu wao wa mamlaka ni wa juu juu tu. Kama wangekuwa na kiasi chochote cha heshima kwa Mungu wangekuwa waangalifu pale wanapozizungumzia tafsiri zao zenye makosa mengi na kutumia tu maneno kama “tafsiri”, “fasiri”, “neno la mwanadamu”, “Maandiko bandia”, “Biblia bandia”, “neno lisilotunzwa, lenye chachu”, “maandiko”, nk. Wasiyatumie vibaya maneno ambayo Mungu mwenyewe ameyachagua kwa ajili ya neno Lake lililovuviwa, lisilo na makosa, takatifu. Na halafu pale wanapolilazimisha lile wanaloliita “Neno la Mungu” kupiga magoti na kusalimu amri mbele ya mamlaka ya concordance – kitu ambacho hata wao wanajua chanzo chake ni wanadamu – wanafanya kufuru zaidi na hivyo wanadhihirisha kwa matendo yao kwamba wao ni humanists wanaotukutuza Reason (Mantiki) na kuiweka juu ya ufunuo [wa Mungu]. Funzo la Zab. 138:2b na Matt. 12:32 ni kwamba Wakristo wanapaswa kuwa waangalifu zaidi juu ya wanachokisema kuhusu neno la Mungu kuliko jinsi wanavyolitumia jina Lake. Nini, hukulijua hilo!?

 

Iko njia sahihi – njia ya Kibiblia – ya kulitafuta neno la kweli la Mungu, na ziko njia zisizo sahihi (njia zote zisizo sahihi msingi wake ni falsafa) za kuchagua tafsiri ya Biblia. Kwanza, kwa kuwa bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebr. 11:6), tunapaswa kuanza kwa kuamini kwamba Mungu yupo na kwa kuamini alichokisema kuhusu neno Lake. Pili, Mungu anasema kwamba tunapaswa kuwatambua kwa matunda yao, kwa maana ya mti ulioharibika hauwezi kuzaa matunda mema. Hivyo basi tukitafuta na kuipata tafsiri ya Biblia isiyo na makosa wala migongano tunaweza kumaizi kwa uhakika kabisa kwamba ule Mti uliozaa tunda hilo jema si Mtume Paulo wala Westcort and Cort, wala ile Kamati ya Kutafsiri ya Mfalme Yakobo / James – bali ni Mungu mwenyewe. Na ikiwa tutakutana na tafsiri ya Biblia iliyo na makosa na migongano, tunaweza kwa uhakika kabisa kumaizi kwamba tunda hilo lenye chachu halikutoka kwa Mungu, bali lilitoka kwa mwanadamu, na tunda hilo halitofaa kuchukuliwa kama neno la Mungu, wala Maandiko, wala Biblia.

Hili nililolisema sasa hivi linalazimu na limejengwa juu ya msingi wa imani kwa Mungu, hili ndilo tatizo walilo nalo Wakristo wengi. Ulazima wa imani kwa Mungu unapingana moja kwa moja na msingi mkuu wa falsafa: imani ya Kidini hairuhusiwi kuhusishwa na mchakato wa fikra; Reason pekee ndiyo inatumika; mbinu za kisayansi pekee ndizo zinatumika. Mkristo wa leo anataka kukubalika katika jamii ya kidunia ya watu wasiomjua Mungu hivyo anatumia juhudi kubwa kuwaonyesha walimwengu hao [wasiomjua Mungu] kwamba uanazuoni wake ni “halali” na “makini” kwa kuacha umaizi / utambuzi wa kiroho na kukumbatia Natural Reason (unaweza kuiita Mantiki Asilia) kinyume na 1Wakor. 2:14. Kama hauna makubaliano na hiki nilichosema hapa (na Wakristo wengi hawaafiki), ni vigumu kwa somo hili kukusaidia; kwa sababu bila imani huwezi kumpendeza Mungu (Waebr. 11:6), Naye hatakupa ruksa ya kuuelewa uhalisia wa mambo (Luka 24:45; 1Wakor. 1:19,20) kwa sababu kila unachofanya ambacho msingi wake ni sayansi badala ya imani ni dhambi dhidi Yake (War. 14:23b). Wengi kati yenu ninyi Wakristo mna mashaka – kwa sababu mbalimbali – juu ya Ukristo mnaouona kati yenu. Lakini mna desturi ya kufikiria – na kujitetea – kwamba viongozi hao wote na wanazuoni wote waliojenga mfumo huu katika karne zilizopita ambao leo tunauita Ukristo haiwezekani kwamba wamekosea. Yawezekana vipi kwamba watu hao wote waliochukua kozi kama Ancient Middle Eastern Architecture 101, Dead Language Studies 201, Mastering Church Economics 301, na The Mechanics of Successful Preaching Techniques 201, wamekosea?! Na unaweza vipi kujua kwamba wamekosea? Mimi nasema kwamba Wakristo wangeutumia muda wao vyema zaidi kama wangelima bustani ya nyanya kuliko kuchukua kozi hizo. Nasema hivyo kwa sababu kozi hizo zimewasababishia wawe na uhusiano hasi na Bwana Yesu Kristo; kulima bustani ya nyanya hakuathiri uhusiano huu. Ninajuaje hili? Ni kwa sababu mimi naijua Biblia.

 

Ili uwe na fikra za Kristo, ili uwe na umaizi wa kiroho utakaotuwezesha kubainisha kila kitu (1Wakor. 2:14-16), unapaswa kuyatumia maneno ya kiroho yaliyomo katika Biblia (1Wakor. 2:13; Yoh. 6:63; 14:23-26). Kwa maneno mengine: kama unaijua Biblia, hakuna chanzo kingine chenye mamlaka kuhusiana na Ukristo ambacho wewe hujakisoma; unajua kila chanzo cha mafundisho kilichotumiwa na kinachotumiwa na wahubiri na wanazuoni katika historia yote. Kila kanuni waliyoifundisha na wanayoifundisha inatakiwa kutoka katika Biblia pekee kwa sababu hakuna chanzo kingine. Ni Biblia pekee itakayokuonyesha ukweli wa Zab. 119:97-100. Ni kwa njia hii pekee ndiyo unaweza kujua na kuwa na uhakika wanakosea, au la.

 

Hao wote wanaijua Biblia pia, sivyo? Hapana, wameisoma na kujifunza. Lakini hawaamini kwamba chochote walichokisoma na kujifunza katika Biblia ni neno la Mungu kama alivyofafanua Yeye mwenyewe katika neno Lake. Ukosefu huo wa imani umesababisha Mungu asiufungue ufahamu wao, na hivyo hawawezi kuzishinda tabia za kimwili za mtu [wao wa ndani] wa kidunia ambazo sisi sote tunapaswa kupambana nazo na kushinda mara baada ya kuzaliwa upya. Reason / Mantiki hiyo ya kidunia inawazuia hao wote kupata ufahamu unaozidi ule wa waalimu na wanazuoni wao. Kwa hakika, [Mantiki] imesababisha wakubaliane na busara za kipumbavu za wanadamu wanaopingana na Mungu kwa kusema, “Utawatambua kwa asili yao; tunapaswa kurudi kwenye nyaraka za zamani za Kiebrania na Kiyunani ili kuupata ukweli kwa sababu haupo katika Biblia yoyote tuliyo nayo siku hizi.” Wanafikiri – kwa mantiki sahihi kabisa – kwamba nyaraka za zamani zilikuwa na muda mfupi zaidi wa kuharibiwa na watu kwa hiyo yamkini zina makosa machache zaidi. Wazo hili la ovyo limetokana na philosophy kupitia kwa Antiquarians. Ninawezaje kusema kitu kilicho na mantiki namna hiyo kuwa ni cha ovyo? Kwa sababu kama mtumishi wa Yesu Kristo sina ruksa ya kutegemea Reason / Mantiki – natakiwa kutegemea ufunuo. (Sentensi hii iliyopita ndiyo kiini cha kitabu hiki chote). Mantiki yao ni ya kidunia na inamdharau Mungu kabisa na alichoahidi kufanya juu ya neno Lake. Hivyo hawawezi kuutumia ukweli kwamba Biblia inasema neno la Mungu ni la milele. Hii inamaanisha kwamba haliathiriwi wala kupotoshwa na wakati, mkondo wa bahari, au watu. Tizama mfano wa Kristo katika neno Lake, KJB: Katika Matt. 22:31,32 anasema “Mimi ni ...” (I am) kauli ambayo inasemwa katika wakati uliopo (present tense); na katika 2Tim. 3:15,16 anasema “Maandiko yote yanatolewa” (All scripture is given …) kauli ambayo nayo iko katika wakati uliopo (present tense). Hawa watu wanashindwa kuufuata mfano huu wa Kristo. Tizama pia katika Waebr. 4:12 “Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu …” (Wakati uliopo / present tense!).

 

Ebu sasa tuchunguze nyaraka za Kiebrania na Kiyunani ambazo wanazuoni na wahubiri wanataka wewe uziheshimu sana.

NYARAKA ZENYE MAKOSA / DOSARI (ERRORS)

 

Wakristo wengi wanadhani kwamba nyaraka asilia za Kiyunani zipo wakati huu hapa duniani, kwa sababu wahubiri wao mara nyingi wanalisahihisha neno la Mungu kwa kunukuu “the original Greek” (yaani Biblia katika Kiyunani cha kale). Hakuna nyaraka kama hizo kwa wakati huu, hii ni hadithi ya kubuni tu. Nyaraka za kwanza za Biblia katika Kiyunani, Kiebrania, Kiarami / Kikaldayo – ambazo pia huitwa “the originals” au “the original autographs” – hazipo. Hata nakala za hizo nyaraka za mwanzo hazipo. Kwa hakika, katika miaka takriban 1,500 iliyopita hakuna mhubiri, mhubiriwa, mwanazuoni, mwana-akiolojia wala mtafsiri wa Biblia yeyote aliyeona nyaraka za kwanza wala nakala za nyaraka za kwanza za Biblia.

 

Kilichopo ni nini? Ni maelfu ya vipande, sehemu za kurasa za tafsiri za Biblia za zamani, kutoka karne ya 4 hadi ya 13. Kwa nini mimi ninaziita “tafsiri” za Biblia badala ya kuziita “Biblia” au “nyaraka” za Biblia? Kwa sababu zote hazifanani, kila moja inazungumzia mambo tofauti. Sasa, kutoka hizi tafsiri tofauti wanazuoni wanachukua na kuchagua nyaraka na vipande vya kurasa wanavyopenda na wasivyopenda wao kwa kutumia vigezo wanavyoviamua wao wenyewe, kama vigezo ambavyo Wakristo wanavitumia siku hizi wanapoingia katika duka la vitabu “vya Kikristo” na kununua tafsiri ya Biblia wanayoitaka wao wenyewe. Kama kusingekuwa na tofauti katika maelfu ya mabaki ya hivi vipande chakavu, vinavyozidi kuoza vya karatasi, ngozi, mafunjo, nk, wanazuoni wasingeweza kuweka katika makundi na familia za makundi mabaki haya. Kuna familia mbili zinazohusika katika mjadala wa tafsiri za Biblia.

 

Kundi au familia ya kwanza ndiyo kubwa zaidi (inahusisha 90% hadi 95% ya nyaraka za kale) na kundi hili halipendelewi sana na wanazuoni na wahubiri. (Kumbuka, japokuwa neno nyaraka linatumika mara nyingi, neno hili linarejea na kuhusisha kurasa moja moja, vipande vya kurasa, sehemu za sura na sehemu za vitabu.) Kwa sababu kundi hili ni kubwa zaidi, familia yake inaitwa Majority Text. Pia kwa kawaida familia hii huitwa Receved Text au Textus Receptus (kwa Kilatini), kwa sababu yenyewe inahusisha sehemu kubwa ya nyaraka zote tulizopokea (“received”) kutoka ulimwengu wa kale.

 

Kwa ujumla, Wakristo wachache wanaopendelea familia ya nyaraka zilizoharibika za Textus Receptus wanafanya hivyo kwa sababu wameambiwa kwamba King James Bible imetokana na familia ya Textus Receptus, na kwamba familia hii haina dosari nyingi kama ile familia inayoshindana nayo ya tafsiri za Minority Text. Sasa, KJB haitoki katika familia ya Textus Receptus. Lakini pia ni kweli kwamba nyaraka za Majority Text hazina makosa mengi kama zile za Minority Text, ingawa ukweli huu hauna umuhimu wowote. King James Bible haikutoka katika kundi / familia ya Textus Receptus kwa sababu familia hii haikuwepo katika mwaka 1611 (KJB ilianza kuandikwa 1604). Tunahesabu zaidi ya karne mbili baada ya kuchapwa kwa KJB ndipo tunaona watu wakianza kuhifadhi vipande mbali mbali vya karatasi (za nyaraka za kale) walivyookota maeneo mbalimbali. Watu wengi pia walianza kutafuta vipande hivi kwa sababu walianza kuamini kwamba Mungu hakulitunza neno Lake na kwamba wao walipaswa kupekua mambo ya kale ili kuvumbua hekima [ya Mungu] iliyopotea. Walipopata vipande vingi zaidi wakaunda makundi na familia za makundi na wakaamua kuweka nyaraka zilizotumiwa na waandishi / wana-taaluma wa KJB katika familia ya Textus Receptus kwa sababu nyaraka za TR hazikuwa na makosa mengi au zilikuwa na makosa ya aina tofauti na yale yaliyokuwa katika familia shindani. Lakini sisi tunajua kwamba Authorized King James Bible haikutokana na familia ya nyaraka za TR, na hii ni kwa sababu KJB haiendani na nyaraka yoyote katika familia ya TR. Kwa hakika, KJB ina maandishi ndani yake ambayo hayako katika nyaraka za kundi au familia yoyote hapa duniani.

 

Wakristo wengi wanaichukulia KJB kuwa ni sehemu ya familia ya Textus Receptus kwa sababu mantiki yao ya kimwili (na si imani ya kiroho) inawazuia kukubali, kuamini, na kutumia aya hizi: 1Tim. 1:4 na Matt. 7:20. Wanafikiri wataonekana mahiri wanapounda shajara za familia za nyaraka kwa kubuni shajara za nyaraka zinazofanana ili waweze kufanya uchunguzi wa “nyaraka za mwanzo kabisa”. Ndiyo maana wanaziita familia za nyaraka. Wanajidhihirisha kwamba wao ni wapinga Biblia wasio na imani kila mara wanapofungua vinywa vyao.

 

Kwa upande wa pili, familia nyingine ya nyaraka ni ndogo; hii ina 5% ya mabaki yaliyoko leo. Kwa kuwa nyingi kati ya nyaraka hizi zimeunganishwa na mji wa Alexandria huko Misri, kilichokuwa kitovu kikuu cha uanazuoni hapo kale, familia hii inaitwa “the Alexandrian Texts”. Hili ndilo kundi linalopendwa na ndilo lenye nyaraka zinazotumiwa katika kutengeneza tafsiri nyingi za kisasa za Biblia. Kinachowavutia wanazuoni wengi katika familia hii ni kwamba vipande vya karatasi vilivyoko humu ni vya kale zaidi kuliko vile vilivyomo katika Textus Receptus. (Kumbuka, kama tulivyoona hapo kabla, miaka haina umuhimu katika mambo ya milele kama neno la Mungu.)

 

Nyaraka kuu mbili zinazopendwa katika familia ya Alexandria ni nyaraka za Sinai na nyaraka za Vatican. Nyaraka za Sinai zilipata jina hilo kwa sababu zilipatikana katika shimo la taka la nyumba ya watawa karibu na (unaokisiwa kwamba ni) mlima [wa kale] wa Sinai. Nyaraka za Sinai zinamilikiwa na Vatican ya Kanisa la Rumi. Licha ya imani kwamba umri mkubwa (kama wa nyaraka hizi) unamaanisha makosa (au dosari) chache zaidi, familia hii ya nyaraka ina makosa mengi zaidi kuliko ile familia changa zaidi ya Textus Receptus. (Hata hivyo, hili halina umuhimu wowote; uwepo wa makosa ndilo jambo muhimu, na si idadi ya makosa.)

 

Ingawa nyaraka hizi zinaitwa the Textus Receptus na the Alexandrian Text, siyo kwamba iko moja! Nyaraka zote mbali mbali ndani ya kila familia zinatofautiana. Sababu nyingine inayonifanya mimi nizinukuu hizi nyaraka za kale kama tafsiri za Biblia ni kutilia mkazo kwamba mwanazuoni fulani anapozungumzia “the Textus Receptus” huwezi kujua anazungumzia vipande gani vya karatasi za kale. Wahubiri wanapuuza idadi ya makosa, migongano, na tofauti kati ya nyaraka zinazounda familia moja kwa sababu wanajaribu kukuaminisha kwamba kuna “kitabu” kimoja kinachowakilisha familia hiyo. Hivyo wanapenda kuzungumzia asilimia za tofauti zilizoko kwa sababu neno asilimia linasaidia kupunguza kishindo / mshituko utakaoupata pale unapotajiwa idadi yenyewe ya makosa / dosari, migongano, tofauti zilizoko pale wanapozungumzia neno la Mungu. Katika kukuonyesha tu jinsi nyaraka au tafsiri hizi zinavyotofautiana, ebu tutizame takwimu moja hapa: Hata nyaraka zilizo ndani ya familia moja (yaani zile nyaraka au tafsiri zinazochukuliwa kwamba “zinakubaliana”) zina wastani wa tofauti 6 hadi 10 katika kila sura – na kuna sura 1,189! Baadhi ya tofauti hizo zinachukuliwa kuwa ni “ndogo” pale zinapochukuliwa kwamba hazina kishindo kikubwa katika maana ya sura husika.

 

Hivi punde tutachunguza baadhi ya makosa hayo ili tuweze kudhihirisha kwamba ni makosa halisi, lakini mpaka hapo ninatumaini kwamba umeanza kuelewa kwamba msimamo wa wengi wa wahubiri, waumini, na wanazuoni ambao hawaamini kwamba Mungu amelitunza neno Lake kwa ajili ya kanisa Lake la leo msingi wake ni fikra za mpangilio za kibinadamu na Mantiki, na si ufunuo na imani. Na wanadhihirika kuwa ni wanafiki kwa udanganyifu wanaoutumia wanapozungumzia aya za Biblia zinazofasiri neno la Mungu na zinazotufundisha kwamba Mungu amelitunza neno Lake kwa ajili yetu. Mhubiri fulani (ambaye wana-kanisa wake walinihakikishia kwamba yeye anaamini kweli kweli kwamba KJB ni neno la Mungu) alitumia balagha za kila aina nilipokuwa naye katika mazungumzo ya faragha ambapo nilimwuliza kuhusu kanuni za Biblia anazoamini. Alikuwa anatamka kauli za juu juu kama: “Nakiamini hiki Kitabu cheusi cha kale kutoka jalada la mbele mpaka la nyuma, naliamini hata jalada lake”; “Naamini KJV ni tafsiri pekee ambayo ndiyo neno la Mungu na Wakristo wanapaswa kuitumia hiyo pekee.” Nilipombana awe bayana akakubali kwamba kwa kuwa Textus Receptus ina makosa, [basi] naye anaamini kwamba King James ina makosa pia, na kwamba kwa kweli yeye anaamini kwamba ni zile nyaraka za kwanza pekee ambazo sasa zimepotea ndizo zilikuwa na pumzi ya Mungu na zilikuwa hazina makosa. Akasema Mungu alizifanya nyaraka zile za kwanza zipotee ili kuzuia dhambi ya kuabudu kitabu. Akasema kwamba Mungu anataka uwepo wa makosa katika tafsiri zetu za Biblia kwa sababu hiyo hiyo. Nilipomwuliza kuhusi aya zinazosema kwamba neno la Mungu lipo leo akasema [yeye] anaamini neno la Mungu lipo – [lakini] lipo na Mungu mbinguni. (Mungu hakubaliani na hili: Kumb. 30:10-14.) Akanipa siri kwamba alikuwa ananiambia mambo ambayo hayazungumzi na waumini wa kanisa lake kwa sababu wengi wao hawana uwezo wa kuhimili ukweli; ukweli utaangamiza imani yao – wana uhitaji wa kufikiri kwamba ukweli umo mikononi mwao. Mimi niliweza tu kupata haya yote kutoka kwake kwa sababu yeye ni mtu anayejiheshimu na hakuweza kusema uwongo nilipomshinikiza awe bayana juu ya imani zake. Sababu nyingine alikubali wazi wazi kubainisha msimamo wake ni ukweli unaosikitisha kwamba imani zake hizi hazichukuliwi kuwa ni uzushi na sehemu kubwa ya wanazuoni wa Kikristo – wote wanaamini mambo hayo hayo.

 

Sasa, tukirudi kwenye familia za nyaraka, ipi ni bora zaidi, the Alexandrian au the Textus Receptus? Ukitumia mantiki [ya kibinadamu] unaweza kuchagua yoyote kati ya hizo mbili; uchaguzi unategemea moyo wako umeelekea wapi, kama unavyoingia katika mini-market na kuchagua chokoleti moja kati ya nyingi katika kikapu. Lakini ukitumia viwango vya Kibiblia, zote mbili ni takataka na zinafaa tu kutumiwa kutengeneza kitanda cha kulalia paka. Zuzu yoyote yule anaweza kunukuu Wagalatia 5:9, “Chachu kidogo tu huchachua donge [zima la unga]”, lakini Wakristo wanaotumia mantiki yao wenyewe hawajui kutumia Maandiko katika maisha wanayoishi. Hivyo wanakimbia huku na huko wakizitangaza familia za nyaraka zao zenye chachu kwamba ni “za kale na za kuaminika zaidi” na “zemependekezwa na wanazuoni”. Washindani wao wanawajibu kwa kusema familia yao yenye chachu ina dosari chache zaidi na imekuwa ikitumiwa na Waprotestanti hadi miaka michache iliyopita. Makundi yote mawili yanatetea na kukuza matunda yaliyooza – tofauti iko katika kiasi cha uozo tu.

 

Mungu hatengenezi wala hahifadhi chachu Anapojishughulisha na neno Lake. Watu wanaposema Mungu aliongoza uandishi wa nakala [za Biblia] za kwanza halafu wanadamu wakaziharibu na kuzipotosha katika karne zilizofuata, unaweza kuwapuuza kwa sababu wao wanampuuza Mungu. Hilo ni neno Lake, na pia ni Yeye mwenyewe aliyetoa kauli imara juu ya neno Lake; Yeye ndiye aliyesema atalihifadhi na atatutathmini na kutuhukumu kwa kulitumia neno hili. Kwa hiyo kamwe, kamwe usimweke nje ya majadiliano juu ya neno Lake. Sababu inayozifanya zile nyaraka za kale kuwa si kitu bali mabaki yanayooza ni kwamba zimekataliwa na Mungu mwenyewe kwa kuwa ni chachu zilizojaa dosari, makosa na migongano. Jambo la Mungu kuzikataa nyaraka hizi linatia moyo kweli kweli, kwani hili linaonyesha kwamba Yeye si kivuruge aliyesema atalihifadhi neno Lake na kushindwa kufanya hivyo ambaye Wakristo wengi wanamwona hivyo. Hivyo, kwa kuwa wanazuoni waasi wameunda makundi ya familia ya nyaraka kulingana na Mantiki yao binafsi ilivyowaongoza, basi ni jambo la kufaa kwa wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo kumtukuza Bwana wao kwa kutumia imani na ufunuo kufanya hivyo hivyo katika namna ya kufaa zaidi. Kwa kuwa nyaraka zote za familia zote mbili zimeharibika, na kwa kuwa uharibifu huu ndio tabia kuu na muhimu katika nyaraka hizi, basi nyaraka zote katika familia zote mbili zinawekwa katika kundi moja na kuitwa kama “E.R.R.O.R. manuscripts.” ERROR ni akronimi inayosimama kama kumbukumbu ya kile tunachokizungumzia pale tunaposema vitu kama “Kiyunani cha kale” na “Textus Receptus”. E.R.R.O.R. inamaanisha Existing Remnants of Rotten Old Rejects.

 

Sasa unaposikia watu wakisema vitu kama, “Familia hii ya nyaraka inaaminika zaidi”, utagundua kwamba wamesema hivyo kwa sababu hawawezi kutamka kwamba haina makosa kabisa. Zote ni nyaraka zenye makosa, dosari, migongano. Na hiyo Textus Receptus inapaswa kuitwa Textus Rejectus!

 

MAANDISHI YA LUGHA ZILIZOKUFA

 

Mhubiri wako anaposema, “Kwa mujibu wa maandishi ya Kiyunani (au Kiebrania) neno hili katika “Biblia” zetu [kiuhalisia] linapaswa kuwa …” je anazungumzia nyaraka za ERROR? Hapana, lakini anakuacha wewe uendelee kudhani kwamba yeye ananukuu zile nayaraka za ERROR: hajawahi hata kukiona kimoja tu kati ya maelfu ya vipande [vilivyobaki] vya nyaraka za ERROR na wala hatoweza kuvisoma hata kama akikiona [kipande hicho] kwa sababu nyaraka hizi ziliandikwa katika lugha ambazo [sasa] zimekufa; hakuna jamii wala kikundi chochote cha watu wanaozungumza lugha hizo kwa sasa. Kiebrania kinachozungumzwa siku hizi ni tofauti; na hali ni hiyo hiyo kwa Kiyunani cha Agano Jipya. Kiyunani kile ni lahaja [mojawapo] iliyokufa ambayo hata Wayunani wenyewe hawaizungumzi tena. Hapa nina ulazima wa kukuelezea kuhusu haya maandishi ya lugha zilizokufa kabla sijazungumzia maandishi / nyaraka ambazo mhubiri wako anazitumia.

 

Nyaraka za ERROR zinatokana ma maelfu ya maandishi ya lugha zilizokufa (zaidi ni Kiyunani na Kiebrania). Idadi ya nyaraka hizi ni kubwa kweli kweli. Kila moja inatofautiana na mwenzake katika maeneo mengi. Katika maeneo mengine zinakubaliana. Na katika maeneo mengine unaweza kukisia mwenyewe. Sasa hao ERRORists ni wale wanazuoni wanaopekua maelfu haya ya vipande na kujaribu kugundua ipi kati ya aya zinazotofautiana ina uwezekano wa kuwa na usahihi zaidi.

 

Huyu ERRORist, kwa mfano, atapitia idadi fulani ya hizi nyaraka alizozichagua yeye na kuamua kwamba aya fulani inatakiwa kusomwa hivi, na kuzikataa namna nyingine ambazo aya ile ile inaweza kusomwa. Uhariri wake msingi wake unatokana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na msimamo wa dhehebu lake, mtazamo wake binafsi, upendeleo wake, nk. Katika maeneo mengi ya nyaraka hizi ana uhuru mkubwa wa kuamua ni maneno gani ayachague. Kazi yake ni kutengeneza “Biblia” moja [itakayosomwa katika lugha zilizokufa] kutokana na maelfu ya nyaraka za lugha zilizokufa. Kwa maneno mengine, mwanazuoni wetu anaandika kile anachodhani Mungu “alimaanisha”. Inampasa kupambana na wastani wa tofauti 6 hadi 10 za maneno katika kila sura na aamue ipi atakayoitumia kati ya hizo, au atumie maneno mengine atakayoamua mwenyewe. Wakati mwingine, anapofikiri / anapodhani aya fulani haina uhalisia, anairuka aya hiyo kabisa (nitakuonyesha mifano hapa chini). Anapohakikisha kila neno na kila aya vipo katika namna anavyofikiri yeye vinapaswa kuwa, basi anachapisha kitabu hicho katika lugha iliyokufa ya Kiyunani kama Smith’s Greek Text. Hapo anatokea mwanazuoni mwenzake anayeitwa Mr. Jones ambaye anaipitia kazi hii ya Mr. Smith na haamini jinsi ilivyo mbovu na mbaya! Hivyo bwana Jones anafikiri bwana Smith alipaswa kutumia mabaki / vipande fulani ambavyo amevipuuza, alipaswa kutumia maneno tofauti katika aya fulani, alipaswa kuchagua nyaraka za kale zaidi, au nyaraka zenye kurasa nyingi zaidi zilizo nzima (na si vipande), au alipaswa kutumia marginal notes katika nyaraka hizo, nk. Kwa hiyo bwana Jones anachapisha Agano Jipya lake mwenyewe na kukiita kitabu hicho Jones’ Greek Text. Miaka kadhaa baadaye wote wawili wanazitizama kazi zao hizi na hawana furaha nazo. Hivyo wanafanya masahihisho na mabadiliko na wanachapisha matoleo ya pili. Sasa, matoleo yote 4 yanabakia sokoni kwa sababu kila kamati ya tafsiri ya Biblia ina mambo yake inayoyapenda na mengine isiyoyapenda.

 

Kisha anatokea Mr. Brown; naye anaipitia Smith’s Greek Text, Second Edition, na anatikisa kichwa chake kwa kicheko cha dharau. Smith aliamua kutumia kipande cha karatasi-ngozi 225 katika kuandika sehemu ya kwanza ya aya fulani, na Brown anafikiri / anadhani kwamba alipaswa kutumia p46 au labda angetumia hata B katika kuiandika aya yote. Brown pia anaona kwamba Smith alitumia Db, H, P, na 436 katika kuandika aya fulani na wala hakujali uandishi ulio tofauti sana lakini ulio bayana kabisa uliopo katika K. Ni kweli, maandishi haya tofauti ya aya hii hayaonekani katika nyaraka nyingi tu, lakini ukweli kwamba iko bayana namna ile unapaswa kuipa karatasi-ngozi K uzito fulani! Pia anafahamu kwamba Smith alihitimu chuo kabla karatasi-ngozi 0208 haijavumbuliwa na wana-akiolojia, na ingawa wanazuoni wengi wanaukataa uhalali wa 0208, mmoja kati ya wanaotambua kuwa 0208 ni halali ni profesa wa lugha zilizokufa wa huyo huyo bwana Brown! Na hili linatuonyesha kwa nini tafsiri ya neno fulani ya bwana Brown ilikuwa tata namna ile.

 

Hapo anaingia ndugu mwingine anayeitwa Mr. Miller; naye anasema kwamba kwa jinsi anavyomjua, bwana Brown ana tabia ya kufuata mawazo yake mwenyewe tu, hapendi kusikiliza wengine. Kwani walipofanya kazi pamoja katika kutengeneza kazi yao iitwayo Brown-Miller Greek New Testament, Miller alikuwa bado mdogo na hakuwa na uzoefu sana. Kwa sababu hiyo akamwacha Brown amlazimishe kukubali maneno fulani yaandikwe ambayo Miller aliona kuwa msingi wake umejikita sana katika ajenda ya kijamii ya Brown, yalikuwa na ushahidi / msingi mdogo sana wa kinyaraka, na yalikuwa yanapotosha au kudanganya kabisa. Kusema kweli, kama isingekuwa kwamba uandishi huu ulikuwa fursa ya kwanza ya Miller kuchapishwa na kupata pesa nzuri, Miller angejitoa katika kazi ile. Miaka kadhaa baadaye Miller alichapisha Greek New Testaent yake mwenyewe ambayo aliamini kwa dhati kabisa kwamba ilikuwa bora kwa kiasi kikubwa kuliko ile Brown-Miller Text. Kazi hii ya Miller haikufikia hata 50% ya kujulikana kama ile ya Brown-Miller Text kwa sababu Brown alikuwa mtu wa kujikomba kwa watu na alikuwa anafahamika na wakubwa wengi katika ulimwengu wa uchapishaji. Miller alikuwa akikereka sana kwa sababu the Brown-Miller Text ilikuwa ikitumika kwa karibu 25% katika kutengeneza tafsiri ya Biblia moja iliyokuwa na wafadhili wenye pesa sana na kwa karibu 20% katika kutengeneza tafsiri ya Biblia ingine inayopendwa sana ambayo imefanya vizuri namna ile kwa sababu tu idara ya masoko ya wachapishaji walitumia pesa nyingi katika kuipamba na kuipendezesha pamoja na matangazo katika media na hawakutumia muda wa kutosha katika kamati ya uandishi.

 

Kuna mamia ya ERRORists ambao mara nyingi huunda matoleo mengi. Kila toleo linatofautiana na mengine yote, na hii maana yake ni kwamba kuna mamia ya matoleo ya nyaraka za lugha zilizokufa na kila moja inasimama kama tafsiri ya kipekee ya Biblia. Ukweli huu pekee ni ushahidi tosha kwamba hakuna kitu kinachoitwa “waraka wa Kiyunani” au “waraka wa Kiebrania”. Kuna mamia ya nyaraka, zote zinatokana na matakwa na fikra za watu, na zote zinatofautiana. Na nyaraka mpya zinazuka kila wakati. Hawa ERRORists wanaochapisha hizi nyaraka kama utitiri hawaamini kama kuna yoyote kati ya hizo kazi zao ambazo ni neno lililotoka kwa Mungu; wanajua hivi kwa sababu maandishi yao yana makosa, dosari na migongano mingi mno.

 

Hivyo utakapomsikia mtu fulani anazungumzia “katika Kiyunani” au “katika nyaraka za Kuyunani” basi sasa unajua anazungumzia moja kati ya mamia ya vitabu vinavyochapishwa na hao ERRORists. Hivyo basi, ili mambo yawe bayana siku zote mwulize mtu wa namna hii ni waraka gani wa Kiyunani anaounukuu. Je, ni Brown-Miller Greek New Testament au ni Second Edition of Smith’s Greek Text, au ananukuu kutoka sehemu mbali mbali za nyaraka tofauti? Na unapomsikia mtu fulani akiisahihisha Biblia kwa kusema “Kiyunani cha kale kinasema …” sasa unajua kwamba nyaraka za kwanza za Biblia hazipo, kwamba nakala za nyaraka za kwanza nazo hazipo, kwamba alipaswa kusema “Brown-Miller Text inadai kwamba kipande fulani cha karatasi-ngozi 0208 cha nyaraka za ERROR kinasema …”, kwamba yumkini halifahamu suala la tafsiri mbali mbali za Biblia kama unavyolifahamu wewe sasa, kwamba huyu jamaa ni mpuliza-upepo mwenye majivuno anayeeneza kufuru juu ya neno hai la Mungu aliye hai.

 

 

UTENGENEZAJI WA TAFSIRI YA BIBLIA

 

Wanakamati wa tafsiri za Biblia za kisasa kamwe hawajisumbui kuzitazama zile nyaraka za ERROR. Wanachagua kutoka katika nyaraka za Kiebrania au Kiyunani zilizochapishwa na ERRORists kama zile za Brown na Miller wanazoziona zinawapendeza na kutafsiri kutoka hizo. Kutafsiri kutoka katika lugha iliyokufa si kazi rahisi.

 

Kamati za kutafsiri ni wale watu wanaochukua nyaraka za lugha zilizokufa ambazo zimechapishwa na ERRORists mbali mbali na kutokana na hizo wanajaribu kumaizi maana za maneno mbali mbali katika hizo lugha zilizokufa za Kiyunani na Kiebrania na namna tofauti maneno hayo yalitumika. Kwa mfano kama sentensi katika lugha iliyokufa inasoma “You are kidding me!” watajaribu kutafuta maandishi ya kale mengi iwezekanavyo na kuyachunguza hayo ili waweze kumaizi maana ya neno kidding. Mwishowe watagundua kwamba neno hili linamaanisha baby goat. Hivyo wataitafsiri sentensi hii hivi: “You are treating me like a young animal!” na wataichapisha katika tafsiri ya Biblia na kuiita The Revered Version. Baada ya miaka kadhaa kupita inakuja kamati nyingine ya kutafsiri na kuipitia kazi hii kwa malengo ya “kuiboresha”. Hawa jamaa wataamua kwamba muktadha wa sentensi hii unaonyesha kwamba kinachomaanishwa ni upumbavu au ujinga zaidi ya “unyama” hivyo wataitafsiri sentensi yetu hivi: “You are treating me as if I were as stupid as a young goat!” Wataichapisha hii kama “The New Revered Version”. Kamati ya kutafsiri ya mchapishaji mwingine itatumia maandishi ya kale yaliyopuuzwa na kila mtu na, wakifikiri kwamba wao wamevumbua ufahamu mzuri zaidi wa maana halisi ya sentensi hii, wanaichapisha katika Biblia yao “The New Light Bible kama, “Kama mbuzi anavyozaa, [wewe] unasababisha wazo jipya moyoni mwangu.” Baadaye, mchapishaji mwingine ataingia katika soko lenye pesa nyingi la biashara ya kuchapisha [na kuuza] Biblia kwa kuasisi kamati ya kimataifa ya kutafsiri Biblia na kuchapisha The Global Standard Version na kuiandika sentensi yetu kama, “You are being as playful with me as a baby goat!” Ni muhimu kuelewa kwamba majaribio yote haya ya kupata maana ya neno [hili] yataingizwa katika kamusi za Kiebrania – na Wakristo ambao, bila kuujua uhaini ulioko nyuma yake, wataamini kwamba fafanuzi hizi za kamusi zina mamlaka na ni za kuaminika watakuwa na tabia ya kuchagua mojawapo kati ya maana hizi za neno hili ili “kuwaonyesha” Wakristo wengine waliochagua maana tofauti ya neno lile lile [katika kamusi zile zile] kwamba “wamekosea”. Unaweza mwenyewe kutizama maneno kadhaa katika kamusi za Kiyunani na Kiebrania ili kuhakikisha hili, utaona mara nyingi wana maana tofauti za neno moja ambapo utatakiwa wewe mwenyewe kuchagua ipi unaiona sahihi (ziko kamusi kadhaa unazoweza kupakua bila gharama / bure mtandaoni).

 

=0=

 

NB: Mahala / sehemu nyingine utaona uanazuoni mbovu kabisa, ambao kwa wazi umetokana na utafiti wenye dosari.

 

Mfano ni Yona 1:7 katika SUV: Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.

KJB. Jonah 1:7 And they said every one to his fellow, Come, and let us cast lots, that we may know for whose cause this evil [is] upon us. So they cast lots, and the lot fell upon Jonah.

SUV. 1.26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.

KJB. Acts 1:26 And they gave forth their lots; and the lot fell upon Matthias.

 

Tafsiri za Kiswahili zinatafsiri “casting of lots” kama “kupiga kura”. Lakini Webster’s Dictionary inatupa tafsiri gani? “Determine an outcome by throwing dice or some other object.” Na kamusi yetu ya Kiswahili (TUKI) inasemaje? “Lot – bahati nasibu”; “kupiga kura” (kwa kuokota karatasi au kijiti kutoka kwenye kasha”. Msemo “kupiga kura” unamaanisha “kuchagua” – hivyo kwangu mimi, msemo huu si sahihi hapa. Walipaswa kuandika “kuchagua”. “Casting lots” ina rejeo la wazi la kumwachia Mungu afanye uchaguzi husika. Wakati “kupiga kura” kama ilivyo katika Yona 1:7 na Mdo. 1:26 ni uchaguzi unaoamliwa na mapenzi ya wanadamu.

 

=0=

 

Kama ukifanya majadiliano na kikundi cha watu ambao wamemaliza tu kutengeneza tafsiri mpya ya Agano la Kale kama sehemu ya fasili mpya ya Biblia na ukamwuliza mmoja wao jinsi walivyofanikikisha suala hili, atakwambia hivi ndivyo walivyofanya. Na ukumbuke, huu ndio utaratibu unaokubalika:

 

“Mahala pa kuanza mara unapoamua kutafsiri Agano la Kale kutoka katika Kiebrania cha kale [na kuja katika lugha yako] ni kusoma nyaraka mbalimbali zilizotunzwa na wanazuoni wa Masorah (Masoretic Texts) katika lugha ya Kiebrania. Moja kati ya tafsiri za kale zaidi za nyaraka za Masorah ni ule waraka wa Ben Asher. Lakini wanazuoni fulani / kadhaa wanakubaliana na Daniel Bomberg kwamba waraka wa Ben Asher hauko katika kiwango cha juu, hivyo wao wanaanza kazi yao ya kutafsiri Agano la Kale kwa kutumia nakala iliyosahihishwa na Daniel Bomberg ya waraka ule ule wa Ben Asher. Miaka iliyofuata, Jacob ben Chaim alichapisha nyaraka zake mwenyewe za Agano la Kale, katika Kiebrania, ambazo zinaheshimiwa sana, kwa sababu kwa mtazamo wake aliona kwamba kazi za hao wanazuoni wote waliomtangulia hazikuwa tafsiri sahihi za Agano la Kale “halisi”. Halafu Rudolf Kittel akachapisha matoleo mawili tofauti ya kazi ya Ben Chaim yaliyotenganishwa na miaka sita kati yao kwa sababu aliona kwamba hata toleo la kwanza la kazi yake mwenyewe lilipaswa kusahihishwa. Akaja Paul Kahle pia, ambaye alichapisha toleo lake lililoegemea sana katika moja kati ya tafsiri za Ben Asher za kale kabisa.

 

“Ah, kila wakati tunalazimika kufanya maamuzi tu, mwanangu! Hii ndiyo kazi yetu – kufanya maamuzi ya kisomi. Katika miaka takriban kumi na mmoja katika kazi hii ya kutafsiri Biblia, mimi ni mmoja kati ya wafasiri waandamizi katika kamati hii, na ninaweza kukusimulia hadithi kadhaa za vituko mbali mbali nilivyoshuhudia!! Anyway, kati ya mamia ya nyaraka zilizochapishwa na wanazuoni waliowaitwa ERRORists hapo juu, tuliamua kutumia waraka wa Daniel Bomberg. Hata hivyo, waraka huu haujitoshelezi, hivyo tulichagua baadhi ya maandiko kutoka Stuttgart Hebrew Edition ya Agano la Kale ambayo siku hizi haisikiki sana. Pia “tuliazima” aya kadhaa kutoka katika tafsiri ya Kiyunani ya Septuagint (LXX) ya nyaraka za kale za Kiebrania, pamoja na waraka wa Latin Vulgate, kwa sababu huu ulipendwa kwa miaka mingi sana katika kanisa Katoliki. Hata hivyo tulihisi kulikuwa na umuhimu wa kubadilisha baadhi ya maana za aya fulani, maamuzi tuliyoyafanya kutokana na kitabu tulichokisoma kinachohusu utafiti mpya kabisa katika zile nyaraka zilizovumbuliwa katika Dead Sea.

 

“Wakati mwingine, tulipoona tafsiri yetu itasomeka vizuri zaidi ikiwa tutachomeka irabu (vowels) tofauti na zile zilizotumika katika Kiebrania cha kale cha nyaraka za Masorah, tulifuata hisia zetu na kufanya hivyo. Sehemu zingine tulizibadilisha kutokana na nyaraka fulani za kale zaidi ambazo tuliona kwa kuwa ni za kale sana basi zilipaswa kupewa heshima kwa kiasi fulani. Lakini, si kila wakati tulifurahishwa na vyanzo tulivyoviorodhesha hapa juu; hivyo tulichagua pia aya kutoka nyaraka zingine za Kiebrania ambazo tofauti kati yao zilitupatia fursa nyingi za kutumia ubunifu wetu wenyewe. Nyaraka hizi ni kama: Aquila, Symmachus and Theodotian, Syriac Peshitta, Targums, na Juxta Hebraica. Pia tulitumia kamusi na vitabu mbalimbali vya Kiebrania vinavyofundisha juu ya chanzo cha lugha. Wakati mwingine tuliposhindwa kuamua namna ya kusoma na kuelewa lugha hii ya kale, na tulipokosa aya tuliyoipenda kwa pamoja, tuliuliza wanazuoni nje ya kamati ambao tuliwaona wana ustadi wa kutosha na ambao wanakubaliana na sisi katika kanuni za imani. Wakati wote katika kazi yetu hii tulibarikiwa kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu kati yetu. Tuligundua pia kwamba kazi ya ma-ERRORist inayoitwa the Samaritan Pentateuch ina maneno na aya tunazopenda kutumia. Na wakati mwingine tuliamua kutelekeza sehemu kubwa za nyaraka tulizo nazo na badala yake tukatumia maoni ya watu wasiojulikana ambao waliyaandika ukingoni mwa [nakala za] nyaraka zetu. Katika kutambua maana ya maneno na misemo tata tulitazama jinsi maneno na misemo hiyo ilivyotafsiriwa katika tafsiri mbalimbali za kisasa za Kiingereza na za lugha nyingine za kigeni. Na ili kuweka maana wazi kabisa, wakati mwingine tuliongeza maneno ambayo hayakuwa katika nyaraka zetu kwa sababu mitazamo yetu ni mizuri na sahihi kama ile ya watu wengine. Na wakati mwingine tulifanya mabadiliko katika aya ili kutoingilia hakimiliki ya tafsiri nyingine ambazo wamiliki wake wanaweza kutupeleka mahakamani ambako vita ya gharama ya hakimiliki inaweza kutokea kati yetu kwa upande mmoja, na wachapaji na wamiliki wa tafsiri hizo kwa upande wa pili.

 

“Kwa kuwa sisi tunaounda kamati za tafsiri mpya za kisasa tumeweka msingi wa tafsiri hizo tunazozizalisha katika kazi za ERRORists ambazo bado zina migogoro badala ya nyaraka zenyewe zenye ERRORs, tunaamini kwamba ni jambo la busara na la lazima kuchukua na kuchagua, kushauriana, kulinganisha, kufanya midahalo, kuamua, kurudia upya, kukataa, na kuandika upya ili kuzitumia vyema nyaraka zilizotajwa hapo juu na kuzalisha na kuweka sokoni bidhaa ambayo ni ya kiwango cha juu ambayo itawapendeza ninyi wateja – kwa bei muafaka.

 

“Katika maeneo fulani ya tafsiri yako unaweza kuona aya fulani inakosekana. Hii ni kwa sababu tuliamua kwamba aya hiyo yumkini haipo kwenye nyaraka asilia. Hivyo tukaiondoa aya hiyo na tukaruka namba ya aya hiyo ili tuendelee kufuata mfumo wa namba za aya ulioanzishwa karne kadhaa zilizopita na ambao utamalaki wa karne nne wa Authorized 1611 King James Version ukathibitisha kama mfumo rasmi wa namba za aya za Biblia.

 

Mfano kutoka NRSV. Aya namba 21 imerukwa:

 

19 Then the disciples came to Jesus privately and said, "Why could we not cast it out?" 20 He

said to them, "Because of your little faith. For truly I tell you, if you have faith the size of a mustard seed, you will say to this mountain, 'Move from here to there,' and it will move; and nothing will be

impossible for you." ****** 22 As they were gathering in Galilee, Jesus said to them, "The Son of Man is going to be betrayed into human hands, 23 and they will kill him, and on the third day he will be raised." And they were greatly distressed. Matthew 17.

 

Aya hii imo katika King James:

 

{17:19} Then came the disciples to Jesus apart,

and said, Why could not we cast him out? {17:20} And

Jesus said unto them, Because of your unbelief: for verily I

say unto you, If ye have faith as a grain of mustard seed, ye

shall say unto this mountain, Remove hence to yonder

place; and it shall remove; and nothing shall be impossible

unto you. {17:21} Howbeit this kind goeth not out but by

prayer and fasting.

{17:22} And while they abode in Galilee, Jesus said unto

them, The Son of man shall be betrayed into the hands of

men: {17:23} And they shall kill him, and the third day he

shall be raised again. And they were exceeding sorry.

Matthew 17.

 

“Kwa hakika, ile King James (Biblia ya Mfalme Yakobo ya mwaka 1611) kwa namna fulani hivi ikaja kuwa ndiyo kiwango ambacho tafsiri zote za Biblia zinapimwa. Kwa mfano, kwa sababu ya ushawishi wa karne nyingi wa ile Tafsiri ya King James, utaona si kila wakati tunazitoa zile aya ambazo sisi tumeamua kwamba zimeharibika kutoka katika tafsiri zetu – jambo linalotukera sana. Lakini hii ni tasnia inayoendeshwa na walaji na sisi tunahitaji pesa za hawa watumiaji wasiojua lolote wanaponunua tafsiri zetu. Tulijifunza kutokana ni kilio cha hasira kilichotoka kwa wasomaji Wakristo pale ile Revised Standard Version lipotoka na hivyo tunakuwa waangalifu. Pale Wakristo walipogundua kwamba ile hadithi yao pendwa ya kitoto ambapo Yesu anamzungumzia yule mwanamke wa kubuni anayekamatwa katika tendo la uzinzi, “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe – SUV” haimo katika RSV ila imezikwa katika rejeo / tanbihi, walishikwa na hasira kali. Ni kama vile walipinga vikali, si tu kwa kuondolewa hekaya ile, bali pia kwa maneno yaliyotumika katika rejeo / tanbihi ile. Rejeo / tanbihi ile iliweka wazi kwamba ingawa nyaraka kadhaa za Kiebrania zimeweka aya kutoka Yohana 7:53 hadi Yohana 8:11, nyaraka hizo za kipuuzi hazikubaliani juu ya kuiweka hekaya hiyo hapa, au mwishoni mwa injili ya Yohana, au mwishoni mwa Luka 21. Rejeo / tanbihi ile pia iliwaudhi waumini wa Biblia wa ile inayoitwa ‘Bible Belt’ ya hapa Marekani kwa sababu iliweka wazi kwamba hata maneno yaliyotumika yanatofautiana sana katika nyaraka chache ambamo hekaya ile inaonekana. Wachapishaji wa Biblia siku hizi hawatoi ruksa kwetu ya kutumia maneno ya aina ile tena. Na hawatoi ruksa ya kuanza Yohana 8 na aya ya 12 tena, isipokuwa katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Mashahidi wa Yehova. Tunaweza kuiweka hekaya ile katika parandesi, lakini ni lazima ibaki katika Biblia zetu. Na tunaweza kusema katika rejeo / tanbihi yetu kwamba aya za Yohana 7:53 – 8:11 hazimo katika nyaraka “bora” au “za kale” au “za kuaminika” zaidi, lakini kwa kweli ni zile Biblia za bei rahisi pekee ndizo zinazoweza kuiweka rejeo / tanbihi kamili kwa sababu hizo zina soko tofauti na la kwetu. Sehemu pekee ambapo jambo hili linafundishwa kwa uhuru na kwa wazi ni katika shule / vyuo vya Biblia kwa sababu mtu wa kawaida hana uweza wa kuelewa na kuhimili ukweli. Unajua, sisi tunafikiri kuwa kuna mtu fulani (hapo kale) ambaye alitunga hii hekaya yote ya “… na arushe jiwe la kwanza” kwa sababu zisizojulikana na akaiandika katika nyaraka moja ya kale ya Biblia. Halafu mtu mwingine ambaye labda aliisikia hekaya hii au aliisoma katika waraka huo akachomeka alichokumbuka katika hadithi hii katika waraka mwingine – ila akaweka katika sura nyingine kabisa. Tunafikiri hadithi hii ilienea kwa sababu tu ilipendwa sana. Hii ndiyo maana hatudhani hekaya hii ina ukweli wowote.

 

“Haya yote ninayokusimulia yatakusaidia kuelewa kwa nini kuna umuhimu mkubwa wa kutafsiri kila kitu katika maneno ya Kiingereza ambayo ni rahisi kuelewa na ya kisasa. Watu wetu wanaohusika na masoko wamatuambia kwamba watu wengi wanapenda kutizama maana za maneno katika kamusi za Kiyunani na Kiebrania kwa sababu hata kama hawajifunzi chochote, hii inawafanya wajione wao ni wasomi na wamazuoni wa kisasa. Lakini hawapendi kutafuta maana za maneno katika kamusi za Kiingereza kwa sababu hii inawafanya wajione wapumbavu! Hawaoni kwamba kuboresha msamiati wao ni jambo bora! Ila mimi ninakubali kwamba wengi kati yetu sisi wakalimani hatutakuwa na ajira ikiwa Wakristo wengi wangeweza kuelewa hata Kiingereza rahisi cha msingi. Maana yangu ni kwamba, kama wangekuwa wanakiweza Kiingreza basi wote wangenunua Biblia ya King James badala ya kulalama kwamba kila wakati wanalazimika kutafuta katika kamusi maana ya maneno kama “thee” na “thou”. Katika biashara yetu hii, ambayo kwa kweli imekaa kimchongo-mchongo hivi, inabidi tuchukue tahadhari kubwa: kwani inabidi tushushe kiwango cha bidhaa yetu ili mtumiaji wa kawaida aweze kuitumia, na wakati huo huo tuwasifie kwa kuifanya bidhaa ionekane ya kijanja na ya kisasa. Utafiti wa masoko unaonyesha kwamba kuuza vitu visivyo na maana sana kama ramani za Israeli ya kale, visaidizi katika kujifunza, matoleo maalum, nk, husaidia sana katika mauzo ya Biblia. Hatuwapendi watu wa idara ya mauzo kwa sababu kila tafsiri ya Biblia tunayoifanyia kazi ina sehemu kubwa ya bajeti yake katika mapambo tu. Lakini hii ndiyo unayouza hizi Biblia. Na malengo yetu ni kuuza.”

 

Na hivi ndivyo tafsiri [mpya ya kisasa] ya Biblia inavyotengenezwa. Kama ulivyoona mwenyewe, mchakato wake si haswa wa kisayansi. Hakuna nyaraka za Kiebrania wala za Kiyunani zenye mamlaka ya kihistoria nyuma yake. Na fasili au ufafanuzi wa maneno ya Kiyunani na Kiebrania katika kamusi zinazotumika kufasili lugha hizo ni mkusanyiko wa majaribio ya nia njema kabisa – lakini yanatofauti nyingi – ya miaka mingi na ya watu wengi tofauti ya kutafuta jinsi maneno yalivyotumika wakati maneno hayo yalipokuwa sehemu ya lugha hai. Hii ndiyo sababu Wakristo wenye imani wanavyozidi kupevuka wanagundua kwamba hili jambo lote la “uanazuoni” si lolote bali ni “… kujifunza siku zote ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa ukweli”. Hivyo kwa nia na kwa sala wanaanza kuiweka kando sayansi / elimu na kwa imani wanaanza kulitafuta neno halisi la Mungu kutokana na matunda yake – kutokuwa na dosari – badala ya kuifuata mizizi yake katika historia ya kale. Hapa ninamkumbuka mhubiri mwenye jina kubwa ambaye aliheshimiwa sana kwa sababu ya uadilifu na upendo wake kwa Mungu na mbaye kwa wazi kabisa anaitumia Biblia ya King James lakini haamini kwamba hii Biblia ndiyo neno halisi la Mungu. Yeye alikaribishwa kuwa mjumbe wa heshima katika kamati moja ya kuunda tafsiri [mpya] ya Biblia miaka kadhaa iliyopita. (simulizi hii nimeipata kutoka kwa mmoja kati ya waumini waliokuwa wakisali katika kanisa lake). Mradi ule ulipewa jukumu la kuunda Biblia mpya kutoka katika nyaraka za Textus Receptus. Mhubiri yule alifikia mahala akapoteza imani na kushikwa na karaha kwa mambo aliyoyaona yakifanyika hata akajiuzulu kiti chake.

 

Moja kati ya sababu nyingi kubwa wahubiri na waumini wanachoshwa, wanakuwa wabeuzi, wanakuwa wanafiki ni kwamba wanaanza kuhisi neno la Mungu halipo mahala popote. Na jinsi wanavyozidi kuzitumia lugha zilizokufa kama mamlaka ya kulisahihisha neno hai la Mungu, ndivyo wanavyozidi kujiona wa bandia. Na sentensi hii inaturejesha kwa kile mhubiri wako anakitumia pale anapomsahihisha Mungu.

 

VISAIDIZI VYA MLEI (LAYMAN’S AIDS)

 

Tafsiri ya Biblia ambayo mhubiri wako anaishika mkononi mwake ni matokeo ya uanazuoni bora kabisa, uliogharimu pesa nyingi. Wale ma-ERRORRist wametumia muda na nguvu nyingi katika kufikia kiwango cha kuwa wataalamu wa nyaraka za ERROR na lugha zilizokufa. Wameutumia umahiri wao mkubwa katika kuzalisha nyaraka mpya za Agano la Kale katika Kiebrania na Agano Jipya katika Kiyunani. Mhubiri wako hana sifa hata za kumfanya aguse upindo wa mavazi ya hawa ERRORIsts. Hii ndiyo maana hawezi kuwa hata na ndoto za kuchapisha nyaraka zake mwenyewe katika lugha hizi zilizokufa.

 

Watafsiri wa Biblia wako katika hali hiyo hiyo: wametumia muda na nguvu nyingi ili wawe manguli katika nyanja yao. Wamesahau mambo mengi katika nyanja ya lugha zilizokufa na medani za kutafsiri lugha hizo kuliko yale aliyojifunza mhubiri wako katika muhtasari wake wa Dead Languages 101 – hata kama alipata alama nzuri katika masomo yake. Hii ndiyo maana hakuna mchapishaji atakayemwajiri mhubiri wako kwa ajili ya kazi ya kuzalisha Biblia mpya.

 

Mhubiri wako siku moja aliingia dukani akanunua tafsiri fulani ya Biblia. Mabingwa wa kutafsiri waliozalisha Biblia hii walifanya maamuzi mengi kwa kutumia ujuzi wao kuhusu nyaraka gani watumie kati ya nyaraka nyingi za Kiebrania na Kiyunani. Halafu wakapitia juzuu (tome) nyingi nyingine ili kuboresha nyaraka walizochagua na maneno halisi yatakayotumiwa katika tafsiri hiyo. Mhubiri wako akaipenda tafsiri hiyo hata akatoa pesa na kuinunua.

 

Lakini mhubiri wako hana ujanja wa kutosha kujua kwamba mbele za wajanja yeye hafui dafu. Kwa hiyo anadhani kwamba yale mafunzo aliyopitia kule Bible school katika Dead Languages 101 yamemfanya nguli katika lugha zilizokufa na katika uzalishaji wa kazi za kutafsiri kuliko mabingwa ambao maisha yao yote wamekuwa wakifanya kazi hiyo. Anataka kuonyesha ubingwa wake mbele ya manguli hao. Kwa hiyo katika kuonyesha ujanja wake huu anahitaji kutumia vitabu vinavyoitwa visaidizi vya walei (layman’s aids).

 

Kuna aina nyingi sana za visaidizi vya walei. Vyote hivi vimetengenezwa ili vitoe kiasi fulani cha msaada wa taarifa za msingi. Baadhi ya visaidizi vinavyojulikana sana ni kamusi za Kiyunani na Kiebrania, concordances, na interlinear Bibles. Baadhi ya interlinear Bibles zinalinganisha tafsiri moja ya Biblia na tafsiri nyingine. Nyingine zinalinganisha tafsiri moja ya Biblia ya Kiingereza na nyaraka za Kiyunani na Kiebrania. Hizi zinaweza kuwa na taarifa kuhusu vipande gani vya nyaraka za ERROR zilitumika katika kuzitengeza na kuhusu tofauti katika nyaraka mbalimbali. Concordances na interlinears huwa zinapendwa sana kati ya walei kama wahubiri na waumini wa kawaida kwa sababu ni rahisi kutumia na zinaweza kutumiwa haraka tu.

 

Kama mhubiri wako alisoma katika Bible school basi inawezekana amerudi na baadhi ya vitabu walivyomlazimisha kununua. Kama kitabu hicho ni kigumu kutumia basi huenda akanunua concordance, interlinear au kamusi fulani iliyo rahisi na haraka kuitumia wakati wa mahubiri.

 

Mhubiri wako huyu atafanya yafuatayo. Kama ana desturi ya kuchukua mahubiri yake kutoka katika vitabu vya mahubiri [yaliyotayarishwa], mara nyingi vitabu hivyo vitamwonyesha maneno [ya Kiyunani na Kiebrania] ya kusahihisha katika tafsiri ya Biblia anayoitumia. Masahihisho haya mara nyingi yatatokana na dhehebu la kanisa husika – usisahau, chanzo cha madhehebu ni tofauti ya kanuni zao za imani. Kama anatayarisha mahubiri yake mwenyewe, basi aghalabu hatasahihisha tafsiri yake ya Biblia mara nyingi kwa sababu hajui kipi cha kusahihisha. Kama anasahihisha Biblia yake katika mahubiri yake mwenyewe, utagundua tu kwa sababu masahihisho yake aghalabu yatakupotezea muda tu, kwa sababu hayataleta maana sana. Kwa mfano, mhubiri mmoja aliwaambia wasikilizaji wake kwamba neno la Kiingereza “conscience” (maana yake dhamiri) linatokana na muunganiko wa maneno mawili “con” linalomaanisha “with” na “science” linalomaanisha “knowledge”. Halafu akasema kwamba neno la Kiyunani linalomaanisha “conscience” ni suneidesis, ambalo linaundwa na maneno ya Kiyunani “sun” linalomaanisha “with” na “eidesis” linalomaanisha “knowledge”! Ebu niambie, mpendwa Mkristo, kanisa la Bwana wetu linafaidika vipi na upuuzi kama huu!? Ila tu ni kwamba, lengo la hawa jamaa siyo kukusaidia bali wanataka wewe uwaone wao ni mabingwa. Mwisho wa siku, hata hivyo, wanajionyesha tu kwamba wanajaribu kuogelea katika maji marefu kuwazidi na hawafai kuchunga kundi la kondoo wa Bwana.

 

Lakini ni pale wanaposahihisha tafsiri yao ya Biblia (toleo lolote lile) wakisema, “Tafsiri hii inasikitisha kabisa; maana halisi ya neno hili la Kiebrania ni …” ndipo wanapojidhihirisha wenyewe kuwa ni watu wasio na imani na ni vichekesho. Wasiokuwa na imani, kwa sababu hawaamini kwamba neno la Mungu lipo; na vichekesho kwa sababu wanafikiri wewe utawaona wao ni wataalamu katika nyaraka za ERROR na katika mbinu za kutafsiri kuliko wale mabingwa wanaolipwa kwa kazi hiyo! Ukweli kwamba mhubiri wako huyu anaweza kutumia dakika 3 akipekua kamusi halafu aonekane kuwa ni mtaalamu kuliko kamati za kutafsiri Biblia unaonyesha kwamba huyu jamaa hayuko katika kiwango sahihi. Haelewi lugha kwa ujumla, na haswa lugha zilizokufa, kamusi, na wala kwa nini ile kamusi ya Kiyunani na Kiebrania iliyomo mwishoni mwa concordance yake mara nying ina fasili nyingi tofauti za kuchagua kutoka neno moja tu. Anafikiri wanakamati waliozalisha tafsiri ya Biblia yake hawakuzijua zile fasili nyingine za maneno hayo? Mhubiri huyu angetoa picha nzuri zaidi kwa kunukuu tafsiri nyingine za Biblia na kitu kama “Huyu ‘mnyama mtoto’ katika tafsiri yetu ametafsiriwa kama ‘mbuzi mtoto’ katika Swahili Global Translation. Ninaheshimu utaalamu wa kamati zote mbili, lakini nafikiri ‘mbuzi mtoto’ inaendana zaidi na muktadha wa aya hii na pia kanuni zetu za imani.” Kama akiendelea kunukuu tafsiri nyingine basi angalau ananukuu kazi za mabingwa badala ya “kusahihisha” kazi za mabingwa.

 

Huwezi kutumia visaidizi vya walei na kozi yako ya Dead Languages 101 ya Bible School na ukategemea kuwashinda mabingwa. Utakachofanikisha ni kuonekana kama mtu mwenye majivuno ambaye ameikataa Biblia. Hata hivyo, hii ndiyo sababu visaidizi vya walei vinachapishwa (sababu ingine ni kupiga hela); ili utengeneze tafsiri ya Biblia yako mwenyewe na uwe mtaalamu katika macho yako mwenyewe. Huna haja ya kuzikubali nyaraka za ERROR, waandishi wake, waliotafsiri, tafsiri za Biblia, wala wahubiri kama watu wenye mamlaka katika kazi zao; unachoweza kufanya ni kinachoonekana sahihi katika nafsi yako ... kama watu wengine wote.

 

Sasa, acha niweke kitu kimoja wazi kuhusiana na nyaraka na tafsiri za Biblia. Kwa ujumla tafsiri zote za Biblia hapa duniani, isipokuwa Biblia ya King James, ni kazi aminifu, sahihi za wanazuoni wa nyaraka za ERROR za lugha zilizokufa. Tofauti kati ya tafsiri za Biblia zinatokana haswa na uchaguzi wa wanakamati za kutafsiri wa nyaraka zipi za ERROR watumie kati ya nyaraka nyingi, na kwa kiasi kidogo katika uhuru halali kabisa walio nao katika kutafsiri maneno mbalimbali na kudhihirisha maana zake. Tafsiri hizo nyingine zinaposema kwamba simulizi ya mwanamke aliyekamatwa akizini haipo katika nyaraka nyingi walizotumia, hawasemi uwongo. Na pale watu wanaposema kwamba kuna aya katika Biblia ya King James ambazo hazipo katika Biblia nyingine hapa duniani, hawasemi uwongo. Biblia ya King James si tafsiri aminifu, sahihi, ya kisomi, ya nyaraka za Textus Receptus wala ya nyaraka zozote zile hapa duniani. Na watu wanapokwambia kwamba zile nyaraka za ERRORists zimejaa makosa / dosari, na tafsiri za Biblia zinazotokana nazo kwa uaminifu na usahihi zimerithi makosa / dosari hizo, wako sahihi kabisa.

 

Lakini wanaposema kwamba Biblia ya King James imetokana na nyaraka za uharibifu za Textus Receptus, kwamba ina makosa / dosari, kwamba siyo neno la Mungu, na kwamba neno la Mungu halipo mahala popote duniani, hapo wanakosea, na hawajui maandiko wala uweza wa Mungu.

 

Ni muhimu sana kujua kwamba wengi kati ya watetezi wa Biblia ya King James hawaitetei Biblia ya King James kama Mungu Mwenyewe alivyofasili. Wanaitetea Biblia hii kama tafsiri iliyo na makosa / dosari chache kuliko zote. Tazama kitu ambacho mmoja kati ya watetezi maarufu wa Biblia ya King James wanaojiita “King James only movement” alichosema: Ütunzaji wa nyaraka za Agano Jipya haukua wa kimiujiza … Waandishi na wapiga chapa hawakuvuviwa … Hivyo kuna baadhi ya aya za Agano Jipya ambamo maana halisi haiwezi kupatikana … nyaraka za Textus Receptus zina mgongano na zile za Traditional [Majority] text … matoleo kadhaa ya Textus Receptus na ya Majority Text yanatofautiana kati yao, na baina yao na Biblia ya King James. Na … hali ni hiyo hiyo katika Agano la Kale.” Halafu anaendelea: “Nakubali tafsiri hii [Iliyoamriwa] si timilifu … ukitokea uhitaji wa … tafsiri mpya ya Kiingereza … basi Biblia ya King James pekee ipitiwe na siyo vyanzo vyake katika Kiyunani na Kiebrania.” (Kwa maneno mengine, anataka ile Textus Receptus, yenye makosa machache, isichanganywe na Alexandrian text, yenye makosa mengi zaidi, na ile Alexandrian isichukue nafasi ya TR).

 

Mtetezi mwingine wa AV/KJB anasema, “Lengo la sura zifuatazo ni kudhihirisha kwamba ile TR ambayo ndiyo msingi / chanzo cha KJB inatunza na kuendeleza kwa uaminifu zaidi [kuliko Alexandrian Text] ufunuo uliovuviwa … hatusemi kwamba KJB haina makosa. Kuna mabadiliko ambayo yanaweza kufanywa na yanapaswa kufanywa katika kuongeza ubora wake.”

 

Haya, tumethibitisha kuwa wale ERRORIsts hawaiheshimu kazi yao wenyewe kuwa ina mamlaka. Tumeona kwamba wanakamati za kutafsiri hawaheshimu kazi zao wenyewe wala kazi za ERRORists. Tumeona kwamba wengi katika kambi ya “KJB Only” wanafundisha kwamba Biblia ya King James wanayoitumia siyo neno la Mungu. Na tumeona kwamba wahubiri na waumini wanaowahubiria hawaheshimu kitu chochote kwamba kina mamlaka wakiwa na visaidizi vyao vya walei bila kuogopa, wakipinga na “kusahihisha” kila kitu. Na tumedhihirisha kwamba wanafanya hivi kwa sababu ya kutoamini; hawaamini kwamba neno la Mungu lipo. Hawaamini kwamba iko Biblia yenye mamlaka inayoweza kuwasahihisha wao na kanuni wanazoamini.

 

Ni kitu gani ninachokijua mimi ambacho wao hawakijui? Ninajua kwamba hawa wanalichukulia suala hili kinyume-nyume kwa sababu ya kutoamini kwao. Ninajuaje hili? Kwa sababu Biblia inanifundisha hivyo. Lakini ilinifundisha hivyo pale tu, kwa imani, nilimwamini Mungu Naye akaufungua uelewa wangu. Ni rahisi tu: zuzu yeyote asiyeokolewa anaweza kuelewa msimamo wangu. Lakini hawezi kuamini anachokiona.

 

Sasa na tutazame matunda ya hizi tafsiri za Biblia, badala ya kuwajua kwa kutizama mizizi yao ilikotoka.

 

“MAKOSA” / “ERRORS”

 

Wakristo wasioamini uwepo wa neno la Mungu wanapotaka kueneza imani yao ya kinafiki, mara nyingi hutumia sayansi. Ebu na tuone jinsi “wanavyothibitisha” kwamba Biblia si neno la Mungu.

 

Leviticus 11:6 And the hare, because he cheweth the cud, but divideth not the hoof; he is unclean unto you.

 

Walawi 11:6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.

 

Kwa miaka mingi sana, wanazuoni walivunja mbavu zao waliposoma aya hii kwa sababu watu wa leo wanajua kwamba sungura hawacheui – hawana hata chakula-mrudio (cud). Wakristo walioijua Biblia yao walisimama imara, kimya, wakitumaini kwamba kwa namna moja ama nyingine neno la Mungu lilikuwa sahihi. Ukisoma kitabu cha zamani kidogo (miaka 30 au 40 iliyopita) juu ya ufugaji wa sungura, watakwambia kwamba ni lazima usafishe vibanda vyao kila wakati ili kuwazuia wanyama hawa wanaotia kinyaa kula “kinyesi” chao wenyewe. Vitabu vipya, hata hivyo, vitakwambia kwamba sungura wanacho na wanakula chakula-mrudio, “cud”. Hawakitolei mdomoni kama ng’ombe, mbuzi, na kondoo; wanakitolea nyuma yao na kiko katika mfumo na umbile la yai dogo, na wanaweka katika mafungu. Baadaye wanarudia sehemu hii na kula tena chakula-mrudio hiki ambacho ni lishe bora sana kwao; mwisho wa mzunguko huu wanajisaidia kinyesi chenye ukubwa mdogo sana, na mviringo. Hivyo wanaokataa Biblia wamefungwa midomo kwa ugunduzi huu muhimu, kwani “uthibitisho” wao kwamba sungura hana wala hatumii chakula-mrudio umegonga mwamba. Hiki ni kitabu cha maajabu! Tulijuaje kwamba sungura wana mfumo wa chakula-mrudio? Ni kupitia Biblia ya King James! (Ukweli kwamba simulizi hii iko pia katika Biblia zingine za kawaida si jambo kuu – hii inamaanisha tu kwamba ni kweli au siyo kweli). Hivyo ukiona fungu la kinyesi cha sungura, jichekee tu na uwaambie familia yako kwamba huo ni mnara stahiki kwa wale wasioamini!

 

Numbers 25:9 And those that died in the plague were twenty and four thousand.

1 Cor. 10:8 Neither let us commit fornication, as some of them committed, and fell in one day three and twenty thousand.

 

Hesabu 25:9 Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao.

1 Wakorintho 10:8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

 

Miaka kadhaa iliyopita, chapisho fulani la kitaifa la Kikristo liliandika makala iliyokuwa na kichwa, Inerrancy: The Bible is the Word of God. Makala hiyo ilikuwa na sehemu iliyodai kwamba Biblia zote zina makosa. Hesabu 25:9 inayosema kwamba watu elfu 24 walikufa kwa ugonjwa wa tauni, inapingana, mwandishi yule Mkristo alidai, na idadi inayotajwa katika 1 Wakorintho 10:8. Mwanazuoni yule alishindwa kuona ukweli kwamba katika Hes. 25:9 watu elfu ishirini na wanne ni jumla, wakati katika 1 Wakorintho 10:8, walikufa watu elfu ishirini na watatu katika siku moja.

 

Makala ile iliendelea kusema kwamba tafsiri zote za Biblia ni tafsiri tu, wala si “Neno la Mungu”. (Ndiyo, ile N iliandikwa kwa herufi kubwa. Wakristo wengi ambao hawajajifunza kutoka katika Tafsiri Iliyoidhinishwa na Mungu kutazama kwa utondoti, wanakosa mambo kama hayo; “neno” la Mungu linapaswa kutofautishwa na Neno la Mungu). Makala ile ilisema (kwa usahihi), kwamba kila waraka katika Kiebrania na katika Kiyunani una migongano na makosa. Ikasema pia (si kwa usahihi) kwamba “nyaraka asilia” pekee ndizo zilizovuviwa na zisizo na makosa, na tumshukuru Mungu kwamba haziko tena kwa sababu Yeye hataki mtu yeyote aabudu kitabu kwa kudhani kuwa kitabu hicho ni neno Lake lililovuviwa! Makala ile haikueleza ni vipi Biblia ni neno la Mungu ikiwa neno la Mungu halipo tena, lakini kama ambavyo “uthibitisho” katika Hesabu 25:9 / 1Wakor. 10:8 unavyoonyesha, ukifanya masihara na neno la Mungu, Yeye atavuruga akili yako.

 

Nafikiri sasa unaanza kuona hili suala la tafsiri za Biblia lina maana gani. Suala hili linahusiana na Biblia Iliyoidhinidhwa ya King James. Ndiyo hivyo; kama kusingekuwa na Biblia Iliyoidhinishwa ya King James, kusingekuwa na mtakatifu yeyote ambaye angeamini kwamba neno la Mungu liko mahala popote hapa duniani – bila doa kama Mfalme alivyosema litakuwa. Hapo kabla nilisema kwamba Biblia inasema mambo yaleyale inayoyasema juu ya Neno la Mungu na neno Lake. Biblia inasema … “… jiwe ambalo waashi wamelikataa, hilo [hilo] limefanywa kuwa jiwe kuu la pembeni. 8 Tena limekuwa jiwa la kujikwaa, na mwamba wa chukizo, kwa wale wanaojikwaa katika neno, … Na wengi kati yao watajikwaa, na kuanguka, na kuvunjika, na kunaswa mtegoni, na kuchukuliwa mateka.” (1 Petro 2:8; Isa. 8:15).

 

Tukumbuke hili, wakati tunaona jinsi wanazuoni Wakristo waliozaliwa upya wanapothubutu kufungua midomo yao na kutamka maneno dhidi ya neno la Mungu, maneno ambayo watayasikia tena katika siku ya hukumu.

 

Ge 1:1 In the beginning God created the heaven and the earth.

Ge 2:1 Thus the heavens and the earth were finished, and all the host of them.

 

Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.

Mwanzo 2:1 Hivyo mbingu [zikamalizika] na dunia ikamalizika, pamoja na jeshi lao lote.

 

Huna haja ya kwenda mbali ili kupata sehemu katika Biblia Iliyoidhinishwa ambamo wanazuoni wa leo wanafikiri kuna makosa / dosari. Mwanzo 1:1 inasema mbingu – heaven - (singular / moja) Mwanzo 2:1 inasema mbingu – heavens – (plural / zaidi ya moja). Wanazuoni wa leo wameibadilisha Mwanzo 1:1 iandikwe heavens (plural / zaidi ya moja) ili ioane na Mwanzo 2:1 katika kila tafsiri ya Biblia ya kisasa yenye hakimiliki, ikiwa ni pamoja na New King James Version. Walifanya hivyo kwa sababu walifundishwa katika Sunday school kwamba Mwanzo 1:1 ni maelezo ya ujumla ambayo ni utangulizi wa uumbaji wa siku saba za Mwanzo 1:3 hadi Mwanzo 2:3. Na kwa kuwa Mwa. 2:1 na Mwa. 2:4 zinasema heavens (mbingu plural), na kwa kuwa tunajua kwamba kuna mbingu tatu (2 Wakor. 12:2), ile heaven (singular) ya Mwa. 1:1 ilionekana kama ni kosa kwao. Na yumkini ni vigumu kwao kubadilisha tafsiri zao za kisasa zisome heaven tena kwa sababu hii italazimu kazi kubwa ya kujifunza Biblia kwa upande wao ili wanyooshe kanuni zao za Biblia. Kwa sababu somo hili lilijadiliwa kwa utondoti mkubwa katika sura D4, hapa nitasema tu kitu kimoja juu ya kamati za kutafsiri Biblia: Ingawa wao ni mabingwa katika nje na ndani za kazi za kutafsiri, hawa jamaa – kama Wakristo wengi wenye Enlightenment (tizama kamusi yako, tafadhali) – hawajui mambo mengi kuhusu Bwana Mungu na neno lake adhimu.

 

Watu wote ambao wameikufuru Biblia Iliyoidhinishwa siku zote wamekuwa wakosaji walioshindwa kuthibitisha hata kosa moja ndani ya KJB. Lakini hili haliwazuii watu kuendelea kufundisha kwamba hakuna neno la Mungu hapa duniani leo.

 

Acts 7:45 Which also our fathers that came after brought in with Jesus into the possession of the Gentiles, whom God drave out before the face of our fathers, unto the days of David;

 

Matendo 7:45 Ambalo pia baba zetu waliokuja baadaye walikuja nalo wakiwa na Yesu, likaingia katika milki ya watu wa mataifa, ambao Mungu aliwafukuza mbele ya baba zetu, mpaka siku za Daudi;

 

Aya hii inatuingiza katika tatizo lingine linalosababishwa na Reason: Yawezekana vipi kwa Yesu kuwaongoza Wayahudi katika kuvuka mto Yordani na kuingia katika Nchi ya Ahadi karne nyingi kabla hajazaliwa? Tafsiri zote za kisasa za Biblia, ikiwa ni pamoja na New King James Version, zimebadilisha Mdo 7:45 ili isome Yoshua, ingawa katika Kumb. la Torati 31:3a na b tunasoma kwamba wote Yesu na Yoshua walihusika katika kuvuka. Sasa kosa liko wapi katika Biblia Iliyoidhinishwa? Na kwa kuwa Biblia inampa sifa na utukufu Yesu Kristo zaidi ya Yoshua kwa kuvuka mto ule, (Kumb. 31:6,8,20,21; 32:12), ni vipi basi hizi tafsiri za kisasa zinaweza kudai kwamba zinaaminika zaidi na ziko sahihi zaidi wakati zinapuuza maandiko yanayomtukuza Mfalme wetu na badala yake wanamkweza mtu?

 

Soma pia hii: Waebrania 4:8 For if Jesus had given them rest, then would he not afterward have spoken of another day. [4:8 Maana kama Yesu angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye.] Ukiisoma katika muktadha wake, utaona anazungumziwa Bwana wetu katika mazingira ya Agano la Kale.

 

Kumbuka: Kuwa makini unapoenda kununua King James Bible. Wachapishaji watakuambia kwa udanganyifu kwamba wanayokuuzia ni Biblia Iliyoidhinishwa bila ya kusema kwamba wamebadilisha baadhi ya maneno, baadhi ya tahajia, na baadhi ya herufi kubwa. Sehemu nzuri ya kutazama kama Biblia yako ni KJB kweli ni Mdo 7:45; kama wameibadilisha na kuwa Yoshua, basi watakuwa wamevuruga sehemu nyingine pia. Kama inasoma Jesus, basi hiyo iko sawa. Kiashiria kingine kinachoonyesha wameivuruga hiyo Biblia ni 2 Tim. 3:17. Kama tahajia (spelling) ya neno throughly imebadilishwa na kusomeka thoroughly hiyo ni kwa sababu kuna ‘mjanja’ fulani amethubutu kuvuruga neno la Mungu. Tafadhali usinielewe vibaya; Biblia inadhihirisha kwamba mawasiliano ndiyo lengo la lugha – na si tahajia (spelling) na sarufi. Lakini mtu akivuruga hata nukta na koma ambazo Mungu ameziweka katika neno lake halafu anadanganya kwa kusema hiyo ni Biblia Iliyoidhinishwa, hii ni dalili ya jinsi utumbo wake mnene ulivyojaa. Anyway, aya hizo mbili ndizo huwa za kwanza kubadilishwa katika yale matukio nadra ambapo wachapishaji wamejaribu kuivuruga KJB. Ila ikiwa sehemu hizo mbili ziko sawia katika KJB yako basi jua uko na kitabu sahihi.

 

MAKOSA YALIYOMO KATIKA NYARAKA ZA E.R.R.O.R.

 

Sasa tunaingia katika makosa / dosari zenyewe katika tafsiri ambazo watu wamezichapisha. Makosa / dosari hizi zinathibitisha kwa uhakika kabisa kwamba tafsiri za kisasa haziwezi kuitwa neno la Mungu. Mimi situmii mifano ambayo inategemea sana kutojua maandiko kwa upande wa wasomaji wangu. Kwa mfano, ukisoma uandishi unaofanywa na watetezi fulani wa KJB utakutana na hoja kama hii:

 

“Ile New International Version inashambulia kanuni ya Uungu wa Kristo katika Warumi 14:10 na 12, wakati King James inaweka wazi kwamba Yesu Kristo ni Mungu.”

 

KJV Ro 14:10 But why dost thou judge thy brother? or why dost thou set at nought thy brother? for we shall all stand before the judgment seat of Christ.

KJV Ro 14:12 So then every one of us shall give account of himself to God.

 

War. 14:10 Lakini kwa nini wewe unamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdbarau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.

War. 14:12 Hivyo basi, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari za nafsi yake mbele za Mungu.

 

Linganisha na uandishi wa NIV:

 

NIV Ro 14:10 You, then, why do you judge your brother? Or why do you look down on your brother? For we will all stand before God’s judgment seat.

NIV Ro 14:12 So then, each of us will give an account of himself to God.

 

Ukisoma nukuu hii, unaweza kushikwa na hasira dhidi ya waandishi wa NIV. Lakini sisi hatutafuti tofauti kati ya tafsiri mbalimbali pale tunapolitafuta neno halisi la Mungu; tunatafuta makosa / dosari. Wale wanaonyooshea kidole aya kama hii hapo juu kama uthibitisho wa kutofaa kwa tafsiri za kisasa, kwa mfano, wanatumaini (mioyoni mwao) kwamba hautosoma kitabu kinachotumia hoja hiyo hiyo yao “kuthibitisha” kwamba KJB inashambulia Uungu wa Kristo katika aya kama Tito 2:13 na 2 Petro 1:1 kwa kutouweka wazi sana Uungu wa Kristo:

 

KJV Titus 2:13 Looking for that blessed hope, and the glorious appearing of the great God and our Saviour Jesus Christ;

Tito 2:13 Tukilitazamia tumaini lililobarikiwa, na ufunuo mtukufu wa Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo;

 

NIV Tito 2:13 while we wait for the blessed hope – the glorious appearing of our great God and Savior, Jesus Christ.

 

KJV 2 Pet. 1:1 Simon Peter, a servant and an apostle of Jesus Christ, to them that have obtained like precious faith with us through the righteousness of God and our Saviour Jesus Christ:

2 Petro 1:1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waiiopata imani yenye tunu kama [imani] yetu, kutokana na uadilifu wa Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

 

NIV 2 Pe 1:1 Simon Peter, a servant and apostle of Jesus Christ, To those who through the righteousness of our God and Savior Jesus Christ have received a faith as precious as ours:

 

Hoja ya aina hiyo hiyo inafanywa na watetezi wa KJB kuonyehsa jinsi tafsiri zisizoidhinishwa zinavyofundisha kanuni “zinazoshambulia” Uungu wa Kristo. Watakuonyesha aya katika KJB ambazo zinasoma “Bwana Yesu” wakati aya hizo hizo katika tafsiri zisizoidhinishwa zinasoma tu “Yesu”. Lakini hawatakuonyesha aya katika KJB ambazo zinasoma tu “Yesu” wakati aya hizo hizo katika tafsiri za kisasa zinasoma “Bwana Yesu”. Aina hii ya hoja si tu kwamba haithibitishi chochote, bali inaonekana kuwa ni ya udanganyifu. Hivyo weka hili akilini mwako wakati tunatafuta makosa / dosari halisi katika tafsiri za Biblia.

 

Nitatumia tafsiri tano za Biblia katika uchunguzi wa makosa / dosari. Authorised 1611 King James Version, Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa © 1995, 2001, Swahili Union Version, Revised Swahili Union Version, na Kiswahili Contemporary Version au NEN Biblia, ingawa hii katika mtandao inaonekana kuishia katika kitabu cha Yuda (June 2025)!! Ninaamini hizi zinawakilisha zile tafsiri ambazo watu wengi wanazisoma katika sehemu ya dunia ambamo Kiswahili kinatumika. Makosa / dosari hizi zimo pia katika tafsiri nyingine za Kiswahili, kama zile za Mashahidi wa Yehova, zinazoitwa kwa ujumla, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya (kuna matoleo kadhaa ya hizi – TUM). Kama unatumia tafsiri nyingine isiyoidhinishwa au isiyo na hakimiliki, tofauti na hizi hapa, usiwe na shaka; humo utayapata mengi kati ya makosa / dosari hizi hizi pia, kwani hata hiyo ni kazi ya wanazuoni wanaofanya makosa, ambao walijitahidi wanavyoweza katika kutafsiri kwa usahihi kabisa makosa / dosari zilizomo katika zile nyaraka za ERROR na kuziingiza katika tafsiri nyingine iliyo na chachu ile ile mbaya ya kale. Kwa sababu ya kile Mungu alichotufundisha katika neno Lake tunahitaji kupata kosa moja tu ili tuiondoe tafsiri nzima katika orodha ya kile tunachoweza kukiita kwa kujiamini kabisa kwamba ni Kitabu Chake.

 

KJV Isa. 14:12 How art thou fallen from heaven, O Lucifer, son of the morning! how art thou cut down to the ground, which didst weaken the nations!

KJV Ufu. 22:16 I Jesus have sent mine angel to testify unto you these things in the churches. I am the root and the offspring of David, and the bright and morning star.

 

Hakuna tatizo katika aya hizi hapa juu. Utambulisho wa kila nafsi uko wazi.

 

SUV Isa. 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!

SUV Ufu, 22.16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.

 

Kutoka Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa, Tanzania na Kenya, © 1995, 2001:

Isaya 14:12 “Jinsi gani ulivyoporomoshwa kutoka mbinguni, wewe uliyekuwa nyota angavu ya alfajiri. Jinsi gani ulivyoangushwa chini, wewe uliyeyashinda mataifa!

Ufunuo 22:16 Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi.

 

Hapa katika Swahili Union Version (SUV) na Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa tunamwona “Mungu” akijipinga mwenyewe kuhusiana na nafsi gani ndiyo “nyota ya asubuhi / alfajiri’! Kuna njama hapa? Hapana, wanakamati za kutafsiri Biblia ni watu wema wanaojaribu kufanya mema kwa kujituma vyema kabisa katika kazi ya kutafsiri zile nyaraka zenye makosa / dosari za Kiyunani na Kiebrania. Baadhi ya watu wanaweza kuona kosa hili si kubwa sana, lakini itabidi ukubali kwamba uandishi wa KJB ni bora zaidi.

 

Ni wakati wa maswali na majibu. Nani alimuua Goliati? Ebu tutizame katika KJB ili tuone kama jibu lako (Daudi) ni sahihi:

 

KJV 1 Sam. 17:4,7,51 And there went out a champion out of the camp of the Philistines, named Goliath, of Gath, whose height was six cubits and a span… 7 And the staff of his spear [was] like a weaver’s beam ... Therefore David ran, and stood upon the Philistine, and took his sword, and drew it out of the sheath thereof, and slew him, and cut off his head therewith. And when the Philistines saw their champion was dead, they fled.

KJV 2 Sam. 21:19 And there was again a battle in Gob with the Philistines, where Elhanan the son of Jaareoregim, a Bethlehemite, slew the brother of Goliath the Gittite, the staff of whose spear was like a weaver’s beam.

KJV 1 Mamb. 20:5 And there was war again with the Philistines; and Elhanan the son of Jair slew Lahmi the brother of Goliath the Gittite, whose spear staff was like a weaver’s beam.

 

Hakuna mgongano wowote katika aya hapa juu kuhusu ni nani aliyemwua Goliati. Kila mwanafunzi [Mkristo] wa shule ya msingi anajua kwamba Daudi ndiye alimwua Goliati. Lakini sasa ebu tutazame tafsiri za kisasa ili tuone wanasemaje kuhusu ni nani haswa aliyemwua Goliati:

 

Swahili Contemporary Version (NEN Biblia):

 

1 Sam. 17:4 Shujaa aliyeitwa Goliathi, aliyetoka Gathi, akajitokeza kutoka kambi ya Wafilisti. Alikuwa na urefu dhiraa sita na shibiri moja … 7 Mpini wa huo mkuki ulikuwa kama mti wa mfumaji … 51 Daudi akakimbia na kusimama juu yake. Akaushika upanga wa huyo Mfilisti na kuuvuta kutoka kwenye ala yake. Baada ya kumwua, akakata kichwa chake kwa ule upanga.

2 Sam. 21:19 Katika vita vingine na Wafilisti huko Gobu, Elhanani mwana wa Yaare-Oregimu, Mbethlehemu, alimuua nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.

1 Mamb. 20:5 Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa mpini kama mti wa mfumaji.

 

Tafsiri zote za kisasa zinaonyesha aya zote tatu zikiwa na mgongano. Ya mwanzo hapo inasema Daudi alimwua Goliati, ya pili hapo inasema Elhanani ndiye aliyemwua Goliati, na ya tatu inasema kwa hakika ni ndugu wa Elhanani ndiye aliyemwua Goliati. Katika kuona migongano mitatu ya aina hii, tumethibitisha bila shaka yoyote kwamba tafsiri hii si neno la Mungu kwa sababu ina kosa / dosari. Hatuwezi kuthibitisha aya ipi si sahihi, lakini tunajua kwamba haziwezi zote kuwa sahihi. Ebu fikiria hili: Wale wanaoabudu nyaraka za ERROR kuwa zenye mamlaka halisi na wale wanaotumia visaidizi vya walei “kusahihisha” Biblia, na wale wanaotumia tafsiri ya kisasa kwa sababu wanafikiri “ni sahihi zaidi” na “haina hitilafu”, hawana mamlaka ya ki-nyaraka yanayoweza kuwafanya wasimame imara na kusema ni nani alimwua Goliati! Nyaraka za ERROR na matunda / tafsiri za kisasa zinazotokana nazo zina ushahidi tosha unaosema kwamba Elhanani ndiye alimwua Goliati na vivyo hivyo kwa Daudi. Unajua kwa nini wengi kati ya wahubiri na waumini – wale wanaoabudu nyaraka za ERROR na wanaotumia nyaraka zisizo na mamlaka – hawazunguki na kuhubiri kwamba kulingana na tafsiri zao, hatupaswi kusema kwa uthabiti wa kiimani kwamba Daudi alimwua Goliati? Ni kwa sababu mapokeo yana mamlaka katika maisha yao kuliko “Biblia Takatifu” wanazozipenda sana au nyaraka zao za lugha zilizokufa!

 

Kufuru zenye mgongano kama hizo haziwasumbui Wakristo ambao hawana imani kwa Mungu wala neno Lake. Hawajawahi kutumia hata dakika tano katika kujaribu kulitafuta neno Lake lililovuviwa Naye na lisilo na dosari kwa sababu hawaamini kwamba liko mahala popote. Hao ni watu wasioamini. Hii ndiyo maana makosa / dosari tunazozizungumzia katika nyaraka za ERROR haziwasumbui. Na, bila kujua neno la Mungu lipo, wanapoenda kununua tafsiri ya Biblia wanataka tafsiri ya kisasa ambayo “imeyatunza” makosa / dosari na migongano iliyomo katika nyaraka za ERROR; wanafikiri kwamba nyaraka zilizoharibika za ERROR ni vyanzo vya kuaminika zaidi vya kweli ya Mungu isiyoweza kuharibika hapa duniani.

 

Ebu tuone kama hawa Wakristo waliozaliwa upya, wa kisasa, wasioamini, wamepata tafsiri “aminifu” walizokuwa wakizitafuta. Tizama kwa makini maneno yaliyo katika chapa-mlazo katika 2 Sam. 21:19 ya KJB hapo juu. Maneno hayo “the brother of” (ndugu yake) yako katika chapa-mlazo kwa sababu waliotafsiri waliyaongeza wakiwa chini ya ufunuo wa Mungu. Maneno hayo hayamo katika Textus Receptus wala familia yoyote ya nyaraka za ERROR. Kwa hiyo, wale wanaotumia New International Version (NIV), Swahili Union Version (SUV) na tafsiri nyingine ambazo hazijaidhinishwa (isipokuwa ile ya NKJV) wanayo tafsiri ambayo inatunza na kuendeleza kwa usahihi na uaminifu ule uharibifu wa nyaraka za lugha zilizokufa. Ndiyo, tafsiri zao hizi ni uchafu ulioharibika na hazijafunuliwa na Mungu, lakini kwa mtazamo wa kiutu / kibinadamu na kisayansi, hizi ni tafsiri aminifu za ERROR. Mungu aliwapa walichokitaka, lakini alituma ukondefu katika mioyo yao (Zab. 106:15). Kwa maneno mengine, wananaswa katika mtego wao wenyewe.

 

Ukweli kwamba KJB siyo tafsiri aminifu ya nyaraka au familia yoyote ya nyaraka imekuwa jambo jema kabisa. Kitu chochote ambacho ni tofauti na nyaraka za ERROR angalau kina nafasi ya kuwa neno la Mungu. Kumbuka, hatuwezi kutumia utofauti katika kuthibitisha kitu fulani si neno la Mungu; ni lazima tuone makosa / dosari. Tofauti zote zilizoko zinathibitisha tu kwamba KJB ni tofauti na Textus Receptus, na vitu ambavyo ni tofauti basi haviko sawa. Ile Textus Receptus ina mgongano katika suala la nani aliyemwua Goliati kama ilivyo katika tafsiri za kisasa. Hivyo tunajua kwamba ile Textus Receptus si neno la Mungu. Ukweli kwamba KJB pekee haina mgongano katika aya hizi hauthibishi kwamba yenyewe ndiyo neno la Mungu, lakini angalau bado iko katika mstari wa mbele wa mbio hizi kwa sababu hakuna chochote ilichoandika – katika chapa-mlazo au za kawaida – kimeonekana kuwa na dosari. Watu wanaoabudu nyaraka za ERROR wakati wote wanataka kukuaminisha kwamba chochote kilichomo katika KJB ambacho ni tofauti na kile kilichomo katika nyaraka za ERROR basi hiyo ni dosari / kosa. Lakini kwa nini, nakusikia msoaji, Mkristo yeyote akiwa katika akili yake timamu atataka kusoma tafsiri kutoka katika nyaraka zilizoharibika? Sasa hilo ndilo suala muhimu la kujiuliza; hawako katika akili yao timamu, wako katika akili yao ya kimwili. Kinachozungumza kupitia midomo yao ni kanuni za kidini za kipagani walizozipata kutoka katika mafunzo yao ya falsafa za Kiyunani; wanadhani hakuna kitabu kilichotoka kwa Mungu kwa sababu wao wana imani katika Reason, katika Mantiki. Wao ni waumini katika misingi ya utu (humanists) ambao wanapuuza alichokisema Mungu kile atakachofanya katika neno Lake, na ambao kama vipofu wanaukubali uozo uliodhihirishwa wa mabaki ya nyaraka za lugha zilizokufa kama “mamlaka”. Wanatenda dhambi kwa sababu kwanza wanafanya jambo hili bila imani, na pili hawampi Mungu utukufu kulingana na neno Lake. Na pale wanapotumia Mantiki katika majadiliano na wewe na kudai kwamba hoja zinazohusiana na tafsiri za Biblia kama hii uliyoisoma hapa – ambazo msingi wake ni kwamba Mungu na neno Lake wanaishi kulingana na neno Lake linavyosema – msingi wake ni Mantiki ya mduara (circular Reasoning), basi mwambie kwamba kamwe hutompa Mungu mgongo kwa kutumia hoja zao ambazo msingi wake ni falsafa. Waambie kwamba hoja zako msingi wake ni imani – siyo Mantiki. Imani iko katika Mungu na neno Lake, na kama hawapendi lulu hizi za hekima basi wanayo ruksa yako ya kurejea katika matapishi yao. Wape taarifa kwamba hawana tumaini la kukushawishi wewe wala Mungu kwa kufuru wala upujufu wao. Tumaini letu na maisha yetu msingi wake ni ufunuo wa Mungu; tumaini lao na maisha yao msingi wake ni Mantiki inayotoka katika tunda lililokatazwa la mti wa ujuzi [wa mema na mabaya].

 

Ili kufafanua jinsi na kwa nini Wakristo wanatumia tofauti kati ya Tafsiri Iliyoidhinishwa (KJB) na nyaraka za ERROR, nitasimulia tukio lililotokeo wakati nilipotembelea kanisa moja lililoko maeneo ya kaskazini (mwa USA). Baada ya ibada, na waumini kuondoka, mhubiri, mashemasi, na mimi tulibaki nyuma na tukawa na mazungumzo ya wazi kuhusu masuala ya Kikristo. Walipogundua imani yangu kuhusu masuala ya tafsiri za Biblia, basi hilo likawa ndilo suala la mazungumzo. Yule mhubiri mwanzoni tu akakaa kimya akisikiliza, kwani ilikuwa wazi hakujua lolote kuhusu suala hili. Lakini mmoja kati ya mashemasi alikuwa akizungumza kwa msisitizo mkubwa kwamba neno la Mungu (kama alivyofasili Yeye) halipo tena. Mimi nilipomjibu kwamba KJB pekee haina makosa / dosari, akasema kwa hakika KJB ina makosa na yeye anaweza kuthibitisha hili. Kama kawaida yangu nikamwambia afanye hivyo. Tofauti na Wakristo wengi, yeye hakujibu kichocheo changu hiki kwa kusema, “Aaah, unajua, sina nukuu ya haraka-haraka kichwani, lakini nimesoma sehemu fulani kwamba Wakristo wengi wanasema hivyo.” Yeye alisema, “Fungua Biblia yako usome Warumi 8:1”.

 

KJB. Rom. 8:1 There is therefore now no condemnation to them which are in Christ Jesus, who walk not after the flesh, but after the Spirit.

 

Warumi 8:1 Hivyo basi, kwa sasa hakuna hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wanaoenenda, si kwa jinsi ya mwili, bali kwa jinsi ya Roho.

 

Akaendelea kusema, “Sehemu ya pili ya aya hii, yaani kila neno baada ya Kristo Yesu, haina mamlaka ya ki-nyaraka, yaani, haionekani katika waraka wowote wa kale hapa duniani. Wakalimani na waandishi wa Biblia ya King James waliiongeza wenyewe tu. Na wakapuuza hata kusema kwamba waliiongeza wenyewe kwa kuiweka katika chapa-mlazo.”

 

Nikautizama ukurasa ule kwa muda halafu nikamwambia, “Tazama aya ya nne.”

 

KJB Rom. 8:4 That the righteousness of the law might be fulfilled in us, who walk not after the flesh, but after the Spirit.

 

War. 8:4 Ili wema unaoamriwa na sheria (torati) utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata jinsi ya mwili, bali jinsi ya Roho.

 

Nikamwuliza, “Je, unasema pia kwamba sehemu ya pili ya aya hii ya nne, yaani kila neno baada ya ‘in us / ndani yetu’ haina mamlaka ya ki-nyaraka?”

Akasema, “Hapana, iko sahihi katika aya ya nne, lakini haiko sahihi katika aya ya kwanza.”

Nikamwuliza, “Hivyo unasema kwamba tunahukumiwa tusipotembea kwa jinsi ya mwili, bali tukitembea kwa jinsi ya Roho?”

Akajibu, “Hapana, aya ya kwanza ni sahihi kikanuni. Ila ninasema sehemu ya pili ya aya hii haipaswi kuwa pale, kwa sababu haina mamlaka ya ki-nyaraka.”

Ebu tumchambue shemasi huyu:

1) Hii ni dondoo ndogo tu, lakini kwa ajili ya usahihi, nitaijadili: Hakuwa sahihi kuhusu aya hii kutokuwako katika nyaraka yoyote. Aya hii haimo katika tafsiri nyingi (kwa mfano NIV), lakini rejeo / tanbihi katika NIV, kwa mfano, inasema, “Baadhi ya nyaraka za baadaye zinaongeza: who do not live according to the sinful nature but according to the Spirit / ambao hawaishi maisha yao kulingana na hulka ya dhambi bali kwa njia ya Roho. Kwa nini mimi nilisema hii ni dondoo ndogo tu? Je, hii haitoi ushindi mkubwa kwa KJB? Je, ukweli aya hii inayo mamlaka ya ki-nyaraka hausababishi sisi wapenzi wa KJB kuvuta pumzi ndefu ya ridhaa? Hapana! Sisi hatujali juu ya kilichoandikwa katika kipande fulani cha karatasi inayochakaa. Nyaraka za ERROR si mamlaka na hazina mamlaka! Waraka pekee hapa duniani wenye mamlaka yoyote na wenye mamlaka yasiyo na kikomo ni Biblia Iliyoidhinishwa ya King James ya 1611.

2) Shemasi huyu ana tatizo lile lile ambalo Wakristo wengi waliovurugwa na ulimwengu wanalo: anazikubali nyaraka haribifu za lugha zilizokufa kama mamlaka juu ya neno hai lisiloharibika la Mungu! Kuna mtu yeyote aliyemnyoshea kidole na kumwamrisha, “Utaziabudu nyaraka za ERROR kama mamlaka yako?” Hapana, alidhani tu kwamba nyaraka hizi zinapaswa kuwa ndiyo mamlaka kwa sababu watu wasio na imani kama yeye hufikiri kwa kutumia hulka yao ya kimwili (Reason / Mantiki) na si jinsi ya Roho.

3) Kwa kuwa anazikubali (kwa makosa) nyaraka za ERROR kama zenye mamlaka, na kwa kuwa anao uelewa wa msingi wa kanuni ya mamlaka, basi anafikiri chochote kinachotofautiana na nyaraka zake za ERROR kina makosa. Ili awe Mkristo mwema anahitaji kulifanya neno lisilo na makosa la Mungu kuwa ndiyo mamlaka katika fikra yake na kuondoa kabisa tafsiri za nyaraka za ERROR. Halafu uelewa wake wa msingi wa mamlaka unaweza kusitawi naye akawa imara katika mamlaka yasiyo na kosa, yaliyoongozwa na Mungu, ya Biblia Iliyoidhinishwa ya King James na pia anapoanza kuona kwamba chochote kinachotofautiana na KJ1611 kina makosa kwani hii AV1611 pekee ndilo neno la Mungu.

4) Kama huyu jamaa angekuwa Mkristo mwenye hekima anayetembea kwa tahadhari angekuwa mwangalifu sana kuhusu kukisema vibaya kitu ambacho kinaweza kuwa neno la Mungu. Kwa mfano, ingawa yeye anafikiri kwamba yuko sahihi kuhusu kukosa mamlaka ya kinyaraka kwa Warumi 8:1, na ingawa anafikiri kwamba AV1611 si neno la Mungu, na ingawa anafikiri kwamba neno la Mungu halipo hapa duniani, anapaswa kuwa na angalau kiasi cha kutosha cha imani na woga wa Mungu na afunge mdomo wake ili tu ikiwa ni kweli kwamba Mungu ni mkuu kama anavyosema, basi awe na angalau kanafasi ka kupona ghadhabu Yake.

5) Lakini kwa sababu hana woga wa Mungu, amefungua mdomo wake usio na hekima na kujiingiza katika matatizo: Siku ya hukumu ataulizwa kwa nini alifikiri kwamba ni wajibu wake wa Kikristo kujaribu kunishawishi mimi kwamba neno la Mungu halipo duniani. Alijaribu kunifanya mimi niamini katika uwongo kwamba hakuna Biblia hata moja hapa duniani ambayo ni neno la Mungu. Kama ukichunguza muktadha wa Jer. 28:15,16, utagundua kwamba kosa la shemasi yule ni kubwa kuliko kosa la Hanania. Hanania alifikiri, kimakosa, kwamba ule ujumbe mkali ulioletwa kwao na mwanadamu tu ambaye wote walikuwa wakicheza naye kombolela walipokuwa wadogo – Jeremia – haukuwa neno la Mungu, na akajaribu kuwashawishi wengine juu ya hili. Kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na kwa sababu ya utiifu kamili ambao Mungu anautaka kwa neno Lake, Mungu anasema katika aya ya 16 kwamba Hanania alikuwa anafundisha ulozi! Ukishapitia muktadha wa aya hii na ukajidhihirishia mwenyewe kwamba niko sahihi katika hili, fikiria kuhusu dhambi ya shemasi huyu kwa kuilinganisha na ile dhambi ya Hanania: Hanania alijaribu kuwashawishi Wakristo kwamba alichokisema Jeremia hakikuwa neno la Mungu. Shemasi yule alijaribu kunishawishi mimi kuwa hakuna neno la Mungu! Unaweza kufikiria kitu chochote habithi zaidi ya kitendo cha kuhujumu msingi pekee wa Ukristo wetu?! Kama Biblia si neno la Mungu, basi Ukristo unakoma kuwa Dini ya Kweli na badala yake unakuwa dini nyigine kati ya dini nyingi za dunia hii.

6) Bwana aliposema kwamba adui wa [Mkristo watakuwa] ni wale wa nyumbani mwake (Matt. 10:36), alikuwa anausema uhalisia ambao unaonekana mara nyingi katika Biblia yake. Kama unajaribu kushawishi Wakristo wenzako kwamba neno la Mungu halipo, je, Mungu atakuchukulia wewe kuwa ni rafiki au adui? Hmm?

 

Baada ya kuisoma sura hii na ukaamua kuisoma na kujifunza Biblia ya King James, utakuta baadhi ya vitu katika KJB ambavyo haviko sahihi au vina mgongano. Jambo hili litakutikisa kidogo na utajaribu kutafuta suluhu ya “tatizo” hilo. Baada ya kupata ufumbuzi wa “matatizo” kadhaa, utakuwa bora zaidi katika kutathmini “matatizo” na utaona jinsi mengi katika haya “matatizo” yanaweza kutatuliwa. Kwa mfano, moja kati ya “matatizo” katika tafsiri zote za Biblia ni kiasi cha maji kilichokuwamo katika chombo cha chuma kilichosubiwa na Hiramu; kiasi kile cha maji kilikuwa bathi 2,000 au bathi 3,000? Pia, kwa kuwa uzingo wa duara ni pai (π) mara kipenyo chake, na ukizidisha 3.14 X kipenyo cha dhiraa 10 hautopata dhiraa 30, je, hili si kosa / dosari iliyothibitishwa, katika Biblia?

 

1Kings 7:23 And he made a molten sea, ten cubits from the one brim to the other: it was round all about, and his height was five cubits: and a line of thirty cubits did compass it round about.

1 Kings 7:26 And it was an hand breadth thick, and the brim thereof was wrought like the brim of a cup, with flowers of lilies: it contained two thousand baths.

2 Chr. 4:5 And the thickness of it was an handbreadth, and the brim of it like the work of the brim of a cup, with flowers of lilies; and it received and held three thousand baths.

 

1Wafalme 7:23 Tena akatengeneza chombo cha kusubu, dhiraa kumi toka ukingo hata ukingo, kilikuwa duara, na dhiraa tano ilikuwa [toka chini] kwenda juu yake; na kamba ya dhiraa thelathini kuizunguka [yote] kabisa.

1Wafalme 7:26 Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu mbili.

2 Mamb. 4:5 Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake.

 

Mimi sijui majibu. Lakini kuna mapendekezo kadhaa yanayoweza kutatua “tatizo” hili. Ebu tupambane na mahesabu yake kwanza. Kingo za chombo hiki zilikuwa na upana / unene wa nyanda nne (nyanda ni urefu kutoka dole gumba hadi kidole cha kati). Huu ni wastani wa inchi tatu. Tunajua kwamba chombo hiki kiliundwa kama kikombe kwenye ule mzunguko wa juu. Hivyo inawezekana mzunguko wa juu ulipinda kuelekea nje (kama vikombe vilivyo). Hatujui ile alama (kamba) ya dhiraa thelathini ilikowekwa: labda ilikuwa upande wa nje, au juu ya ukingo uliopinda kama kikombe, au upande wa ndani wa huo ukingo wa juu, au ndani chini kidogo ya ukingo wa juu ambapo patakuwa na alama ya “jaza mpaka hapa maji yakipungua”. Kwa kuwa kuna namna nyingi za kusubu upande wa juu wa kikombe kile kikubwa pamoja na namna kadhaa nilizozitaja hapo juu za ule msitari wa ujazo, hatutoweza kujua kwa uthabiti chombo hiki kilikuwa na muundo gani. Lakini ukicheza na hizo namba kama nilivyofanya mimi, utaona ule mzunguko katika Biblia si mkubwa kupita kiasi wala si mdogo kupita kiasi. Tunajua kitu kimoja kwa uhakika; Bwana wetu alijua kwamba baadhi ya Wakristo watalitumia hili kama kisingizio cha kukataa mamlaka ya neno Lake: Alipanga tangu mwanzo kwamba neno Lake litakuwa jiwe la kujikwaa na mwamba wa maudhi kwa wale wenye imani haba.

 

Je, ni vipi kama chombo kile kilikuwa kinaweza kubeba bathi elfu tatu kikijazwa mpaka juu, au bathi elfu mbili kikijazwa mpaka kwenye ile alama ya “jaza mpaka hapa”? Na kama kiliweza kufikisha bathi elfu tatu kikijazwa mpaka juu, je, hakikuweza kufikisha bathi elfu mbili katika ile alama ya “jaza mpaka hapa”? Ni vipi kama ukingo wa juu unafikisha bathi elfu tatu na ile alama inafikisha bathi elfu mbili? Sidhani kama kuna ulazima wa kujadili hili zaidi, hivyo ebu tutazame “kosa” lingine katika Biblia.

 

2 Sam. 24:9 …and there were in Israel eight hundred thousand valiant men that drew the sword; and the men of Judah were five hundred thousand men.

1 Chr. 21:5 …And they of Israel were a thousand thousand and an hundred thousand men that drew sword: and Judah was four hundred threescore and ten thousand men that drew sword.

 

2 Sam. 24:9 … Katika Israeli kulikuweko mashujaa 800,000 wenye uwezo wa kupigana kwa upanga: na katika Yuda watu 500,000.

1 Nyakati 21:5 … Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga: na katika Yuda watu 470,000.

 

Watu wengine wananyooshea kidole aya hizi na kusema watu 800,000 katika Israeli si sawa na watu 1,100,000, na watu 500,000 katika Yuda si sawa na watu 470,000. Mkristo asiyeamini kwamba neno la Mungu lipo, kwa sababu fulani ya ajabu atatafuta makosa katika neno la Mungu, na tofauti katika namba yanatoa visingizio kwa wengi. Lakini mtu wa imani anaanza kwa kuamini kwamba kila kitu katika Biblia ni kweli. Hivyo akisoma aya hizi mbili anaanza kufikiri, “Hey, hii ni nini hapa?” - kama mtu yeyote yule. Juu juu tu, anaona “kosa” lille lile linaloonekana na yule asiye mwaminifu. Lakini yeye anachimba zaidi na kutambua kwanya kabati lenye viatu 12 linaweza kusemekana kuwa na jozi 6 za viatu, na linaweza kusemekana kuwa na jozi 2 za viatu vyeupe. Kwa maneno mengine, unavyozidi kuweka vivumishi katika idadi fulani, basi idadi ya vitu vya aina moja inazidi kupungua. Fahamu hapo kwamba kati ya hizo seti mbili za namba kwa Israeli na Yuda, mara zote mbili kila mara namba zinapokuwa ndogo kuna vivumishi zaidi vimeunganishwa. Mimi ninapenda uthabiti wa neno la Mungu, wewe je? Ni wazi kabisa, “mashuja wenye uwezo wa kupigana kwa upanga” wanaweza kuwa wazoefu wa vita, na watu “ambao wangeweza kutumia upanga” wanaweza kuwa ni wanaume mashujaa pamoja na kuruta wasio na uzoefu wa vita. Na “watu” pekee inaweza kujumuisha raia (wasio askari), askari waliopumzishwa, waliostaafu, ambao hawajawahi kuwa askari, n.k. (Tazama, mfano huu unaihusisha tu Biblia ya King James kwa sababu baadhi ya hizo Biblia nyingine hazina vivumishi husika na hivyo kufanya baadhi ya aya hizi kuonekana kama zina makosa / dosari. Lishike neno la Mungu nawe hautakuwa na matatizo).

 

Hii ndiyo namna muumini wa Biblia anavyokisoma Kitabu. Kama tukiukubali ukweli kwamba Mungu anajua anachokifanya, tutakuwa waangalifu sana katika kutafuta namna ambazo anaweza kuwa sahihi. Kama tukishindwa kufanya hivyo na badala yake tukachukulia kirahisi tu kwamba hakulitunza neno Lake kama alivyosema kwamba atalitunza, basi tutagundua katika siku ya Hukumu kwamba Yeye analithamini neno Lake zaidi ya Jina lake.

 

Sasa tutaendelea kutafuta makosa / dosari katika tafsiri za kisasa. Na katika kila mfano tutalinganisha aya zake zisizoidhinishwa na zile za Tafsiri Iliyoidhinishwa ili kuthibitisha kwamba hii haina uharibifu katika sehemu zile zile. Hii haitathibitisha kwamba AV1611 ndiyo neno la Mungu; itathibitisha tu kwamba hizo tafsiri nyingine siyo. Halafu, tunapotambua kwamba AV1611 ndiyo tafsiri pekee iliyobaki yenye uwezekano wa kuwa neno la kweli la Mungu, tutautumia ukweli kwamba tulianza tu kulitafuta neno la Mungu kwa sababu tulikubali kwa imani kuwa lipo [mahala fulani], nasi tutaikubali kwa imani hii hii Biblia Iliyoidhinishwa kubwa ndilo neno la Mungu tulilopewa kwa Mamlaka ya Mfalme mwenyewe.

 

RSV Matt. 5:22 But I say to you that every one who is angry with his brother shall be liable to judgment; whoever insults his brother shall be liable to the council, and whoever says, ‘You fool!’ shall be liable to the hell of fire.

RSV Mrk 3:5 And he looked around at them with anger, grieved at their hardness of heart, and said to the man, “Stretch out your hand.” He stretched it out, and his hand was restored.

 

Kama unavyoona, RSV yaani Revised Standard Version, na NAS yaani New American Standard Bible, na NIV yaani New International Version, zote hizi zinamfanya Yesu kuwa mwenye dhambi kwa sababu aliwakasirikia ndugu zake. Hii inagongana na sehemu za Biblia ambazo zinatuambia Kristo hakutend adhambi. Tunaupokea ukweli huu kwa imani, kwamba Kristo hakuwa na dhambi, na imani hiyo hiyo inathibitisha kwamba haya ni matunda kutoka mti wa uharibifu.

 

KJV Mt 5:22 But I say unto you, That whosoever is angry with his brother without a cause shall be in danger of the judgment: and whosoever shall say to his brother, Raca, shall be in danger of the council: but whosoever shall say, Thou fool, shall be in danger of hell fire.

KJV Mk 3:5 And when he had looked round about on them with anger, being grieved for the hardness of hearts, he saith unto the man, Stretch forth thine hand. And he stretched it out: and his hand was restored whole as the other.

 

5:22Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake ghadhabu bila sababu, ataingia katika hatari ya hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Raka, atakabiliwa na baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu.

3:5Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili:

 

Katika KJB, msemo “bila sababu” katika Matthayo 5:22 unamwondoa Yesu kutoka orodha ya wenye dhambi katika Marko 3:5.

 

NAS Mk 1:2 As it is written in Isaiah the prophet, “BEHOLD, I SEND MY MESSENGER BEFORE YOUR FACE, WHO WILL PREPARE YOUR WAY;

3 THE VOICE OF ONE CRYING IN THE WILDERNESS, ‘MAKE READY THE WAY OF THE LORD, MAKE HIS PATHS STRAIGHT.’”

 

SUV 1.2 Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.

1.3 Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.

 

Hii inakufanya ufikiri kwamba nukuu hii imetoka katika kitabu cha Isaya, sivyo? Tafsiri nyingi, kama NIV, wameamua kuwa wakweli kuhusu aya hii mapema kabisa; wameweka rejeo / tanbihi kwenye ukurasa husika ambao unakiri kwamba nukuu hii inatoka Malaki 3:1, na siyo Isaya 40:3. Kama utakavyoona, Mungu alijua kwamba nukuu hii haitoki katika kitabu cha Isaya pekee, na hivyo ameweka rekodi iliyonyooka katika Kitabu Chake. Tazama:

 

KJV Mk 1:2,3 As it is written in the prophets, Behold, I send my messenger before thy face, which shall prepare thy way before thee. The voice of one crying in the wilderness, Prepare ye the way of the Lord, make his paths straight.

 

1:2 Kama ilivyoandikwa katika Manabii,

Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako,

Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.

1:3 Sauti yake aliaye jangwani,

Itengenezeni njia ya Bwana,

Nyosheni mapito yake.

 

TAZAMA KWA MAKINI!! Nukuu ya SUV (Swahili Union Version) ina ugonjwa huu huu. Hakuna hata Biblia moja katika Kiswahili ambayo imetoka katika KJB, zote ni matokeo ya uharibifu wa ERROR manuscripts.

 

Kama “usahihi” katika tafsiri ya Biblia maana yake ni “uaminifu kwa nyaraka zilizoharibika za Kiebrania na Kiyunani”, na kama “usahihi” ndicho unachokitaka, basi jinunulie tafsiri ambayo Mungu hakuiidhinisha. Lakini kama unataka kweli ya Mungu, basi kikumbatie Kitabu pekee hapa duniani ambacho kinakidhi vigezo vyote vya Mungu alivyoviweka kwa neno Lake.

 

Kama ukiitwa kwenda kwa jirani yako ukatoe pepo aliyempagawisha mtu, na licha ya juhudi zote hupati mafanikio, unafikiri utafanya maombi, au badala yake utafuata mfano wa Martin Luther wa kurusha uchafu? Ndiyo, ni wazi kabisa utafanya maombi mengi tu, wakati unajiandaa kumfukuza pepo huyo na wakati wa juhudi za kumfukuza pepo huyo – Mkristo yeyote yule atafanya hivyo. (Hata Martin Luther atafanya hivyo ikiwa atajikuta uso kwa uso na pepo halisi badala ya mzuka ulio kichwani mwake mwenyewe). Ila inawezekana – na yumkini – hutafikiria kufunga katika matayarisho yako ya tukio hilo:

 

KJV Mk 9:28,29 And when he was come into the house, his disciples asked him privately, Why could not we cast him out? And he said unto them, This kind can come forth by nothing, but by prayer and fasting.

 

Bwana alipowaambia hivyo, yumkini walitizamana na kusema, “Aaah, ndiyo maana hatukuweza kumfukuzo pepo yule – hatukufunga!” Lakini tazama kile NIV, NASB, na RSV katika Kiingereza na SUV, NEN, na wengine katika Kiswahili wanavyotaka kukuaminisha:

 

NAS Mk 9:28,29 And when He had come into the house, His disciples began questioning Him privately, “Why could we not cast it out?” And He said to them, “This kind cannot come out by anything but prayer.”

 

SUV 9.28 Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?

9.29 Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.

 

Mtu anaweza kudhani, kutokana na masimulizi tunayoyapata kutoka NAS na SUV na wenzao wote, kwamba wanafunzi wa Bwana walitizamana halafu wakasema, “Kati ya vitu vyoooote tulivyotakiwa kufanya katika maandalizi, hatukufikiria kufanya maombi!” Unaweza pia kulinganisha KJB na hizo Biblia nyingine katika 1 Wakor. 7:5; Matendo 10:30; na Matthayo 17:21. Zote hizo zimesahau kuweka neno “kufunga”. Ni muhimu sana kuwa dhaifu katika mwili na kuwa mkuu kabisa katika roho.

 

Okay, sasa turudi tena kwenye maswali na majibu: Kulingana na Mungu, kwa nini watu walio na ulemavu walilala kuzunguka bwawa lililoitwa Bethesda jirani na Mlango wa Kondoo katika Yerusalemu? Hujui? Ebu basi tuulize ndani ya NIV, RSV, na NASV:

 

NIV Jn 5:3 Here a great number of disabled people used to lie – the blind, the lame, the paralyzed.

NIV Jn 5:4 [Nothing, nada, zippo, zilch, goose egg, empty space, skipped verse, brackets, or footnotes. Yaani hakuna kitu kilichoandikwa au wanaweka mabano au rejeo / tanbihi.]

NIV Jn 5:5 One who was there had been an invalid for thirty-eight years.

NIV Jn 5:6 When Jesus saw him lying there and learned that he had been in this condition for a long time, he asked him, “Do you want to get well?”

NIV Jn 5:7 “Sir,” the invalid replied, “I have no one to help me into the pool when the water is stirred. While I am trying to get in, someone else goes down ahead of me.”

 

Kitu gani kiliyafanya maji “yatikisike”? Mamba!? Kwa nini wote walitaka kuingia katika bwawa lile? Je, ni kwa sababu walitaka wauwawe na mamba huyo [ili waondokane na mateso yao]? Kwa nini haikuwa na faida kuwa wa pili, wa tatu, au wa nne kuingia ndani ya maji? Mamba yule alishiba baada ya kumla mtu mmoja na kwenda kulala? Hii ni sehemu nyingine kati ya zile zinazowachukiza wanazuoni. Wanafikiri suala lote ni upuuzi tu, lakini hawathubutu kuacha majibu ya maswali yao nje ya Biblia ingawa nyaraka zao bora kabisa katika ya zile ERROR hazina majibu. Hivyo wanairuka aya hii na kuiweka katika rejeo / tanbihi (kama ilivyo katika tafsiri ya Kiswahili ya Ushirikiano wa Makanisa), au wanaiweka katika mabano halafu wanakuambia katika rejeo / tanbihi kwa nini haipaswi kuwa hapo. Mungu anacheka tu kwa sababu alipanga historia ili mfumo wa namba za aya uliokuwepo wakati KJB inatoka utakuwa kiwango-mamlaka (authoritative standard) duniani kote mpaka mwisho wa dahari. Hivyo kila mfasiri anayetaka kulipunguza neno la Mungu itampasa kupambana na ukweli kwamba kuruka namba za aya kutamfanya aonekane kwa hakika kuwa amepunguza neno kutoka katika kitabu cha unabii huu.

 

KJV Jn 5:3 In these lay a great multitude of impotent folk, of blind, halt, withered, waiting for the moving of the water.

KJV Jn 5:4 For an angel went down at a certain season into the pool, and troubled the water: whosoever then first after the troubling of the water stepped in was made whole of whatsoever disease he had.

KJV Jn 5:5 And a certain man was there, which had an infirmity thirty and eight years.

 

5.3 Ndani yake jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yatikiswe.

5.4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye anayeingia kwanza baada ya maji kutibuliwa, hupona ugonjwa wote uliomsibu.]

5.5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hajiwezi muda wa miaka thelathini na minane.

5.6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?

5.7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia bwawani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine huwa keshaingia mbele yangu.

 

Tumshukuru Mungu kwani tunalo neno Lake: Kama kusingekuwa na KJB yumkini tungekuwa gizani tukihangaika na nadharia za mamba alifanya hivi au vile! Kukosekana kwa aya yaweza kuwa kosa au dosari iliyothibitika lakini hii inaonyesha kwamba KJB ndiyo tafsiri tunayopaswa kuisoma.

 

NAS Jn 7:8,10 “Go up to the feast yourselves: I do not go up to this feast because My time has not yet fully come.”…But when His brothers had gone up to the feast, then He Himself also went up, not publicly, but as it were, in secret.

KJV Jn 7:8,10 Go ye up unto this feast: I go not up yet unto this feast; for my time is not yet full come…But when his brethren were gone up, then went he also up unto the feast, not openly, but as it were in secret.

Yoh. 7:8,10 Ninyi nendeni kwenye hii karamu: mimi sitaenda bado kwenye karamu hii; kwani wakati wangu haujatimia bado...Lakini ndugu zake walipopanda kwenda, ndipo naye akaenda kwenye karamu, bali si kwa wazi, bali kwa kificho.

 

Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa: Yoh. 7:8,10 Nyinyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayo haijafika.” ... 10 Baada ya ndugu zake kuenda kwenye sikukuu, Yesu naye alikwenda, lakini hakuenda kwa hadhara bali kwa siri.

 

Kuachwa / kuondolewa kwa ile “bado” ya kwanza (au kuwekwa katika parandesi au rejeo / tanbihi) katika NAS, NIV, na RSV, au Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa kunamfanya Yesu kuwa mwongo. Nilikuwa nazungumza na jamaa mmoja Mkristo mwenzangu (ambaye alikuwa mtu mzuri sana) wakati fulani na nikaona amebeba Biblia yake tafsiri ya NAS. Nikamwambia kwamba tafsiri yake hii inamfaya Kristo aonekane mwongo na nikamwonyesha aya hii. Akashituka sana. Nilipomwambia kwamba King James haijaharibika na haijamfanya Kristo kuwa mwongo, akashangaa zaidi kwa sababu hakuwa anajua suala la tafsiri za Biblia na alidhani tafsiri zote zilitokana na nyaraka halisi na safi za Kiebrania na Kiyunani. Nikamwacha alinganishe KJB yangu katika sehemu hii na sehemu zingine. Alishikwa na bumbuwazi kuu kwa kuona uharibifu kama huu umewekwa wazi miaka hii yote na yeye hakuwa na ufahamu. Alikuwa na maswali mengi sana, nami nilikuwa na majibu mengi pia ambayo yalileta maana kwake. Nilipokutana naye wiki moja baadaye alikuwa ni mtu aliyebadilika na hakutaka kusema na mimi. Kumbe ndugu yake ni mhubiri na alipitia kozi za teolojia katika shule fulani ya “Biblia”. Jamaa yangu alimpigia ndugu yake simu na akamsimulia baadhi ya mambo niliyomwonyesha. Walijadiliana kwa zaidi ya saa nzima ambapo jamaa yangu alijifunza mambo mengi. Aligundua kwamba neno la Mungu halipo. Alijifunza kwamba NAS ndiyo tafsiri pekee anayotakiwa kuitumia kwa sababu ile shule ya Biblia inatumia tafsiri hiyo pekee. Alijifunza kwamba Biblia ya King James imejaa makosa / dosari (ingawa ndugu yake huyu hakuweza kumwonyesha hata kosa / dosari moja). Alijifunza kwamba kuna kikundi kidogo cha watu ndani ya Ukristo kilichoghilibika ambacho kinaamini neno la Mungu lipo, na kwamba hii KJB – ambayo ni tafsiri ya kibinadamu tu – ndilo neno hilo. Aliambiwa mambo mengi sana kwani baada ya kumaliza kunikaripia akanitazama machoni na kuniambia ananionea huruma na ataniombea kwani mimi ni mfungwa wa Shetani. Hii ilikuwa mara ya mwisho yeye kuongea na mimi.

 

Swali linalofuata katika kipindi chetu cha maswali na majibu: Je, kuna masharti yoyote yanayotakiwa kutimizwa kabla ya ubatizo au tunapaswa kumbatiza mtu yeyote aliye katika foleni? Ebu tena tufanye ulizo katika NAS, NIV, na RSV.

 

RSV Acts 8:36 And as they went along the road they came to some water, and the eunuch said, “See, here is water! What is to prevent my being baptized?”

RSV Acts 8:37 [Blank, footnote, or brackets / hakuna kitu, au wanaweka rejeo au tanbihi au parandesi – tizama Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa]

RSV Acts 8:38 And he commanded the chariot to stop, and they both went down into the water, Philip and the eunuch, and he baptized him.

 

Kulingana na tafsiri hii yeyote yule ikiwa ni pamoaj na watoto wachanga, anaweza kubatizwa kwa sababu hakuna ulazima wa kukiri imani katika Kristo. Ebu tuone anachokisema Mungu:

 

KJV Acts 8:36 And as they went on their way, they came unto a certain water: and the eunuch said, See, here is water; what doth hinder me to be baptized?

KJV Acts 8:37 And Philip said, If thou believest with all thine heart, thou mayest. And he answered and said, I believe that Jesus Christ is the Son of God.

KJV Acts 8:38 And he commanded the chariot to stand still: and they went down both into the water, both Philip and the eunuch; and he baptized him.

 

36 Walipokuwa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule towashi akasema, Kitu gani kinanizuia nisibatizwe?

37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, unaweza [kubatizwa]. Akajibu, akasema, Naamini kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.

38 Akaamuru lile gari lisimame: wakateremka wote wawili wakaingia majini; Filipo na yule towashi: akambatiza.

 

Aya ya 37 ni mfano mzuri wa tatizo kubwa ambalo kamati za tafsiri za kisasa linalo dhidi ya Biblia ya King James: Inatumia maneno kama thou, believest, thine, na mayest yote katika sentensi moja na hii inahakikisha wahubiri na waumini wakimbilie kamusi zao ili kujaribu kumaizi maana ya aya hii ngumu ya Kiingereza rasmi cha zamani!

 

Biblia inasema uchamungu ni jambo jema na uchamungu ni njia ya kupata baraka kwani Mungu huwapa thawabu wachamungu (1 Tim. 4:8; 6:6; Zab. 19:11). Lakini NKJV, NAS, na RSV zinapinga hili:

 

NKJV 1 Tim 6:5 useless wranglings of corrupt minds and destitute of the truth, who suppose that godliness is a means of gain. From such withdraw yourself.

6.5 mazozano ya watu walioharibika nafsi zao, walioikosa kweli, wanaodhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. Jitenge na watu wa aina hii.

 

Katika neno Lake, Mungu anasema si tu kwamba uchamungu ni njia ya kubarikiwa (Matt. 6:33), bali mali za kidunia si dalili ya uchamungu:

 

KJV 1 Ti 6:5 Perverse disputings of men of corrupt minds, and destitute of the truth, supposing that gain is godliness: from such withdraw thyself.

6:5 na majadiliano potofu ya watu walioharibiwa nafsi zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa mali ni [dalili ya] uchamungu; jitenge na watu kama hao,

 

Wakati tukiwa katika 1 Tim. 6, acha nijaribu kueleza umuhimu na thamani ya kuwa na neno la kweli la Mungu. Tafsiri zote za kisasa zinapingana na King James katika 1 Tim. 6:10. Aya hii haina thamani katika mjadala wa tafsiri za Biblia kwa sababu namna zote mbili za uandishi wake zinaweza kuchukuliwa kuwa ni sahihi – namna hizi mbili ni tofauti tu:

 

KJV 1 Tim. 6:10 For the love of money is the root of all evil: which while some coveted after, they have erred from the faith, and pierced themselves through with many sorrows.

NKJV 1 Tim. 6:10 For the love of money is a root of all kinds of evil, for which some have strayed from the faith in their greediness, and pierced themselves through with many sorrows.

 

Lakini baada ya kutambua kwamba kila neno katika King James lilichaguliwa kwa makusudi na kwa uangalifu kwa ajili ya sababu mahususi, unaanza kufuatilia maneno, kama alama za barabarani, katika Biblia. Kwa mfano, nilijiuliza ni vipi kupenda pesa kunaweza kuwa ni mzizi / chanzo cha uovu wote. Ni kwa namna gani kupenda pesa kunaweza kuwa mzizi / chanzo cha Kaini kumwua Abeli? Halafu nikaona kupenda pesa katika Eze. 28 na nikaanza kujiuliza kama kuna uhusiano. Halafu neno uovu likanivuta katika Isa. 45:7. Na nikajiuliza kama neno ‘walitamani’ katika 1Tim. 6:10, ambalo wazi kabisa limeunganishwa na kupenda pesa kuwa ni mzizi / chanzo cha uovu wote, lina muunganiko na 1 Sam. 15:23 kwa sababu aya hizi mbili zinaunganishwa katika 1Wakol. 3:5. Kwa nini tamaa ni uasi na kuabudu sanamu? Je, ni kwa sababu ya mamlaka na Uungu wa Mungu? Hili linahusiana vipi na Yoh. 8:44 na 1 Yoh. 3:8? Na, ni kwa namna gani Lucifer alimwua Kondoo anayeishi milele? Yote haya yalitokea katika kipindi cha miaka mingi na yalihusisha kujifunza maana ya maneno mengi katika Biblia. Nilijifunza mengi kuhusu mamlaka, uasi, tamaa, utiifu, nk. Uamuzi huo huo wa kujifunza maana ya maneno katika Biblia unaweza kukusababisha wewe uone kwamba uovu ambao Mungu aliuumba katika Isa. 45:7 ulikuwa ni tamaa, kama nilivyofikiria mimi hapo mwanzo. Lakini tamaa ni dhambi wakati wote. Na dhambi aliyoiumba Mungu ilikuwa zaidi ni kishawishi, majaribu, kitu ambacho kinaweza kupelekea au kutopelekea katika dhambi. Usawa unaweza kuwa ndio dhambi hii (aliyoiumba Mungu) kwa sababu usawa unaweza kutupeleka katika kishawishi cha kutamani bila ya kushindwa kukishinda kishawishi cha kutamani.

 

Huu ni mfano wa jinsi tunavyotakiwa kulisoma neno la Mungu na kulitafakari. Na hii ndiyo jinsi neno hili linavyoweza kujizidisha kutoka boflo moja ya Mkate na kuwa nyingi zisizohesabika za Mkate. Tatizo la tafsiri ambazo hazijaidhinishwa ni kwamba hakuna alama za barabarani zinazomwongoza msomaji katika Biblia kwa sababu maneno yale hayakutoka kwa Mungu; yametoka kwa watu. Kwa sababi hii huwezi kuliamini hitimisho utakalolipata kutoka katika kujifunza maana za maneno yake. Hii ni sababu kuu Ukristo wa kisasa umeshindwa kujifunza kutoka kanuni zinazofundishwa katika Age of Reason.

 

Mara utakapoelewa haya yote, utajua kwamba neno fulani kutoka katika tafsiri yoyote au waraka wowote wa kale ambalo lina tofauti tu na neno lililoko katika aya husika ya Biblia ya King James si sahihi. Kama King James imeandika, “Akaelekeza macho yake katika samawati ya mbingu” na tafsiri nyingine imeandika, “Akatizama juu mbinguni”, basi neno mbinguni si sahihi kwa sababu Mungu alitaka iandikwe samawati. Samawati yaweza iwe au isiwe muhimu katika kukamilisha seti nzima ya alama za barabarani wakati wa kutafuta maana za maneno, lakini kamwe si sahihi katika mazingira yoyote yale kubadilisha maneno aliyoweka Mungu.

 

Makosa yafuatayo yenye mgongano yanapatikana katika NIV, RSV, na NKJV. Katika aya hizi utamwona Roho Mtakatifu akijipinga Mwenyewe. Tizama kwa makini katika kile Mungu (Roho) anataka, na kile Paulo (roho) anataka. Na utaiona migongano hiyo:

 

NKJV Acts 19:21 When these things were accomplished, Paul purposed in the Spirit, when he had passed through Macedonia and Achaia, to go to Jerusalem, saying, “After I have been there, I must also see Rome.”

NKJV Acts 20:22 “And see, now I go bound in the spirit to Jerusalem, not knowing the things that will happen to me there,

NKJV Acts 21:4 And finding disciples, we stayed there seven days. They told Paul through the Spirit not to go up to Jerusalem.

NKJV Acts 21:11 When he had come to us, he took Paul’s belt, bound his own hands and feet, and said, “Thus says the Holy Spirit, ‘So shall the Jews at Jerusalem bind the man that owns this belt, and deliver him into the hands of the Gentiles.’ ”

 

Kwa upande mwingine, Biblia ya King James haina chachu ya makosa / dosari na migongano:

 

KJV Acts 19:21 After these things were ended, Paul purposed in the spirit, when he had passed through Macedonia and Achaia, to go to Jerusalem, saying, After I have been there, I must also see Rome.

KJV Acts 20:22 And now, behold, I go bound in the spirit unto Jerusalem, not knowing the things that shall befall me there:

KJV Acts 21:4 And finding disciples, we tarried there seven days: who said to Paul through the Spirit, that he should not go up to Jerusalem.

KJV Acts 21:11 And when he was come unto us, he took Paul’s girdle, and bound his own hands and feet, and said, Thus saith the Holy Ghost, So shall the Jews at Jerusalem bind the man that owneth this girdle, and shall deliver him into the hands of the Gentiles.

 

Katika King James Mungu hajipingi Mwenyewe, na tunagundua kwamba safari ya Paulo ya kwenda Yerusalemu ilikuwa kinyume na mapenzi Yake. Tafsiri za kisasa zinafanikiwa tu kudhihirisha jinsi zilivyo matunda ya uharibifu.

 

Mifano ya hapo juu ilichaguliwa kwa sababu inawakilisha aina ya makosa / dosari yaliyomo katika nyaraka za ERROR na katika tafsiri za kisasa zinazotokana na hizo nyaraka. Katika kutafuta neno la kweli la Mungu mifano hii inatusaidia kuelewa mambo kadhaa:

 

Tafsiri zote za kisasa za Biblia ni matunda ya Enzi ya Mantiki (Age of Reason) na jamii za kidemokrasia ambazo msingi wake ni Mantiki (Reason). Zote zimetokana na “njia za uhakiki wa juu wa maandishi / nyaraka / hati” ambazo chanzo chake ni falsafa za Kiyunani ambazo ziliasiliwa na wakusanyaji wa mambo / vitu vya kale.

Tafsiri zote za Biblia za kisasa ni matunda ya sayansi kwa sababu zimezalishwa na utu-wa-kidunia (secular humanism) na hivyo hazima ushawishi wa kiimani, wa kidini, wala wa kitu chochote ambacho kinatokana na mfumo wa kisayansi. NB: Wakristo wengi wa leo ni humanists, yaani ni waumini katika falsafa ya utu. Hii ni kinyume na mafundisho ya Biblia, ingawa hii ni vigumu sana kuamini mpaka pale utakapojifunza Biblia kwa usahihi. Nakushauri ufanye utafiti wako mwenyewe. Hili ni suala muhimu sana!

Kwa ujumla, tafsiri zote za kisasa haziegamii upande wowote na ni tafsiri sahihi za nyaraka / hati za ERROR za Kiebrania na Kiyunani.

Ile NKJV (New King James Version) siyo tafsiri aminifu ya familia iliyochachuliwa ya Textus Receptus ambayo mzizi wake ni nyaraka za ERROR. Ndiyo, katika sehemu [zake] fulani inaakisi dosari / makosa ya Textus Receptus, lakini katika maeneo mengine inaitelekeza Textus Receptus (bila maelezo) na kunakili aya za King James Bible. Hivyo, waumini wa Biblia wanaitweza kwa sababu ina uharibifu, na wanazuoni wanaidharau kwa sababu ina utata (kama huo ulioelezwa).

Biblia Iliyoidhinishwa ya mwaka 1611 ya King James (James = Yakobo!) si uzao wa Enzi ya Mantiki wala si uzao wa jamii ya kidemokrasia. Ilizalishwa ya chini mmoja kati ya wafalme wa mwisho katika dunia hii ambaye maisha na utawala wake ulishawishiwa kwa kiasi kikubwa sana na imani yake katika Bwana Yesu Kristo.

Kila mahala ambapo uharibifu umo katika nyaraka za ERROR basi KJB inatofautiana na chachu hiyo na inadhihirisha kweli. Hakuna nyaraka zinazoakisi maeneo / aya za KJB ambazo zinatofautiana na TR kwa sabau maneno yaliyomo katika KJB hayajaonekana katika nyaraka zozote hapa duniani, na hakuna chanzo chochote hapa duniani ambacho kimethibitishwa kuwa ndiyo chimbuko la Biblia ya King James. Kwa sababu KJB si matokeo ya uhakiki wa juu wa nyaraka ambao mzizi wake ni sayansi ya ki-utu (humanistic science) ya Kiyunani, na kwa sababu KJB si tafsiri aminifu ya nyaraka zozote zilizoko hapa duniani, basi wanazuoni wa Kikristo wanaojiita Enlightened wana mtazamo kwamba KJB ni tafsiri iliyo chini ya viwango.

Kwa sababu ya makosa / dosari zilizothibitishwa katika familia zote za nyaraka za ERROR, na kwa sababu dosari / makosa hayo yamo katika tafsiri zote za Biblia za kisasa, hakuna mtu yeyote hapa duniani ambaye amefanya uchunguzi wa suala hili ambaye anaamini tafsiri yoyote ya kisasa ya Biblia au nyaraka za kale ni neno la Mungu kama alivyolifasili Yeye. Hawa wote si wapumbavu, wako sahihi.

Sababu pekee ya uwepo wa mabishano kuhusiana na tafsiri za Biblia ni hii Biblia ya King James. Nasema tena, kama AV1611 isingekuwapo basi kusingekuwa na mabishano kuhusu tafsiri za Biblia. Huu ni waraka pekee hapa duniani ambamo wanazuoni wameshindwa kupata makosa / dosari yoyote inayoweza kuthibitishwa. Huu ni waraka pekee wa Biblia hapa duniani ambao watu wa Mungu wanasimama imara na kusema kwamba [hili] ndilo neno la Mungu. Biblia ya King James ni ya pekee: hakuna kitu kingine hapa duniani ambacho ni kweli, kweli yote, na kweli tupu.

Kama KJB isingekuwako, wahubiri wote wasiokuwa na ufahamu na/au wasiokuwa na imani, pamoja na waumini wao wangekuwa sahihi katika kusema kwamba neno la Mungu halipo mahala popote hapa duniani.

Sasa unajua kwa nini waumini wa Biblia hawapotezi muda wao katika kamusi za Kiebrania na Kiyunani: Hakuna buku / juzuu la Kiebrania wala la Kiyunani lenye mamlaka juu ya neno hai la Mungu. Matumizi ya Kiebrania ni dalili halisi ya ujinga na ni dalili yamkini ya uasi.

Ukweli kwamba tafsiri zote za kisasa za Biblia, matoleo yote katika Kiebrania na Kiyunani ya nyaraka za ERROR zinakotoka Biblia hizo, visaidizi vyote vya walei vinavyotumika kuwasahihisha wanazuoni, na ukweli kwamba marejeo (references) yote ya wanazuoni yanayotumika na mabingwa katika nyanja hii yana hakimiliki hauna umuhimu wowote – mpaka unapotambua kwamba hii AV1611 imetoka kwa Mungu. Waraka wa Biblia ya King James haumilikiwi na mwanadamu yeyote. Sheria za hakimiliki za mwanadamu zinalinda na kutunza uharibifu wa tafsiri nyingine, lakini katika miaka 400 iliyopita Mungu pekee amelinda na kutunza usafi na upekee wa Biblia ya King James kwa sababu hii ni sheria Yake. Biblia ya King James ndiyo pekee ambayo haijatunzwa na hakimiliki za mwanadamu na sheria za mwanadamu.

Yeyote anayetumia tafsiri za kisasa hana ufahamu kamili wa suala la mamlaka.

 

Inawezekana umeng’amua kwamba nimetumia msemo “kwa ujumla” katika dondoo ya tatu hapo juu. Hii ni kwa sababu baadhi ya tafsiri zimezalishwa kwa malengo ya kukidhi mafundisho ya kanuni za madhehebu husika. Ebu tuitizame tafsiri inayoitwa New World Translation (Tafsiri ya Ulimwengu Mpya) inayotumiwa na Mashahidi wa Yehova kama mfano. Mashahidi wa Yehova, kama watu wengi wengine wanapojaribu “kuthibitisha” kwamba tafsiri nyingine zina dosari / makosa, hawaonyeshi makosa / dosari, wanaonyesha tofauti. Kwa mfano, wanadai kwamba King James Bible na tafsiri nyingine mara nyingi zimeandika LORD / BWANA mahala ambapo wanapaswa kuandika “Yehova”. Wanaonekana kwamba hawawezi kuelewa kuwa si makosa kumwita Mungu “LORD / BWANA” na pia kwa kusema kwa ujumla, “Lord” – hayo si makosa. Na kwa upande wa jina “Yehova”, KJB kwa usahihi kabisa inalirekodi hili kama mojawapo kati ya majina mengi ya Mungu. Hakuna tatizo na hakuna makosa / dosari.

 

Ile NWT / TUM (Tafsiri ya Ulimwengu Mpya), kama tafsiri zote za kisasa, ni uzao ulioharibika wa nyaraka za ERROR na una tunda lile lile ovu kama ilivyo katika tafsiri za kisasa. Lakini katika ari yao ya kimadhehebu ya kutaka kulitenganisha na kulipa hadhi ya kipekee moja kati ya majina mengi ya Mungu, hawa MJs wameifanya tafsiri yao kuwa yenye uharibifu zaidi. Tazama, kwa mfano, katika 1 Wafalme 22:5-8. Katika aya ya 5 mfalme wa Kikristo wa Yuda, Yehoshafati, anamtaka mfalme wa kipagani, Ahabu, kumwuliza Mungu wa kweli kitu gani cha kufanya. Ahabu na makuhani wake wa Baali hawakuwa wakimwabudu Mungu wa kweli, Yehova. (Nitapiga mstari chini ya maneno kwa msisitizo. Na kumbuka, “BWANA” ikiwa na herufi zake zote kubwa ni rejeo mahsusi kwa Mungu; “Bwana” ikiwa na ile B peke yake katika herufi kubwa inaweza kuwa rejeo kwa Mungu au kwa nafsi ingine.)

 

KJV 1 Kings 22:5 And Jehoshaphat said unto the king of Israel, Enquire, I pray thee, at the word of the LORD to day.

NWT 1 Kings 22:5 However, Jehoshaphat went on to say to the king of Israel: “Inquire, please, first of all the word of Jehovah.”

 

Mpaka hapo hakuna tatizo kwa sababu tunaona hati zote mbili zikimsimulia mfalme Yehoshafati akiomba mahususi kwa ajili ya kile Yehova atakachosema, lakini punde tu mabadiliko yatatokea.

 

KJV 1 Kings 22:6 Then the king of Israel gathered the prophets together, about four hundred men, and said unto them, Shall I go against Ramothgilead to battle, or shall I forbear? And they said, Go up; for the Lord shall deliver it into the hand of the king.

NWT 1 Kings 22:6 So the king of Israel collected the prophets together, about four hundred men, and said to them: “Shall I go against Ramoth-gilead in war, or shall I refrain?” And they began to say: “Go up, and Jehovah will give it into the king’s hand.”

TUM 1 Wafa. 22:6 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawakusanya pamoja manabii, wanaume wapatao 400, akawauliza: “Je, niende kupigana vita dhidi ya Ramothi-gileadi, au nisiende?” Wakasema: “Panda uende, na Yehova atalitia jiji hilo mikononi mwako.”

 

Dhahiri kabisa, makuhani wa kipagani hawana mawasiliano na Mungu wa kweli, na KJB kwa usahihi kabisa inatumia kivumishi [cha] jenasi “Bwana” kuonyesha ukweli kwamba mungu wao siyo BWANA. Tazama sasa hawa wakalimani wa Mashahidi wa Yehova, katika ari yao ya kubadilisha kila “LORD / BWANA” iwe “Yehova”, hawakuutizama muktadha kwa makini na wakafanya kosa la kumfanya Baali achukue nafasi ya Yehova.

 

KJV 1 Kings 22:7 And Jehoshaphat said, Is there not here a prophet of the LORD besides, that we might enquire of him?

NWT 1 Kings 22:7 But Jehoshaphat said: “Is there not here a prophet of Jehovah still? Then let us inquire through him.”

TUM 1 Wafa. 22:7 Kisha Yehoshafati akasema: “Je, hakuna nabii wa Yehova mahali hapa? Acheni tumuulize yeye pia.”

Aya zote hizi mbili zinasema kitu kile kile, lakini aya ya TUM inamwonyesha Yehoshafati, ambaye ameambiwa sasa hivi katika aya iliyopita kile alichokisema “Yehova”, anarudia tena kuuliza nini kitasemwa na Yehova! Biblia ya King James, kwa usahihi kabisa inamwonyesha Yehoshafati, ambaye ombi lake katika aya ya 5 lilipuuzwa pale alipoambiwa kitu “Bwana” wa kipagani alichosema katika aya ya 6, anasisitiza kwamba Mungu wa kweli aulizwe.

 

KJV 1 Kings 22:8 And the king of Israel said unto Jehoshaphat, There is yet one man, Micaiah the son of Imlah, by whom we may enquire of the LORD: but I hate him; for he doth not prophesy good concerning me, but evil. And Jehoshaphat said, Let not the king say so.

NWT 1 Kings 22:8 At that the king of Israel said to Jehoshaphat: “There is still one man through whom to inquire of Jehovah; but I myself certainly hate him, for he does not prophesy good things concerning me but bad – Micaiah the son of Imlah.” However, Jehoshaphat said: “Do not let the king say a thing like that.”

 

Aya zote hizi mbili zinasema kitu kile kile, lakini ili kuwa na msimamo mmoja na kuendelea katika muktadha ule ule NWT / TUM ilipaswa kutuonyesha mfalme Ahab akiguta, “Nini, Yehoshafati, una kichaa au umekuwa kiziwi? Tumekwambia sasa hivi alichosema Yehova! Unataka kutusikia mara ngapi tukisema hili?” Ni baada ya Ahabu kumleta nabii wa kweli ndipo wale wa uwongo wakaanza kudai kujua kile kilichosemwa na BWANA wa kweli.

 

Sasa, nataka kuwaonyesha kitu fulani ninyi wahubiri mnaotumia tafsiri za kisasa. Mlifundishwa kusema mambo kama haya kwa makundi yenu: “Sisi hatutazami sana asilimia ndogo ya dosari / makosa na migongano katika nyaraka za Kiebrania na Kiyunani. Tuna furaha sana kwamba neema ya Mungu imezitunza nyaraka hizi na kuhakikisha makosa / dosari na migongano hii iko katika kiwango cha chini sana, na sisi tunatazama zaidi kiwango cha kushangaza cha juu cha makubaliano pale tunapolinganisha nyaraka mbali mbali za Kiebrania na Kiyunani. Kanuni zetu zote kuu za msingi zinanyumbulishwa kwa usawa na nyaraka zote hizi za kale.” Usiseme tena mambo kama haya, ndugu yangu, kwa sababu kauli hii haina msingi katika kitu chochote kinachosemwa na Biblia kuhusu neno la Mungu (!) na kiuhalisia inapuuza kila kitu kinachosemwa na Biblia (!) kuhusu neno la Mungu juu ya utunzaji wake na usafi wake. Pia hautotaka waumini wa kanisa lako wakukamate katika unafiki. Kwa mfano, ukisema kwamba Daudi alimwua Goliati (2 Sam. 21:19!), au kwamba tamko la imani linatakiwa kabla ya ubatizo (Matendo 8:37!), au ukimnukuu Kristo akisema, “Yeye asiye na dhambi kati yenu na arushe jiwe la kwanza (Yoh. 8:7!), unafundisha kinafiki kanuni ambazo hazimo katika nyaraka na Biblia yako ambayo ina “kiwango cha juu cha kushangaza cha makubaliano katika nyaraka” hizi za kale. Je, hujawahi kukaa chini na kutafakari? Hujawahi kusoma marejeo / tanbihi pamoja na notisi za kuzingatia juu ya aya zinazokosekana katika Biblia yako? Ulisoma?! Kwa hiyo siku zote hizi umekuwa ukifundisha kanuni ambazo hazimo katika “nyaraka za kale na za kuaminika zaidi”! Hapo sasa, ndugu yangu, licha ya tabia yako njema, licha ya “msimamo wako imara juu ya familia” na mahubiri yako yenye kugusa na kutia moyo, wewe ni kaburi lililopakwa rangi nyeupe, umejaa porojo. Ninakupa onyo, uikimbie ghadhabu inayokuja kwa kutubu. Nenda ukajinunulie Biblia pekee ambayo inafundisha hayo yote yaliyotajwa hapo juu, ukaisome, ukajifundishe kuhusu imani ni nini, uyazingatie mafundisho hayo katika maisha yako. Utakapofanya hayo ndipo utakuwa umefuzu kulichunga kundi la kondoo wa Mungu. Kwa nini mimi nimelileta neno “imani” hapa? Mimi sijalileta neno hili – wewe umelileta neno hili pale ulipodai kwamba tunaweza kuziamini kanuni kwa sababu sehemu kubwa ya nyaraka tofauti inakubaliana kuhusu kanuni hizo! Nani alikufundisha kwamba makubaliano kati ya waongo kadhaa kwa namna fulani yanaunda uaminifu? Kwa nini unataka kujenga imani yako juu ya uharibifu ulio dhahiri? Umekosa mwamba imara wa neno la Mungu kama msingi wako na hii imepelekea uwe na migongano, kutobarikiwa na aibu katika mafundisho yako. Na migongano katika misimamo yako inathibitisha kwamba hujajifunza kiasi cha kutosha kuwa na mpangilio mwanana katika Ukristo wako (kitu ambacho kinaonyesha wewe hujapevuka kiasi cha kutosha hata uanze kuhubiri), au umekuwa kaburi lililopakwa rangi nyeupe kama yule jamaa wa Matthayo sura ya 7. Jichunguze na ujipange upya, ndugu yangu.

 

ENZI MBALIMBALI ZA NENO LA MUNGU

 

Haya, somo la tafsiri za Biblia limekwisha. Sasa nitakwambia kuhusu neno la Mungu katika enzi mbalimbali ambazo nimeziunganisha kutoka katika mapokeo yasiyoaminika ya historia (nje ya Biblia), kutoka katika Biblia yenyewe (ambayo inaaminika), na kutoka kile nilichojifunza kuhusu Mfalme wangu na jinsi Anavyotenda kazi yake. Kama utakavyoona, ninaiamini na kuitumia kanuni inayofundishwa katika Mhubiri 1:9,10 na ninategemea sana matumizi ya Mungu ya ruwaza.

 

KIPINDI CHA AGANO LA KALE:

Adamu hadi Musa: Hakukuwa na Biblia. Mungu alitembea bustanini na Adamu, akasema na Abrahamu, akapokea na kujibu maswali kutoka kwa Abrahamu. Mambo ya aina hii hayatokei tena leo, na yanaonyesha kwamba Mungu – kwa sababu ni Mchungaji Mwema – aliwaongoza watu wake kwa jinsi inavyofaa wakati neno Lake halijaandikwa bado.

 

Musa hadi Malaki: Mungu aliliandika Agano lote la Kale katika kipindi hiki cha miaka takriban 1600. Kipindi hiki kilianza na Ayubu takriban miaka 2000 kabla ya Ujio wa Kwanza wa Bwana wetu, na kuendelea hadi kanoni ilipofungwa, ikahitimishwa na kutimilishwa na Malaki takriban miaka 400 kabla ya Ujio wa Kwanza. Mungu alitumia lugha gani katika kuandika Agano la Kale? Watu wengi watakujibu Kiebrania, Kiarami, na Kikaldayo. Jibu hili si sahihi – kwa namna fulani. Agano la Kale liliandikwa ili kufanikisha Agizo la Kale la Mungu. Ili kufanya hili, ililazimu Agano hili liwe katika lugha ya watu wa Mungu. Lugha hii ni Kiebrania kwa sababu Waebrania ndio watu pekee ambao Mungu alikuwa akijaribu kuwasiliana nao na kuwafikia wakati huo.

 

Kuna vipindi, wakati wa miaka ile 1500 ya kuandika Agano la Kale, neno la Mungu lilipotea kwa muda (soma 2 Wafa. 22:5-13). Kundi la Mungu liliwezaje kuishi bila neno la Mungu? Ninaamini kwamba Mchungaji Mwema aliwalea watu wake wakati huo katika njia stahiki. Biblia inasema njia zake zilihusisha kuwatumia manabii na miujiza, lakini njia zote hizi (labda na nyingine tusizozijua) ni mambo ambayo si lazima kwetu kuyafahamu.

 

Vipi kuhusu watu katika sehemu nyingine za dunia ambao hawakuijua lugha ya watu wa Mungu na ya Kitabu Chake – Kiebrania? Hawa walikuwa mbwa ambao Mungu hakujihusisha nao (Zab. 22:16; Matt. 10:1,5-7; 15:22-27; Marko 7:24-28; Wafi. 3:2; Ufu. 22:15) kwa sababu Agizo Kuu lilikuwa halijachukua nafasi ya Agizo la Kale. Kama malkia wa Sheba, au “watu wenye hekima” kutoka mashariki, au mtu yeyote wakitaka kusoma Biblia basi walilazimika kuisoma katika Kiebrania au kupata tafsiri ya Biblia iliyotoka katika Kiebrania.

 

Malaki hadi Kristo Mwana-kondoo: Hiki ndicho kinachoitwa “kipindi cha ukimya katika Agano la Kale” kati ya kukamilishwa kwa kanoni ya Agano la Kale (Malaki) na mwanzo wa Agano Jipya.

Kilikuwa kipindi cha “ukimya” kwa sababu Mungu hakuwa tena akiwasiliana na watu wake moja kwa moja, wala kwa njia ya manabii na wala hawakuiona miujiza Yake. Kwa nini? Kwa sababu mambo hayo hayakuwa na uhitaji tena kwani Maandiko ya Agano la Kale yalikuwa yamekamilika. Mungu sasa alikuwa akienenda “kwa Kitabu” katika mawasiliano na watu Wake. Kwa masikitiko makubwa kabisa, alipokuja katika Ujio wa Kwanza, akakuta watu wake hawajafanya kazi nzuri ya kujifunza, kuamini, na kuyatenda Maandiko Yake.

 

 

KIPINDI CHA AGANO JIPYA:

Kristo hadi Mfalme James (mfalme Yakobo): Mungu alikuwa akifanya kazi ya kuliandika Agano Jipya katika kipindi hiki cha takriban miaka 1,600. Kipindi hiki kilianza takriban miaka 2,000 kabla ya Ujio wake wa Pili na kikadumu mpaka kanoni ikafungwa, ikahitimishwa, ikatimilishwa na kuwa Biblia Iliyoidhinishwa ya Mfalme James (Yakobo) ya mwaka 1611, takriban miaka 400 kabla ya Ujio wa Pili. Mungu alitumia lugha gani kwa ajili ya Agano Jipya? Watu wengi watajibu Kiyunani. Jibu hili si sahihi – kwa namna fulani. Agano Jipya liliundwa ili kufanikisha Agizo Kuu la Mungu. Ili kufanya hili, Agano hili lilipaswa kuandikwa katika lugha ya watu wa Mungu. Agizo Kuu sasa likayafanya mataifa yote ya dunia yafikiwe na injili. Hii ilimaanisha kwamba Mchungaji Mwema, ili awachunge watu Wake kwa usahihi (dunia nzima) chini ya Agizo Lake Kuu, alipaswa kulitoa neno Lake katika lugha iliyoenea katika pande zote za ulimwengu / dunia.

 

Kwa sababu Waebrania walimkataa Yeye, naye Bwana akawakataa wao, na kama ishara ya uasi huu, Bwana akaifanya lugha ya wale waliomkataa kuwa lugha iliyokufa kama vile wale waliomkataa walivyokuwa wafu bila Yeye. Hii ndiyo maana Kiebrania cha Agano la Kale ni lugha iliyokufa. Mwokozi aliyefufuka akawafanya wanafunzi wake waliokuwa wazungmzaji wa Kiebrania, waandike Agano Lake Jipya katika lugha ya Kiyunani kwa sababu hii ilikuwa sasa lugha ya watu Wake. Yeye habadiliki na historia hujirudia kama Anavyosema (Mhu. 1:9,10).

 

Kiyunani kilikuwa ndiyo lugha inayozungumzwa duniani kote tangu utawala wa Aleksanda Mkuu. Kwa mfano pale Hanibal wa Karthago aliposafiri katika rasi ya Iberia (ambayo sasa ni Hispania na Ureno), akipanda na kushuka milima ya Alps na kuingia Italia wakati wa uvamizi wake mashuhuri wa kijeshi, alikuwa na wakalimani wawili wa Kiyunani ili aweze kuwasiliana na mataifa mbali mbali akiwa njiani – mataifa ambayo lugha yao asilia si Kiyunani. Kwa kuwa Kiyunani kilikuwa lugha ya kimataifa kwa muda mrefu kiasi hicho, je, haikumpasa Mungu kuliandika Agano lake jipya katika lugha hiyo badala ya Kiebrania ili awafikie watu wengi zaidi? Hapana, kwa sababu ya Agizo la Kale (Matt. 10:5-7) Mungu hakutaka kuwafikia watu wote. Kama watu wa Mataifa walitaka Biblia ya Kiyunani itengenezwe kwa kuitafsiri ile ya Kiebrania, hamna shida; lakini walipaswa kukukmbuka kwamba Biblia waliyo nayo ni tafsiri tu. Maandiko ya Kiebrania pekee ndiyo yalikuwa Biblia yenye mamlaka ya neno la Mungu.

 

Ndiyo, Agano Jipya liliandikwa na Waebrania katika lugha ya Kiyunani kwa sababu Kiyunani kilikuwa ndiyo lugha ya watu wa Mungu chini ya Agizo Kuu. Na Biblia inasema neno la Mungu lilifika dunia nzima (War. 10:18; Wakol. 1:6). Lakini mataifa mengi waliikataa Injili. Waarabu wakaenda zo na Muhammad, Wachina wakawa na Buddha na Shing Moo, na Wahispania, Waitalia, na Wafaransa wakang’ang’ana na “Wakili wa Kristu”. Ni kundi moja pekee la watu likamgeukia Mungu wa Biblia – wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza. Na historia ikaanza kujirudia tena.

 

Wakati ulienda, na Kanisa Katoliki la Rumi likaja kuwa nguvu kuu ya kimataifa “ya Kikristo”, kitu ambacho kilikaribia kukifanya Kilatini kuwa lugha ya kimataifa ya dunia. Lakini kanisa hili ni aina ya Babeli Mkuu (Ukristo wa kimwili, Shetani akijibainisha katika mwili), Mungu akakifanya Kilatini kuwa lugha iliyokufa ili watu Wake wasije wakajichanganya na kufikiri tafsiri za Biblia za Kikatoliki zilizo katika lugha ya Kilatini ndilo neno Lake. Biblia ya King James ilishushwa na Mungu kwa sababu biashara ya tafsiri za Biblia (ambayo ililazimu kuwepo kwa sababu hakukuwa na nyaraka asilia wala nakala zake) iliingiwa na utapeli, vurugu na uharibifu wa nyaraka husika (mkono wa Shetani haukuwa mbali na hali hii). Kwa maneno mengine, kama ambavyo neno la Mungu lilipotea kwa kipindi fulani wakati wa Agano la Kale, vivyo hivyo Neno la Mungu lilipotea kwa muda wakati wa Agano Jipya.

 

Kama nyaraka za uharibifu za ERROR ni dalili / ishara ya kupotea kwa neno la Mungu, ni vipi basi kundi la Mungu (ambalo lipo wakati wote katika kila taifa – War. 11:3-5) liliweza kuishi kabla hajaifunua Biblia ya King James? Ninaamini yule Mchungaji Mwema aliwalea watu Wake kwa njia mwafaka: Biblia inasema njia Zake zilihusisha mitume, wanafunzi, na miujiza, lakini utondoti wa njia hizi si jambo la lazima kwetu kuufahamu. Hata hivyo, kwa kuwa Biblia ya King James haina makosa / dosari, tunajua hii ndiyo jinsi Mchungaji wetu anavyotuongoza leo hii.

 

Katika Biblia ya King James, Mungu kwa mara ingine tena akalifunua neno Lake katika lugha ya watu Wake. Lakini Alifanya zaidi ya hayo. Kwa kuwa mataifa ya ulimwengu yalimkataa, Mungu alitoa ishara ya kuifanya historia ijirudie tena kwa kuifanya lugha hai ya ulimwengu ya Kiyunani cha Agano Jipya iwe mfu. Na kwa kuwa Agizo Kuu bado lipo akaifanya lugha mpya ya Kiingereza kuwa lugha hai ya ulimwengu mzima, na Akaifanya Kiingereza si tu kuwa lugha ya Agano Jipya, bali kuwa lugha ya Biblia yote – yaani Maagano yote mawili – ili ulimwengu wote upate fursa ya kujifunza “Kiingereza asilia” kilichoko katika Biblia Yake aliyoiidhinisha ya King James ya mwaka 1611 – waraka / hati pekee isiyo na makosa / dosari ya Biblia hapa duniani. Katika hizi zama za Agizo Kuu, ni kwa kiasi gani Mungu ameifanya lugha ya Biblia kuwa lugha “hai ya ulimwengu wote”? Chukua China kama mfano kwa kuwa huko ni mbali sana kutoka nchi zinazozungumza Kiingereza – kijiografia na kiutamaduni: Watu wengi wanazungumza Kiingereza nchini China kuliko raia wote wa nchi ya Marekani. Tafiti mwenyewe ujiridhishe na ukweli huu.

 

Na hivi ndivyo, katika mwaka 1611, takriban miaka 1600 tangu Agano Jipya lilipoanza, na takriban miaka 400 kabla ya Ujio wa Pili, kanoni ikafungwa. Na hii, pamoja na uharibifu / uozo wa nyaraka za ERROR, ndiyo sababu tafsiri zote za kisasa za Biblia zinapaswa zifanywe kwa urahisi kabisa kutoka katika Biblia ya Kiingereza iliyoidhinishwa ya King James na kamati za kutafsiri zinazoundwa na watu wanaokifahamu Kiingereza kwa kiasi cha kutosha kuweza kupambanua maana za maneno kama thou na thee yaliyomo katika neno la Mungu. Badala yake, Wakristo wanaenenda kimwili wakiwa na silaha yao ya Reason / Mantiki badala ya imani, wanarudi katika lugha zilizokufa ambazo Mungu alizilaani katika nyaraka haribifu za ERROR kwa matumaini kwamba kwa njia ya sayansi watalipata neno lililo hai!

 

Kutoka Mfalme James (Yakobo) hadi Kristo Mfalme: Hiki ndicho kipindi kinachoitwa miaka mia nne ya ukimya katika Agano Jipya kati ya kukamilishwa kwa kanoni (KJV) na Ujio wa Pili. Ni kipindi cha “ukimya” kwa sababu Mungu hana tena uhitaji wa kutuongoza kwa njia za zamani kama kuzungumza nasi moja kwa moja, kwa njia ya manabii Wake, na kwa kutuonyehsa miujiza Yake. Kwa nini? Kwa sababu vitu hivyo havina uhitaji tena kwani Maandiko yamekamilika. Mungu sasa “anatumia Kitabu”. Kwa masikitiko makubwa kabisa, Atakapokuja Mara ya Pili atawakuta watu Wake hawajafanya kazi nzuri ya kujifunza, kuliamini, na kulitenda neno Lake.

 

Mungu alimchagua mfalme mwenye Jina lake, James / Yakobo, kukamilisha kanoni ya Biblia Yake yote, kwa mamlaka [ya mfalme]. Katika KJB Mungu alifanya mambo matano: 1. Aliweka Jina Lake juu Kitabu Chake. 2. Alilikamilisha katika namna kamili / halisi aliyoitaka Yeye. 3. Kwa kuwa Amejiwajibisha kwa Agizo Kuu, Mungu amekiondoa Kiyunani na kuweka Kiingereza mahala pake kama lugha ya dunia yote. 4. Amekibadilisha Kiebrania cha Agano la Kale na kuwa Kiingereza ili ulimwengu wote usome neno Lake. 5. Amelikamilisha Agano Jipya katika Kiingereza ili dunia nzima iweze kulisoma neno Lake.

 

Wakati AV1611 inatoka, Kiingereza kilikuwa lugha changa. Ili aweze kulieneza neno Lake katika ulimwengu wote kulingana na matakwa ya Agizo lake Kuu, Mungu akaufanya ufalme mdogo (kwa wakati huo) wa Great Britain uenee na kuwa ufalme mkuu wa kidunia katika muda mfupi sana. Kila mahala ufalme ulikoenda na Biblia ya King James ilienda nao. Walowezi wa mwanzoni waliounda dola 13 za Marekani walienda huko na Biblia zao za AV1611. Magari yao ya farasi yalipoanza kuelekea magharibi mwa dola / makoloni yale ya Marekani kimoja kati ya vitabu vichache vilivyokuwamo ndani ya magari hayo ni AV1611. Hakuna mtu aliyekuwa na kamusi. Kwa hakika, AV1611 ilipotoka, Kiingereza kilikuwa lugha mpya sana kiasi kwamba ilichukua miaka takriban 100 kwa kamusi kuingia katika jamii. Hivyo Biblia ya King James ndiyo iliyoweka kiwango cha tahajia na sarufi. Wakristo walilelewa wakiongea “Kiingereza cha Mfalme”. NB: Hapa kwetu Afrika ukoloni ina sifa mbaya, lakini yumkini Mungu aliutumia ukoloni huu katika kutuletea neno Lake. Fanya utafiti wako mwenyewe kujihakikishia hili.

 

Baadaye wanazuoni wakafanya kosa la kupandikiza kanuni za sarufi za lugha iliyokufa ya Kilatini zilizokuwa zikitumika na Kanisa katoliki la Roma kwenye lugha iliyo hai ya Kiingereza. Na mara Kiingereza rasmi cha neno la Mungu kikawa si sahihi ki-sarufi. Na – hapo umekisia sahihi – wanazuoni “wasomi” wakaanza kusema “makosa” ya sarufi katika Biblia yalithibitisha kwamba hilo si neno tumilifu la Mungu. Leo, tunapozungumza na Wakristo wanaonukuu Maandiko, wale walio wa kundi Lake na wanaoijua sauti Yake, bado wanaweza kumaizi kwa urahisi kabisa kama Kiingereza hai cha Mfalme kinatumika au kama tafsiri ya lugha zilizokufa inatumika.

Mimi na mke wangu tunapotaka kuwalisha kondoo wetu tunaita, “Sheep!” Kule vilimani vichwa vyao vinasimama ghafla na kwa mpigo, halafu wote wanakuja mbio. Wageni wetu wanapojaribu kuita, “Sheep!” hakuna kinachotokea. Je, yawezekana kwamba moja kati ya namna ya kwamba Kundi la Mungu litaweza kumaizi kwamba Antichrist (Mpingakristo) na wale makristo wa uwongo si Mfalme wa kweli, itakuwa ya kwamba wakati hawa walaghai watakaponukuu Biblia hawatatumia Kiingereza cha Mfalme?

 

Mara nyingi mimi hutumia ‘concordance’ ili kutafuta aya katika Biblia na kufuata alama za barabara ninayopita kama Mkristo. Lakini kamwe siitumii ile section ya lugha zilizokufa kule mwishoni [mwa concordance] ambayo inanyumbulisha maana za maneno zinatakiwa kuwa nini. Nilishapata utangulizi wa ubaya wa vile visaidizi vya walei katika lugha zilizokufa nilipokuwa Mkristo mchanga. Nilishajifunza kiasi cha kutosha na nikaacha kuitumia RSV niliyokuwa nayo pale mwanzoni mara baada ya kuokolewa na Bwana, na sasa nikawa natumia Biblia ya King James. Na pia, kama Wakristo wengi wachanga wanaogundua kwamba hakuna makosa / dosari wala migongano katika Biblia ya King James, nikaanza kuyashughulikia matatizo yanayoonekana kwa juujuu tu katika Biblia hii. Wakati fulani mwamba wangu wa maudhi ulikuwa ni mgongano wa juujuu kati ya turtledoves katika Luka / Luke 2:24 na Levi. / Walawi 12:6, na turtles wa Levi. / Walawi 12:8. Sikuweza kuona jinsi ndege na mnyama mtambaazi mwenye koa wanaweza kuwa ni kitu kilekile. Nilihitaji msaada. Imani yangu changa ilikuwa ikishambuliwa na Reason/Mantiki yangu iliyopevuka. Nikaenda kwa pastor wangu ili nipate msaada. Akachukua kisaidizi cha mlei, akakipekua kwa dakika kadhaa, na akasema kwamba ile turtles ya Levi. 12:8 katika Biblia ya King James ni kosa; neno la Kiebrania lililotumika pale maana yake ni turtledoves. Akanieleza kwamba hii KJV tunayoitumia sisi wote ni tafsiri tu, tena ni nzuri sana, lakini wanadamu hufanya makosa na hii ndiyo sababu kosa / dosari hii imo katika Biblia ya King James.

 

Nikaenda nyumbani. Ghafla tu KJB yangu ikawa haina tofauti na ile RSV ya zamani. Inaweza kuwa na makosa / dosari chache zaidi ya RSV lakini hili ni suala la kiasi tu – bado ilikuwa na uharibifu (Waga. 5:9; Hag. 2:11-24). Nikajiuliza kwa nini watu waliridhika kubeba kitabu ambacho walikuwa wanakisifia mdomoni tu wakati walikuwa na vyombo vyenye mamlaka halisi katika visaidizi vya walei. Kwa nini basi, sisi sote tusitumie visaidizi vya walei, au, bora zaidi, tusitumie tu zile Biblia zilizotokana na Kiebrania na Kiyunani cha kale ambazo zinaendana na visaidizi hivyo? Nilikuwa na mengi ya kujifunza, na njia ndefu sana ya kwenda. Lakini Mchungaji Mwema ana njia zake za kuwaongoza wale wanaompenda na wanaoutafuta ukweli Wake: nikaamua kufanya kitu ambacho Wakristo wengi hawapendi kukifanya: kutizama maana za maneno katika kamusi ya Kiingereza. Pale katika neno turtle, nikaona imeandikwa, “Archaic (maana yake matumizi ya kale ya neno hili), a turtledove!!” NB: Kamusi ile haikuwa sahihi saana iliposema archaic: Kuna baadhi ya hua ambao hata leo hii wanaitwa na wataalamu wa ndege kama “the turtle group”.

 

Kwenda kutafuta msaada katika lugha zilizokufa hakukunisaidia kutatua tatizo langu, kwani tatizo langu lilikuwa mimi sikuwa fundi wa Kiingereza ingawa nimesema Kiingereza tangu nizaliwe! Hata hivyo, simaanishi kwamba kamusi ya Kiingereza itimike kama mamlaka ya kuisahihisha Biblia. Kila mahala ambapo kamusi inatofautiana na Biblia, basi kamusi hiyo ina makosa. Tangu wakati huo nimejifunza kwamba ni kufuru kuliweka neno la Mungu chini ya mamlaka ya usahihishaji ya nyaraka za ERROR zilizoharibika, zilizolaaniwa za lugha zilizokufa pamoja na visaidizi vya walei vinavyoendana nazo.

 

Watu wanapenda kusema kuhusu Biblia: “Mimi nakiamini Kitabu hiki kutoka jalada la mbele mpaka jalada la nyuma, na ninaliamini hata jalada lenyewe!” Mimi mwenyewe husema hivyo pia. Lakini hapa sizungumzii yale maandiko “Biblia Takatifu” yaliyoko katika jalada la mbele ambayo watu wanazungumzia. Mimi nazungumzia kichwa chote cha Biblia hii: AUTHORIZED 1611 KING JAMES BIBLE yaani Biblia Iliyoidhinishwa ya mwaka 1611 ya King James. Ebu tuone maana yangu ni nini.

 

AUTHORIZED / ILIYOIDHINISHWA: Kwa sababu suala [muhimu] mi mamlaka, Mungu alitaka kuitambulisha na kuihalalisha Biblia ipi kati ya tafsiri nyingi katika hii enzi ya Agano Jipya iliyozalishwa chini ya mkono Wake wa uongozi. Hivyo akahakikisha neno Lake halina hakimiliki kama zilivyo tafsiri zilizozalishwa na wanadamu. Ebu tuitizame hakimiliki ya hii New King James Version kama mfano:

“All rights reserved. No part of this publication may be reproduced in any form or by any means without the publisher’s prior written permission.”

Yaani: “Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote ya chapisho hili katika jinsi au mfumo wowote bila ruksa iliyoandikwa na mchapishaji.” Mungu kamwe hataliweka neno Lake chini ya vifungo vya aina hii.

 

1611: KJB ilitoka mwaka 1611 kwa sababu:

1) Ilifunga kanoni takriban miaka 1611 baada ya uandishi wa Agano Jipya kuanza

2) Hii ilikuwa takriban miaka 400 kabla ya Ujio wa Pili.

3) Ilifuata ile ruwaza / sampuli ambayo Mungu aliiweka katika mpangilio wa Agano la Kale na katika kitabu cha Malaki.

 

KING: Hii ni haki na cheo cha Mungu. Maana yake ni mamlaka kamili. Mungu alihakikisha Kitabu Chake kinazalishwa na raia wa ufalme Wake, Mfalme Mkristo James I wa Great Britain. Ilipangwa kwamba Mungu aliamua kuzalisha neno Lake chini ya mfalme na si katika mfumo wa utawala wa kidemokrasia.

 

JAMES / YAKOBO: Ukiwatazama kwa juujuu, Mfalme James na mwanawe, Mfalme Charles ni mifano ya Yesu Kristo. Mfalme James alitoka katika ufalme wake huko kaskazini, Scotland, akaja hadi Uingereza, ili kuziunganisha falme hizo mbili chini ya jina moja, na kujenga jamii ya Kikristo chini ya mfalme mmoja. Mama yake mfalme James aliitwa Maria, na mwana wake wa pekee [wa kiume] alihukumiwa kifo na watu wake mwenyewe kutokana na mchakato wa kidemokrasia katika mashitaka bandia, na kuuwawa. Mwana huyu wa mfalme James alikataa kushiriki katika mashitaka yale na akaenda katika kifo chake kama mwanakondoo. Bwana wetu anapenda mifano, sivyo?

 

Lakini ukitizama kwa undani zaidi utaona kwamba ni kawaida kwa watu kuweka majina yao katika majalada ya vitabu vyao, na Mungu wetu amefanya vivyo hivyo. Yeye ana majina mengi. Moja kati ya majina Yake ni Yakobo (Zab. 24:6). Yakobo na James ni jina lile lile. Ni rahisi tu: kama ambavyo Kristo ni neno la Kiyunani lililotafsiriwa kutoka katika neno la Kiebrania Messiah, vivyo hivyo James ni neno la Kiyunani lililotafsiriwa kutoka katika jina la Kiebrania Yakobo. Hii ndiyo sababu Wayahudi wengi wanawapa watoto wao jina James, kutokana na jina la Kiebrania Yakobo. Na hii ndiyo maana pia aina ya Kiingereza kilichokuwa kikizungumzwa wakati wa Mfalme James na Malkia Elizabeti imepewa jina “Jacobethan English” na pia ndiyo maana mitindo ya ujenzi ya wakati ule imepewa jina “Jacobethan architecture”. Na ndiyo maana mawakili au wapenzi wa Mfalme James II wanaitwa Jacobites.

 

Hivyo, Mungu anaitwa Messiah na Kristo katika Biblia Yake ya King James kwa sababu ni nomino moja, Naye anaitwa Yakobo na James katika Biblia Yake ya King James kwa sababu hili ni jina moja.

 

By the way, haiwezekani kuthibitisha kwamba Mfalme wa [kidunia wa] Uingereza James ndiye aliyeidhinisha hii AV1611: Majengo ya Whitehall pale London yaliungua moto mwaka 1618 na nyaraka zote kutoka mwaka 1600 hadi 1613 ziliteketea. Hivyo hakuna ithibati kwamba mamlaka ya kidunia ndiyo yaliyotoa amri ya kuidhinisha AV1611 kuwa ni neno lenye mamlaka la Mungu. Mungu wetu ni wa kustaajabisha katika uweza Wake wa kupanga mambo kwa utondoti mkuu, sivyo? Haswa mambo hayo yanapohusiana na mamlaka Yake na neno Lake.

 

Mpaka hii AV1611 ilipozalishwa, hakukuwa na tafsiri yoyote ile – kabla na baada yake – ambayo ilikuwa na iliaminika kuwa ni neno lililofunuliwa la Mungu; matoleo yale yasiyoidhinishwa yalikuwa ni tafsiri tu zenye makosa / dosari nyingi. Lakini watu walipoanza kulinganisha maandiko ya Biblia hii ya King James na maandiko ya matoleo mengine – pia na nyaraka za Kiebrania na za Kiyunani – na kumaizi kwamba ni KJB pekee ndiyo haikuwa na kosa / dosari, polepole watu wakaanza kuitambua KJB kuwa ni waraka pekee hapa duniani ambao ulikidhi vigezo vya Mungu vya neno Lake takatifu, lililofunuliwa, la uhakika. Wakristo walianza kuandika kuhusu sifa hizi za AV1611 tangu miaka ya mwishoni ya 1700. Ni nyaraka / hati asilia na hii AV1611 pekee ndizo zimekubalika na watakatifu wa Mungu kuwa ni Maandiko Matakatifu. Ilipofika miaka ya 1950 ndipo uhakiki wa maandiko “wa kisayansi” ukaanza kuchapisha kwa kasi tafsiri za Biblia na Wakristo wengi wakaanza kuyapuuza maneno katika Biblia yanayolifasili neno la Mungu, na kupuuza ile hali ya kutokuwa na kosa / dosari ya maandiko ya KJB na kuacha Reason / Mantiki iwashawishi kwamba neno la kweli la Mungu halipo. Ujinga na mapokeo yao vikasababisha wakubali, bila kuuliza na kutafiti, nyaraka za ERROR kuwa ni aina fulani ya “Maandiko” yaliyoharibika – ingawa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na Maandiko!

 

Tunajua neno la Mungu linaitwa mkate, na tunajua tunatakiwa kula neo la Mungu (mkate). Kula mkate uliotiwa chachu kutatutia upofu na kulemaza mwendo wetu wa Kikristo. Ukiichanganya dhana hiyo pamoja na Waru. 12:1 na halafu uitumie katika Malaki 1:7,8,12 na utaona kwamba tuna matatizo yanayofanana na yale yaliyowasibu Wakristo wa siku za Malaki. Kanuni zetu zimetofautiana kabisa na kweli ya Mungu kiasi kwamba Mal. 2:17 inatuhusu sisi katika siku hizi. Na kama kitabu cha Malaki hakikulifunga Agano la Kale kwa maneno ya tahadhari na makemeo kabla ya Ujio wa Kwanza, na kama Biblia ya King James ni kifanani cha Agano Jipya/Ujio wa Pili, basi yaweza kuwa kuna maana fulani kwamba Bwana aliizalisha Biblia ya King James kwa ajili ya wale wanaoiunganisha na jina Lake (Mal. 3:16), ambalo ni Mfalme Yakobo (Mal. 1:14; 2:12). Mwisho, kwa kuwa umaizi / utambuzi unahusisha kuyachambua maneno yaliyofunuliwa ya Mungu (1 Wakor. 2:13,14; Yoh. 6:63; Isa. 28:9,10; Mal. 3:18), na Mungu aliwakemea watu Wake katika Ujio Wake wa Kwanza kwa kutoamini kila neno Lake lililofunuliwa (Luka 24:25; Matt. 22:31,32,43,44), ni wale tu walio nalo na wanaoliamini neno Lake wana uwezo wa kuzifuata na kufaidika na alama za barabarani (zilizopangwa kama masazo ya mkate) zilizo katika Kitabu Chake kisicho na makosa. Je, kitabu cha Malaki ni mfano wa Biblia ya King James? Yaweza kuwa; Biblia ya King James pekee inafundisha kwamba historia inajirudia, ilifunuliwa katika wakati mwafaka, inaruhusu / inalazimu umaizi katika kuisoma, ina Jina na cheo cha Mungu juu yake, haimilikiwi na mwanadamu, hairuhusu demokrasia, si uzao wa uhakiki wa juu wa nyaraka / hati, inatamka kwa uthabiti kwamba suala muhimu katika Biblia ni utiifu kwa mamlaka, na imeandikwa katika lugha sahihi. (Kwa kusema hili ninamaanisha lugha ya Kiingereza kabla haijabadilishwa na sheria na kanuni za sarufi za lugha iliyokufa ya Kilatini inayotumiwa na Kanisa la Rumi. Kwa maneno mengine, hata Kiingereza cha Biblia ya King James hakijaingiliwa na kuvurugwa na “usahihisho” wa mwanadamu kwa sababu ilitolewa kabla Kiingereza hakijavurugwa na sheria na kanuni za sarufi ya Kilatini.) AV1611 inakidhi fasili imara za Mungu [alizoziweka] kwa ajili ya neno Lake, inatunza usahihi na uhalali wa wakati uliopo (present tense) katika 2 Tim. 3:15,16, inatuwezesha kutoka katika hali ya utumishi usio na uelewa hadi kufikia hali ya marafiki wenye uelewa (Yoh. 15:15; 10:4,5), na tukiiweka Yoh. 12:48 akilini, tunapata ruksa ya kusema kwa unyenyekevu na kwa shukrani 2 Tim. 4:6-8. Na, kama kitabu origino cha Malaki, Biblia ya King James ni hati / waraka origino kwani hii si tafsiri (kama watu wenye mioyo haribifu, wasiokuwa na kweli, wanavyodhani) kwa sababu haiendani na waraka wowote wa ERROR katika familia yoyote ya nyaraka. Ni origino ya kipekee kabisa.

 

Mungu na neno Lake [wote] ni halisi. Ametupatia neno Lake, amelitunza kwa ajili yetu, amefanya iwe rahisi kulieneza duniani kote. Ni makosa kutafuta toleo la Biblia kwa kutumia falsafa kama mwongozo wetu badala ya kutumia maelekezo Yake. Na kwa kuwa sisi ni raia katika ufalme Wake, sisi hatuna ridhaa ya kuchagua toleo la Biblia tunalopenda; wajibu wetu ni kulipokea kwa utiifu tunda lolote safi alilotutayarishia.

 

Ndugu zangu, nilipokuja kwenu, sikuja kwa ufasaha wa maneno yangu wala na maneno ya ushawishi ya hekima ya mwanadamu, bali katika dhahiri ya imani kwa Mungu na uweza Wake: ili imani yenu isiwe na mhimili wake katika hekima ya wanadamu, bali katika udhihirisho wa Roho na wa uweza. Ikiwa yeyote kati yenu anaonekana mwenye hekima katika ulimwengu huu, basi na awe [kwanza] mpumbavu, ili aweze kuwa mwenye hekima. Kwani hekima ya ulimwengu huu ni upumbavu mbele za Mungu.

 

=0=